Maisha yetu ya kila siku ni mithili ya mapambano kuelekea jambo fulani kwenye kufikia hatma za maisha yetu.Kila siku tunafanya vitu mbali mbali kuweza kufikia hatma iliyo bora ya maisha yetu.Hakuna mtu anayependa kuwa na hatma mbaya kwenye maisha.Iwapo utafanikiwa hata kukaa na mlevi wa matapu tapu karibu akiwa amelewa chakari ukimuuuliza unataka kwenda jehanamu atakwambia hapana nataka kwenda mbinguni pamoja na ulevi alio nao.Wazuoni wachache siku za nyuma walisema Maisha ni Mapambano,Sehemu yeyote inayokuwa na mapambano maana yake ni vita baani ya pande mbili zinazotofautiana kimaslahi.Mmoja anaona anaonewa na mwingine anaona yuko sawa.

Ni hatari kuingia kwenye mapambano fulani bila kujua adui yako yukoje kwenye uwanja wa vita na pia ni hatari kutokulijua eneo la kupigani vita lakini pia silaha za kupigania vita na jeshi la aina gani linaweza kupigana vita.Unapokosa kujua vyote hivi ni rahisi kupoteza aina yeyote ya vita kwenye maisha yako.


Mara nyingi tumeingia kwenye mapambano bila kujua adui tunayepambana nao kwa wakati huo kwenye maisha yetu na kutupelekea sisi wenyewe kupapasa pasa kwenye kila jambo ambalo tunalifanya.Ni rahisi kwa mlokole kukemea pepo la umaskini na kuendelea kuomba bila kuchukua hatua fulani kwenye maisha.

Umaskini hautoki kwa maombi bali kwa kufanya kazi kwa bidii na bila kukataa tamaa na kufwata kanuni halali za kiutendaji.Ujinga ni tatizo kubwa kwenye jamii yetu juu ya adui ambaye tunafikiri tunapambana naye.Ni rahisi kupambana na CCM tukiwaona kama ni shida kumbe tatizo sio wao ni msingi mibovu ilojengwa tangu mwanzo wa uongozi na fikra zao.


Tunaweza kujua adui ambaye tunapambana naye kwenye maisha yetu ya kila siku ili kuweza kufikia hatma bora ya maisha ya kila siku lakini tatizo linakuja namna ya kujua eneo la mapambano,je ni jangwani au msituni au kwenye maji..??je kama ni jangwani je ramani ya jangwa hilo ikoje na kama ni msitu je msitu huo ukoje??

Ni muhimu kujua eneo ambalo utalitumia kama eneo la mapambano  ya vita vyako vya kila siku.Ni rahisi kwa mwanafunzi mpya wa chuo kujua course anayoifikiria kuisoma chuo lakini kipi ni chuo bora na chenye walimu bora juu ya course anayotaka kusoma.Unapokosa kujua battle ground yako ni bora usianzishe vita maana kuna uwezekano wa adui yako kukushinda maana eneo na uwanja wa vita ana ufahamu wa kutosha.


Silaha za kupia vita vyovyote inategemea na adui unayepigana naye na eneo ambalo mnalotumia kupigana vita.Ni ngumu kurusha makombora ya masafaa marefu zaidi ya kilomita 1500 kwa saa na huku ukiwa unapigana vita na Kisiwa cha Mafia.

Adui yako ndio anayekupa lead ya kwamba ni aina gani ya silaha utumie kupigana naye.Miaka ya mwanzo mwa 1990 tuliambiwa mtu akienda chuoni anapewa pesa lakini kutokana na wrong info basi tulijua mtu anapofika chuoni ni maisha ya burudani na raha lakini kumbe ni kinyume chale unapaswa kuweka jitihada zaidi.Kama ulikuwa ukikesha kusoma mara mbili kwa mwaka ulipokuwa Sekondari unapofika chuo kulala usiku wa manane ni jambo la kawaida tu lisilo na mjadala.Mara ya kwanza watu wengi hupata shida sababu hawakuelewa adai aliyeko mbele yao.


Kuna aina tofauti tofauti za department za jeshi linapofika swala la mapambano kwenye vita haiwezekani vita ikawa inapiganwa kwenye Eneo la Bahari wewe ukapeleka jeshi za miguu au vita ikapigana kwenye msitu wewe ukapelekea jeshi la maji.Kila sehemu inachagua aina gani ya jeshi unaloweza kulitumia kwenye mapambano ya vita vyako as long as umeshajua adui,eneo,silaha na pia unaweza kujua aina ya jeshi unaloweza kutumia kwenye uwanja wa mapambano.

Kwenye Jeshi kuna aina mbali mbali za wataalamu ni lazima ujue kama unaweza kutumia expert wachache tu na ukamaliza vita kwa upesi au unaweza ukatumia aina gani ya wataalamu kufikia hatma yako kwenye maisha.Maisha ni mapambano hakuna anayefikiri kushindwa lakini tangu mwanzo wa vita yeyote ni rahisi kujua yupi ni mshindi na yupi ni mshindwa.


.....Kupigana Vita usiyoijua nia Kucheza Kamali Karibu na Kituo cha Polisi.......