Maisha ya mwanadamu yamejengwa katinga msingi wa uwajibikaji wa mtu binafsi kwenye maswala mbali mbali ambayo tunakutana nayo kila siku kwenye maisha yetu.Bila uwajibikaji a kuchukua hatua kwenye kila jambo na kuwa watendaji kwenye kile tunachokiamini ni sawa na kupigia mbuzi gitaa ukitegemea acheze,Wahenga walisema Kuwa Ukitwanga PiliPili kwenye Kinu Mshahara wake ni Kukohoa,Kwa Maana nyingine kile anachopanda mtu ndicho anachovuna mtu.Ukipanda maisha ya kulaumu kwa makosa na changamoto mbali mbali kwenye maisha unayokutana nayo hakukufikishi kokote,mwisho wa siku utaishia kuvuna lawama na malalamiko.
Maisha yetu ya jamii na utendaji wetu wa kila siku tumeyajenga kwenye kulaumu chanzo cha tatizo zaidi badala ya kutumia muda mrefu kujadili sulihisho la tatizo.Utamaduni wa kulaumu kwenye maisha ya mtanzania ni kama uji na mgonjwa.Mara zote tunashindwa kuweza kutafuta suluhisho wa tatizo na changamoto tunazokumbana nazo.
Siku za Karibuni tumepatwa na Kifo Cha Mwanamuzi wa Bongo Fleva Anyejulikana kwa Jina la Albert Magwair.Baada ya Kifo chake kutokea Watu wametumia Muda Mrefu kukilaumu kwamba Kituo Fulani cha Radio ndio Kimesababisha Kifo chake,Baada ya Kusoma Report ya Madaktari ambayo imekuwa ikisambazwa kwenye mitandao Mbali Mbali Imekujulikana Kwamba Ndugu yetu alikufa kutokana na Uchovu na Matumivi ya Vilevi na Dawa Za Kulevya Baada ya Mwili wake kufanyiwa Uchunguzi(Habari Zisizo Rasmi).Nikajiuliza Je Kituo hiki Ndio Kilimtuma atumie Vilevi na Madawa ya Kulevya.Je Kama Kituo Hiki kilimnyonya na Kusabishia Msongo Wa Mawazo Kwanini Yeye Binafsi asingetafuta njia Mbadala ya Kujinasua Kwenye Jambo hili la Kunyonywa?Kuna Mengi Sana.Lakini Baada ya tukio la Kifo kutokea Je hawa wengine waliobaki ambao wengine ni waathirika wa Matumizi ya Madawa ya Kulevya na Vilevi tunawasaidiaje?Malaumu hayasaidii.Tunapaswa kutafuta suluhisho la kudumu juu ya matatizo yetu Binafsi yanayotukabili badala ya Kutupia wengine lawama.
Mtu binafsi ndiye Suluhisho la Matatizo na Changamoto zake Binafsi,Hakuna mtu anayeweza kusimamia kukusaidia kuleta utatuzi wa changamoto zako binafsi.Unapolaumu wengine na wao wankulaumu pia kwa uzembe ulioufanya.
Wewe binafsi ndio unaweza kusimama na kuweza kutafuta suluhisho la kudumu kwenye kila kunachokukabili kwenye kila hali maishani mwako.Muda Mwingi wa lawama na malaumu hausaidii.Mara nyingi tumekutana na mfano wa Kesi za Mama wa Kambo na Watoto wa Kambo.Watoto hawa wa tumewajengea uwezo mkubwa wa kuwalaumu wamama ambao wanawalea na kuwafanya waonekane wabaya.Pamoja na Changamoto wanazokutana nazo tulipaswa kwajengea uwezo wa kupambana na changamoto wanazokutana nazo badala ya kuwajengea uwezo wa kulaumu.Kumbuka hata wakiwa watoto ipo siku Moja watakuwa watu wazima je hapo wataendelea kuwalaumu Mama zao wa Kambo .hapana.Hapa ndipo watapaswa kujisimamia wenyewe kwa majukumu yao ya kimaisha.Suluhisho la Mtu na Changamoto ni Mtu Mwenyewe na Sio Lawama.
Shangazi yangu siku Moja alinieleza kwamba mara nyingi watu ambao wengi ni wepesi wa kulaumu basi hata utendaji wao na maisha yao ni ya kubahatisha.Ni Rahisi kuilaumu Serikali Yetu haitupi fursa za maendeleo lakini cha kushangaza kuna watu wanaendelea je hawa wanaendeleaje?Je wao wana Mabawa au Wao ni Super Human?
Maisha ya Maendeleo ya Jamii Ni Watu wenyewe,Serikali yoyote duniani unayoiona ni Taswira ya Wananchi wake.Kuishutumu Serikali Kwenye Miasha yetu mabovu ya kila siku ni Kama kujaribu Kupigana na Kivuli Chako Mwenyewe.Unapoona Ubabaishaji kwenye Serikali,Tafuta Muda uangalie utendaji wa maisha ya Wananchi wake wa kila siku,ndipo utagundua serikali na wananchi wake hawatofautiani kwenye maswala mbali mbali.Kumbuka Serikali ni Watu na Iliwekwa na Watu.Kuendelea kulaumu hakusaidi.Dawa ni Kutafuta Suluhisho kile kinachotukabili kwenye maisha yetu ya kila Siku.Tutumie Muda mwingi kufikria kitu gani tunapaswa kuwa nacho maishani mwetu badala ya kulaumu kusiko na sababu za msingi.Sisi tuwajibike kwanza ndipo tutafute mengine.
Wakati unatumia muda mwingi kulaumu kwenye tatizo ulilo nalo Wengine wanatumia fursa za lawama zako kuendelea.
Wakati wewe unaona lawama ndio suluhisho la maisha yako ndipo wenye akili wanapokaa chini na kusaidia kutafuta sulusho ya lawama zako na mwisho wa siku suluhisho la mtu mwingine kwako huwa la Muda tu sababu hajui ni haswa unahitaji maishani mwako,Suluhisho la kudumu lipo Ndani yako,Na watu wanapoendelea kutafuta suluhisho zaidi juu ya tatizo lako kwenye maisha yako ya lawama siku zote utaendelea kuwa mtumwa kwao,maana utatumia nguvu nyingi na gharama kubwa kuweza kupata suluhisho la Muda la mtu mwingine kwenye maisha yako.Kuchukua kutumia suluhisho la Mtu Mwingine kwenye maisha yako ni kama kujaribu Kuiba Kivuli cha Jirani yako Kisha Ukitegemea kifwanane na wewe na kikutoshe.
Mwisho wa Siku wakati Lawama zako zinaendelea kwa watu wengine Maisha Bado yanaendelea kila siku na Watu wanafanikiwa kwenye ndoto zao kwa Kukufanya mtumwa wa kutumumikia ndoto zao.Kufa kwa Imamu Sio Mwisho wa Ibada,Maisha yanaendelea na kazi zinaedelea na Ujenzi wa Fikra Huru na za Haki Unaendelea.Unapoendelea kulaumu hata siku zako za kuishi zinakuwa chache maana utayatumikia matatizo badala ya kutumikia Kufurahia maisha ambayo wewe binafsi ndio jibu la Maisha yako.