Kila asubuhi jamii kubwa ya wanadamu wanaamka na kwenda sehemu mbali mbali kwa ajili ya kwenda kujishughulisha ili kupata mahitaji muhimu ya kila siku kwenye maisha yao na jamii kwa ujumla.Tumekuwa tukizungukwa na changamoto mbali mbali kutokana na sababu mbali mbali lakini mwisho wa siku lazima lengo halisi litimie kufikia maswala muhimu ya kimaisha na kijamii.Maisha huchosha na hukatisha tamaa iwapo tunapoona njia ya kufikia yale tunayoyataka kuwa ngumu kupita kawaida lakini Unapofikiria Kuchoka Kabla ya Muda wa Kuchoka Haujafika unakuwa sawa sawa na mkulima anayepanda mbegu zake kwenye Jiwe akitegemea ziote.
1.Mazingira
Mazingira tunayoishi kila siku tangu tunaingia kwenye sayari hii itwayo Dunia yamekuwa na nguvu kubwa ya kututengeneza namna tunavyoweza kupambana na changamoto mbali mbali za kimaisha tunazokutana nazo,Ukitaka kufahamu ili kama ni ukweli au uongo mchukue Mang'ati aliyekaa porini tangu siku anazaliwa kisha baada ya miaka 20 mlete Mjini ndipo utaelewa nachosema.Ndio maana kuna mwingine Changamoto inapotokea hukimbilia kusema huu ndio mwisho wa maisha yangu lakini kwa mwingine husema huu ndio wakati muafaka wa kusonga mbele.Ukifwatilia kwa ukaribu kati ya hawa watu wawili Mazingira na vitu walivyokutana navyo vinawapa uwezo wa kujua iwapo wanaweza kuvuka juu ya changamoto fulani au hapana.
2.Watu
Kariba za watu wa aina mbali mbali tunaokutana nao zinauwezo mkubwa pia wa kutufanya tufikiri namna tunavyoweza kushinda vikwazo na taabu mbali mbali tunazokutana nazo kila siku.Wakati mtu mmoja akikutana na Pope Benedict XVI swali la kwanza watakalomuuliza ni kwanini Umejiuzulu kuwa Pope Mtu Mashuhuri zaidi Ulimwenguni?Lakini kuna watu wengine hawafikiria kumuuliza kwanini Amejiuzulu "Watamuuliza Je umefanikiwaje kufika kwenye Hiki cheo cha Kuwa Kiongozi wa Kanisa lenye wafuasi wengi zaidi Duniani?Ukifwatilia kuna mwingine amekutana na watu wenye mtazamo wa kimaskini lakini mwingine amekutana na watu wenye mtazamo wa kujua mbinu za kufikia mafanikio.Jiulize wewe je ukikutana na Mengi leo Utakimbilia Kumwomba Pesa au Utamwomba Ushauri ambao utakaokuzalishia Pesa zaidi ya alizokupa Siku hiyo?
3.Ufahamu
Mtu jasiri anayejua anapokwenda kufikiria kuchoka kabla ya Safari yake haijafika ni mwisho.Mtu mwenye kutafuata maarifa na ufahamu juu ya namna ya kuendesha na maisha na kushinda changamoto siku zote hawezi kuwa mkata tamaa.Unapofikiria Kuchoka Kabla ya Muda wa Kuchoka Haujafika ni sawa na kujaribu Kujaribu kuendesha gari lenye pancha ukitegemea litakufikisha Mbeya wakti ndio kwanza unatoka Sinza KIjiweni.Ufahamu hukupa mbinu mbadala za namna ya kutatua changamto husika bila ya kuweza kuishia njia.Tambua vita yeyote duniani unayoiona kwanza huanza kwenye Kichwa cha mtu.Hakuna vita inayoanza nje ya kichwa cha mtu.Jaribu kutafuta ufahamu kila siku.Safari bado ni ndefu usifikiri kuishia njiani wakati unaanza safari ulijua utafika.Jipe Moyo na Usonge Mbele VIkwazo na Changamoto ni sehemu ya maisha ndio maana viliwekwa kuonyesha namna ulivyo hodari na shujaa.
Hakuna Hodari wa Vita anayeweza kujisifia ni Mshindi wakati haukuwahi kupigana vita vya namna yeyote.Changamoto na vikwazo ni Sehemu ya Ushindi ndio maana vipo.Changamoto na vikwazo havikuwekwa kwa ajili ya wanyonge bali kwa ajili ya washindi.Changamoto na Vikwazo havikuwekwa kwajili ya Wanyama ,Viliwekwa kwa ajili ya Binadamu.Siku zote Mshindi hupata Ushindi kabla ya Kufika Eneo la Mapambano La Vita lakini Watu dhaifu hushindwa kabla hawajafika hata eneo la Mapambano.Acha Kufikiria kuchoka kabla y.a Muda wa Kuchoka Kufika.Changomoto na Vikwazo kwenye maisha nivifwananisha na Gereza ambalo hawakutengezewa Kuku bali Watu na ndivyo Changamoto zilivyo ni Kwa ajili ya Watu ambao wamejizatiti kufikia hatma yao ya Maisha na Sio Aina Nyingine ya Viumbe Visivyokuwa na Utashi.