Wakati tukiwa tunafikiri maajabu yameisha kumbe ndio kwanza yaanaanza siku za karibuni Kitabu(Guinness World Records)  cha maajabu Duniani Kimefanikiwa Kuingiza katika Rekodi yake Balbu ambayo Haijawahi kuzima kwa muda mrefu wala Kuungua kwa takribani Zaidi ya Miaka 110 kwenye Kituo cha Zimamoto  namba 6 nchini Marekani katika Jimbo la California Eneo linaloitwa Livermore.

Balbu hii ambayo iliwekwa mwaka 1901 na kwanza kufanya rasmi kazi mwaka huo huo siku ya Tarehe 18 mwezi wa Saba.Balbu hiyo ambayo inafanya kazi Masaa 24 bila kuzimwa kwenye eneo la Injini.

Mwaka 1976 Balbu hiyo ilihamishwa kutoka kwenye eneo moja kwenda lingine huku kumbukumbu zake za uhamishwaji zikiwa zimetunzwa kwa ustadi mkubwa.Balbu hiyo ilipumzishwa kwa saa 22 tu mfululizo na ndipo ilowekwa tena na kuendelea kufanya kazi mpaka leo.


Adolphe A. Chaillet 
Mbunifu wa Balbu hiyo alijulikana kwa jina la Adolphe A. Chaillet na kisha kutengenezwa na kampuni ya Balbu ijulikanayo kwa jina la Shelby Electric Co. nchini Marekani.

Mpaka sasa wataalamu wengine wameshindwa kutoa sababu kwanini Balbu hiyo haijaungua kwa Muda mrefu lakini pia wameshindwa kutengeneza Balbu Nyingine kama hiyo ambayo yenyewe uwezo wa kuhimili muda mrefu bila Kuungua.

Kwa sasa Balbu hii imefungiwa Kamera Maalumu zakuipoza na Kuingalia muda wote kuendelea kupata kumbu kumbu na utendaji mzima wa Balbu hii yenye Maajabu ya aina yake.
|
0 Responses