Huyu ndiye DNG

Baada ya Siku Chache zilizopita Kusadikika kwamba Mwanamuziki wa Secular Music Jaguar kutoka nchini Kenya ndiye aliyelipwa fedha nyingi zaidi na Kupitia chama Cha Mgombe U-Raisi Raila Odinga Katika Kipindi cha Kampeni lakini  Siku Ya Chache zilizopita Imekuja kugundulika kwamba Mwanamuziki wa Injili nchini Kenya DNG ndiye aliyelipwa fedha nyingi zaidi kwenye  Kipindi cha Kampeni na Mgombea wa kiti cha U-Raisi nchini Kenya Uhuru Kenyatta.
Inasadikika Mwanamuziki huyu amelipwa Mara 8 zaidi ya Mwanamuziki Jaguar kuendesha Burudani kwenye Kampeni Nchini Kenya kupitia Chama Cha Uhuru Kenyatta.
Wahenga walisema Tabia ya Mtu ni Mtu Mwenyewe.Hakuna mtu anayeweza kuishi nje ya tabia yake ambayo imo ndani mwake.Jinsi unavyomwona mtu mara zote na vitu anavyovifanya ndivyo alivyo.Tabia ya mtu ni udhihirisho wa vitu vingi sana vilivyo ndani mwake.Unapoona mtu anafanya kitu fulani si kitu ambacho kinaibuka mara moja na kutokeza tu bali ni hali ya ndani iliyojengwa muda mrefu kutokana na mambo kadha wa kadha anayokutana nayo kwenye maisha.

Mwanazuoni Mmoja alisema kwa asili Binadamu ni Wabaya lakini wanajaribu kujibadilisha kutoka kwenye ubaya kuelekea kwenye Uzuri wao.Akaendelea kusema kubadilisha tabia si kazi rahisi kama ilivyo kubadilisha nguo ya mwili.Inakuchukua muda mrefu na kufanya vitu mbali mbali kutoka kwenye ubaya wa tabia kwenda kwenye tabia nzuri.


Mwanazuoni mwingine aliibuka na kusema mtu hawezi kuishi nje ya tabia yake ya asili aliyoijenga maishani mwake na akaendelea kusema zaidi kwenye maisha ya binadamu hakuna siri.Tabia za mtu unazoziona kwenye maisha yake ni udhihirisho wa siri nyingi zilizo ndani mwake,Ingawa kwa sisi binadamu hatupendagi kufwatilia tabia ya mtu hatua moja kwenda nyingine.Lakini Unapofanikiwa kufwatilia tabia na namna wanavyoishi ndipo kuna uwezekano wa kugundu mambo kadha wa kadha ndani ya mtu huyo.

Kujenga tabia mpya na njema kwenye maisha ya mtu ni maamuzi na sio aina fulani ya nguvu ambayo inahitajika kutoka nje.Mungu alipomuumba mwanadamu alimuumba kwa ukamilifu wote ikiwa na uwezo wa kukibadilisha kila anachokutana nacho kwenye maisha.Mfano Dunia iliiumbwa katika Utupu bali kulikuwa na Malighafi tu ambazo zilikuwa hazitumiwa kwa namna yeyote.Baada ya Binadamu Kuumbwa ndipo mabadiliko yalipoanza kutokea kutokana na utumizi wa rasilimali hizo.Kila badiliko unalolitaka kwenye maisha yako lipo ndani yako.Hakuna mtu mzee zaidi ambaye ataamua kubadilisha tabia yake akashindwa.


Maisha ya Binadamu ni mfano wa Chupa ya Maji iliyojaa maji machafu Lakini Chupa hii inapokwenda kuikingwa maji kwenye Bomba la Maji ndipo Maji safi yapozidi kuingia na Maji machafu yanapozidi kutoka,Unapofanya kitu hiki kwa muda mrefu utakuja jua maji machafu yameshatoka na masafi ndiyo yaliobakia.Unapotaka kubadilisha tabia mbaya kwenda nje jaribu kutafuta tabia mpya nzuri ianze kuishi bila kuangalia tabia mbaya ulio nayo,Unapoendelea kuishi inafika siku unakuta una tabia mpya ambayo ni njema lakini mbaya imeshaondoka.

