Wakati nchi yetu ikiwa katika mchakato wa kukusanya maoni juu ya mbadiliko ya Katiba kwenye nhi yetu asilimia kubwa ya watanzania hawajui kinachoendela kabisa na umuhimu wake katika nhi yetu ya Tanzania kwa Miaka ijayo.
Tangu nchi hii kupata uhuru hatujawahi kuwa na Katiba yetu kama watanzania bali tumekuwa na Katiba ambayo ilaandaliwa na baadhi ya watu wachache kuendesha nchi yetu.Lakini 
kadri Siku zinavyozidi kwenda tumekuja kuona Katiba iliyopo sasa haikidhi mahitaji kwa kiasi kikubwa kulingana na wakati wa mabadiliko makubwa tulio nayo kwenye namna ya uendeshaji wa nchi na mifumo yake mbali mbali kuanzia kwa Watawala na Watawaliwa.
Kinachochangaza Watanzania tulio wengi ndio tulidai mabadiliko ya Katiba kwenye nchi yetu lakini katika mchakato huu wa Makusanyo ya Maoni ya mabadiliko ya Katiba kunashangaza,Tumekuwa waongeaji sana wa mitaani na vijiweni lakini kwenye utendaji kuwasilisha maoni yetu tumekuwa wavivu.Kumbuka unanaposhindwa kutoa maoni yako kuhusu namna Katiba ya nchi yako iweje siku maamuzi yanapotolewa usiwe wa kwanza kulalamika tena.Na itakupasa kulipa gharama kwa Muda wa Kipindi Kirefu kijacho.Maisha ya nchi hii wewe na vizazi vyako vyote vijavyo inategemea unafanya nini kwa sasa.

Takwimu kutoka kwenye Tovuti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba

Katika awamu ya tatu iliyomalizika tarehe 6 Novemba, 2012, Tume ilifanya mikutano 522 katika mikoa yote tisa ingawa ilipanga kufanya mikutano 496. Hali hii ilitokana na mahitaji mapya katika maeneo mbalimbali ya mikoa hiyo na kuifanya Tume kuitisha mikutano ya ziada ili kuwapa fursa wananchi wengi zaidi. Katika awamu ya pili, Tume ilifanya mikutano 449 ambapo Awamu ya kwanza Tume ilifanya mikutano 388.
 Katika awamu hii ya tatu, jumla ya wananchi 392,385 walihudhuria mikutano. Jumla ya wananchi 21,512 walitoa maoni yao kwa kuzungumza katika mikutano hiyo na wananchi 84,939 walitoa maoni yao kwa maandishi. Aidha, katika awamu hii ya tatu, jumla ya wananchi 1,639 walitoa maoni yao kwa kuzungumza na pia kwa maandishi katika mikutano hiyo.
Mwitikio wa wananchi kuendelea kutumia simu za mkononi, ukurasa wa facebook, tovuti na posta kutoa maoni nao umeongezeka kwa kiasi kikubwa. Kwa mfano, jumla ya wananchi 27,992 walikuwa wametembelea ukurasa wa facebook wa Tume katika kipindi cha awamu ya tatu tofauti na watu 21,789 waliotembelea katika kipindi cha awamu ya pili. Aidha, ujumbe mfupi wa simu (sms) 6,909 umepokewa na Tume katika awamu hii ukilinganishwa na sms 75 katika kipindi kilichopita;
Idadi ya wananchi wanaohudhuria na kutoa maoni katika mikutano nayo imeongezeka. Kwa mfano, idadi ya wananchi waliohudhuria mikutano ya awamu ya kwanza walikuwa 189,526.  Awamu ya pili ni 325,915 wakati wananchi waliohudhuria mikutano ya awamu ya tatu ni 392,385. Aidha, wananchi waliotoa maoni kwa kuzungumza katika mikutano ya awamu ya   kwanza walikuwa 17,127. Awamu ya pili walikuwa 12,334 wakati wananchi 21,512 walizungumza katika awamu ya tatu;

Ukifwatilia hizi takwimu hapa juu utagungua Maamuzi ya Nchi hii yanye watu takribani Milioni 40 na kuendela kwa sasa watu ambao hawafiki hata milioni tatu ndio wanaamua nini kifanyike juu ya nchi hii kwa Miaka mingine Mingi ijayo.
Inatia Hasira kuona watu wachache namna hii ndio wanato maamuzi ya nch hii sisi wengine Vijiweni,kuchati facebook,Twitter,kwenye simu zetu za mkononi,Kusubiri Ze Comedi ni lini au Tamasha La Fiesta ni lini au Rose Muhando anazindua lini?
Ni muhimu kujua habari mbali mbali katika nchi lakini Kumbuka kuna baadhi ya vitu maishani mwako vinaamua hatma yako kwenye kila jambo.

Njia Ambazo Unaweza kutuma Maoni yako.

1. Njia ya simu 
+255 22 2133425
2. Barua pepe 
katibu @katiba.go.tz
3. Tovuti ya Tume ya Mbadiliko ya Katiba 
http://www.katiba.go.tz/index.php/toa-maoni-yako
4.Facebook
https://www.facebook.com/pages/Tume-ya-Mabadiliko-ya-Katiba-Tanzania/323414977745643?fref=ts
5.Tume ya Mabadiliko ya Katiba
Makao Makuu
Sanduku La Posta 1681,
Dar es Salaam, Tanzania.

MUNGU IBARIKI AFRICA , MUNGU IBARIKI 
TANZANIA