1.Bill Clinton and Hillary Clinton

Aliyekuwa Raisi wa Marekani Bill Clinton na Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje Bibi Hillary Clinton ndio Ndoa ambayo inashikilia namba moja kuwa Ndoa ambayo imewavutia watu wengi zaidi katika mwaka 2012 kwa mujibu wa mitandao mbali mbali.Ndoa hii ilifungwa mwaka  1975,Octoba 11.Kwa mara ya kwanza walikutana mwaka 1970.Pamoja na Ndoa hii kupita kwenye misuko suko mbali mbali lakini bado imeendelea kuwa Imara na Inaonekana kuwa ni ndoa yenye afya zaidi kuliko nyingine zaidi katika mwaka 2012.

2.Bill Gates and Melinda Gates 

Pamoja na Bill Gates kushikilia namba moja kwa utajiri lakini bado anaendelea kufanya vizuri kwenye ndoa yake yeye pamoja na mkewe Melinda.Ndoa ya Bill Gates na Melinda ndio inashikilia namba mbili kwa kupendwa na kuvutiwa zaidi na watu wengine duniani kulingana na mitandao mbali mbali kwa mwaka 2012.Ndoa hii ilifungwa mwaka 1994 January 1 kwenye visiwa vya Hawaii.BAdo ndoa hiii haijatetereka hata kidogo kwa muda mrefu wamekuwa wakifanya kazi pamoja ikiwa ni Pamoja na mfuko wao wa Misaada ulimwenguni kote wenye Jina la Bill and Melinda Gates Foundation.

3.Barack Obama and Michelle Obama

Raisi wa Marekani Barack Obama na Mkewe Michelle Obama ndio ndoa ambao inashikilia namba tatu ilionyesha kuwavutia watu zaidi katika mwaka 2012 kwa mujibu wa mitandao mbali mbali.Kwa mara ya kwanza wanandoa hawa walikutana mwaka 1989 lakini harusi Rasmi ilifungwa Octoba 3,1991.Huyu ndie Rais wa 44 wa Taifa lenye Nguvu zaidi na Ushawishi mkubwa zaidi Ulimwenguni kwa sasa.
Mwaka 2012 katika Uchaguzi wa Nchii Hiyo familia yake ndio inahesibika ilitoa mchango mkubwa kwenye ushindi wa kiti cha U-Raisi kwa mara nyingine baada kuonekana kwamba Baba wa Familia hiyo angelishindwa kwa mujibu wa kura za maoni na maneno ya mitandao mbali mbali.

4.Marissa Mayer na Zack Bogue.

Mwaka 2009 ndipo Marissa Mayer na Zack Bogue walipoamua kuoana na kuwa mke na mume.Ndoa hii ikiwa bado haina muda mrefu lakini imeingia kwenye rekodi katika mwaka 2012 kuonyesha ni moja ya ndoa ambazo zinawavutia watu wengi.Marrisa Mayer(Mwanamke) aliamua kuacha kazi kwenye Kampuni ya Google  kama msaidizi wa CEO na kuamua kujiunga na Kampuni Ya Yahoo na alifanikiwa kuwa CEO wa kampuni ambayo ilikuwa ikipoteza wateja kwa kasi na kupoteza umaarufu wake wa awali na kuifanya kupoteza mapato yake kwa kiasi kikubwa.Mdada huyo utajiri wake kwa mwaka unakadiriwa kufikia kiasi cha dola Milioni $ 300 kwa mwaka.
Pia ndoa hii inaingia kwenye Category ya  ndoa bora miuongoni mwa wanateknolojia(Information Technology Category) katika mwaka 2012.


