Ukomavu kwenye matumizi ya mitandao ya jamii ni swala linalopaswa kwenye jamii ya Watanzania na matumizi ya vyombo mbali mbali vya habari.Je ivi unajisikiaje unavyoyasema mabaya ya mwenzio kwenye mkusanyiko mkubwa wa watu ili hali wewe una ya kwako?Matumizi ya mitandao ya kijamii na Media kwa ujumla inaonyesha namna gani mtu alivyokomaa kwenye uwezo wa kuchambua na kuendesha vitu kwenye maisha yake.Imani na jamii mbali mbali zina mifumo yake ya kutoa hukumu kwa wahusika wanapokosea na sio kuchafuana kwenye mitandao na kuwaacha wengine wakiwa mithiri hawajavaa nguo.Tafakari unasikikia siku Baba yako Mzazi naye amewekwa kwenye Media au kwenye mtandao wa Jamii na ameelezewa mabaya yake Je Utafurahia au utahuzunika?

1.Ki-Imani

Kila imani  ina mfumo wake wakutoa adhabu pale mtu anapokosea iwapo taaratibu za kushtaki kosa husika mahali husika.Inanishangaza sana kuona kosa la mtu mmoja wa Imani fulani linapochukuliwa na mtu wa Imani ile ile mwingine na kwenda kulishikilia bango na kulitangaza kwa watu wengine wasio wa Imani ile.Je unafikiri watu wa Imani nyingine wanawafukiriaje watu wa Imani ambayo mmoja wa waumini wake makosa yake yamewekwa hadharani.Je unajengaje nyumba yako mwenyewe  kwa kubomoa kila baaada ya kumaliza kozi moja ya ujenzi wa matofali?Ufalme ukishajifitini wenyewe hata siku moja hauwezi kuendelea Mbele.Kabla haujaamua kusema mabaya ya mwingine hadharani kwanza jiulize wewe hauna mabaya?Kumbuka kila mtu anachopanda ndicho utakachovuna.Ukimsema vibaya mwenzako wewe subiri tu kuna siku na wewe utasemwa vibaya zaidi na unapoelezea mazuri ya mwenzako tarajia kuna siku watu wataelezea uzuri wako.Baada ya Kufa ni hukumu kumbuka mahesabu yote tunayamaliza hapa hapa.

2.Ki-Jamii

 Kila kwenye jamii ya watu kuna taratibu na sheria husika za kudhibiti wahalifu wa makosa.Je unapomsema mtu hadharani bila kwenda kwenye mamlaka husika je unakuwa umsaidiaje muhusika na wanajamii wengine wasipatwe na tatizo ambalo lilishakukumba kwa kutendewa ubaya na mtu husika au jamii husika ya watu.Facebook na mitandao mingine ya kijamii ikiwa ni pamoja na media mbali mbali kazi yake sio kuelezea na kuonyesha ubaya wa wengine bali kuhakikisha jamii inapata habari kamili na mafunzo ambayo yana tija kwenye jamii.Iwapo unahisi kuna kosa na matatizo juu ya tuhuma kwa watu fulani fwata taratibu za kisheria na kijamii ili kuwasaidia wengine na sio kuishia kuchafuana.Kumbuka unapomchafua mtu akaamu kukufwatilia kisheria na kitaratibu unaweza kushtakiwa na kuadhibiwa kwa kuongea vitu ambavyo havina tija na uhakika kwenye jamii ya watu.

3.Uasili wa Dunia

Namna ulimwengu ulivyotengenezwa na ulivyoumbwa na Mungu ni namna ya ajabu sana.Kumbuka unapofanya kitu kizuri hata kama haukulipwa mazuri kwa muda huo kabla haujaondoka kwenye sayari hii ndivyo utakavyolipwa.Unapoendelea kuelezea makosa ya wengine na ipo siku kabla haujaondoka lazima na sisi tutasikia makosa yako na mabaya yako makubwa kuliko ulivyoelezea ya wengine.Epuka kuwa msemaji wa makosa ya wengine tumia muda wako kuendesha mambo mema na kuwasemea wengine maneno mazuri.Iwapo unaona hauwezi kuchukua hatua basi ni afadhali unyamaze kuliko kuelezea makosa ya wengine mahali pasipo sahihi.Hata siku moja usitegemee kupanda kokoto ukavune maharagwe.Kile unachopanda ndicho unachovuna.



Mwisho,Mitandao ya Kijamii sio sehemu ya kuhukumu dhambi za wengine.Iwapo unaona mtu wa imani yako au wa jamii yako amekosea tafuta msaada ya kisheria na kitaratibu kwenye mahala husika Facebook na kwenye media sio sehemu sahihi ya kuelezana mabaya bali ni sehemu ya kuisadia jamii kuapata maendeleo chanya na yenye tija kwa jamii yetu na taifa kwa ujumla .Safari ni ndefu kwa watanzania kwenye matumizi ya mitandao ya jamii na media kwa ujumla mpaka tukifikia ukomavu wa safari hii basi tumeshajeruhi na kuharibu maisha ya watu wengine wengi sana.


"Ukiona hauwezi kuficha Uchi wa Baba yako Basi Ipo Siku Utamcheka Mkweo kwa Utupu wake."
|
0 Responses