Kirk Franklin |
Kwa sasa unapoongelea mwanamuziki mwenye fedha za kutisha ulimwenguni kwenye Upande wa Muziki wa Injili huwezi kutaja jina Lingine zaidi ya Kirk Franklin.
Utajiri wa Kirk Franklin kwa sasa una thamani ya Dola Milioni $ 8.5.
Mwanamuziki huyu alizaliwa Julai 26,1970 katika jimbo la Texas.
Baada ya Kuzaliwa Mama yake mzazi alimtelekeza na kulelewa na Shangazi yake aitwaye Gertrude .
Aliaanza kujifunza kupiga piano na miaka 4 na akiwa na Miaka 7 alianza kupata mkataba wake wa kwanza wa Kurekodi Albamu yake ya Kwanza Lakini Shangazi yake alikataa.
Mwaka 1996 ndipo alipomuaoa rafiki yake wa Karibu Tammy Collins.Wakati wanaoana watu hawa wawili kila mmoja alikuwa na mtoto mmoja mmoja kutoka kwenye mahusiano yake yaliyopita.Baada ya Kuoana Kirk Franklin pamoja na mkewe wamefanikiwa kupata Watoto wa Wawili na kwa jumla wana familia ya watoto wanne.