Wakati Nchi zetu za Ukanda wa Afrika Mashariki zikiwa na bado na maswali mengi juu ya viongozi wa Dini Wanawezaje kuwa Matajiri wa Kupindukia lakini Sivyo Ilivyo katika nchi za Afrika Magharibi haswaa nchini Nigeria.Siku Chache Zilizopita tumekuwa tukifwatilia mitandao mbali mbali ya chini Nigeria na tukakutana na hiki,Wachungaji wenye Asili Ya Nigeria na Wanaoishi Nigeria ambao ni matajiri zaidi kuliko wachungaji Wengine.
1.Bishop David Oyedepo
Huyu ndie mwanzilishi wa Kanisa na huduma ya Living Faith World Outreach Ministry, a.k.a Winners Chapel Ulimwenguni
mwote.Ndie Mchungaji na Askofu tajiri zaidi kuliko wote nchini Nigeria.Utajiri
wake unakadiriwa kuwa kiasi cha Dola Milioni $ 150.Takwimu hizi zilikusanywa
Mwaka 2011-2012.Huduma ya Living Faith World Outreach
Ministry, a.k.a Winners Chapel ilianzishwa mwaka 1981 pia ndio Kanisa kubwa
zaidi kuwahi kutokea katika bara la Afrika.Kanisa lake linachukua zaidi ya
Washirika 50,000 hawa wakiwa wamekaa kwenye viti bila bugudha yeyote.Mchungaji huyu
anamiliki ndege 4 zake binafsi.Ni Mmiliki wa Chuo Kikuu kiitwacho Covenant
University nchini Nigeria.Amefanikiwa kuwa na Kampuni Yake ya Uchapishaji
Iitwayo Dominion Publishing House.Zaidi ya hapo anamiliki Shule yake
Ya Sekondari Binafsi nchini humo ijulikanayo Kama Faith Academy.
2.Chris Oyakhilome
Huyu
ndiye mwanzilishi wa Kanisa na Huduma ya Believers’ Loveworld Ministries, a.k.a
Christ Embassy.Utajiri wake Unakadiriwa kufikia kati ya dola Milioni $ 35
- $ 50 kwa mwaka 2011-2012.Kanisa la Believers’
Loveworld Ministries, a.k.a Christ Embassy lina Zaidi ya washirika 40,000
duniani kote na wengi wao wakiwa Viongozi wa Serikali na Wamiliki wa Makampuni
Mbali mbali.Anamiliki Vitu mbali mbali ikiwepo Kituo cha Utangazaji cha
Televisheni Chenye jina la LoveWorld TV Network. Pia amefikiria
kuanza kuwekeza kwenye Hoteli na Nyumba za Upangaji sehemu Mbali mbali
Ulimwenguni.
3.TB Joshua
Huyu ndio mwanzilishi wa Kanisa na Huduma ya Synagogue
Church Of All Nations (SCOAN) nchini Nigeria.Utajiri wake unakadiriwa kufikia
kiasi cha Dola Milioni $ 10 - $ 15 .Anamiliki Jengo la Kanisa lenye uwezo wa
kuchukua Washirika 15000 wakiwa wamekaa bila Shika wa tatizo.Kanisa
la Synagogue Church Of All Nations (SCOAN) lilianzishwa Mwaka 1987.Kwa
sasa ana matawi katika nchi Mbali mbali nje na ndani ya Afrika.Miaka Minne
aliyopita alitoa msaada wa Fedha Wenye thamani ya Dola Milioni $ 20 kwa kituo
cha Matibabu cha Jeshi kilichokuwa kinaitwa Niger Delta Militants.Ni mmiliki wa
Kituo Cha Utangazaji cha Televisheni chenye Jina La Emmanuel Tv.
