Maisha yetu ya kila siku ni mithili ya mapambano kuelekea jambo fulani kwenye kufikia hatma za maisha yetu.Kila siku tunafanya vitu mbali mbali kuweza kufikia hatma iliyo bora ya maisha yetu.Hakuna mtu anayependa kuwa na hatma mbaya kwenye maisha.Iwapo utafanikiwa hata kukaa na mlevi wa matapu tapu karibu akiwa amelewa chakari ukimuuuliza unataka kwenda jehanamu atakwambia hapana nataka kwenda mbinguni pamoja na ulevi alio nao.Wazuoni wachache siku za nyuma walisema Maisha ni Mapambano,Sehemu yeyote inayokuwa na mapambano maana yake ni vita baani ya pande mbili zinazotofautiana kimaslahi.Mmoja anaona anaonewa na mwingine anaona yuko sawa.

Ni hatari kuingia kwenye mapambano fulani bila kujua adui yako yukoje kwenye uwanja wa vita na pia ni hatari kutokulijua eneo la kupigani vita lakini pia silaha za kupigania vita na jeshi la aina gani linaweza kupigana vita.Unapokosa kujua vyote hivi ni rahisi kupoteza aina yeyote ya vita kwenye maisha yako.


Mara nyingi tumeingia kwenye mapambano bila kujua adui tunayepambana nao kwa wakati huo kwenye maisha yetu na kutupelekea sisi wenyewe kupapasa pasa kwenye kila jambo ambalo tunalifanya.Ni rahisi kwa mlokole kukemea pepo la umaskini na kuendelea kuomba bila kuchukua hatua fulani kwenye maisha.

Umaskini hautoki kwa maombi bali kwa kufanya kazi kwa bidii na bila kukataa tamaa na kufwata kanuni halali za kiutendaji.Ujinga ni tatizo kubwa kwenye jamii yetu juu ya adui ambaye tunafikiri tunapambana naye.Ni rahisi kupambana na CCM tukiwaona kama ni shida kumbe tatizo sio wao ni msingi mibovu ilojengwa tangu mwanzo wa uongozi na fikra zao.


Tunaweza kujua adui ambaye tunapambana naye kwenye maisha yetu ya kila siku ili kuweza kufikia hatma bora ya maisha ya kila siku lakini tatizo linakuja namna ya kujua eneo la mapambano,je ni jangwani au msituni au kwenye maji..??je kama ni jangwani je ramani ya jangwa hilo ikoje na kama ni msitu je msitu huo ukoje??

Ni muhimu kujua eneo ambalo utalitumia kama eneo la mapambano  ya vita vyako vya kila siku.Ni rahisi kwa mwanafunzi mpya wa chuo kujua course anayoifikiria kuisoma chuo lakini kipi ni chuo bora na chenye walimu bora juu ya course anayotaka kusoma.Unapokosa kujua battle ground yako ni bora usianzishe vita maana kuna uwezekano wa adui yako kukushinda maana eneo na uwanja wa vita ana ufahamu wa kutosha.


Silaha za kupia vita vyovyote inategemea na adui unayepigana naye na eneo ambalo mnalotumia kupigana vita.Ni ngumu kurusha makombora ya masafaa marefu zaidi ya kilomita 1500 kwa saa na huku ukiwa unapigana vita na Kisiwa cha Mafia.

Adui yako ndio anayekupa lead ya kwamba ni aina gani ya silaha utumie kupigana naye.Miaka ya mwanzo mwa 1990 tuliambiwa mtu akienda chuoni anapewa pesa lakini kutokana na wrong info basi tulijua mtu anapofika chuoni ni maisha ya burudani na raha lakini kumbe ni kinyume chale unapaswa kuweka jitihada zaidi.Kama ulikuwa ukikesha kusoma mara mbili kwa mwaka ulipokuwa Sekondari unapofika chuo kulala usiku wa manane ni jambo la kawaida tu lisilo na mjadala.Mara ya kwanza watu wengi hupata shida sababu hawakuelewa adai aliyeko mbele yao.


