Hakuna kitu kilicho kirahisi kwenye maisha ya mwanadamu,Vyote vinahitaji nguvu ya ziada kuweza kufika malengo na kilele cha mafanikio binafsi.Unaweza kuona kitu kwa mtu kinaenda tu kwa njia nyepesi lakini hauwezi jua ameanzi wapi.Ukionacho leo ni Rahisi Kuna siku Kilishawahi kuwa Kigumu.

Kufikia malengo ya kimafanikio kwenye maisha kunahitaji nguvu,uwezo kujitoa na hata kuachana na vitu vingine ili kuweza kufikia maisha ya kimafanikio.
Wakati tunaanza darasa la Kwanza miaka ya nyuma tuliingia tukiwa hatujui kusoma wala kuandika kabisa lakini baada ya kujitoa na kufanya kwa bidii leo hii ukishika kitabu tuu unajua namna ya kusoma na kuandika.


1.Ni Rahisi Kuona Mafanikio Ya Mwingine na Ukayafurahia.

Hakuna jambo lilorahisi kufurahi kama kufurahia mafanikio ya mwingine bila kuja wapi alianzia na maamuzi gani alioyachukua.Sisi tunapoona matokeo ni rahisi kufurahia matokeo bila kutaka kujua mwanzo wa jambo ulikuwaje.
Miaka Michache iliyopita watu tulikuwa hatujui Precision Air lakini wanaojua historia ya Mzee Michael Shirima(Mwenyekiti wa Precision Air) wanaweza kuelewa nini Maana ya Kufilisika na Kurudi Kijijini na Kulima Kahawa na Ndipo Mtu anapata mwanga mpya wa kuanza kujaribu tena kuanza na wazo la kuwa mmiliki wa Kampuni ya Precision Air.
Leo hii sisi tunafurahia matokeo yake kwa kupanda ndege lakini kumbe kuna mtu alifilisika na akarudi kijijini na kuanza tena.Kufikia mafanikio inabidi uyashinde mazoea binafsi maishani mwako

2.Ni Rahisi Kukosoa Mafikio ya Mtu kuliko Kuanza ya Kwako.

Moja ya kipaji ambacho tunacho watu tulio wengi ni cha Kukosoa,Mtu anapoona mwenzake anapiga hatua baada ya kumsaidia kuboresha hatua zake kuweza kufikia mafanikio yake tunaanza kukisoa angefanya hiki au kile alafu unakaa pembeni ukisubiri aanguke uanze kusema nilitabiri mithili ya Nabii fulani.

Hakuna kitu kiachoaanza kikiwa chepesi.Kila ukionacho leo ni Rahisi  Kuna Siku Kilishawahi Kuwa Kigumu .
Hakuna urahisi kwenye jambo lolote wahenga walisema Siku zote Mwanzo ni Mgumu na Njia iendayo uzimani ni Nyembamba na Imesonga.
Ni rahisi sana kuanza kusema vibaya mafanikio ya mwingine kuliko kuweza kuanza ya kwako na ikafikia kipindi ukajivunia.
Mtu shujaa na mwenye mafanikio ya kweli ni yule anayechukua changamoto anazokutana nazo na kuweza kuzitumia kujijenga na kusonga mbele.Kama haukuwahi kukosea juu jambo lolote base tambua haukuwahi kujaribu kufanya kitu siku zote maishani mwako.

 Hakuna Mwanzo ulikokuwa rahisi kwenye kila jambo unapotaka kulianzisha ndio maana ukitaka kufikia mafaniko yako binafsi haupaswi kuishi na makosa ya jana leo na haupaswi kuishi na matarajio ya kesho leo bali unapaswa kuitumia vizuri kila dakika na sekunde unayoweza kuipata leo.
Kumbuka jana ni historia lakini Kesho ni Muujiza.Fanya jambo ambalo litakuwezasha kufikia malengo fulani ukitegemea urahisi wa jambo tambua upotevu uko karibu kuliko unavyodhani.
Laini Laini Maana yake si rahisi.Mwanzo ni Mgumu.Mwanzo wa Neno ni Mgumu kuliko Mwisho wake.

"Kila ukionacho leo ni Rahisi  Kuna Siku Kilishawahi Kuwa Kigumu"
|
0 Responses