4.Pastor Matthew Ashimolowo
Huyu ndiye mwanzilishi wa Huduma na Kanisa lijulikanalo
kwa jina Kingsway International Christian Centre (KICC).Lenye Makazi yake
nchini Uingereza.Utajiri wake
Unakadiriwa kuwa Kiasi cha dola $6 – $10 .Mwaka 2009
Kanisa Kingsway International Christian Centre (KICC) lilitangazwa kwamba
ndilo Kanisa Kubwa Zaidi la Kipentekoste nchini Uingereza.Pastor Matthew
Ashimolowo ni mmiliki wa Baadhi ya Vituo vya Uandishi wa Vitabu ambavyo Huandika
Makala Mbali mbali za Vitabu pamoja na Utengenezaji wa Documentaries Mbali
mbali.
5.Pastor Chris Okotie
Huyu ndiye Mwanzilishi wa Kanisa la Household
of God Church nchini Nigeria.Utajiri wake unakadiriwa kufikia kiasi cha Dola
Milioni $3 -$10.Miaka Michache iliyopita ni mmoja wa wachungaji
waliojitokeza kugombea Uraisi wa Nchi ya Nigeria kwa vipindi vitatu tofauti na
huku akiwa kiongozi wa Chama Chake Binafsi cha Siasa.Kiasi kikubwa cha
Washirika wake ni Macelebrity wa Nigeria pamoja na watu wengine maarufu kwenye
kila eneo.Pia kwenye Miaka ya 1980's ndie Mwanamuziki Mzuri wa Pop kwa kipindi
hicho Nchini Nigeria.Anamiliki Vitu kadha wa Kadha ikiwemo magari yenye thamani kubwa zaidi Ulimwenguni kama Hummer na Porsche.
|
Wahenga walisema Tabia ya Mtu ni Mtu Mwenyewe.Hakuna mtu anayeweza kuishi nje ya tabia yake ambayo imo ndani mwake.Jinsi unavyomwona mtu mara zote na vitu anavyovifanya ndivyo alivyo.Tabia ya mtu ni udhihirisho wa vitu vingi sana vilivyo ndani mwake.Unapoona mtu anafanya kitu fulani si kitu ambacho kinaibuka mara moja na kutokeza tu bali ni hali ya ndani iliyojengwa muda mrefu kutokana na mambo kadha wa kadha anayokutana nayo kwenye maisha.
Mwanazuoni Mmoja alisema kwa asili Binadamu ni Wabaya lakini wanajaribu kujibadilisha kutoka kwenye ubaya kuelekea kwenye Uzuri wao.Akaendelea kusema kubadilisha tabia si kazi rahisi kama ilivyo kubadilisha nguo ya mwili.Inakuchukua muda mrefu na kufanya vitu mbali mbali kutoka kwenye ubaya wa tabia kwenda kwenye tabia nzuri.
Mwanazuoni mwingine aliibuka na kusema mtu hawezi kuishi nje ya tabia yake ya asili aliyoijenga maishani mwake na akaendelea kusema zaidi kwenye maisha ya binadamu hakuna siri.Tabia za mtu unazoziona kwenye maisha yake ni udhihirisho wa siri nyingi zilizo ndani mwake,Ingawa kwa sisi binadamu hatupendagi kufwatilia tabia ya mtu hatua moja kwenda nyingine.Lakini Unapofanikiwa kufwatilia tabia na namna wanavyoishi ndipo kuna uwezekano wa kugundu mambo kadha wa kadha ndani ya mtu huyo.
Kujenga tabia mpya na njema kwenye maisha ya mtu ni maamuzi na sio aina fulani ya nguvu ambayo inahitajika kutoka nje.Mungu alipomuumba mwanadamu alimuumba kwa ukamilifu wote ikiwa na uwezo wa kukibadilisha kila anachokutana nacho kwenye maisha.Mfano Dunia iliiumbwa katika Utupu bali kulikuwa na Malighafi tu ambazo zilikuwa hazitumiwa kwa namna yeyote.Baada ya Binadamu Kuumbwa ndipo mabadiliko yalipoanza kutokea kutokana na utumizi wa rasilimali hizo.Kila badiliko unalolitaka kwenye maisha yako lipo ndani yako.Hakuna mtu mzee zaidi ambaye ataamua kubadilisha tabia yake akashindwa.