Kuna aina tofauti tofauti za department za jeshi linapofika swala la mapambano kwenye vita haiwezekani vita ikawa inapiganwa kwenye Eneo la Bahari wewe ukapeleka jeshi za miguu au vita ikapigana kwenye msitu wewe ukapelekea jeshi la maji.Kila sehemu inachagua aina gani ya jeshi unaloweza kulitumia kwenye mapambano ya vita vyako as long as umeshajua adui,eneo,silaha na pia unaweza kujua aina ya jeshi unaloweza kutumia kwenye uwanja wa mapambano.

Kwenye Jeshi kuna aina mbali mbali za wataalamu ni lazima ujue kama unaweza kutumia expert wachache tu na ukamaliza vita kwa upesi au unaweza ukatumia aina gani ya wataalamu kufikia hatma yako kwenye maisha.Maisha ni mapambano hakuna anayefikiri kushindwa lakini tangu mwanzo wa vita yeyote ni rahisi kujua yupi ni mshindi na yupi ni mshindwa.


.....Kupigana Vita usiyoijua nia Kucheza Kamali Karibu na Kituo cha Polisi.......
Hakuna kitu kilicho kirahisi kwenye maisha ya mwanadamu,Vyote vinahitaji nguvu ya ziada kuweza kufika malengo na kilele cha mafanikio binafsi.Unaweza kuona kitu kwa mtu kinaenda tu kwa njia nyepesi lakini hauwezi jua ameanzi wapi.Ukionacho leo ni Rahisi Kuna siku Kilishawahi kuwa Kigumu.

Kufikia malengo ya kimafanikio kwenye maisha kunahitaji nguvu,uwezo kujitoa na hata kuachana na vitu vingine ili kuweza kufikia maisha ya kimafanikio.
Wakati tunaanza darasa la Kwanza miaka ya nyuma tuliingia tukiwa hatujui kusoma wala kuandika kabisa lakini baada ya kujitoa na kufanya kwa bidii leo hii ukishika kitabu tuu unajua namna ya kusoma na kuandika.


1.Ni Rahisi Kuona Mafanikio Ya Mwingine na Ukayafurahia.

Hakuna jambo lilorahisi kufurahi kama kufurahia mafanikio ya mwingine bila kuja wapi alianzia na maamuzi gani alioyachukua.Sisi tunapoona matokeo ni rahisi kufurahia matokeo bila kutaka kujua mwanzo wa jambo ulikuwaje.
Miaka Michache iliyopita watu tulikuwa hatujui Precision Air lakini wanaojua historia ya Mzee Michael Shirima(Mwenyekiti wa Precision Air) wanaweza kuelewa nini Maana ya Kufilisika na Kurudi Kijijini na Kulima Kahawa na Ndipo Mtu anapata mwanga mpya wa kuanza kujaribu tena kuanza na wazo la kuwa mmiliki wa Kampuni ya Precision Air.
Leo hii sisi tunafurahia matokeo yake kwa kupanda ndege lakini kumbe kuna mtu alifilisika na akarudi kijijini na kuanza tena.Kufikia mafanikio inabidi uyashinde mazoea binafsi maishani mwako

2.Ni Rahisi Kukosoa Mafikio ya Mtu kuliko Kuanza ya Kwako.

Moja ya kipaji ambacho tunacho watu tulio wengi ni cha Kukosoa,Mtu anapoona mwenzake anapiga hatua baada ya kumsaidia kuboresha hatua zake kuweza kufikia mafanikio yake tunaanza kukisoa angefanya hiki au kile alafu unakaa pembeni ukisubiri aanguke uanze kusema nilitabiri mithili ya Nabii fulani.

Hakuna kitu kiachoaanza kikiwa chepesi.Kila ukionacho leo ni Rahisi  Kuna Siku Kilishawahi Kuwa Kigumu .
Hakuna urahisi kwenye jambo lolote wahenga walisema Siku zote Mwanzo ni Mgumu na Njia iendayo uzimani ni Nyembamba na Imesonga.
Ni rahisi sana kuanza kusema vibaya mafanikio ya mwingine kuliko kuweza kuanza ya kwako na ikafikia kipindi ukajivunia.
Mtu shujaa na mwenye mafanikio ya kweli ni yule anayechukua changamoto anazokutana nazo na kuweza kuzitumia kujijenga na kusonga mbele.Kama haukuwahi kukosea juu jambo lolote base tambua haukuwahi kujaribu kufanya kitu siku zote maishani mwako.

