PART II.

Huu ni mwendelezo wa somo amabalo linazungumzia sifa za mtu mwenye majeraha au uchungu ndani ya moyo.Somo hili lilianza wiki iliyopita



6. Ni watu ambao hukaa vinyongo moyoni kwa muda mrefu na hawapendi kusamehe.Mara nyingi watu wa aina hii kusamehe watu wengine ni ngumu sana.Inapofika kwao swala la kusamehe ni afadhali kutafuta mbadala kuliko wao kusamehe mtu makosa waliowafanyia.

7. Ni watu wasumbufu  mara kwa mara na hupenda kulalamika mara kwa mara hata pale ambapo haikupaswa kulalamika bila sababu za msingi.Ulalamishi kwao huwa ni jambo la kawaida ila wao huwa hawapendi kulalamikiwa hata wanapokosea.

8.Hawapendi kushirikiana na watu wengine juu ya mambo mbali mbali ya kijamii mpaka pale watakapojisikia wao wenyewe tu.Pia hawapendi kusaidiwa hata pale ambapo wanapaswa kupata msaada kwa sababu wanajua watajenga ukaribu na watu kitu ambacho wao hawakipendi na wala hawakitaki.

9. Ni watu wanaoongozwa na misisimuko na hisia zaidi kuliko uhalisia.Mara utakuta wana furaha mara baada ya muda mfupi wana huzuni,mara wamekasirika.Hisia zao haziko constant kuwa anafurahi muda wote..au mechukia muda wote.Yaani tabia na hisia zao huwa hazieleweki.Hisia zao huwa kutokana na anavyojisikia siku hiyo au muda huo.


………………Kaa  tayari kwa ajili ya Part III ..ambayo ni ya mwisho..................

Stay tunned…….


| |