Maisha ya Binadamu ni mfano wa Chupa ya Maji iliyojaa maji machafu Lakini Chupa hii inapokwenda kuikingwa maji kwenye Bomba la Maji ndipo Maji safi yapozidi kuingia na Maji machafu yanapozidi kutoka,Unapofanya kitu hiki kwa muda mrefu utakuja jua maji machafu yameshatoka na masafi ndiyo yaliobakia.Unapotaka kubadilisha tabia mbaya kwenda nje jaribu kutafuta tabia mpya nzuri ianze kuishi bila kuangalia tabia mbaya ulio nayo,Unapoendelea kuishi inafika siku unakuta una tabia mpya ambayo ni njema lakini mbaya imeshaondoka.
Information mbali mbali tunazoingiza kwenye maisha yetu kwa njia ya kusoma,mazingira,watu zinaathari kubwa kwenye maisha yetu na tabia kwa ujumla.Mfano mtu anapokuwa muagaliaji wa picha za Ngono kwenye Luninga,Je unafikiri anajenga tabia ya namna gani?Tabia haiingi mara moja tu kwenye maisha ya mtu bali ni mchakato wa muda mrefu ambao unajuisha mambo kadha wa kadha.Hakikisha inaformation unazoingiza kichwani mwako na maishani mwako moja kwa moja zina reflect kuelekea kwenye aina ya tabia ambayo unaipenda.No Body can Act against Information alizonazo kichwani iwe ni nzuri au mbaya.Hakikisha unafanya mabadiliko kuleta tabia mpya na njema kwenye maisha yako ya kila siku.Hakuna fisadi ambaye alianza kuwa fisadi bali alianza kidogo kidogo toka akiwa mtoto na alianza kwa udokozi wa vitu vidogo vidogo.
Mwisho wa Safari yetu siku ya leo kwenye Punch Of The Week Naendea kusema Impossible is The Word Found In Fools Dictionary. Anza hapo ulipo na kitu ulicho nacho kuelekea kwenye tabia njema.Wataalamu wanasema tabia njema si kwa ajili tu ya kukufanya kuishi kwenye jamii kwa amani na furaha bali tabia nje husaidia hata kujenga maisha yako ya kiafya na kiakili,Kuna uwezekano wa tabia zako mbaya zinapeleka kukuharibu kiakili na Kiafya pia.Hakuna mtu aliyezaliwa akiwa anajua kila kitu na kuwa na tabia njema katika kila Idara lakini wote tumezaliwa tukiwa na lengo la kujifunza.Tabia yako kwenye maisha ya kila Siku ni Zaidi ya Upepo wa Kisuli Suli ,Uangamivu wa Maisha yako Inategemea kiasi gani umejenga tabia mbaya.Na kufanikiwa zaidi kwenye maisha inategemea kiasi gani umejenga tabia njema
|
Kila asubuhi jamii kubwa ya wanadamu wanaamka na kwenda sehemu mbali mbali kwa ajili ya kwenda kujishughulisha ili kupata mahitaji muhimu ya kila siku kwenye maisha yao na jamii kwa ujumla.Tumekuwa tukizungukwa na changamoto mbali mbali kutokana na sababu mbali mbali lakini mwisho wa siku lazima lengo halisi litimie kufikia maswala muhimu ya kimaisha na kijamii.Maisha huchosha na hukatisha tamaa iwapo tunapoona njia ya kufikia yale tunayoyataka kuwa ngumu kupita kawaida lakini Unapofikiria Kuchoka Kabla ya Muda wa Kuchoka Haujafika unakuwa sawa sawa na mkulima anayepanda mbegu zake kwenye Jiwe akitegemea ziote.