 Hakuna Mwanzo ulikokuwa rahisi kwenye kila jambo unapotaka kulianzisha ndio maana ukitaka kufikia mafaniko yako binafsi haupaswi kuishi na makosa ya jana leo na haupaswi kuishi na matarajio ya kesho leo bali unapaswa kuitumia vizuri kila dakika na sekunde unayoweza kuipata leo.
Kumbuka jana ni historia lakini Kesho ni Muujiza.Fanya jambo ambalo litakuwezasha kufikia malengo fulani ukitegemea urahisi wa jambo tambua upotevu uko karibu kuliko unavyodhani.
Laini Laini Maana yake si rahisi.Mwanzo ni Mgumu.Mwanzo wa Neno ni Mgumu kuliko Mwisho wake.

"Kila ukionacho leo ni Rahisi  Kuna Siku Kilishawahi Kuwa Kigumu"
Jengo la Ghorofa 15 katikati ya jiji la Dar es Salaam mtaa wa Indra Gadhi limeanguka leo asubuhi  pamoja na Watu wapatao 60 ndani yake mkiwemo watoto wa Madrassa katika jengo hilo. 
Mpaka sasa maiti zilizoopolewa ni 14 na majeruhi zaidi ya 30 wamekimbizwa hospitali.

Pata Habari kwa Picha

Wakati Jengo linaanguka

Muonekano wake Baada ya Jengo Kuanguka

Hili Ndilo Eneo la Tukio

Kazi Uokozi Ikieendelea kwenye Eneo la Tukio
Siku ya Tarehe 23/2/2013 kwenye Ukumbi wa Kanisa la Victory Christian Center Tabernacle (VCCT) kulikuwa na sherehe ya Huduma ya Soul Breakfast Kutimiza Miaka Miwili Tangu ilipoanzishwa Machi,2011.
Huduma Hii ni Maalumu kwa Wanafunzi wa Viwango tofauti tofauti vya Elimu Kuanzia Sekondari Mpaka Elimu za juu hapa nchini Kwetu Tanzania.
Huduma Hii ilianza na wanafunzi wachache sanaa mwaka 2011 lakini mpaka sasa kuna takribani wanafunzi 200 ambao wana hudhuria kwenye huduma hii.Lengo La Huduma Hii ni Kuwawezesha Wanafunzi kupata ujuzi wa kawaida wa maisha ya mtaani baada ya kutoka shule lakini pia na namna ya kutumia fursa zote zinazopatikana wakati wakiwa kwenye maeneo yao ya Elimu wanaposomea.


Ibada ya Sherehe ikianza

Inter -  Collage  Praise and Worship Team ikiwa Jukwaani

Soul Breakfast Team Maurice Okao(Mwenyekiti wa Soul Breakfast) na Director wa Campus Ministry  Samuel Sasali

Praise and Worship Team ikienda Sawa

Pastor Dr Huruma Nkone alikuwepo siku hiyo

Write The Word Coconut kwa Kutumia Mwili Wako

Director wa Campus Ministry Samuel Sasali Akielezea Maana ya Soul Breakfast  

Rivers of Joy International(Junior) Wakienda Sawa

Praise and Worship Imenoga

Cheza muziki wa Yesu

Twende Sawa

Wadau wakienda Sawa na Muziki wa Yesu
Prezzor Chavala akifanya Vitu vyake kwenye Jukwaa

Pastor Dr Huruma Nkone akinena na Watu waliofika Siku Hiyo

Paul Clement kutoka Glorious Team akifanya vitu vyake kwenye Jukwaa

Hawa ndio Presenters na Watu walifanya kazi na Soul Breakfast mwaka 2012-2013 wakiwa wameshika Vyeti Vyao baada ya Kutunukiwa kwa Utayari wao 
Soul BreakFast Committee  wakiwa na Presenter na Wadau Wengine wakipata pich a ya Pamoja na Pastor Dr Huruma Nkone