Information mbali mbali tunazoingiza kwenye maisha yetu kwa njia ya kusoma,mazingira,watu zinaathari kubwa kwenye maisha yetu na tabia kwa ujumla.Mfano mtu anapokuwa muagaliaji wa picha za Ngono kwenye Luninga,Je unafikiri anajenga tabia ya namna gani?Tabia haiingi mara moja tu kwenye maisha ya mtu bali ni mchakato wa muda mrefu ambao unajuisha mambo kadha wa kadha.Hakikisha inaformation unazoingiza kichwani mwako na maishani mwako moja kwa moja zina reflect kuelekea kwenye aina ya tabia ambayo unaipenda.No Body can Act against Information alizonazo kichwani iwe ni nzuri au mbaya.Hakikisha unafanya mabadiliko kuleta tabia mpya na njema kwenye maisha yako ya kila siku.Hakuna fisadi ambaye alianza kuwa fisadi bali alianza kidogo kidogo toka akiwa mtoto na alianza kwa udokozi wa vitu vidogo vidogo.

Mwisho wa Safari yetu siku ya leo kwenye Punch Of The Week Naendea kusema Impossible is The Word Found In Fools Dictionary. Anza hapo ulipo na kitu ulicho nacho kuelekea kwenye tabia njema.Wataalamu wanasema tabia njema si kwa ajili tu ya kukufanya kuishi kwenye jamii kwa amani na furaha bali tabia nje husaidia hata kujenga maisha yako ya kiafya na kiakili,Kuna uwezekano wa tabia zako mbaya zinapeleka kukuharibu kiakili na Kiafya pia.Hakuna mtu aliyezaliwa akiwa anajua kila kitu na kuwa na tabia njema katika kila Idara lakini wote tumezaliwa tukiwa na lengo la kujifunza.Tabia yako kwenye maisha ya kila Siku ni Zaidi ya Upepo wa Kisuli Suli ,Uangamivu wa Maisha yako Inategemea kiasi gani umejenga tabia mbaya.Na kufanikiwa zaidi kwenye maisha inategemea kiasi gani umejenga tabia njema

Kila asubuhi jamii kubwa ya wanadamu wanaamka na kwenda sehemu mbali mbali kwa ajili ya kwenda kujishughulisha ili kupata mahitaji muhimu ya kila siku kwenye maisha yao na jamii kwa ujumla.Tumekuwa tukizungukwa na changamoto mbali mbali kutokana na sababu mbali mbali lakini mwisho wa siku lazima lengo halisi litimie kufikia maswala muhimu ya kimaisha na kijamii.Maisha huchosha na hukatisha tamaa iwapo tunapoona njia ya kufikia yale tunayoyataka kuwa ngumu kupita kawaida lakini Unapofikiria Kuchoka Kabla ya Muda wa Kuchoka Haujafika unakuwa sawa sawa na mkulima anayepanda mbegu zake kwenye Jiwe akitegemea ziote.

1.Mazingira
Mazingira tunayoishi kila siku tangu tunaingia kwenye sayari hii itwayo Dunia yamekuwa na nguvu kubwa ya kututengeneza namna tunavyoweza kupambana na changamoto mbali mbali za kimaisha tunazokutana nazo,Ukitaka kufahamu ili kama ni ukweli au uongo mchukue Mang'ati aliyekaa porini tangu siku anazaliwa kisha baada ya miaka 20 mlete Mjini ndipo utaelewa nachosema.Ndio maana kuna mwingine Changamoto inapotokea hukimbilia kusema huu ndio mwisho wa maisha yangu lakini kwa mwingine husema huu ndio wakati muafaka wa kusonga mbele.Ukifwatilia kwa ukaribu kati ya hawa watu wawili Mazingira na vitu walivyokutana navyo vinawapa uwezo wa kujua iwapo wanaweza kuvuka juu ya changamoto fulani au hapana.

