Ukomavu kwenye matumizi ya mitandao ya jamii ni swala linalopaswa kwenye jamii ya Watanzania na matumizi ya vyombo mbali mbali vya habari.Je ivi unajisikiaje unavyoyasema mabaya ya mwenzio kwenye mkusanyiko mkubwa wa watu ili hali wewe una ya kwako?Matumizi ya mitandao ya kijamii na Media kwa ujumla inaonyesha namna gani mtu alivyokomaa kwenye uwezo wa kuchambua na kuendesha vitu kwenye maisha yake.Imani na jamii mbali mbali zina mifumo yake ya kutoa hukumu kwa wahusika wanapokosea na sio kuchafuana kwenye mitandao na kuwaacha wengine wakiwa mithiri hawajavaa nguo.Tafakari unasikikia siku Baba yako Mzazi naye amewekwa kwenye Media au kwenye mtandao wa Jamii na ameelezewa mabaya yake Je Utafurahia au utahuzunika?

1.Ki-Imani

Kila imani  ina mfumo wake wakutoa adhabu pale mtu anapokosea iwapo taaratibu za kushtaki kosa husika mahali husika.Inanishangaza sana kuona kosa la mtu mmoja wa Imani fulani linapochukuliwa na mtu wa Imani ile ile mwingine na kwenda kulishikilia bango na kulitangaza kwa watu wengine wasio wa Imani ile.Je unafikiri watu wa Imani nyingine wanawafukiriaje watu wa Imani ambayo mmoja wa waumini wake makosa yake yamewekwa hadharani.Je unajengaje nyumba yako mwenyewe  kwa kubomoa kila baaada ya kumaliza kozi moja ya ujenzi wa matofali?Ufalme ukishajifitini wenyewe hata siku moja hauwezi kuendelea Mbele.Kabla haujaamua kusema mabaya ya mwingine hadharani kwanza jiulize wewe hauna mabaya?Kumbuka kila mtu anachopanda ndicho utakachovuna.Ukimsema vibaya mwenzako wewe subiri tu kuna siku na wewe utasemwa vibaya zaidi na unapoelezea mazuri ya mwenzako tarajia kuna siku watu wataelezea uzuri wako.Baada ya Kufa ni hukumu kumbuka mahesabu yote tunayamaliza hapa hapa.

2.Ki-Jamii

 Kila kwenye jamii ya watu kuna taratibu na sheria husika za kudhibiti wahalifu wa makosa.Je unapomsema mtu hadharani bila kwenda kwenye mamlaka husika je unakuwa umsaidiaje muhusika na wanajamii wengine wasipatwe na tatizo ambalo lilishakukumba kwa kutendewa ubaya na mtu husika au jamii husika ya watu.Facebook na mitandao mingine ya kijamii ikiwa ni pamoja na media mbali mbali kazi yake sio kuelezea na kuonyesha ubaya wa wengine bali kuhakikisha jamii inapata habari kamili na mafunzo ambayo yana tija kwenye jamii.Iwapo unahisi kuna kosa na matatizo juu ya tuhuma kwa watu fulani fwata taratibu za kisheria na kijamii ili kuwasaidia wengine na sio kuishia kuchafuana.Kumbuka unapomchafua mtu akaamu kukufwatilia kisheria na kitaratibu unaweza kushtakiwa na kuadhibiwa kwa kuongea vitu ambavyo havina tija na uhakika kwenye jamii ya watu.

3.Uasili wa Dunia

Namna ulimwengu ulivyotengenezwa na ulivyoumbwa na Mungu ni namna ya ajabu sana.Kumbuka unapofanya kitu kizuri hata kama haukulipwa mazuri kwa muda huo kabla haujaondoka kwenye sayari hii ndivyo utakavyolipwa.Unapoendelea kuelezea makosa ya wengine na ipo siku kabla haujaondoka lazima na sisi tutasikia makosa yako na mabaya yako makubwa kuliko ulivyoelezea ya wengine.Epuka kuwa msemaji wa makosa ya wengine tumia muda wako kuendesha mambo mema na kuwasemea wengine maneno mazuri.Iwapo unaona hauwezi kuchukua hatua basi ni afadhali unyamaze kuliko kuelezea makosa ya wengine mahali pasipo sahihi.Hata siku moja usitegemee kupanda kokoto ukavune maharagwe.Kile unachopanda ndicho unachovuna.