Maurice Okao Mwenyekiti wa Soul Breakfast Committee akieleza jambo

Mc wa Soul Breakfast Siku hiyo akienda Sawa

Wadau wakisikiliza jambo kwa Umakini Mkubwa Sana

Mwendo wa Celebration tu hapa

MC akienda Sawa

Vuvuzela Zilikuwa Sehemu ya Sherehe ya Soul Breakfast



Huyu ndie Mc Pilipili Mtoto wa Mama Roda

Kikazi Zaidi Mc Pilipili ya Shughuli


Mwendo wa Kazi tu Hapa

Enzi za Primary hizo 

Paul Clement pamoja na Team yake Wakimaliza Shughuli

Siku zote Rasilimali hazitoshi kwenye maisha lakini hatuachi kuzitumia kutokana na uchache wa rasilimali hizo.Kuweza kufikia kiwango cha juu cha mafanikio ni lazima utumie kwa uangalifu kiasi hiko kidogo cha rasilimali ambazo unazo kwa wakati huo.Hakuna mtu ambaye amefanikiwa kwenye jambo lolote alikuwa na Rasilimali zote  alizozihitaji.Anza Hapo Ulipo,Anza na Hicho ulicho nacho na Utaweza kufikia Kiwango cha juu cha Mafanikio kwenye maisha yako na Ndoto zako kutakuwa ni dhahiri.


Kila kukicha ni ukurasa mpya wa maisha ya mwanadamu lililokuwepo jana silo litakalokuwepo leo,Hakuna mjuzi wa safari hii bali wote tu wanafunzi.Dunia ina kanuni na mfumo wake wa kujiendesha ingawa sisi si wakazi wa muda tu wa ulimwengu huu.Watu wapya huja na wengine huondoka kwa namna mfumo wa dunia ulivyo.Kila kukicha kila mtu anakuwa na mishughuliko ya namna yake.

Mara nyingi tumefikiri kwamba tunapopata ujuzi wa namna fulani kwenye maisha yetu ndio mwisho wa aina fulani ya changamoto lakini unakuja kukuta unapopata ujuzi huo tu unakuta changamoto kama hazikuoni na ujuzi uliokuwa nao na ambao umeupata katika taaluma husika.Ujuzi mpya uliopata hauwezi kuzuia changamoto nyingine zisije bali ndio mwanzo wa aina mpya ya changamoto.Mwamvuli unaweza kuzuia Usilowe lakini Hauwezi kuzuia Mvua isinyeshe.

Baada ya Kupata Ujuzi wa Aina fulani tunahisi ndipo mwanzo wa pumziko wa yale tuliokuwa tunayahitaji kwa muda mrefu.Kumbe tunasahau kwamba ujuzi tulio nao ni  Zana ya  kukusaidia na hauwezi kukusaidia bila kuwa mtendaji wa kazi katika taalamu na uhitaji ulio nao.Taaluma ulio nayo haifanyi matatizo/changamoto zikukimbie bali ndio mwanzo wa mapambano wa changamoto mpya.Ki-ukweli hakuna changamoto zinazobadilika bali sisi mitazamo yetu kuelekea changamoto hizo ndio hubadilika baada ya kupata aina fulani ya ujuzi.

Matatizo na Changamoto nyingi za misongo ya mawazo tilio nayo leo ni kwa sababu tulikuwa tunafikiri kwamba ukiwa na ujuzi wa aina fulani tatizo fulani latakuwa limefika mwisho.Wakati tukiwa wadogo tulikuwa tunaambiwa taaluma fulani ukisoma utakuwa na fedha nyingi sana lakini matokeo yake kuna watu hawakuwahi hata kufikia theluthi ya ujuzi tulio nao na wanafedha kuliko wenye hizi taaluma.Kutokujua uhalisia wa vitu kwenye maisha umetufanya tuwa na mitazamo ya picha tu isiyokuwa halisi kulingana na kanuni za utendaji wa sayari hii.

