1.Bill Clinton and Hillary Clinton
Aliyekuwa Raisi wa Marekani Bill Clinton na Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje Bibi Hillary Clinton ndio Ndoa ambayo inashikilia namba moja kuwa Ndoa ambayo imewavutia watu wengi zaidi katika mwaka 2012 kwa mujibu wa mitandao mbali mbali.Ndoa hii ilifungwa mwaka 1975,Octoba 11.Kwa mara ya kwanza walikutana mwaka 1970.Pamoja na Ndoa hii kupita kwenye misuko suko mbali mbali lakini bado imeendelea kuwa Imara na Inaonekana kuwa ni ndoa yenye afya zaidi kuliko nyingine zaidi katika mwaka 2012.
2.Bill Gates and Melinda Gates
Pamoja na Bill Gates kushikilia namba moja kwa utajiri lakini bado anaendelea kufanya vizuri kwenye ndoa yake yeye pamoja na mkewe Melinda.Ndoa ya Bill Gates na Melinda ndio inashikilia namba mbili kwa kupendwa na kuvutiwa zaidi na watu wengine duniani kulingana na mitandao mbali mbali kwa mwaka 2012.Ndoa hii ilifungwa mwaka 1994 January 1 kwenye visiwa vya Hawaii.BAdo ndoa hiii haijatetereka hata kidogo kwa muda mrefu wamekuwa wakifanya kazi pamoja ikiwa ni Pamoja na mfuko wao wa Misaada ulimwenguni kote wenye Jina la Bill and Melinda Gates Foundation.
3.Barack Obama and Michelle Obama
Raisi wa Marekani Barack Obama na Mkewe Michelle Obama ndio ndoa ambao inashikilia namba tatu ilionyesha kuwavutia watu zaidi katika mwaka 2012 kwa mujibu wa mitandao mbali mbali.Kwa mara ya kwanza wanandoa hawa walikutana mwaka 1989 lakini harusi Rasmi ilifungwa Octoba 3,1991.Huyu ndie Rais wa 44 wa Taifa lenye Nguvu zaidi na Ushawishi mkubwa zaidi Ulimwenguni kwa sasa.
Mwaka 2012 katika Uchaguzi wa Nchii Hiyo familia yake ndio inahesibika ilitoa mchango mkubwa kwenye ushindi wa kiti cha U-Raisi kwa mara nyingine baada kuonekana kwamba Baba wa Familia hiyo angelishindwa kwa mujibu wa kura za maoni na maneno ya mitandao mbali mbali.
4.Marissa Mayer na Zack Bogue.
Mwaka 2009 ndipo Marissa Mayer na Zack Bogue walipoamua kuoana na kuwa mke na mume.Ndoa hii ikiwa bado haina muda mrefu lakini imeingia kwenye rekodi katika mwaka 2012 kuonyesha ni moja ya ndoa ambazo zinawavutia watu wengi.Marrisa Mayer(Mwanamke) aliamua kuacha kazi kwenye Kampuni ya Google kama msaidizi wa CEO na kuamua kujiunga na Kampuni Ya Yahoo na alifanikiwa kuwa CEO wa kampuni ambayo ilikuwa ikipoteza wateja kwa kasi na kupoteza umaarufu wake wa awali na kuifanya kupoteza mapato yake kwa kiasi kikubwa.Mdada huyo utajiri wake kwa mwaka unakadiriwa kufikia kiasi cha dola Milioni $ 300 kwa mwaka.
Pia ndoa hii inaingia kwenye Category ya ndoa bora miuongoni mwa wanateknolojia(Information Technology Category) katika mwaka 2012.
Mwaka 1998 ndipo watu hawa wawili walipoamua kufunga ndoa na kuishi pamoja kama mke na mume.Diane ni moja ya wanawake maarufu na watangazaji wa vipindi mbali mbali kwenye luninga kwa muda mrefu piaalifanikiwa kupata Tuzo kama Director Behind the Scene wa movie mbali mbali kwa kipindi cha nyuma.Ndoa hii inashika namba tano kuwa ni moja ya ndoa inayopendwa na kuvutia watu wengi zaidi kwa mwaka 2012 kupitia mitandao mbali mbali Ulimwenguni.Wote hawa wawili ni wafanyakazi wa vyombo vya habari kwa pamoja.