Mwisho,Mitandao ya Kijamii sio sehemu ya kuhukumu dhambi za wengine.Iwapo unaona mtu wa imani yako au wa jamii yako amekosea tafuta msaada ya kisheria na kitaratibu kwenye mahala husika Facebook na kwenye media sio sehemu sahihi ya kuelezana mabaya bali ni sehemu ya kuisadia jamii kuapata maendeleo chanya na yenye tija kwa jamii yetu na taifa kwa ujumla .Safari ni ndefu kwa watanzania kwenye matumizi ya mitandao ya jamii na media kwa ujumla mpaka tukifikia ukomavu wa safari hii basi tumeshajeruhi na kuharibu maisha ya watu wengine wengi sana.


"Ukiona hauwezi kuficha Uchi wa Baba yako Basi Ipo Siku Utamcheka Mkweo kwa Utupu wake."
Kwa muda mrefu kidogo nchi ya Tanzania ambayo imekuwa ikiitwa Kisiwa Cha Amani ili hali si ukweli ila imekuwa Kisiwa Cha Utulivu na Uoga miongoni mwa wananchi wa Tanzania.Kwa Muda wa Miaka ya Karibuni kumekuwa na kujitokeza kwa aina mbali mbali za vurugu haswa zinazojihusisha na Muonekano wa Kidini lakini Pia na Katika Muonekano wa Kimaslahi kati ya Viongozi wa Serikali na Wananchi wa Nchi yenye Utulivu.Nimekuwa nikijiuliza mengi kila kukicha fujo zinatokea na hakuna ambaye anasimama kuzikemea kwamba haipaswi kuwa namna hii ilivyo sasa.Lakini matokeo yake mambo yalivyo watu wamekuwa wakikaa kimiya na viongozi wamekuwa wakivunga.Je ni nani anayefaidika na Hizi Vurugu zinazoendelea?

1.Vurugu zenye Muonekano wa Kidini.
Vurugu hizi kila kukicha zimekuwa zikiongezeka bila sababu zinazoeleweka na zimekuwa zikifungiwa macho na viongozi wamekuwa wakiendelea kuvunga kanakwamba hakuna kinachotokea kwenye nchi yetu.Taasisi za Dini za Upande mmoja zinaposimama kusema ukweli juu ya Vurugu zinazoendela Utasikia Serikali inasemama na kuzikemea kwamba hazina haki ya Kuwa wasemaji ili hali waumini wa Taasisi wa Dini hizo wamekuwa Wahanga kila kukicha.Je Ni Serikali au Baadhi ya Watu wachache wanaofaidiaka na hizi Vurugu?
Siku za Karibuni kumekuwa na mvutano mkubwa kati ya Upande wa Dini ya Ki-Islamu na Wakristo na Upande mmoja umeonekana ukitetewa na kukaliwa kimiya kwa kila wanachofanya ili hali upande mwingine ukitishia kuchukua hatua huonekana na mbaya Je nani anayefaidika na Vurugu hizi?
Miaka yote tumekuwa tukiishi kwa utulivu huu pamoja na tofauti tuliozo nazo lakini hakuna mtu aliyethubutu kumshambulia mwenzake wala kumdharau Je kwanini wakati huu iwe hivyo?Basi kwa mtazamo wa haraka haraka kuna watu ambao watakuwa wanafaidika moja kwa moja au indirect kutokana na muendelezo wa Vurugu hizi.

2.Vurugu zenye Muonekano wa Kimaslahi(Kifedha na Kiuchumi)
Tumeshuhudia fujo kubwa kwa ndugu zetu wa kanda ya kusini juu ya sakata la gesi linaloendelea.Wananchi wenye mumkari wameshindwa kuvumilia juu ya maamuzi wanayofanyiwa wao bila ya wao kushirikishwa kwa muda mrefu nchi hii watu wachache wamekuwa wakiamua nini kifanyike na nani afanye na nani afaidike kwenye kila mradi unaohusisha fedha nyingi.

Wananchi wanapoamua kudai haki zao kwa kutetea kile wanachotaka wao na wanachoona ni sahihi hugeuka kuwa adui wa maslahi ya watu hao wachache..Miradi Mingi imekuwa ikiendeshwa bila uwepo majadiliano na maamuzi ya wananchi wenyewe kuamua kitu gani wanataka juu ya Rasilimali zao lakini watu wachache wakiamua basi ndio yanatendeka.Hakuna elimu ya kutosha juu ya miradi na faida ambazo wananchi watapata baada ya Serikali kuingia Ubia na Mashirika ya Kimataifa.

