Kwa muda mrefu kidogo nchi ya Tanzania ambayo imekuwa ikiitwa Kisiwa Cha Amani ili hali si ukweli ila imekuwa Kisiwa Cha Utulivu na Uoga miongoni mwa wananchi wa Tanzania.Kwa Muda wa Miaka ya Karibuni kumekuwa na kujitokeza kwa aina mbali mbali za vurugu haswa zinazojihusisha na Muonekano wa Kidini lakini Pia na Katika Muonekano wa Kimaslahi kati ya Viongozi wa Serikali na Wananchi wa Nchi yenye Utulivu.Nimekuwa nikijiuliza mengi kila kukicha fujo zinatokea na hakuna ambaye anasimama kuzikemea kwamba haipaswi kuwa namna hii ilivyo sasa.Lakini matokeo yake mambo yalivyo watu wamekuwa wakikaa kimiya na viongozi wamekuwa wakivunga.Je ni nani anayefaidika na Hizi Vurugu zinazoendelea?

1.Vurugu zenye Muonekano wa Kidini.
Vurugu hizi kila kukicha zimekuwa zikiongezeka bila sababu zinazoeleweka na zimekuwa zikifungiwa macho na viongozi wamekuwa wakiendelea kuvunga kanakwamba hakuna kinachotokea kwenye nchi yetu.Taasisi za Dini za Upande mmoja zinaposimama kusema ukweli juu ya Vurugu zinazoendela Utasikia Serikali inasemama na kuzikemea kwamba hazina haki ya Kuwa wasemaji ili hali waumini wa Taasisi wa Dini hizo wamekuwa Wahanga kila kukicha.Je Ni Serikali au Baadhi ya Watu wachache wanaofaidiaka na hizi Vurugu?
Siku za Karibuni kumekuwa na mvutano mkubwa kati ya Upande wa Dini ya Ki-Islamu na Wakristo na Upande mmoja umeonekana ukitetewa na kukaliwa kimiya kwa kila wanachofanya ili hali upande mwingine ukitishia kuchukua hatua huonekana na mbaya Je nani anayefaidika na Vurugu hizi?
Miaka yote tumekuwa tukiishi kwa utulivu huu pamoja na tofauti tuliozo nazo lakini hakuna mtu aliyethubutu kumshambulia mwenzake wala kumdharau Je kwanini wakati huu iwe hivyo?Basi kwa mtazamo wa haraka haraka kuna watu ambao watakuwa wanafaidika moja kwa moja au indirect kutokana na muendelezo wa Vurugu hizi.

2.Vurugu zenye Muonekano wa Kimaslahi(Kifedha na Kiuchumi)
Tumeshuhudia fujo kubwa kwa ndugu zetu wa kanda ya kusini juu ya sakata la gesi linaloendelea.Wananchi wenye mumkari wameshindwa kuvumilia juu ya maamuzi wanayofanyiwa wao bila ya wao kushirikishwa kwa muda mrefu nchi hii watu wachache wamekuwa wakiamua nini kifanyike na nani afanye na nani afaidike kwenye kila mradi unaohusisha fedha nyingi.

Wananchi wanapoamua kudai haki zao kwa kutetea kile wanachotaka wao na wanachoona ni sahihi hugeuka kuwa adui wa maslahi ya watu hao wachache..Miradi Mingi imekuwa ikiendeshwa bila uwepo majadiliano na maamuzi ya wananchi wenyewe kuamua kitu gani wanataka juu ya Rasilimali zao lakini watu wachache wakiamua basi ndio yanatendeka.Hakuna elimu ya kutosha juu ya miradi na faida ambazo wananchi watapata baada ya Serikali kuingia Ubia na Mashirika ya Kimataifa.

Miradi Mingi imekuwa ikiendesha kiholela holela na pindi wananchi wanapodai haki zao kwa njia ya amani hawasikilizwi na matokeo yake huundiwa zengwe na kuonekana ni wabaya.Na wanapoamua mutumia nguvu huonekana ni wakorofi na wavunjifu wa amani?Je ni heri fujo na uvunjifu wa amani utokee sababu ya watu wachache?Muda utafika watu hawatakuwa tayari kuendelea na ujinga huu watu watasimama na ndipo muda huu wa neema utakapokuwa umekwisha na hapo ndipo nchi itashindwa kutawalika sababu ya misingi mibovu inayojengwa leo.

Mwisho,Niwazacho Mimi Kuna mtu au  watu watakuwa wanafaidika na Vurugu na Uvunjifu wa Utulivu tulio nao la sivyo basi hatua za Makusudi zingekuwa zimechukuliwa na katika kutatua matatizo haya ambayo kila siku yamekuwa yakikua na kuongezeka bila sauti za viongozi.

Je ni nani anayefaidika na Vurugu zinazoendelea Tanzania?

MUNGU IBARIKI AFRIKA,MUNGU IBARIKI TANZANIA
|
0 Responses