JE UPI NI UKWELI KUHUSU KANISA LA UFUFUO NA UZIMA(MCHUNGAJI GWAJIMA) NA JESHI LA POLISI KUHUSU JOSHUA MULINDI(MTESAJI)?
Ama kweli damu ya mtu haiendi Bure .Baada ya Jana kuendelea kuangalia vyombo mbali mbali juu ya sakata la utesaji wa Daktari Ulimboka ,Joshua Mulindi(Mtesaji),Mchungaji Gwajima na Jeshi la Polisi kuna baadhi ya mambo ambayo kama watanzania tumeendelea kujiuliza maswali mengi sana.Je kuna usiri gani juu ya hili sakata na je ni yupi muhusika mkuu wa hii kitu (Master Mind) na Je hao watesaj wengine 14 ambao walikuwa na Joshua Mulindi(Mtesaji) mbona hawajatajwa mpaka leo au ndio hadithi zile zile za siku zote.
Jeshi la Polisi liliibuka kupitia Kamanda Kova kwa mara nyingine kuhusu swala hili likikemea kuhusu malumbano mbali mbali juu ya mjadala huu kati ya Taasisi za Dini za Kikristo na Jeshi la Polisi baada ya swala hili Kufikishwa katika Mahakama …Na haya ndio maswali ambayo tumekuwa tukijiuliza …
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu Dar es Salaam,Suleiman Kova
- Je Katiba Katiba inasemaje Juu ya Kujadili swala ambalo limefikishwa mahakamani ,Je linaruhusu upande mmoja kutoa taarifa na kuuzuia mwingine kujibu ?
- Je katiba inasemaje kuhusu mtu unaporipoti kituo cha Polisi juu ya mtu ambaye analeta fujo kwenye eneo lako?Je anapokamatwa wewe uliyepeleka taarifa unakuwa mtuhumiwa au mshutumiwa bila kuulizwa au kupewa taarifa?
- Je kama kuna uthibitisho juu ya kile kinachodaiwa kuhusu mtuhumiwa(Kanisa la Ufufuo na Uzima) kwanini hakisemwi mpaka mtuhumiwa anapolalamika ndipo wewe ujibu tena kupitia vyombo vya habari ?
- Je ni upi uwezo wa intelijesia yetu juu ya mambo kama haya …..haswa hizi issue za kupika?...Wako wapi waliorudisha fedha za EPA?Au ndio funika kombe mwanaharamu apite?Hapa ndipo unapokuja usemi kwanini walioko jela wengi ni maskini?
….Kumbuka kuwa hata mara zote mtu mkimiya anaponyamaza sio kuwa hana cha kusema bali hutumia busara na uvumilivu…Muda unapofika uvumilivu ukafikamwisho ndio haya sasa tunayoyaona….