1.Mazingira
Mazingira tunayoishi kila siku tangu tunaingia kwenye sayari hii itwayo Dunia yamekuwa na nguvu kubwa ya kututengeneza namna tunavyoweza kupambana na changamoto mbali mbali za kimaisha tunazokutana nazo,Ukitaka kufahamu ili kama ni ukweli au uongo mchukue Mang'ati aliyekaa porini tangu siku anazaliwa kisha baada ya miaka 20 mlete Mjini ndipo utaelewa nachosema.Ndio maana kuna mwingine Changamoto inapotokea hukimbilia kusema huu ndio mwisho wa maisha yangu lakini kwa mwingine husema huu ndio wakati muafaka wa kusonga mbele.Ukifwatilia kwa ukaribu kati ya hawa watu wawili Mazingira na vitu walivyokutana navyo vinawapa uwezo wa kujua iwapo wanaweza kuvuka juu ya changamoto fulani au hapana.
2.Watu
Kariba za watu wa aina mbali mbali tunaokutana nao zinauwezo mkubwa pia wa kutufanya tufikiri namna tunavyoweza kushinda vikwazo na taabu mbali mbali tunazokutana nazo kila siku.Wakati mtu mmoja akikutana na Pope Benedict XVI swali la kwanza watakalomuuliza ni kwanini Umejiuzulu kuwa Pope Mtu Mashuhuri zaidi Ulimwenguni?Lakini kuna watu wengine hawafikiria kumuuliza kwanini Amejiuzulu "Watamuuliza Je umefanikiwaje kufika kwenye Hiki cheo cha Kuwa Kiongozi wa Kanisa lenye wafuasi wengi zaidi Duniani?Ukifwatilia kuna mwingine amekutana na watu wenye mtazamo wa kimaskini lakini mwingine amekutana na watu wenye mtazamo wa kujua mbinu za kufikia mafanikio.Jiulize wewe je ukikutana na Mengi leo Utakimbilia Kumwomba Pesa au Utamwomba Ushauri ambao utakaokuzalishia Pesa zaidi ya alizokupa Siku hiyo?
3.Ufahamu
Mtu jasiri anayejua anapokwenda kufikiria kuchoka kabla ya Safari yake haijafika ni mwisho.Mtu mwenye kutafuata maarifa na ufahamu juu ya namna ya kuendesha na maisha na kushinda changamoto siku zote hawezi kuwa mkata tamaa.Unapofikiria Kuchoka Kabla ya Muda wa Kuchoka Haujafika ni sawa na kujaribu Kujaribu kuendesha gari lenye pancha ukitegemea litakufikisha Mbeya wakti ndio kwanza unatoka Sinza KIjiweni.Ufahamu hukupa mbinu mbadala za namna ya kutatua changamto husika bila ya kuweza kuishia njia.Tambua vita yeyote duniani unayoiona kwanza huanza kwenye Kichwa cha mtu.Hakuna vita inayoanza nje ya kichwa cha mtu.Jaribu kutafuta ufahamu kila siku.Safari bado ni ndefu usifikiri kuishia njiani wakati unaanza safari ulijua utafika.Jipe Moyo na Usonge Mbele VIkwazo na Changamoto ni sehemu ya maisha ndio maana viliwekwa kuonyesha namna ulivyo hodari na shujaa.

