Kumekuwa na Wimbi la Watu Maarafu kwenye Muziki,Watangazaji na Wanaharakati Mbali Mbali wenye Mitazamo tofauti wa Kuingia kwenye Harakati za Kisiasa na Kutangaza nia za Kugombea Nyazifa mbali mbali kwenye Taifa Hili la Tanzania.Kinachonishangaza ni kwamba watu hawa kabla hawatangaza nia za kuingia kwenye siasa na kushika nyazifa mbali mbali katika nchi hii,Huko walipokuwepo wamefanya nini kabla ya kuamua kuingia huku?Sisi Watanzania tunaweza kuwa sehemu ya majaribio kama kichwa cha mwendewazimu kwenye uongozi .Taifa lenye tija na nia ya maendeleo haliwezi kukurupuka kuwapa nyazifa muhimu watu ambao wamelala na kuamka asubuhi na kutamka nia yao ya Kigombea nyazifa Mbali Mbali Kwenye Taifa hili.

Hakuna Jambo Kubwa linaloanza na Ukubwa Wake,Kila jambo linaanza na udogo wake.Swali langu ni kwamba hawa ambao wanataka tuwape nyazifa za uongozi,je huko kwenye nyazifa ndogo ndogo wamefanya nini cha kukumbukwa?Je wameleta mapinduzi namna gani?Kila siku tunaweza kujikuta tunarudi pale pale kwa kuwapa watu uongozi ambao lengo lao ni kuanza kujifunza kwenye nyakati muhimu ambapo sisi tunahitaji kusonga mbele.Baada ya Miaka hamsini ya uhuru hatuhitaji kuwapa watu nyazifa za uongozi kwa nia ya kujifunza bali kwa nia ya kusonga mbele.Tuwapime kwanza si kwa wingi wa maneno ya vyombo vya habari bali kwa utendaji wao wa maisha yao ya kila na kwa kazi ndogo ndogo ambazo wanazo kwa sasa.Inakera na Inauma tunampa mtu uongozi ndio  kwanza yeye anaanza kujifunza kwenye migongo ya watanzania.Tusipoangalia ule msemo wa kichwa cha mwendewazimu hautakaa utoke ndani ya taifa hili la Tanzania.Tusikubali nchi yetu kuwa sehemu ya Mafunzo ya Uongozi.Tuchague watu wenye kujielewa na  kuweza kutufikisha mahali ambapo tunapataka kufika na sio ili mradi tumemaliza kuchagua kiongozi.Siku Moja Wajukuu Wetu watachapa Makaburi yetu Fimbo kwa Utoto ambao tumekuwa tukiufanya kwenye taifa letu kwa kushindwa kujisimamia.

Ni Ngumu sana kujua nia za hawa ambao wanaanza kutangaza nia za kutaka kugombea uongozi na nyazifa mbali mbali lakini kwanza tunaweza kupima nia zao kwenye maisha yao ya kila siku kabla hawajaanza nia ya kuamua kutangaza nia zao za kutaka uongozi.Je hapo Makazini walipo wamewatumikia vyema wafanyakazi wenzao?Je vyao walivyo navyo vimeleta tija kwa wafanyakazi wenzao au ndio Yale Yale ,Wanataka kujifunzia kwa Migongo yetu,Unafikiri kama mtu alikuwa mchoyo kwa Wafanyakazi wenzake unafikiri siku akipata cheo atakuwaje?Je unafikiri kama mtu alikuwa mbaguzi kwa wafanyakazi wenzake unafikiri siku aakipata cheo na nyazifa itakuwaje?Ukitaka kujua Nia ya Mtu na Miasha ya utendaji wake kwa Ujumla nagalia hata anavyoishi na Jirani zake pale mtaani,tutagundua mengi sana juu ya hawa wanaotaka kugombea uongozi na nyazifa mbali mbali.

Uongozi ni Tabia iliyojengeka Ndani kwa Muda Mrefu.Uongozi sio kitu ambacho kinazaliwa leo.Uongozi ni learning process.Iwapo mtu haukuwahi kuwa na tabia ya kujifunza tangu mwanzo wa maisha yake ya namna ya kuwa kiongozi ni ngumu kiongozi huyu kuweza kujifunza kuongoza watu kwa muda mchache.Kuongoza watu ni outcome na manifestation ya tabia fulani iliyojengeka ndani ya mtu kwa muda mrefu na sio kitu ambacho cha kukurupuka.Iwapo mtu anaweza kuuigiza kuwa kiongozi baada ya muda fulani tunaweza kuona uhalisia wake...Mfano Mtu anapotukana Bungeni sio kitu ambacho Kimetokea ghafla ni Kitu ambacho kimekuwepo ndani mtu muda mrefu anaweza asitamke mkiwa wote lakini akiwa pekee yake ndani mwake matusi ndio kitu kilichomo....Kitabu fulani cha Imani fulani Kinasema...Yaliomjaza mtu ndio Yanayomtoka.....Hauwei tukana then ukasema ni Bahati Mbaya,Hawezi Kuwa Mgomvi then Ukasema imetokeo tu. Uongozi ni Zaidi ya Chuki na Hasira za Mtu alizokuwa nazo Moyoni.Unaweza kumchukia mtu mmoja lakini kumbuka kuna wengine mamilioni wako nyuma yako,Wnasaikolojia fulani walisema unapokuwa na hasiri kichwani mwako Unakuwa kipofu kwenye maamuzi yako Mengi.Je Tunaendelea Kuongozwa na watu waliojaa hasira na viasai moyoni mwao?

Uongozi ni Uwakilishi wa Wananchi.Uongozi sio uwakilishi wa wewe na tumbo lako bali ni kujitoa kwa ajili ya wananchi.Iwapo mtu anapotaka kuwa kiongozi lazima ajue namna ya kuwasilisha hoja na matakwa ya wananchi anaowaongozo,Inanishangaza sana kuona inapokuwa kwenye vikao vya Bunge,Mbunge anakosoa bajeti na kueleza mambo kadha wakadha  ambayo mapungufu yake yanaonekana wazi kwenye bajeti mwisho wa siku utasikia Naunga Mkono Hoja,Je Unanga Mkono Makosa uliyo yasema au?Je wanauwezo wa kuishawishi serekali na wadau wake juu ya Maendeleo ya Taifa hili kwa Hoja zenye Mashiko na Msingi ambazo watazisimamia hata wakiwa wamelala kitandani mwao Usiku?

Taifa Letu sio Sehemu ya Mafunzo Ya Uongozi lazima Ifike sehemu tufanye maamuzi magumu kwa kuwakataa wale ambao wanaonekana hata kwenye nyazifa ndogo walizo nazo hawakonyesha mapnduzi ya kifikra wa ujenzi wa jamii huru katika maeneo yao ya kazi.Tusiwaamini Tuwapime kwa nyazifa zao za sasa badala ya Kutulisha maeneo matamu midhili ya Sukari Guru Mwisho wa Siku Watanzania ndio Tunahangaika na Kumbuka Mtu akishainga kwenye Mfumo wa Uongozi kulingana na Katiba yetu ni Ngumu Kumtoa ki-urahisi Labda Tusubiri Miaka Mitano na Muda Hautatungoja....

....Nazungumza Moyoni....Huko Walikotoka Wamefanya Nini....?
|
0 Responses