Misongo Mingi ya mawazo kwenye kizazi chetu inatokana na vitu mbali mbali haswaa kutokujua uhalisia wa vitu.Miaka ya Nyuma tulifikiria kwamba Ukiwa Daktari basi Ugonjwa kwako binafsi ni maarufuku lakini ki-ukweli hata madaktari wenyewe wanaumwa pia na wanatafuta wengine wawape tiba.Miaka ya Nyuma tuliambiwa Ukiwa Mwanasheria basi Utakuwa na Uwezo wa Kukonewa na Vyombo vya Dola.Matokeo yake kumbe Taaluma hizi ni Zana za Kazi kuelekea mapambano ya changamoto zilizopo Mbele yetu.Haijalishi una ujuzi wa namna gani na taaluma kubwa kiasi gani kila mtu anachangamoto zake.Hata kama Ungekuwa na Fedha Nyingi na Kila kitu unachofikiri changamoto hazikimbii bali ni mwanzo mpya wa changamoto fulani.

Mwamvuli unaweza kuzuia Usilowe lakini Hauwezi kuzui Mvua Isinyeshe.Kila Safari Moja huanzisha nyingine.Kila siku kuna changamoto mpya lakini hakuna kitu kipya kwenye sayari hii.Kila unachokiona leo kilashakuwepo zamani.Mara zote napendaga kusema hakuna dhambi Mpya zote za kale.Taaluma ulio nayo ni sehemu ya utatuzi wa Changamoto kuelekea mafanikio yako na sio suluhisho la kila kitu kwenye maisha.Hauwezi kuzia changamoto/matatizo yasije lakini unaweza kuzitatua kwa kutumia taaluma ulio nayo.Changamoto hazikimbiwi bali Hutatuliwa.

Wahenga Walisema "Unapofikiri Kuna Amani Tele Kumbe Ndio Mwanzo wa Vita"

The Meaning of Marriage: Facing the Complexities of Commitment with the Wisdom of God.

Kitabu cha The Meaning of Marriage kimeandikwa na  Mchungaji Timothy J. Keller ambaye  alizaliwa mwaka 1950.
Timothy J.Keller ni Mchungaji wa Kanisa lijulikanalo  Redeemer Presbyterian Church kwenye Mji wa New York nchini Marekani.
Mwaka 1989 alipewa kanisa hili likiwa na Watu 50 tu lakini kwa Sasa lina washirika zaidi ya 5000 ambao wamejisalijili kwenye kanisa hilo la Mchungaji Timothy J.Keller.

Mchungaji Timothy J.Keller anaamini kwamba mafundisho mengi ya ndoa yanayofundishwa siku hizi yamepotosha maana halisi ya ndoa.
Mchungaji Timothy J.Keller ni mpinzani wa ndoa za jinsi moja pia ni mpinzani wa swala la kutoa mimba.Lakini anaamini Ndoa ni sehemu ya kumfanya mtu akue kiroho kufikia kiwango cha juu zaidi cha Maisha yake.

Mchungaji Timothy J.Keller anaamini Biblia ndio Muongozo sahihi kwenye swala linalohusu ndoa.

Kanisa la Mchungaji Timothy J.Keller linahesabika kuwa kanisa la 16 nchini Marekani lenye ushawishi mkubwa zaidi kwenye jamii.

Hiki ni Moja ya Kitabu cha Kikristo kilichofanya Vizuri kwenye gazeti Maarufu ya Nchini Marekani lijulikanalo Kama New York Times.
Mchungaji Tim J. Keller ameoa mke anaitwa Kathy na Sasa wana jumla ya Watoto watatu(David, Michael and Jonathan).

Kionjo Kutoka kwenye Kitabu hiki cha Mchungaji  Timothy J.Keller.