Hakuna Hodari wa Vita anayeweza kujisifia ni Mshindi wakati haukuwahi kupigana vita vya namna yeyote.Changamoto na vikwazo ni Sehemu ya Ushindi ndio maana vipo.Changamoto na vikwazo havikuwekwa kwa ajili ya wanyonge bali kwa ajili ya washindi.Changamoto na Vikwazo havikuwekwa kwajili ya Wanyama ,Viliwekwa kwa ajili ya Binadamu.Siku zote Mshindi hupata Ushindi kabla ya Kufika Eneo la Mapambano La Vita lakini Watu dhaifu hushindwa kabla hawajafika hata eneo la Mapambano.Acha Kufikiria kuchoka kabla y.a Muda wa Kuchoka Kufika.Changomoto na Vikwazo kwenye maisha nivifwananisha na Gereza ambalo hawakutengezewa Kuku bali Watu na ndivyo Changamoto zilivyo ni Kwa ajili ya Watu ambao wamejizatiti kufikia hatma yao ya Maisha na Sio Aina Nyingine ya Viumbe Visivyokuwa na Utashi.
|
Ukomavu kwenye matumizi ya mitandao ya jamii ni swala linalopaswa kwenye jamii ya Watanzania na matumizi ya vyombo mbali mbali vya habari.Je ivi unajisikiaje unavyoyasema mabaya ya mwenzio kwenye mkusanyiko mkubwa wa watu ili hali wewe una ya kwako?Matumizi ya mitandao ya kijamii na Media kwa ujumla inaonyesha namna gani mtu alivyokomaa kwenye uwezo wa kuchambua na kuendesha vitu kwenye maisha yake.Imani na jamii mbali mbali zina mifumo yake ya kutoa hukumu kwa wahusika wanapokosea na sio kuchafuana kwenye mitandao na kuwaacha wengine wakiwa mithiri hawajavaa nguo.Tafakari unasikikia siku Baba yako Mzazi naye amewekwa kwenye Media au kwenye mtandao wa Jamii na ameelezewa mabaya yake Je Utafurahia au utahuzunika?
1.Ki-Imani
Kila imani ina mfumo wake wakutoa adhabu pale mtu anapokosea iwapo taaratibu za kushtaki kosa husika mahali husika.Inanishangaza sana kuona kosa la mtu mmoja wa Imani fulani linapochukuliwa na mtu wa Imani ile ile mwingine na kwenda kulishikilia bango na kulitangaza kwa watu wengine wasio wa Imani ile.Je unafikiri watu wa Imani nyingine wanawafukiriaje watu wa Imani ambayo mmoja wa waumini wake makosa yake yamewekwa hadharani.Je unajengaje nyumba yako mwenyewe kwa kubomoa kila baaada ya kumaliza kozi moja ya ujenzi wa matofali?Ufalme ukishajifitini wenyewe hata siku moja hauwezi kuendelea Mbele.Kabla haujaamua kusema mabaya ya mwingine hadharani kwanza jiulize wewe hauna mabaya?Kumbuka kila mtu anachopanda ndicho utakachovuna.Ukimsema vibaya mwenzako wewe subiri tu kuna siku na wewe utasemwa vibaya zaidi na unapoelezea mazuri ya mwenzako tarajia kuna siku watu wataelezea uzuri wako.Baada ya Kufa ni hukumu kumbuka mahesabu yote tunayamaliza hapa hapa.
2.Ki-Jamii
Kila kwenye jamii ya watu kuna taratibu na sheria husika za kudhibiti wahalifu wa makosa.Je unapomsema mtu hadharani bila kwenda kwenye mamlaka husika je unakuwa umsaidiaje muhusika na wanajamii wengine wasipatwe na tatizo ambalo lilishakukumba kwa kutendewa ubaya na mtu husika au jamii husika ya watu.Facebook na mitandao mingine ya kijamii ikiwa ni pamoja na media mbali mbali kazi yake sio kuelezea na kuonyesha ubaya wa wengine bali kuhakikisha jamii inapata habari kamili na mafunzo ambayo yana tija kwenye jamii.Iwapo unahisi kuna kosa na matatizo juu ya tuhuma kwa watu fulani fwata taratibu za kisheria na kijamii ili kuwasaidia wengine na sio kuishia kuchafuana.Kumbuka unapomchafua mtu akaamu kukufwatilia kisheria na kitaratibu unaweza kushtakiwa na kuadhibiwa kwa kuongea vitu ambavyo havina tija na uhakika kwenye jamii ya watu.