2.Watu
Kariba za watu wa aina mbali mbali tunaokutana nao zinauwezo mkubwa pia wa kutufanya tufikiri namna tunavyoweza kushinda vikwazo na taabu mbali mbali tunazokutana nazo kila siku.Wakati mtu mmoja akikutana na Pope Benedict XVI swali la kwanza watakalomuuliza ni kwanini Umejiuzulu kuwa Pope Mtu Mashuhuri zaidi Ulimwenguni?Lakini kuna watu wengine hawafikiria kumuuliza kwanini Amejiuzulu "Watamuuliza  Je umefanikiwaje kufika kwenye Hiki cheo cha Kuwa Kiongozi wa Kanisa lenye wafuasi wengi zaidi Duniani?Ukifwatilia kuna mwingine amekutana na watu wenye mtazamo wa kimaskini lakini mwingine amekutana na watu wenye mtazamo wa kujua mbinu za kufikia mafanikio.Jiulize wewe je ukikutana na Mengi leo Utakimbilia Kumwomba Pesa au Utamwomba Ushauri ambao utakaokuzalishia Pesa zaidi ya alizokupa Siku hiyo?

3.Ufahamu
Mtu jasiri anayejua anapokwenda kufikiria kuchoka kabla ya Safari yake haijafika ni mwisho.Mtu mwenye kutafuata maarifa na ufahamu juu ya namna ya kuendesha na maisha na kushinda changamoto siku zote hawezi kuwa mkata tamaa.Unapofikiria Kuchoka Kabla ya Muda wa Kuchoka Haujafika ni sawa na kujaribu Kujaribu kuendesha gari lenye pancha ukitegemea litakufikisha Mbeya wakti ndio kwanza unatoka Sinza KIjiweni.Ufahamu hukupa mbinu mbadala za namna ya kutatua changamto husika bila ya kuweza kuishia njia.Tambua vita yeyote duniani unayoiona kwanza huanza kwenye Kichwa cha mtu.Hakuna vita inayoanza nje ya kichwa cha mtu.Jaribu kutafuta ufahamu kila siku.Safari bado ni ndefu usifikiri kuishia njiani wakati unaanza safari ulijua utafika.Jipe Moyo na Usonge Mbele VIkwazo na Changamoto ni sehemu ya maisha ndio maana viliwekwa kuonyesha namna ulivyo hodari na shujaa.

Hakuna Hodari wa Vita anayeweza kujisifia ni Mshindi wakati haukuwahi kupigana vita vya namna yeyote.Changamoto na vikwazo ni Sehemu ya Ushindi ndio maana vipo.Changamoto na vikwazo havikuwekwa kwa ajili ya wanyonge bali kwa ajili ya washindi.Changamoto na Vikwazo havikuwekwa kwajili ya Wanyama ,Viliwekwa kwa ajili ya Binadamu.Siku zote Mshindi hupata Ushindi kabla ya Kufika Eneo la Mapambano La Vita lakini Watu dhaifu hushindwa kabla hawajafika hata eneo la Mapambano.Acha Kufikiria kuchoka kabla y.a Muda wa Kuchoka Kufika.Changomoto na Vikwazo kwenye maisha nivifwananisha na Gereza ambalo hawakutengezewa Kuku bali Watu na ndivyo Changamoto zilivyo ni Kwa ajili ya Watu ambao wamejizatiti kufikia hatma yao ya Maisha na Sio Aina Nyingine ya Viumbe Visivyokuwa na Utashi.
Ukomavu kwenye matumizi ya mitandao ya jamii ni swala linalopaswa kwenye jamii ya Watanzania na matumizi ya vyombo mbali mbali vya habari.Je ivi unajisikiaje unavyoyasema mabaya ya mwenzio kwenye mkusanyiko mkubwa wa watu ili hali wewe una ya kwako?Matumizi ya mitandao ya kijamii na Media kwa ujumla inaonyesha namna gani mtu alivyokomaa kwenye uwezo wa kuchambua na kuendesha vitu kwenye maisha yake.Imani na jamii mbali mbali zina mifumo yake ya kutoa hukumu kwa wahusika wanapokosea na sio kuchafuana kwenye mitandao na kuwaacha wengine wakiwa mithiri hawajavaa nguo.Tafakari unasikikia siku Baba yako Mzazi naye amewekwa kwenye Media au kwenye mtandao wa Jamii na ameelezewa mabaya yake Je Utafurahia au utahuzunika?

