Kanisa la VCCT lililo chini ya Rev. Dr. Huruma Nkone siku ya Jumapili ya tarehe 2 September, 2012 waliweza kuanza kufanya  Ibada Rasmi ndani ya Hema Mpya Ya Kisasa ambayo imeagizwa Kutoka South Africa maalum kwa Ajili Ya Ibada.Hema hii Mpya ya Kisasa ni mwanzo wa kuelekea kwenye maono makubwa ya Kuwa Sanctuary kubwa na ya kisasa katika eneo hili la Mbezi Beach 'A'  ambalo litakuwa linaitwa  VCCS-- Victory Christian Centre Sanctuary.Pata Matukio zaidi katika picha

Huu ndio muonekano wa Hema ya kisasa kwa nje na huu ndio mmoja ya milango mikubwa mitatu ya kuingia ndani ya hema hii ya kisasa
Huyu ndio Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hili Rev Dr Huruma Nkone(Kushoto) akiwa na mtafsiri wake Dr.Joachim Kilemile
Huyu Jamaa anayeongoza Praise and Worship ana zaidi ya kipaji cha kupiga gitaa ya solo
Rivers of Joy Wakienda Sawa
Celebration haikuwa ya Kitoto Baada ya safari ndefu from Muhimbili Hospitali To Mbezi Beach A tena kwenye Tabernacle  
Papa Ze Blogger hakukosa kabisa kwani Mpaka kufikia hapa kanisa hili limekuwa na safari ya takribani ya miaka isiyopungua kumi...Ndio maana watu wanacelebrate mbele za Bwana

Glorious Celebration Hawakukosa kwenye hii siku
Rev Dr Huruma Nkone akiwa na Mke wake Mchungaji Joyce Nkone
 Samwel Fred akimpongeza Mchungaji Joyce Nkone kwa safari ndefu mpaka kufikia hapa.
Huu ni mfano wa vipozeo maalumu vilivyofungwa kwenye Hema hili kwa ajili ya kupooza joto katika Hema hili la kisasa
 Glorious Celebration wakienda Sawa 
 Uwepo wa Bwana uliposhuka watu walishindwa kujizuia wakaamua kulala chini kumsujudia Bwana Mungu wao,JEHOVAH.
 Hawa ndio Wazee Viongozi wa Kanisa hili wakiwa pamoja na Familia zao
  Glorious Celebration wakienda Sawa 
 WanaVCCT wakicheza mbele za Bwana
MC Pilipili Emanuel Mathias a.k.a Pilipili ya Shughuli a.k.a Mtoto wa Mama Rhoda akifanya vitu vyake VCCT
 MC Pilipili Emanuel Mathias a.k.a Pilipili akiwa na Prezzor Chavala walipokuwa wanafanya ukarabati wa Mbavu za watu VCCT
Hapa nikiwa na rafiki yangu Mc Pilipili baada ya Ibada kwisha katika kanisa la VCCT katika siku ya kwanza



NOTE:Shukrani za Pekee ziwaendee Kanisa la VCCT kwa kusaidia kuandaa makala hii.

....Picha zote zilizotumika ni mali ya Kanisa la VCCT....
| |