Kila kukicha ni ukurasa mpya wa maisha ya mwanadamu lililokuwepo jana silo litakalokuwepo leo,Hakuna mjuzi wa safari hii bali wote tu wanafunzi.Dunia ina kanuni na mfumo wake wa kujiendesha ingawa sisi si wakazi wa muda tu wa ulimwengu huu.Watu wapya huja na wengine huondoka kwa namna mfumo wa dunia ulivyo.Kila kukicha kila mtu anakuwa na mishughuliko ya namna yake.
Mara nyingi tumefikiri kwamba tunapopata ujuzi wa namna fulani kwenye maisha yetu ndio mwisho wa aina fulani ya changamoto lakini unakuja kukuta unapopata ujuzi huo tu unakuta changamoto kama hazikuoni na ujuzi uliokuwa nao na ambao umeupata katika taaluma husika.Ujuzi mpya uliopata hauwezi kuzuia changamoto nyingine zisije bali ndio mwanzo wa aina mpya ya changamoto.Mwamvuli unaweza kuzuia Usilowe lakini Hauwezi kuzuia Mvua isinyeshe.
Baada ya Kupata Ujuzi wa Aina fulani tunahisi ndipo mwanzo wa pumziko wa yale tuliokuwa tunayahitaji kwa muda mrefu.Kumbe tunasahau kwamba ujuzi tulio nao ni Zana ya kukusaidia na hauwezi kukusaidia bila kuwa mtendaji wa kazi katika taalamu na uhitaji ulio nao.Taaluma ulio nayo haifanyi matatizo/changamoto zikukimbie bali ndio mwanzo wa mapambano wa changamoto mpya.Ki-ukweli hakuna changamoto zinazobadilika bali sisi mitazamo yetu kuelekea changamoto hizo ndio hubadilika baada ya kupata aina fulani ya ujuzi.
Matatizo na Changamoto nyingi za misongo ya mawazo tilio nayo leo ni kwa sababu tulikuwa tunafikiri kwamba ukiwa na ujuzi wa aina fulani tatizo fulani latakuwa limefika mwisho.Wakati tukiwa wadogo tulikuwa tunaambiwa taaluma fulani ukisoma utakuwa na fedha nyingi sana lakini matokeo yake kuna watu hawakuwahi hata kufikia theluthi ya ujuzi tulio nao na wanafedha kuliko wenye hizi taaluma.Kutokujua uhalisia wa vitu kwenye maisha umetufanya tuwa na mitazamo ya picha tu isiyokuwa halisi kulingana na kanuni za utendaji wa sayari hii.
Misongo Mingi ya mawazo kwenye kizazi chetu inatokana na vitu mbali mbali haswaa kutokujua uhalisia wa vitu.Miaka ya Nyuma tulifikiria kwamba Ukiwa Daktari basi Ugonjwa kwako binafsi ni maarufuku lakini ki-ukweli hata madaktari wenyewe wanaumwa pia na wanatafuta wengine wawape tiba.Miaka ya Nyuma tuliambiwa Ukiwa Mwanasheria basi Utakuwa na Uwezo wa Kukonewa na Vyombo vya Dola.Matokeo yake kumbe Taaluma hizi ni Zana za Kazi kuelekea mapambano ya changamoto zilizopo Mbele yetu.Haijalishi una ujuzi wa namna gani na taaluma kubwa kiasi gani kila mtu anachangamoto zake.Hata kama Ungekuwa na Fedha Nyingi na Kila kitu unachofikiri changamoto hazikimbii bali ni mwanzo mpya wa changamoto fulani.
Mwamvuli unaweza kuzuia Usilowe lakini Hauwezi kuzui Mvua Isinyeshe.Kila Safari Moja huanzisha nyingine.Kila siku kuna changamoto mpya lakini hakuna kitu kipya kwenye sayari hii.Kila unachokiona leo kilashakuwepo zamani.Mara zote napendaga kusema hakuna dhambi Mpya zote za kale.Taaluma ulio nayo ni sehemu ya utatuzi wa Changamoto kuelekea mafanikio yako na sio suluhisho la kila kitu kwenye maisha.Hauwezi kuzia changamoto/matatizo yasije lakini unaweza kuzitatua kwa kutumia taaluma ulio nayo.Changamoto hazikimbiwi bali Hutatuliwa.
Wahenga Walisema "Unapofikiri Kuna Amani Tele Kumbe Ndio Mwanzo wa Vita"