Kuishi kwingi ni Kuona Mengi.Mwanadamu ni munganiko wa vitu vingi sana ambavyo ukiviangalia juu juu unaweza usivielewe.Mkusanyiko wa mambo mengi unayoyaona leo ni mkusanyiko wa tabia nyingi zilizojengeka jana.Hakuna jambo ambalo linaibukaibuka kwa sababu limeibuka tu,kila jambo lina mwanzo wake ingawa inaweza kuwa ngumu kukubali au kulitafuta lilipoanzia.Ujenzi wa jamii bora yenye maendeleo ya kifikra na uhuru wa kuweza kutoa maoni na kusimama katika ukweli wa vitu kwenye Dunia ya tatu imekuwa ngumu kutokana na ujenzi wa jamii yetu tangu mwanzo tunapozaliwa.Unaweza kuona jamii ambao haipendi mabadiliko ukailaumu lakini kumbe ndivyo tangu mwanzo ilivyojengwa.Maisha yamewekwa kufurahiwa na sio kuhuzunika.

Unapomwona mtu leo alivyo na vitu vyake vingi anavyofanya ujue kuna maamuzi fulani aliyafanya jana inaweza isiwe moja kwa moja au inaweza kuwa moja kwa moja.Tabia fulani unayoiona mwa mtu ni matokeo ya kile ambacho mtu amekuwa nacho tangu mwanzo.Jaribu kuangalia jamii ambayo imejengwa kwenye uhuru wa kujielezea na kuthubutu utaona mtoto na Baba wanaweza kuwa marafiki na wakacheka na wakaambiana vitu mbali mbali.Lakini huku kwetu Afrika Baba akiingia Ndani ya Nyumba unaweza fikiri ni Jenerali ameingia nyumbani,Pia Mama akiingia nyumbani unaweza kufikiri ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwakaleli Mbeya.Je unafikiri mtoto anayelelewa kwenye mazingira haya siku akikua akawa na familia unafikiri Yeye naye atakuwaje?
Msingi wa kila jambo kwenye maisha ni kitu Muhimu.Iwapo unafwatilia vitu utakuja kugundua watu wengi ambao ni watu wazima leo wanapenda kusoma vitabu mbal mbali vya kujieleimisha utagundua walivyokuwa watoto walipenda sana kusoma vitabu vidogo vidogo vya Hadithi Mfano Manenge na Mandawa,Juma na Rosa n.k Usomaji wa Hadithi hizo kipindi hicho ndio ulijenga msingi mpaka leo watu hawa wwamekuwa watu wazima kupenda kusoma.Ni ngumu kuanza kitu ukubwani na ukakiendeleza Maana hautaweza kufikia ukamilifu wake na unaweza kukumbwa na vikwazo Mbali Mbali.

Siku za Karibuni tumekuwa na ujio wa Raisi Barack Obama Kutoka Marekani Hapa Nchini Mwetu Tanzania.Ukifwatilia kiumakini mji wa Dar es Salaam umekuwa msafi na wa kupendeza kwa namna ambayo haijawhi kutoke tangu naingi Dar es Salaa Takribani Miaka 23 Iliyopita.
Baada ya Raisi huyu Kumaliza Ziara yake Tumeanza kushuhidia uchafu umeanza kurudi na vurugu za foleni zilizokuwepo Barabarani zimeanza tena,ingawa kwa muda takribani siku mbili Mji ulikuwa tulivu.Je Unafikiri hii ni tabia ya kawaida?Tangu Siku za awali hatujajengewa mfumo wa kuwa wasafi kwenye maeneo yetu na mazingira ya mji je unafikiri hiki ni kitu ambacho kinaweza kuibuka tu?

Ukiona Mtu anaamua kufanya maamuzi magumu kwenye maisha yake ujue kuna mahali ametokea na amaechoshwa na jambo fulani.Ni ngumu kufanya maamuzi magumu kwenye maisha bila kujua umetokea wapi na kipi unachokihitaji maishani mwako.
Jamii yenye kudhubutu na Kuamua ni jamii ambayo tangu mwanzo kuna msingi uljengwa maisha mwako.Ni Raisi kwenda kwenye ATM machine na Unakuta Mlinzi kawekwa na Huku Kwenye Eneo hilo Kuna Kamera za Ulinzi ndani ..Cha kujiuliza Je Teknolojia tunaitumiaje?Ni Raisi Kupanda Kwenye Dala Dala huku Konda anatukana na Nauli Utampa tu..Pamoja na maneno Mabovu anayoongea..Je unafikiri ni sawa?Maamuzi unayoyaona leo ya mtu yameathiriwa na hali fulani ya jana kwenye maisha yake.

Mbwa akishizeeka sana Meno Hung'oka Usitarajie utampa mfupa mgumu atafune kwani kwake itakuwa mateso.Uzee Wa umri pia ni Uzee wa Tabia fulani kwenye maisha yako..Unafikiri Upomuona leo Jambazi alianza na Ujambazi?Hapa alianza kuwa kibaka...Na Tabia ikishajengeka kwenye maisha ya mwanadamu kuiondoa ni shughuli kubwa ni kama kujaribu kuondoa ngozi ya mwili.Inahitaji muda na uvumilivu... 
Ni vizuri Kujenga tabia njema ya ujenzi wa jamii huru kwenye kila jambo tangu mwanzo wa utoto wetu.
Leo Hii tunapata shida kupata Kikosi cha Timu ya Taifa sababu Wachezaji wengi ni Wazee na Wameshachoka.Unafikiri ni Ngumu kumchukua Mchezaji wa miaka 25 au 26 kufundisha namna mpya uchezaji maana tangu mwanzo ndivyo alivyolelewa......Ukiendelea kumlazimisha kwa hapa Tanzania kwetu utaambiwa mnoko na Unaweza kuambulia Matusi tu.

Mbwa Mzee Hafundishwi Mbinu Mpya,Ukimlazimisha Sana Atakung'ata.
|
0 Responses