Kanisa la VCCT lililo chini ya 
Rev. Dr. Huruma Nkone siku ya Jumapili ya tarehe 2 September, 2012 wanatarajia kuanza kufanya  Ibada Rasmi ndani ya Hema Mpya Ya Kisasa ambayo imeagizwa Kutoka South Africa maalum kwa Ajili Ya Ibada.

Hema Hiyo Ya Kisasa yenye uwezo wa Kuchukua Watu takribani 1000 kwa Mara Moja imefungwa katika Kiwanja Cha Kanisa hilo kilicho maeneo ya Mbezi Beach Kawe ambapo Kwa maelezo ya Dr. Huruma Nkone Hema hiyo ni ya Muda Kabla Kanisa halijaanza 
Ujenzi wa Kanisa Kubwa la Kisasa ambalo litaitwa VCCS-- Victory Christian Centre Sanctuary.

                                 Tabernacle Inavyoonekana Kwa Nje 
Kwa Karibu zaidi

 Ndani Ya Kanisa hilo,  Kanisa Zima zileweka Zuria la Kisasa lenye Kunyonya Mawimbi Ya Sauti Kwa ajili Ya Vyombo Vya Muziki kwa ajili ya Kuzuia Mwangwi, Ndani ya Hema hiyo kimefungwa Chomo Maalum Cha Kudhibiti Sauti Ili Sauti Isisumbue Majirani ( Sound Proof), Ndani Ya Hema Hilo Limezunguzwa na AC, Viyoyozi Vya Kisasa kwa ajili ya Kuhifadhi ubaridi wakati wa Ibada na Kuondoa Joto.
Hapa Vijana wakifanya Set Up Ya Venue kwa ajili ya Ibada Viti Vyekundu Ni Maalum kwa Ajili ya Hema.
                       Carpet Maalum kwa ajili ya Kuzia Mwangwi Wa Sauti

                                                        Ndani Ya Hema

The Rivers Of Joy Wanategemewa kuongoza Praise & Worship

Kanisa la VCCT ambalo liko chini ya Dr. Huruma Nkone, asilimia 60 ya Washirika Wa kanisa Hilo ni Wanafunzi, na Asilimila 80-85 Ya Washirika ni Vijana.Kati Ya Vitu ambavyo Pastor Dr. Huruma Nkone ame invest katika Kanisa hilo ni

1. "Quality"---- Katika hili Designing Ya Kanisa aliibuni Pastor Mwenyewe, Events za Kanisa kama Campus  Night, Soul Breakfast, Open Mic Open heart na Zingine ni Za Kiwango Kikubwa.
                                  Pastor Huruma and Pastor Joyce Nkone

2. Raising People's Talents---- Dr. Huruma Nkone amejaaliwa Karama ya Kugundua, Kulea na Kuendeleza Talents Za Watu, The Praise Team, Ushers Organisation, Mcz, teachings, Singing unless mtu hajataka Kutumika lakini yeyote aliye tayari Kutumika Mlango Uko Wazi. Kwa Sasa imeanzishwa Praise Team (Rivers Of Joy Junior) ambayo hii ita raise Praise and Worship Leaders Miaka 10 Ijayo ambao Kwa sasa wako katika professional teachings.
                                                            
3. PFW---Prayer, Fasting and Word Of God---- Ni Lazima Kila Mwezi  Wiki ya Kwanza Utaratibu wa Kanisa Washirika Kufunga na Kuomba Kama Kanisa, na Kuna Maombi Alfajiri, Mchana na jioni, Kila Mwanzo Wa Mwezi Wiki ya Kwanza ni YA Mungu. Washirika Wamegawiwa katika Vikundi Mbalimbali wanakokaa, Vijana, Wanawake, Wanafunzi Kila Jumamosi Ya Mwisho wa Mwezi, Wana taalum kila Mwanzo Wa Mwezi Jumapili, hakuna Kada mbayo imeachwa bila watu wa aina hiyo Kukutana Kwa ajili ya kujifunza Neno la Mungu.
Marafiki wa kanisa la VCC kutoka Mataifa Mbali Mbali 
  
Hili ndilo Tangazo ambalo limeonekana katika page ya kanisa la VCC Facebook kuashiria ni kweli kuwa wako wamehama
Hii ni Picha ambayo imekutwa katika account mbali mbali za washirika wa kanisa hilo Facebook

Mawasiliano ya Mtandao
Www.vcc.or.tz(website ya kanisa la VCC) ,Facebook Page ya Kanisa inaitwa,"Victory Christian Centre (VCC)", Page ya Vijana Inaitwa "The Bridge Youth Ministry" na Page Ya Wanafunzi inaitwa "Soul Breakfast"



Shukrani maalumu ziwaendee Papaa Ze Blogger na  Missionary Paul William Nyanda kwa kushirikiana na blog hii kupata habari hizi
|