Kwa Mara Nyingine Napenda kuchukua nafasi hii kuwaasalimu wadau wote wa blogu katika mwaka 2013,Maana kwa Mara nyingine leo Ndipo tunakuta kwenye Programu yetu ya Kila Ijumaa iitwayo Punch of The Week.Leo katika Punch of The Week tumeamua kuangalia vitu kwa jicho la Pembeni kidogo lisemalo Urahisi wa Njia sio Uhakika wa Safari.
Maisha yetu ya kila siku muda mwingine yamekuwa hayana dira sababu ya kukosa mwelekeo sahihi wa kufanya vitu na kuviendeleza huku tukidhani kwamba hii ndio njia sahihi na huo ndio umekuwa mfumo ambao tumekuwa nao katika kila nyanja.Vitu vingi tumekuwa tikivifanya kwa zima moto huku tukidhani kwamba tunaweza kufikia kilele cha mafanikio ambayo yanaweza kudumu daima.
Maisha yetu yamejengwa kwenye kupenda njia za makato kuliko kufwata kanuni ambazo zipo na ndizo za uhakika kwenye maisha yetu kama wanadamu.Hakuna mtu ambaye amejenga mafanikio ya kudumu kwa kutumia njia za mkato.Uasili wa Dunia jinsi ulivyo ni kwamba ukipata kitu kwa dhuluma kitaondoka kwa dhuluma iwe leo au kesho.Mara nyingi tumeshindwa kuangalia mbele tumeangalia matokeo makubwa ya sasa lakini tunasahau kwamba maisha yanaendelea.Wahenga walisema Ukiua kwa Upanga Basi na Wewe utauwawa kwa Upanga wakimaanisha namna kitu kinavyopatikana ndivyo kitakavyoondoka.
Mafanikio yanayodumu ni yale yanayojengwa kwa mfumo wa Haki na kujituma siku zote.Hakuna mazingaombwe kwenye mafanikio wala uchawi.Iwapo unategemea uchawi,wizi na dhuluma kupata maendeleo habari nilio nayo ni kwamba tunasubiri anguko lako siku yeyote kuanzia sasa hata kama leo unaonekana unakula bata na kufurahia lakini kanuni za asili za kuendesha dunia huwa hazibadiliki siku zote.
Kuna hasara njinyi sana kwenye kutegemea kupata vitu kwa njia ya mkato kuliko kufwata kanuni za msingi za kufanikiwa katika jambo lolote.Je wewe unafikiri ungekuwa umezaliwa siku ya kwanza then siku ya pili tunakuona unakimbia je unafikiri sisi tunaokuzunguka tungefikiria vipi?Au wewe mwenyewe ungewazaje?
1.Njia za Mkato mara zote hazitoi jibu la uhakika na linalodumu siku zote.Njia za mkato au zima moto husaidia kutatua tatizo kwa muda tu lakini mara nyingi hakuna uhakika wa kudumu wa suluhisho ambalo litadumu siku zote za maisha.Fikiria iwapo haujawahi kufanya biashara siku zote za maisha yako ghafla unakuwa na biashara kubwa kesho asubuhi unafikiri biashara hiyo itadumu?Jibu ni hapana sababu hauna mufundisho ya msingi juu ya uendeshaji wa biashara na namna ya kucheza na mzunguko wa fedha.Unapofwata hatua mbali mbali unajenda uwezo binafsi wa kujifunza na kuwa na uhakika wa kutokurudia makosa ambayo hautaweza kuyarudia tena.Kumbuka siku zote Vitu rahisi gharama yake ni kubwa zaidi.Mfano Mzuri ni pale ambapo tunapoumwa kichwa kwa ghafla huwa tunameza dawa za kutuliza maumivu tu lakini huwa bado hatujatatua ugonjwa wa msingi ambao umepelekea kuumwa kwa kichwa.Ili kutibu na kufahamu ugonjwa husika ni lazima umuone daktari upate vipimo na ndipo upewe dawa kamili za kutibu ugonjwa husika.
2.Mtu anayetegemea njia za mkato mara nyingi huwa hakomai kitabia na namna ya kuendesha vitu vyake maishani mwake siku zote.Unapoiona tabia fulani ya mtu ndivyo alivyo mwenyewe.Tabia hujengeka kutoka na mfumo wa maisha wa mtu wa kila siku alio nao.Iwapo unafikiri kwamba wizi ndio njia sahihi ya kuishi basi siku zote hautajua kwamba kuna namna nyingine ya kuishi sababu ndivyo ulivyojijengea.Maisha huenda na kubadilika kila siku kuna siku utashindwa kuiba je utaishi kwa namna gani?Ukiona mtu anakuwa na hasira na maamuzi mabaya siku zote usikimbiliea kumlaumu fwatilia ni wapi ameanzi na amekulia katika mazingira gani maana hayo ndiyo yaliyojenga mfumo maisha yake.Mara zote nimesema hakuna mtu anayeweza kusihi nje ya information mtu ambazo anazo kichwani.Na information hupatika katika njia tofouti tofauti
(I)Mazingira
(II)Marafiki
(III) Malezi
(IV)Vitu mtu anavyosoma kila siku n.k.
Ukomavu wa tabia nzuri huja kutokana na mafundisho magumu ya kufwata kanuni mbali mbali na mfumo wa asili wa dunia ulivyoweka bila kukubali kufwata njia za mkato na urahisi.
3.Mafanikio ni Mchakato na sio Mkato.Mafanikio yanayodumu yamejengwa kwenye njia ngumu ambazo mara nyingi tumeambiwa lakini tumekuwa tukipuuzia.Mafanikio yanayodumu yamejengwa kwenye uvumilivu ambao umejengwa katika muda mrefu ambao ndani yake kunakuwa na mchakato mgumu wa mafundisho ya asili na ambayo muda mwingine sio rahisi kuyaelewa na usipokuwa makini utaishia kulalamika na kukata tamaa.Waswahili Wanasema Njia Nyembamba na isiliyosonga ndio Inayoelekea uzimani n lakini njia nene ndio inayoelekea upotevuni.Hakuna mkato kwenye mafanikio yanayodumu.
4.Njia ya Mkato haikujengei nidhamu ya kuheshimu na kuyatunza mafanikio ambayo umeyapata.Unapojifunza kujijenga kwa njia sahihi unajenga uwezo binafsi wa wewe kuheshimu na kuthamini mafanikio ambayo umeyapata kwa nguvu zako mwenye pia unasikia ufahari wa kujivunia kila ambacho umekipigani siku zote.Fikiria kama umetoa mtoto au mke wako sadaka kwa mizimu unafikiri wakati wa kujivuni mafanikio yako utajivunia Damu uliyoimwaga ya wapendwa wako au utakuwa mnafiki wa kujifanya unafurahi wakati ki ukweli moyoni unajua sivyo ilivyo?Mafanikio yaliyopatikana kwa juhudi binafsi hukujengea uwezo binafsi wa hata kuheshimu na kuthamnini wengine bila kuwadharau.
Kumalizia safari hii ya Urahisi wa Njia Sio Uhakika wa Safari jifunze kujenga mafanikio yako kwenye msingi utakaodumu vizazi na vizazi na hata ambapo hautakuwepo lakini mafanikio yako yatakuwepo na kuelezea sifa zako nzuri kwa jamii nzima ya wanadamu.Fikiria umekufa halafu Kizazi ulichokiacha kinatukanwa na mafaniko ya wizi iwapo utakuwa na bahati ya kuona huko ulipo utajisikiaje.
Tukatane tena Week Ijayo Kwenye Punch Of The Week