Leo katika segment ya Punch of The Week tunaendelea kujadili mambo mbali mbali ambayo yanaweza kutusaidia kubadilisha mfumo wetu wa kufikiri na namna ambavyo tunaweza kuangalia vitu kwa namna ya pekee.

Tanzania ni moja ya nchi ambayo imebahatika kuwa na rasilimali nyingi sana za aina tofauti tofauti katika kila nyanja lakini sisi watanzania tumekuwa tukiendelea kubaki katika hali ya kutojitambua na kuendelea kulaumu mifumo mbali mbali katika uendeshaji wa vitu.Lakini cha Kushangaza Pindi wageni wanapokuja ndani ya nchi wanatumia rasilimali tulizo nazo na wanapata upenyo wa kufanikiwa huku tukiendela kuwaona kama wachawi.Kumbuka unapokiona wewe kitu hakifai na kukidharau au kutokuwa na mtazamo sahihi ndipo inakuwa nafuu kwa mchukuzi.Kuvuja kwa pakacha ya nafuu ya mchukuzi.

Katika eneo hili tumejaribu kuangalia mambo machache amabayo yanaweza kukusaidia kuweza kujitambua kuweza kusonga mbele katika maisha yao bila woga na kujidharau huku ukijua faida yake katika siku zijazo.Ukiwa kama ndugu,jamaa,rafiki,unaweza ukaamua kufanya mabadiliko yako mwenyewe bila kushurutishwa wala kulazimishwa na mtu.

1.Social Yardstick(VIpimo vya Kijamii)
Muda mwingine kwenye maisha yetu tumeshindwa kuzitumia fursa ambazo tunazo sababu tumetumia jamii kama sehemu ya kipimo chetu cha kuendesha mambo na vitu vyetu.Mfano Utasikia "Yaani mtoto wa fulani hakufanikiwa na alikuwa na akili sana wewe ndio utafanikiwa?.Unaposikia ivyo mara njingi watoto wetu wamedumaa na hata akili zetu zimeduma tumeshindwa kujua watu wengine ni wengine na sisi ni sisi.Jaribu wewe mwenye usitumie mtu mwingine kama kipimo chako cha maendeleo."CHEZA MUZIKI KUTOKANA NA MDUNDO UNAOUSIKIA KICHWANI MWAKO NA SIO HUO UNAOUSIKIA KWA JIRANI YAKO"
Kuitumia jamii kama kipimo chako cha kuendesha vitu ni makosa jaribu kutumia uwezo wako na nguvu zako ili kuweza kupiga hatua kwenye nyanja nyingi za maisha yako binafsi hata ya familia yako.”Mfano…”Mara nyingi familia nyingi zimetumia watoto wengine kama kipimo cha malezi kwa watoto wa familia zao na sio wao kama wao wanaweza kulea na kuwakuza watoto wao,uzuri au ubaya wa mototo hautokani kuwa mototo wa jirani yako ni mzuri au mbaya.

 2.Comparison(Kujilinganisha)
Hili limekuwa miongoni mwa matatizo makubwa kwa tumetumia watu wengine kama sehemu ya kipimo cha mafanikio Fulani ingawa si vibaya kujua mwingine anafanya nini.Unapotumia muda mwingi kujilinganisha na mwingine unapoteza uwezo wako halisi wa kufanya vitu katika uwanda mpana wa maisha yako.Kumbuka kila mtu ana maono na ndoto zake kwenye maisha yake unapojaribu kuwa kama yeye unaishi maisha yake wakati wewe sio yeye.Jifunze kuishi maisha bila kujilinganisha linganisha na wengine maisha ni kujaribu kutumia fursa zilizopo.Kumbuka unaweza ukafanya ziaidi kuliko mtu unayejilinganisha naye kwa kufanya ziaidi vizuri sana.
Unaweza ukajikuta unafanya vitu chini ya kiwango kumbe uwezo wako unaweza ukawa ni mukubwa zaidi ya hapo.
“Fikiria Steve Paul Jobs au Bill Gates wangejilinganisha bila kila mmoja wao kuaamua kuishi kama yeye leo kuna baadhi ya vitu ambavyo tungekuwa tunakosa kwenye Ulimwengu huu.

 "CHEZA MUZIKI KUTOKANA NA MDUNDO UNAOUSIKIA KICHWANI MWAKO NA SIO HUO UNAOUSIKIA KWA JIRANI YAKO"