Watanzania na jamii yetu kwa ujumla tumejengwa na kukuzwa zaidi katika hali ya kupenda kufikiria kushindwa kuliko kushinda katika maisha yetu na kila siku kutokana  na malezi na namna mfumo wa vitu vingi wa maisha unavyoendeshwa.Mfumo wa maisha yetu tangu tunaanza tungu nyumabani tukiwa wadogo na hata tunapoanza shule mazingira yetu hayaamini katika kushinda kuliko kushindwa.Kujiamini katika kila tunachofanya ni kama umekuwa mzimu ulio hai unaosumbua maisha yetu tangu tungali wadogo mpaka watu wazima.Muda mwingine tumejitungua misemo ambayo ukifwatila haina mashiko zaidi ya kutaka kutuondoa uoga tu na sio zaidi...."Tukiwezeshwa Tunaweza".Swali la msingi je hao waliweza waliwezeshwa na na nani na wana vichwa vingapi na wamewezaje kufika hapo.
Tukiendelea kwa namna hii safari ya ukombozi katika nyanja mbali mbali yaani Kifikra,Kiuchumi,Kijamii,Kisiasa na hata kidini itakuwa ni kama kumtafuta kuku anayenyoshesha tukitaka atupatie maziwa....


 Mambo machache ambayo yanaweza kutufanya tupende kufikiria  katika kushindwa zaidi kuliko katika kushinda................


1.System(Mfumo)
Mfumo wetu wa malezi kuanzia watoto na hata mfumo wa uongozi katika nchi yetu katika nyanja mbali mbali hauutupi mwanya wa kuweza kufikiria na kuamini katika kushinda katika kila tunalolifanya zaidi ya kufikiria na kupenda kushindwa zaidi bila ya sisi wenyewe kujua nini tatizo limeanzia wapi.
             
Pamoja na mfumo mbovu katika kila nyanja ya maisha yetu ambao tumekutana nao sio kigezo cha kutufanya iwe kisingizio kwamba tusiamini katika kushinda zaidi ya kufikiria katika kushinda.."System haipo kwa ajili ya walio nje ya system bali system ipo kuwapa favour  wale waliopo kwenye system tu"Ni jukumu lako kuamua kubadilisha mfumo wako mwenyewe kwenye fikra zaidi kuiko kuendelea mfumo sababu utaishia kulaumu tu na hautafika kokote.

2.Historical  Background(Maisha yetu na Historia za Nyuma)

Familia zetu nyingi za kiafrika haziamini katika kushinda zaidi kuliko kushindwa.Ni familia bora na chache sana ambazo zinaweza kuamini katika kushinda kuliko kushindwa tangu tukiwa wadogo..Familia nyingi zimekuwa na mtazamo hafifu tangu watoto wanapoanza shule kuanzia maneno wanayotakiwa mpaka matendo wanayofanyi katika nyanja mbali mbali hii haikupi njanya ya kufikiria na uwanda mpana wa kuamini ushindi unawezeka..utasikia wanasema ..."Yaani Baba yako aliishia hapo ,Babu hapo hapo,Mimi mwenyewe mama yako pamoja na wote sisi kuwa na akili kwenye ukoo wetu bado nimeishi hapo ...je wewe utaweza au ndio unajifanya una akili sana?"Wanashindwa kujua wao ni wao na sisi ni sisi kwani kuna vitu vingi vimebadilika sana.
          
Ndio utasikia hata mtu akishindwa kwenye jambo dogo tu...Yaani sisi sijui tunamikosi gani....Yaani hii ni tatizo kubwa katika jamii...wewe ndio mkosi wa kwanza wa kushindwa kufanya maamuzi sahihi.


3.Relationship Break ups.

Katika kizazi chetu kutokana na sarakasi nyingi za kimahusiano ambazo tumekuwa zikitupata kwa kuvunjika na kushindwa kuwa na mahusiano bora ya kimapenzi imetupelekea kushindwa na kujiamini katika kila tunachokifanya.Huu msuko suko wa kupiga vibuti na kupigwa vibuti(Kuacha na Kuachwa) limekuwa ni tatizo kubwa la kufanya watu wengi kutosonga mbele na kupiga hatua mpya katika maisha yetu ya kila siku.
                         
Mara tu anapoonza kugika hatua mpya ndani yake bado anasutwa unasikia maneno haya "lakini wewe umeachwa na sijui kama utapendwa tena".Matokeo yanayopelekea watu kujitungia maneno ya ambayo hayana hata mashiko na uelewa timamu.Utasikia watu wanasema."Wanaume wote si sawa..yaani wote baba na mama mmoja au Wanawake wote si wale wale".Ukisikia mtu anasema hivyo fwatilia yaani kuna sehemu katendwa.

4.Past Failures.

Baada ya watu kuweza kushindwa katika maisha yetu katika kipindi fulani cha nyuma imepelekea mioyo yetu kushindwa kujiamini katika kila hatua mpya ambayo tunataka kuichukua ili kuweza kuendelea mbele.Kushindwa katika jambo fulani katika kipindi cha nyuma haina maana ya kwamba hauwezi kushinda katika jambo lingene katika maisha....Mfano "Watoto wengi wakifeli Kidato cha Nne huamini kuwa maisha yameishia hapo kumbe maisha bado yanaendelea ."
                     
Kumbe ni wakati wakujaribu fursa mpya za kimaisha na mambo Mengine.Imekupasa kujaribu tena katika kila unachokifanya hata kama ulishindwa nyuma hiko sio kigezo kwamba utashindwa tena na wala sio sababu ya msingi ambayo unaweza ukaeleza watu.Fanya tena na tena...

"Mbunge wangu wa Ubungo Mh.John Mnyika alipojaribu mwaka 2005 kugombania Ubunge kwenye jimbo la Ubungo alishindwa lakini hiyo haikuwa tiketi ya kukata tamaa matokeo yake mwaka 2010 alijaribu tena..ndipo ushindi ulipopatikana..Leo hii tunachekelea na kufurahia kumbe ni hatua ya mtu aliyoamua kuchukua maamuzi mwenyewe.

........Jenga tabia ya  kufikiria kushinda zaidi kuliko kushindwa zaidi...