Miradi Mingi imekuwa ikiendesha kiholela holela na pindi wananchi wanapodai haki zao kwa njia ya amani hawasikilizwi na matokeo yake huundiwa zengwe na kuonekana ni wabaya.Na wanapoamua mutumia nguvu huonekana ni wakorofi na wavunjifu wa amani?Je ni heri fujo na uvunjifu wa amani utokee sababu ya watu wachache?Muda utafika watu hawatakuwa tayari kuendelea na ujinga huu watu watasimama na ndipo muda huu wa neema utakapokuwa umekwisha na hapo ndipo nchi itashindwa kutawalika sababu ya misingi mibovu inayojengwa leo.

Mwisho,Niwazacho Mimi Kuna mtu au  watu watakuwa wanafaidika na Vurugu na Uvunjifu wa Utulivu tulio nao la sivyo basi hatua za Makusudi zingekuwa zimechukuliwa na katika kutatua matatizo haya ambayo kila siku yamekuwa yakikua na kuongezeka bila sauti za viongozi.

Je ni nani anayefaidika na Vurugu zinazoendelea Tanzania?

MUNGU IBARIKI AFRIKA,MUNGU IBARIKI TANZANIA
Kwa Mara Nyingine Napenda kuchukua nafasi hii kuwaasalimu wadau wote wa blogu katika mwaka 2013,Maana kwa Mara nyingine leo Ndipo tunakuta kwenye Programu yetu ya Kila Ijumaa iitwayo Punch of The Week.Leo katika Punch of The Week tumeamua kuangalia vitu kwa jicho la Pembeni kidogo lisemalo Urahisi wa Njia sio Uhakika wa Safari.

Maisha yetu ya kila siku muda mwingine yamekuwa hayana dira sababu ya kukosa mwelekeo sahihi wa kufanya vitu na kuviendeleza huku tukidhani kwamba hii ndio njia sahihi na huo ndio umekuwa mfumo ambao tumekuwa nao katika kila nyanja.Vitu vingi tumekuwa tikivifanya kwa zima moto huku tukidhani kwamba tunaweza kufikia kilele cha mafanikio ambayo yanaweza kudumu daima.

Maisha yetu yamejengwa kwenye kupenda njia za makato kuliko kufwata kanuni ambazo zipo na ndizo za uhakika kwenye maisha yetu kama wanadamu.Hakuna mtu ambaye amejenga mafanikio ya kudumu kwa kutumia njia za mkato.Uasili wa Dunia jinsi ulivyo ni kwamba ukipata kitu kwa dhuluma kitaondoka kwa dhuluma iwe leo au kesho.Mara nyingi tumeshindwa kuangalia mbele tumeangalia matokeo makubwa ya sasa lakini tunasahau kwamba maisha yanaendelea.Wahenga walisema Ukiua kwa Upanga Basi na Wewe utauwawa kwa Upanga wakimaanisha namna kitu kinavyopatikana ndivyo kitakavyoondoka.


Mafanikio yanayodumu ni yale yanayojengwa kwa mfumo wa Haki na kujituma siku zote.Hakuna mazingaombwe kwenye mafanikio wala uchawi.Iwapo unategemea uchawi,wizi na dhuluma kupata maendeleo habari nilio nayo ni kwamba tunasubiri anguko lako siku yeyote kuanzia sasa hata kama leo unaonekana unakula bata na kufurahia lakini kanuni za asili za kuendesha dunia huwa hazibadiliki siku zote.

Kuna hasara njinyi sana kwenye kutegemea kupata vitu kwa njia ya mkato kuliko kufwata kanuni za msingi za kufanikiwa katika jambo lolote.Je wewe unafikiri ungekuwa umezaliwa siku ya kwanza then siku ya pili tunakuona unakimbia je unafikiri sisi tunaokuzunguka tungefikiria vipi?Au wewe mwenyewe ungewazaje?