1.Ki-Imani

Kila imani  ina mfumo wake wakutoa adhabu pale mtu anapokosea iwapo taaratibu za kushtaki kosa husika mahali husika.Inanishangaza sana kuona kosa la mtu mmoja wa Imani fulani linapochukuliwa na mtu wa Imani ile ile mwingine na kwenda kulishikilia bango na kulitangaza kwa watu wengine wasio wa Imani ile.Je unafikiri watu wa Imani nyingine wanawafukiriaje watu wa Imani ambayo mmoja wa waumini wake makosa yake yamewekwa hadharani.Je unajengaje nyumba yako mwenyewe  kwa kubomoa kila baaada ya kumaliza kozi moja ya ujenzi wa matofali?Ufalme ukishajifitini wenyewe hata siku moja hauwezi kuendelea Mbele.Kabla haujaamua kusema mabaya ya mwingine hadharani kwanza jiulize wewe hauna mabaya?Kumbuka kila mtu anachopanda ndicho utakachovuna.Ukimsema vibaya mwenzako wewe subiri tu kuna siku na wewe utasemwa vibaya zaidi na unapoelezea mazuri ya mwenzako tarajia kuna siku watu wataelezea uzuri wako.Baada ya Kufa ni hukumu kumbuka mahesabu yote tunayamaliza hapa hapa.

2.Ki-Jamii

 Kila kwenye jamii ya watu kuna taratibu na sheria husika za kudhibiti wahalifu wa makosa.Je unapomsema mtu hadharani bila kwenda kwenye mamlaka husika je unakuwa umsaidiaje muhusika na wanajamii wengine wasipatwe na tatizo ambalo lilishakukumba kwa kutendewa ubaya na mtu husika au jamii husika ya watu.Facebook na mitandao mingine ya kijamii ikiwa ni pamoja na media mbali mbali kazi yake sio kuelezea na kuonyesha ubaya wa wengine bali kuhakikisha jamii inapata habari kamili na mafunzo ambayo yana tija kwenye jamii.Iwapo unahisi kuna kosa na matatizo juu ya tuhuma kwa watu fulani fwata taratibu za kisheria na kijamii ili kuwasaidia wengine na sio kuishia kuchafuana.Kumbuka unapomchafua mtu akaamu kukufwatilia kisheria na kitaratibu unaweza kushtakiwa na kuadhibiwa kwa kuongea vitu ambavyo havina tija na uhakika kwenye jamii ya watu.

3.Uasili wa Dunia

Namna ulimwengu ulivyotengenezwa na ulivyoumbwa na Mungu ni namna ya ajabu sana.Kumbuka unapofanya kitu kizuri hata kama haukulipwa mazuri kwa muda huo kabla haujaondoka kwenye sayari hii ndivyo utakavyolipwa.Unapoendelea kuelezea makosa ya wengine na ipo siku kabla haujaondoka lazima na sisi tutasikia makosa yako na mabaya yako makubwa kuliko ulivyoelezea ya wengine.Epuka kuwa msemaji wa makosa ya wengine tumia muda wako kuendesha mambo mema na kuwasemea wengine maneno mazuri.Iwapo unaona hauwezi kuchukua hatua basi ni afadhali unyamaze kuliko kuelezea makosa ya wengine mahali pasipo sahihi.Hata siku moja usitegemee kupanda kokoto ukavune maharagwe.Kile unachopanda ndicho unachovuna.