3.Uasili wa Dunia
Namna ulimwengu ulivyotengenezwa na ulivyoumbwa na Mungu ni namna ya ajabu sana.Kumbuka unapofanya kitu kizuri hata kama haukulipwa mazuri kwa muda huo kabla haujaondoka kwenye sayari hii ndivyo utakavyolipwa.Unapoendelea kuelezea makosa ya wengine na ipo siku kabla haujaondoka lazima na sisi tutasikia makosa yako na mabaya yako makubwa kuliko ulivyoelezea ya wengine.Epuka kuwa msemaji wa makosa ya wengine tumia muda wako kuendesha mambo mema na kuwasemea wengine maneno mazuri.Iwapo unaona hauwezi kuchukua hatua basi ni afadhali unyamaze kuliko kuelezea makosa ya wengine mahali pasipo sahihi.Hata siku moja usitegemee kupanda kokoto ukavune maharagwe.Kile unachopanda ndicho unachovuna.

Mwisho,Mitandao ya Kijamii sio sehemu ya kuhukumu dhambi za wengine.Iwapo unaona mtu wa imani yako au wa jamii yako amekosea tafuta msaada ya kisheria na kitaratibu kwenye mahala husika Facebook na kwenye media sio sehemu sahihi ya kuelezana mabaya bali ni sehemu ya kuisadia jamii kuapata maendeleo chanya na yenye tija kwa jamii yetu na taifa kwa ujumla .Safari ni ndefu kwa watanzania kwenye matumizi ya mitandao ya jamii na media kwa ujumla mpaka tukifikia ukomavu wa safari hii basi tumeshajeruhi na kuharibu maisha ya watu wengine wengi sana.
"Ukiona hauwezi kuficha Uchi wa Baba yako Basi Ipo Siku Utamcheka Mkweo kwa Utupu wake."
|
Mwanamuziki
wa Injili anayeishi nchini Sweden Katika Mji wa Malmo anayejilikana Kwa Jina Rachel Sharp katika siku ya Jumamosi 26/1/2013 alizundua Albamu yake ya Pili hapa nchini
Tanzani ijulikanayo kwa jina "NI MUNGU WA AJABU" yenye jumla ya nyimbo 10
zilizo katika mfumo wa CD na nyimbo 8 zilizo katika DVD.
Rachel Sharp alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari katika Eneo ya Nyumba yake katika
Eneo La Tegeta Ambapo ndipo uzinduzi ulipofanyika alitoa Rai kwa Wanamuziki wa
Tanzania Kuendelea Kuenzi Muziki wetu wa Asili kama Ilivyo Mdumange na Mdundiko
pia aliongezea kwa kusema Lugha ya Kiswahili kwenye Muziki inalipa zaidi kuliko
ilivyo Lugha za Kigeni tunazojaribu kutumia.Akitoa mkazo zaidi aliendelea
kusema tuache kuiga miziki ya watu na sisi tukae chini tubuni aina yetu ya
muziki ambayo inaweza kutumika kama utambulisho wetu kwenye soko la kimataifa
la Muziki.
 |
Mc wa Event Ritha Chuwalo akimtambulisha Rachel Sharp |
 |
Rachel Sharp akiwatambulisha Wazazi wake Kwa Waandishi |
 |
Rachel Sharp Akitoa Wito kwa Waandishi kufikisha Ujumbe alioukusudia |
Mume wa Mtangazaji Maarufu Zawadi Machibya akiweka wakfu Albamu ya Rachel Sharp.
