Mtandao wa Amazon ni miongoni mwa mitandao michache Ulimwenguni inayofamika kwa kufanya mauzo ya vitu mbali mbali kupitia njia ya Mtandao.Mtandao huu unauza Muziki na vitu kadha wa kadha kupitia njia ya Online lakini siku ya Leo Tumeamua Kuangalia Muziki wa Injili na Wanamuziki wake wanaofanya vizuri kwenye Mauzo kwa Muda mrefu zaidi kulingana na Mtandao huo.
5.Grace & Mercy
1.Mountain High... Valley Low
Mountain High... Valley
Low ni Albamu ya Muziki wa Injili iliyoachiliwa mwaka 1999 na Mwanamuziki
Maarufu wa Injili nchini Marekani Yolanda Adams chini ya Lebo yake ya Elektra
Records.Albamu hii mpaka sasa imeshachukua
tuzo mbali mbali kama Grammy Award pia kwa Mujibu wa Mitandao mingine ya
Mauzo kwa ujumla mpaka sasa Yolanda Adams na Albamu Hii ameshafanya mauzo ya
Nakala milioni 2,374,000.Albamu hii ina nyimbo takribani 11 na zote zimefanywa
kwenye Studio ya Elektra Records.Hii ndio Albamu inayoshikilia namba moja
kulingana na mtandao wa Amazon.
2.Tri-City4.Com
Mwaka 2001 Kundi la TRI-CITY SINGERS lilifanikiwa kupewa tuzo ya Grammy baada ya albamu yao ya TRI-CITY4.COM kufanya
vizuri mwaka 2000.Albamu hii iliachili rasmi mwaka 200,februari 29.Albamu hii
ina nyimbo takribani 16 zilizotengenezwa chini ya Lebo ya EMI Gospel.Kundi
hili lilianza kufanya vizuri baada ya mwanamuziki Donald Lawrence kushika
hatamu baada ya Director aliyekuwepo kung’atuka kwenye nafasi aliyokuwa
anaishikili.Hili ni Kundi la Nchini Marekani ambalo lilichukulia kama kwaya
bora kuwahi kufanya mauzo zidi kwenye Mtandao wa Amazon.Hiii ni Albamu namba
Mbili kwa Mauzo kulingana na Mtandao wa Amazon.
3.2nd Chance
Siku ya July 30,2002 ndipo
Albamu ya Pili Ya Mwanamuziki Karen
Clack Sheard ndipo ilipoingia Sokoni rasmi ikiwa na Jina la 2nd
Chance.Kabla ya Kuachilia Albamu hii Mwanamuziki Karen Clack Sheard
alisumbuliwa na Tatizo la Mishipa ya Damu ya kwenye paji la Uso
Kupasuka.Madaktari walisema Uwekano wa kupona Ugonjwa huo ni Asilimi 2% na
asilimia iliyobaki ilikuwa ni Kifo tu haya yote yalitokea mwaka 2001.Baada ya
Kuanza kuachia Mauzo ya Albamu hii mwaka 2003 kupitia wimbo wa The Heavens Are
Telling ndipo alipoweza kuchaguliwa kuingia kweny Kinyang’anyiro cha Tuzo za
Grammy nchini Marekani.Mpaka sasa Albamu hii yenye nyimbo 13,Inaendelea
kushikilia nafasi ya tatu kwa kufanya
mauzo makubwa ambayo hayajawahi kufikiwa mpaka sasa kwenye mtandao wa Amazon.
4.I Believe
Mwaka 1996 mwezi Machi
tarehe 12 Mwanamuziki Marvin Sapp ndipo alipoingia rasmi kwenye game za
Muziki wa Injili nchini Marekani.Mpaka Sasa Marvin Sapp ameshaachilia albamu 9
za Muziki wa Injili.Kwa Mujibu wa Mtandao wa Amazon Albamu ya I Believe
iliyoachiliwa June 11, 2002 ndio inayoshikilia
nafasi ya Nne kwenye Mtandao huo kwa Mauzo makubwa kuwahi kutokea.Albamu hii
ina jumla ya nyimbo takribani 13.Albamu hii ilitolewa chini ya Lebo ya Verity nchini Marekani.Hii ndio albamu ambayo rekodi yake pia ya mauzo haijawahi kuvunjwa na Inaendeelea kushikilia namba nne kwenye mtandao wa Amazon.
5.Grace & Mercy
Mwaka 1967 Mwanamuziki Marvin Sapp ndipo alipozaliwa kwenye mji Grand Rapids, Michigan nchini Marekani.Baada ya Mwaka 1996 kuamua kuimba Kama mwimbaji Binafsi mwaka Desemba 16,1997 ndipo alipoachilia albamu ya Grace & Mercy.Mwaka 1998 albamu hii ichaguliwa kuingia kwenye Kinyang’anyiro cha Tuzo za Grammy.Albamu hii ina takribani Nyimbo 10 pekee yake.Huu ndie mwanamuziki pekee aliyefanikiwa sasa kuingiza Albamu 2 kwenye Tano bora kwa Mauzo ya Muda mrefu na yanayoshikilia Rekodi ambayo mpaka sasa haijavunjwa wala kuondolewa katika nafasi ya nne na ya tano kulingana na mtando huo wa Amazon.