Wakati tukiwa tunafikiri maajabu yameisha kumbe ndio kwanza
yaanaanza siku za karibuni Kitabu(Guinness World Records) cha maajabu Duniani Kimefanikiwa Kuingiza
katika Rekodi yake Balbu ambayo Haijawahi kuzima kwa muda mrefu wala Kuungua
kwa takribani Zaidi ya Miaka 110 kwenye Kituo cha Zimamoto namba 6 nchini
Marekani katika Jimbo la California Eneo linaloitwa Livermore.
Balbu hii ambayo iliwekwa mwaka 1901 na kwanza kufanya rasmi
kazi mwaka huo huo siku ya Tarehe 18 mwezi wa Saba.Balbu hiyo ambayo inafanya
kazi Masaa 24 bila kuzimwa kwenye eneo la Injini.
Mwaka 1976 Balbu hiyo ilihamishwa kutoka kwenye eneo moja
kwenda lingine huku kumbukumbu zake za uhamishwaji zikiwa zimetunzwa kwa ustadi
mkubwa.Balbu hiyo ilipumzishwa kwa saa 22 tu mfululizo na ndipo ilowekwa tena
na kuendelea kufanya kazi mpaka leo.
Adolphe A. Chaillet |
Mbunifu wa
Balbu hiyo alijulikana kwa jina la Adolphe A. Chaillet na kisha kutengenezwa na
kampuni ya Balbu ijulikanayo kwa jina la Shelby Electric Co. nchini
Marekani.
Mpaka sasa wataalamu wengine wameshindwa kutoa sababu kwanini Balbu
hiyo haijaungua kwa Muda mrefu lakini pia wameshindwa kutengeneza Balbu
Nyingine kama hiyo ambayo yenyewe uwezo wa kuhimili muda mrefu bila Kuungua.
Kwa sasa Balbu hii imefungiwa Kamera Maalumu
zakuipoza na Kuingalia muda wote kuendelea kupata kumbu kumbu na utendaji mzima
wa Balbu hii yenye Maajabu ya aina yake.