Marriage has the power to set the course of your life as a whole. If your marriage is strong, even if all the circumstances in your life around you are filled with trouble and weakness, it won't matter. You will be able to move out into the world in strength.”
Siku ya Jamamosi tarehe 23/03/2013,Huduma ya Soul Breakfast Chini ya kitengo cha Campus Ministry cha Kanisa la Victory Christian Center Tabernacle  a.k.a VCCT kutakuwa na sherehe ya Kutimiza miaka miwili toka huduma hii ya wanafunzi ianzishwe.Napenda kuchukua nafasi hii kama mmoja ya Wadau wa Huduma hii ya Wanafunzi kwenye mji wa Dar es Salaam kukukaribisha.
Inter-Collage Praise Worship Team ndio itaongoza Kusifu na Kuabudu.
Comedy itaongozwa na Mc Pilipili na King Chavala.
Msemaji Mkuu atakuwa Pastor Dr Huruma Nkone.
Vyeti Vitatolewa Siku Hiyo ...n.k

Usafiri wa Kwenda na Kurudi Utukuwepo bure kuanzia Saa Mbili na Nusu Asubuhi kwenye Kituo Cha Mwenge kama Uneelekea Maeneo ya Kiwanda Cha Coca Cola. 
Chai ya Nguvu itatolewa Bure.

Karibuni wote

Kirk Franklin

Kwa sasa unapoongelea mwanamuziki mwenye fedha za kutisha ulimwenguni kwenye Upande wa Muziki wa Injili huwezi kutaja jina Lingine zaidi ya Kirk Franklin.

Utajiri wa Kirk Franklin kwa sasa una thamani ya  Dola Milioni  $ 8.5.
Mwanamuziki huyu alizaliwa  Julai 26,1970 katika jimbo la Texas.


Baada ya Kuzaliwa Mama yake mzazi alimtelekeza na kulelewa na Shangazi yake aitwaye Gertrude .
Aliaanza kujifunza kupiga piano na miaka 4 na akiwa na Miaka 7 alianza kupata mkataba wake wa kwanza wa Kurekodi Albamu yake ya Kwanza Lakini Shangazi yake alikataa.


Mwaka 1996 ndipo alipomuaoa rafiki yake wa Karibu Tammy Collins.Wakati wanaoana watu hawa wawili kila mmoja alikuwa na mtoto mmoja mmoja kutoka kwenye mahusiano yake yaliyopita.Baada ya Kuoana Kirk Franklin pamoja na mkewe wamefanikiwa kupata  Watoto wa Wawili na  kwa jumla wana familia ya watoto wanne.


Wakati tukiwa tunafikiri maajabu yameisha kumbe ndio kwanza yaanaanza siku za karibuni Kitabu(Guinness World Records)  cha maajabu Duniani Kimefanikiwa Kuingiza katika Rekodi yake Balbu ambayo Haijawahi kuzima kwa muda mrefu wala Kuungua kwa takribani Zaidi ya Miaka 110 kwenye Kituo cha Zimamoto  namba 6 nchini Marekani katika Jimbo la California Eneo linaloitwa Livermore.

Balbu hii ambayo iliwekwa mwaka 1901 na kwanza kufanya rasmi kazi mwaka huo huo siku ya Tarehe 18 mwezi wa Saba.Balbu hiyo ambayo inafanya kazi Masaa 24 bila kuzimwa kwenye eneo la Injini.

Mwaka 1976 Balbu hiyo ilihamishwa kutoka kwenye eneo moja kwenda lingine huku kumbukumbu zake za uhamishwaji zikiwa zimetunzwa kwa ustadi mkubwa.Balbu hiyo ilipumzishwa kwa saa 22 tu mfululizo na ndipo ilowekwa tena na kuendelea kufanya kazi mpaka leo.


Adolphe A. Chaillet 
Mbunifu wa Balbu hiyo alijulikana kwa jina la Adolphe A. Chaillet na kisha kutengenezwa na kampuni ya Balbu ijulikanayo kwa jina la Shelby Electric Co. nchini Marekani.

Mpaka sasa wataalamu wengine wameshindwa kutoa sababu kwanini Balbu hiyo haijaungua kwa Muda mrefu lakini pia wameshindwa kutengeneza Balbu Nyingine kama hiyo ambayo yenyewe uwezo wa kuhimili muda mrefu bila Kuungua.

Kwa sasa Balbu hii imefungiwa Kamera Maalumu zakuipoza na Kuingalia muda wote kuendelea kupata kumbu kumbu na utendaji mzima wa Balbu hii yenye Maajabu ya aina yake.