PART III


Ikiwa tunamalizia sehemu ya mwisho ya nini cha kufanya baada ya kuongelea SIFA ZA MTU MWENYE MAJERAHA AU UCHUNGU NDANI YA MOYO
Tambua uchungu/majeraha ya ndani mwasisi wake ni shetani kwa maana nyingine ni mbegu ya shetani kwenye maisha na jamii za watu. Ili uweze kupona majeraha ya ndani au uchungu ni muhimu kuzingatia yafwatayo.

1.Kubali kwanza umejeruhiwa na una uchungu moyoni.Unapokiri wewe mwenyewe kuwa una uchungu au majeraha ya ndani kwenye moyo ni mwanzo wa ukombozi wa maisha yako.Uchungu na majeraha ya ndani husababishwa na vitu mbali mbali kwenye maisha yako.Unapokiria kuwa una majeraha ya ndani ni dalili ya kuwa umeshatambua kosa lako wewe binafsi.Na ni mwanzo wa hatua mpya katika maisha yako binafsi

2.Jifunze kusamehe na kuachilia kabisa.Majeraha ya ndani na uchungu husababishwa  na vitu mbali mbali ikiwemo watu,vitu na hata wewe binafsi.Watu wengi wameshindwa kujisamehe kutokana na makosa waliofanyiwa au kujifanyia wao wenyewe kwenye maisha yao.Kuishi na majeraha ndani ya moy/uchungu hakusaidii kuponya moyo au kuleta amani ya kudumu bali huendelea kujenga chuki kwa muda mrefu ambapo hata kipindi utakapotaka kuchukua hatua ya kusamehe pia itakuchukua muda mrefu.

3.Chukua hatua mpya ya maisha yako.Usiendelee kukaa pale pale kwenye maisha ya uchungu na majeraha ya ndani.Amua kufanya kitu ambacho kitakuletea amani na furaha kwenye maisha yako.Amua kuongeza ujuzi mpya.Amani na Furaha ni kitu cha muhimu kuliko kitu chochote kwenye maisha ya mwanadamu.



"Linda Moyo wako kuliko vyote ulindavyo maana shina la uchungu lisije chipuka ndani yako."


...................................THE END............................................
| |