1.Njia za Mkato mara zote hazitoi jibu la uhakika na linalodumu siku zote.Njia za mkato au zima moto husaidia kutatua tatizo kwa muda tu lakini mara nyingi hakuna uhakika wa kudumu wa suluhisho ambalo litadumu siku zote za maisha.Fikiria iwapo haujawahi kufanya biashara siku zote za maisha yako ghafla unakuwa na biashara kubwa kesho asubuhi unafikiri biashara hiyo itadumu?Jibu ni hapana sababu hauna mufundisho ya msingi juu ya uendeshaji wa biashara na namna ya kucheza na mzunguko wa fedha.Unapofwata hatua mbali mbali unajenda uwezo binafsi wa kujifunza na kuwa na uhakika wa kutokurudia makosa ambayo hautaweza kuyarudia tena.Kumbuka siku zote Vitu rahisi gharama yake ni kubwa zaidi.Mfano Mzuri ni pale ambapo tunapoumwa kichwa kwa ghafla huwa tunameza dawa za kutuliza maumivu tu lakini huwa bado hatujatatua ugonjwa wa msingi ambao umepelekea kuumwa kwa kichwa.Ili kutibu na kufahamu ugonjwa husika ni lazima umuone daktari upate vipimo na ndipo upewe dawa kamili za kutibu ugonjwa husika.

2.Mtu anayetegemea njia za mkato mara nyingi huwa hakomai kitabia na namna ya kuendesha vitu vyake maishani mwake siku zote.Unapoiona tabia fulani ya mtu ndivyo alivyo mwenyewe.Tabia hujengeka kutoka na mfumo wa maisha wa mtu wa kila siku alio nao.Iwapo unafikiri kwamba wizi ndio njia sahihi ya kuishi basi siku zote hautajua kwamba kuna namna nyingine ya kuishi sababu ndivyo ulivyojijengea.Maisha huenda na kubadilika kila siku kuna siku utashindwa kuiba je utaishi kwa namna gani?Ukiona mtu anakuwa na hasira na maamuzi mabaya siku zote usikimbiliea kumlaumu fwatilia ni wapi ameanzi na amekulia katika mazingira gani maana hayo ndiyo yaliyojenga mfumo maisha yake.Mara zote nimesema hakuna mtu anayeweza kusihi nje ya information mtu ambazo anazo kichwani.Na information hupatika katika njia tofouti tofauti  
(I)Mazingira 
(II)Marafiki 
(III) Malezi 
(IV)Vitu mtu anavyosoma kila siku n.k.
Ukomavu wa tabia nzuri huja kutokana na mafundisho magumu ya kufwata kanuni mbali mbali na mfumo wa asili wa dunia ulivyoweka bila kukubali kufwata njia za mkato na urahisi.

3.Mafanikio ni Mchakato na sio Mkato.Mafanikio yanayodumu yamejengwa kwenye njia ngumu ambazo mara nyingi tumeambiwa lakini tumekuwa tukipuuzia.Mafanikio yanayodumu yamejengwa kwenye uvumilivu ambao umejengwa katika muda mrefu ambao ndani yake kunakuwa na mchakato mgumu wa mafundisho ya asili na ambayo muda mwingine sio rahisi kuyaelewa na usipokuwa makini utaishia kulalamika na kukata tamaa.Waswahili Wanasema Njia Nyembamba na isiliyosonga ndio Inayoelekea uzimani n lakini njia nene ndio inayoelekea upotevuni.Hakuna mkato kwenye mafanikio yanayodumu.

4.Njia ya Mkato haikujengei nidhamu ya kuheshimu na kuyatunza mafanikio ambayo umeyapata.Unapojifunza kujijenga kwa njia sahihi unajenga uwezo binafsi wa wewe kuheshimu na kuthamini mafanikio ambayo umeyapata kwa nguvu zako mwenye pia unasikia ufahari wa kujivunia kila ambacho umekipigani siku zote.Fikiria kama umetoa mtoto au mke wako sadaka kwa mizimu unafikiri wakati wa kujivuni mafanikio yako utajivunia Damu uliyoimwaga ya wapendwa wako au utakuwa mnafiki wa kujifanya unafurahi wakati ki ukweli moyoni unajua sivyo ilivyo?Mafanikio yaliyopatikana kwa juhudi binafsi hukujengea uwezo binafsi wa hata kuheshimu na kuthamnini wengine bila kuwadharau.

Kumalizia safari hii ya Urahisi wa Njia Sio Uhakika wa Safari jifunze kujenga mafanikio yako kwenye msingi utakaodumu vizazi na vizazi na hata ambapo hautakuwepo lakini mafanikio yako yatakuwepo na kuelezea sifa zako nzuri  kwa jamii nzima ya wanadamu.Fikiria umekufa halafu Kizazi ulichokiacha kinatukanwa na mafaniko ya wizi iwapo utakuwa na bahati ya kuona huko ulipo utajisikiaje.

Tukatane tena Week Ijayo Kwenye Punch Of The Week