Mwaka 1996 Sheria ya Ndoa za Jinsia Moja ilisainiwa na aliyekuwa Raisi wa 42 wa Marakeni Bill Clinton
ijulikanayo Kama Defense of Marriage Act a.k.a DOMMA.
Siku chache zilizopita Raisi huyu amaiomba Mahakama Kuu nchini Marekani
kuifuta Sheria Hii kwa sababu ya Mapungufu Mbali Mbali yaliopo kwenye hii
Sheria.
Raisi huyu Ameendela kueleza kwamba kwenye Sheria ya Ndoa ijulikanayo
kama DOMA (Defense of Marriage Act )kusema wazi
kwamba ndoa ni Muunganiko kati ya Mwanamke na Mwanaume tu na sio zaidi ya Hapo.Lakini
zaidi ya hapo Mahakama Kuu ya Marekani imesema itatoa maamuzi yalio rasmi
kisheria mwezi Juni mwaka huu kuhusu ndoa za jinsia moja.
Majaji wataamua kama Defense of Marriage Act kama
inashabiliana na kanuni za Taifa linaloheshimu uhuru ,usawa na haki kwa ujumla na
ambazo hazipingani na Katiba Mama ya Nchi Ya Marekani.
Raisi huyo aliendelea kusema kwamba
Wakati anapitisha Sheria hiyo Ulikuwa ni wakati tofauti na Sasa sababu hakuna
hata jimbo moja lililokuwa linatambua ndoa za jinsia mmoja lakini majimbo
mengine yilikuwa yinafikiria kufanya hivyo na wengi walikuwa wanataka
mabadiliko ya haraka.Kwa Mfano Mpaka kufikia sasa Majimbo zaidi ya Tisa ikiwemo
Colombia District watu wenye mahusiano ya jinsia moja hawewezi kupatiwa huduma
za kajamii kama ilivyo kwa watu wenye mahusiano ya jinsia tofauti…..USA Today
ndio limeripoti .
Hii inaonyesha kwamba Viongozi wa Kisiasa wanapokuwa madarakani wanapenda
kufanya maamuzi ambayo yatawapelekea wao kubaki kwenye madaraka au kulinda
hadhi za vyama vyao vya kisiasa au kwa maslahi yao binafsi ama ya kundi fulani
bila kuangalia athari zake za badae.