Miaka michache iliyopita nilikutana na msemo huu( "If you want to hide something from a Black Man Put it in a Book"). ambao ulinitia hasira kidogo na kunifanya nijiulize mara mbili mbili kwanini.Msemo huu miaka ya nyuma ulitumika nchi Marekani ambao ulikuwa una lengo la kuwabagua watu weusi kupata haki ya msingi ya kujifunza maana walikatazwa kusoma na kujifunza vitu kadha wa kadha.Lakini Baadaye baada ya kufwatilia kidogo nilikuja kugundua tatizo lilikuwa halipo kwa waliotunga aina hii ya taratibu bali lilikuwa kwa waliowekewa utaratibu huu.Watu weusi walikuwa ni watu wasiopenda kujifunza na kusoma baada yake waliamua kutumia muda mwingi kufanya vitu visivyo na tija kwa muda mrefu ambavyo vilitumia nguvu zaidi kuliko akili zaidi.

Mfano Michezo kama Basket na Rugby na michezo kadha wa kadha.Waafrika hawa walibuni michezo mingi kadha wakadha ili kujiletea burudani na maisha yao kuendelea lakini walishindwa kushika nyazifa muhimu na kupata maendeleo yaliyobora.Watu weusi wachache waliopata kupenda kusoma walipewa nafasi kubwa na hata uwezo wao wa kusoma na kuendesha vitu ulikuwa tofauti na wengine.

Tukirejea hapa Afrika kwetu na Haswa Nchi yetu ya Tanzania kwa miaka mingi Kutafuta maarifa na elimu ambayo yatakufanya uendelea kudumu zaidi kwenye changamoto za maisha imekuwa ngumu.Tumekuwa tukilalamika kuhusu swala la maendeleo lakini Upande wa pili je tuna uwezo wa ziada ambao unaweza kutufanya tuendelee kwa haraka.Baada ya kufwatilia kwa kiasi kikubwa nimekuja kugundua wasomaji wa vitu ni wachache na wafwatiliaji wa vitu niwachache.Ukitaka kujua uwezo wa mtu na anavyojua vitu angalia hata namna ambavyoa anaendesha maisha yake na anavyofikiria na kuchambua vitu.Katika pita pita zangu za kusoma vitu nilikuna na huu msemo usemaao.."
“Insanity is doing the same thing, over and over again, but expecting different results" by Albert Einstein.


1.Maarifa ni jambo linalodumu ndani ya Mtu Binafsi.

Unapoweza kujiongezea maarifa kwa kusoma na kujiendeleza katika aina tofauti tofauti ya ujuzi kichwani mwako wewe ndio utafaidika kwa sehemu kubwa kwa maisha yako daima.Mtu anaweza akakupokonya cheti au kikapotea lakini Maarifa ya mtu hayawezi kupokonywa wala kupotea maana ni jambo lililoko ndani ya mtu daima na swala ambalo linadumu mpaka siku za mwisho za uhai wake hapa ulimwenguni.Ubongo wa Binadamu ni mithili ya Viungo vingine tu vya mwili kadri vinavylozidi kutumimiwa ndivyo vinavyozidi kudumu daima na kuwa imara.Ubongo ni mfano wa Mguu wa Mcheza Mpira,Maana Mcheza Mpira asipofanya mazoezi kwa muda mrefu au kucheza uwanjani kipaji huanza kupotea taratibu na mwishowe hufa kadhalika ubongo wa mwanadamu ndivyo ulivyo unavyotumika zaidi ndivyo unavyofanya kazi katika hali ya ubora na utadumu kwa muda mrefu zaidi.

2.Kila maarifa yaliyopo kichwani yanathamani yake.

Kila siku tumekuwa tukienda kuomba kazi na kufanya usahili kwenye maofisi ya watu mbali mbali ili mradi tupate ajira.Unapokweenda kwenye usahili mara nyingi hauingi na hata karatasi lengo kubwa linakuwa ni kujua una uwezo na una maarifa kiasi gani kuhusu ulichokisoma na unaweza kuleta tija kwenye kampuni husika?Baada ya kufanya usahili wanaweza kukuajiri na kukupangia kiasi fulani cha malipo ambacho ndicho kinakuwa sawasawa na thamani ya Maarifa yako.Ndio maana kuna viwango vya Mishahara kazini.Ofisi Nyingi mtu anapoenda kusoma akirudi Mshahara huongezeka,Ni kwa sababu ameongez kiwango cha maarifa kichwani mwake.Unapongeza Maarifa mbali mbali kichwani mwako ne ya maisha ya kawaida ya watu wengine ndivyo Thamani yako Hupanda kwa maana nyingine...Mshahara unaolipwa na Maarifa yako vinatosha na vinaenda Kabisa.


3.Maarifa ni Jambo linalorithishwa kutoka kizazi hadi Kizazi kama ulivyo Ujinga.

Familia nyingi zilizo bora kwenye maisha yetu ya kila siku ni familia ambazo ziliwekeza kwenye maarifa siku za nyuma kwenye maisha yao ya kila siku.Mara nyingi tumepika kelele kuhusu swala ma maendeleo na vitu mbali mbali lakini tunashindwa kujiuliza je watu walitumia muda gani kuwekeza katika maarifa.Kun msemo wa wahenga wansema alivyo Baba na Mama ndivyo Watoto walivyo.Tumendelea kupiga kelele kwamba Tanzania kuna anguko la Elimu(Maarifa) maana yake tumejua kuna athari zake katika vizazi vijavyo.Unapokuwa na maarifa zaidi ni rahisi kuwasaidia hata watoto wako kwenye njia iliyobora.Usiwalaumu watoto wa kizazi hiki Bila kujua uwezo wa wazazi wao katika kuwekeza katika swala zima la maarifa.Je wanatumia muda gani na wanawekeza kiasi gani.Na rudi pale pale .Maarifa ni jambo la Urithi kwa Watoto kama ulivyo Ujinga.Kama hautaki watoto wako wawe wajinga siku zote wekeza kwenye maarifa nao watafaidi katika maisha yao yajayo hata usipokuwepo.



.....Maarifa Huuwisha Nafsi Daima Bali Ujinga Hushakaza Mwili......Unapokuwa na maarifa zaidi ndivyo unavyostawi zaidi kuanzia kwenye nafsi na daima lakini Unapokosa maarifa unakuwa Mtumwa wa wengine ambao wanakuwa na maarifa ziadi yako.