 |
Hadi Kieleweke.....Mwanamuzi wa Injili Rachel Sharp akiwa kwenye Stage |
 |
Mwanamuziki wa Injili Rachel Sharp akienda sawa kwenye |
 |
Nguli wa Muziki Nchini Tanzania Upendo Kilahiro akifanya kazi kwenye Stage |
 |
Rachel Sharp na Upendo Kilahiro wakiwa kwenye Jukwaa Moja |
Mwisho wa yote Rachel Sharp alisisitiza Kuwa Mafanikio Yetu hayaji kirahisi kwenye Kila Kitu imetupasa kujituma katika kila jambo bila kujali wengine wanatonaje,akimaliza alisema Upendo na Umoja Miongoni mwa wanamuziki wa Injili kukaa chini na kuja na ubunifu mpya kutawaongezea mafanikio katika tasnia ya Muziki wa Injili ndani na Nje ya Mipaka ya Tanzania.
|
Miaka Michache iliyopita Tanzania kulikuwa na Blogs Chache sana na tulikuwa tunajiuliza ivi mtu anawezaje kumiliki blog,Lakini baada ya muda fulani kupita watu wengi tulijifunza angalau namna ya kuanzisha na kuendesha blog.Miaka ya 2005 teknolojia ya blog Tanzania ilikuwa ngeni kidogo lakini nashukuru kwamba kadri siku zinavyozidi kwenda blogs zinaongezeka na zimekuwa nyingi zaidi lakini pamoja na haya yote kutokana na ukuaji wa teknolojia hii nchi yetu imekuwa taratibu sana kutunga sheria au kufanya mabadiliko ya sheria mbali mbali yatakayoendana na ukuaji wa teknoloji mbali mbali.Sina mengi ya kujadili kwa upande huo.
Baada ya kufanikiwa kupitia blogs nyingi hapa Tanzania hata mwanzo naanzisha blog hii nilijua copying and Paste ndio namna ya uendeshaji wa blog lakini baadae baada ya kufwatilia kiundani kidogo nikajiuliza je mtu alianzisha teknolojia ya blog alikuwa na maana hii ya copy and paste au kulikuwa na maana nyingine zaidi?
Blog sio copying and Paste blog ni sehemu ya kuonyesha kile ulichonacho kwenye ubongo wako,Baada ya kufwatilia sana nimekuja kugundua tasnia ya uandishi hapa Tanzania ina Critical Thinker wachache na hata waliopo hawaandiki maswala yanayohusu jamii na maisha yetu ya kila siku katika kuikwamua jamii yetu.
Blog sio sehemu ya matangazo baada ya kufwatilia tena nimekuja kugundua yaani sisi huwa vitu vingi tunafanya kinyume nyume yaana baada ya kwenda mbele sisi tunarudi nyuma.Yaani siku hiz utakuta blog ina matangazo mpaka unaboreka,hata hamu ya kuendelea kuangalia blog hauna hamu.Na tatizo kwa walio wengi sio vibaya kuwa na matangazo lakini sababu na maana ya msingi ya kuwepo blog isifutwe au kupotezwa kwa tamaa ya fedha.
Blog ni kama diary ambayo unaweka kumbukumbu zako muhimu za maisha ambazo zinaweza kuwasaidia wengine na kuweza kutoa majibu ya maswali amabayo wengine wanayo juu ya maisha na maswala mbali mbali ya kijamii katika kila nyanja yaani kiuchumi , kijamii na hata kisiasa ili kuweza kuleta hamasa kwenye jamii yetu katika maisha yetu ya kila siku.
Je Blogger ni Mwandishi wa Habari ?Kuna tofauti gani kati ya Blogger na Mwandishi wa Habari?
Mwisho jifikirie kuna tofauti gani kati ya website na blog...Na kama blog ni website ndogo kwani kuna website kubwa....Nini maana ya neno www.ww.com na nini maana ya www.fm.blogspot.com
Then come up with answers,tuifanye tasnia ya blog kuwa kivutio na sio kero kwa watu.Fikiria na ufanye mabadiliko.Hivi ndivyo Niwazavyo Mimi
Heri ya Mwaka Mpya kwa Bloggers Wote Wa Tanzania 2013
|