5.Diane Sawyer and Mike Nichols

Mwaka 1998 ndipo watu hawa wawili walipoamua kufunga ndoa na kuishi pamoja kama mke na mume.Diane ni moja ya wanawake maarufu na watangazaji wa vipindi mbali mbali kwenye luninga kwa muda mrefu piaalifanikiwa kupata Tuzo kama Director Behind the Scene wa movie mbali mbali kwa kipindi cha nyuma.Ndoa hii inashika namba tano kuwa ni moja ya ndoa inayopendwa na kuvutia watu wengi zaidi kwa mwaka 2012 kupitia mitandao mbali mbali Ulimwenguni.Wote hawa wawili ni wafanyakazi wa vyombo vya habari kwa pamoja.
Hakuna mtu ambaye ameishi kwenye sayari hii katika siku zote za uhai wake bila kukosea kwenye jambo lolote.Mafanikio yote tunayoyaona leo yametokana na makosa mengi ambayo watu waliyafanya siku za nyuma.Yaani kwa maana nyingine hatuwezi kujua tumepatia juu ya jambo fulani bila kujua kutokupatia kuna sura gani.Ili shilingi ijulikane ni shilingi lazima iwe na pande mbili.Hakuna shilingi ambayo siku zote ina upande mmoja ndivyo pia maisha yalivyo.
Ukisoma Historia za watu mbali mbali maarufu na mashuhuri utakuja kukuta hapo mwanzo walikosea sana juu ya kile walichokuwa wanakifanya baada ya kugundua kwamba wamekosea ndipo hujaribu kufanya marekebisho kwanza kuleta muonekano bora juu ya jambo waliloliamini kuwa ni sahihi.


1.Makosa Uliyoyafanya Wewe Binafsi(You are Own Past Mistakes)

Kukosea ni sehemu ya maisha lakini sio maisha yote,Unapogundua umekosea unanyanyuka na kuendelea mbele.Makosa yako binafsi ni moja ya walimu wazuri waliokufandisha ndio maana leo upo hivyo ulivyo,Hauwezi kuishi zaidi ya makosa ambayo uliyoyaona kwako binafsi.
Kama uliwahi kufukuzwa kazi kwa sababu umekosea kufanya jambo fulani kwa uangalifu,Siku unapopata kazi mpya unajitahidi sana kile kilichokufukuzisha kazi  usikirudie tena.Iwapo Kuna wakati huwa tunatumiaga hela zote bila kujali siku unapopatwa na dharura inayohitaji fedha ya muhimu sana na wewe fedha zote ulitumia vibaya inakufundisha kwamba siku ukipata fedha nyingi lazima kuna kutunza kiasi fulani cha fedha hata iwapo dharura itatokea tena usiaibike.Usiogope kukosea maana makosa yako ya leo ndio yanakusaidia kutengeneza maisha yako ya kesho.
Iwapo tusingejua maisha ya dhambi yakoje  na matokeo yake hapa Ulimwenguni tusingejua hata Mungu anafwananaje kwenye maisha yetu ya kila siku.
Mwanzuoni mmoja aliibuka na kusema Kwamba kama Haukuwahi Kukosea juu jambo lolote basi tambua haukuwahi kujaribu kitu kipya kwenye maisha yako.



2.Makosa ya Watu Wengine(Others Mistakes).

Wahenga walisema ukiona mwenzio ananyolewa Nywele basi wewe wewe weka maji Kichwa.Unapofanikiwa kumuona Mtu anakata mti na panga butu alafu akashindwa kumaliza kazi kwa wakati basi wewe kesho ukitaka kukata mti utajifunza kulinoa panga hilo.Hakuna mtu ambaye ana uwezo wa kuishi na kufanya kila kitu na kujifunza kwa makosa ya kwake binafsi tunawahitaji wengine ili kuweza kujifunza.Makosa ya mtu mwingine leo ndio Mafanikio yako ya kesho.
Ukiona mtu amefilisika na matumizi mabaya yake ya fedha na kushindwa kuendesha miradi alioianzisha siku zote utatumia makosa ya mtu yale kama sehemu ya rejeo ili kutoweza kufanya makosa aliyoyafanya yakapelekea matokeo mabaya.Mara nyingi watu waliojifunza kusikiliza na kuangalia makosa ya wengine juu ya jambo fulani kwa umakini wamekuwa na mafanikio zaidi kwenye jambo husika kuliko hata yule ambaye mwenyewe ambaye amewahi kukosea.
Tunawahitaji wengine ili kuweza kuendelea mbele.



Mwisho wa Siku tunaendelea kusema Epuka kuishi kwenye makosa yaliyopita lakini yatumie makosa kama mwalimu wako,Yaliopita si ndwele lakini tugange yajayo.Usiogope kukosea jaribu kufanya vitu vipya kukosea ni sehemu ya maisha.Maisha ni safari ambayo haina mjuzi bali wote tuwanafunzi kwenye kila jambo.Ishi ndoto zako jaribu kutafuta fursa mpya za maisha na jaribu kuzitumia bila woga kwa sababu Makosa yako ya Jana ndio Mafanikio yako ya Kesho.