Mwisho,Mitandao ya Kijamii sio sehemu ya kuhukumu dhambi za wengine.Iwapo unaona mtu wa imani yako au wa jamii yako amekosea tafuta msaada ya kisheria na kitaratibu kwenye mahala husika Facebook na kwenye media sio sehemu sahihi ya kuelezana mabaya bali ni sehemu ya kuisadia jamii kuapata maendeleo chanya na yenye tija kwa jamii yetu na taifa kwa ujumla .Safari ni ndefu kwa watanzania kwenye matumizi ya mitandao ya jamii na media kwa ujumla mpaka tukifikia ukomavu wa safari hii basi tumeshajeruhi na kuharibu maisha ya watu wengine wengi sana.


"Ukiona hauwezi kuficha Uchi wa Baba yako Basi Ipo Siku Utamcheka Mkweo kwa Utupu wake."
Kwa muda mrefu kidogo nchi ya Tanzania ambayo imekuwa ikiitwa Kisiwa Cha Amani ili hali si ukweli ila imekuwa Kisiwa Cha Utulivu na Uoga miongoni mwa wananchi wa Tanzania.Kwa Muda wa Miaka ya Karibuni kumekuwa na kujitokeza kwa aina mbali mbali za vurugu haswa zinazojihusisha na Muonekano wa Kidini lakini Pia na Katika Muonekano wa Kimaslahi kati ya Viongozi wa Serikali na Wananchi wa Nchi yenye Utulivu.Nimekuwa nikijiuliza mengi kila kukicha fujo zinatokea na hakuna ambaye anasimama kuzikemea kwamba haipaswi kuwa namna hii ilivyo sasa.Lakini matokeo yake mambo yalivyo watu wamekuwa wakikaa kimiya na viongozi wamekuwa wakivunga.Je ni nani anayefaidika na Hizi Vurugu zinazoendelea?

1.Vurugu zenye Muonekano wa Kidini.
Vurugu hizi kila kukicha zimekuwa zikiongezeka bila sababu zinazoeleweka na zimekuwa zikifungiwa macho na viongozi wamekuwa wakiendelea kuvunga kanakwamba hakuna kinachotokea kwenye nchi yetu.Taasisi za Dini za Upande mmoja zinaposimama kusema ukweli juu ya Vurugu zinazoendela Utasikia Serikali inasemama na kuzikemea kwamba hazina haki ya Kuwa wasemaji ili hali waumini wa Taasisi wa Dini hizo wamekuwa Wahanga kila kukicha.Je Ni Serikali au Baadhi ya Watu wachache wanaofaidiaka na hizi Vurugu?
Siku za Karibuni kumekuwa na mvutano mkubwa kati ya Upande wa Dini ya Ki-Islamu na Wakristo na Upande mmoja umeonekana ukitetewa na kukaliwa kimiya kwa kila wanachofanya ili hali upande mwingine ukitishia kuchukua hatua huonekana na mbaya Je nani anayefaidika na Vurugu hizi?
Miaka yote tumekuwa tukiishi kwa utulivu huu pamoja na tofauti tuliozo nazo lakini hakuna mtu aliyethubutu kumshambulia mwenzake wala kumdharau Je kwanini wakati huu iwe hivyo?Basi kwa mtazamo wa haraka haraka kuna watu ambao watakuwa wanafaidika moja kwa moja au indirect kutokana na muendelezo wa Vurugu hizi.

2.Vurugu zenye Muonekano wa Kimaslahi(Kifedha na Kiuchumi)
Tumeshuhudia fujo kubwa kwa ndugu zetu wa kanda ya kusini juu ya sakata la gesi linaloendelea.Wananchi wenye mumkari wameshindwa kuvumilia juu ya maamuzi wanayofanyiwa wao bila ya wao kushirikishwa kwa muda mrefu nchi hii watu wachache wamekuwa wakiamua nini kifanyike na nani afanye na nani afaidike kwenye kila mradi unaohusisha fedha nyingi.

Wananchi wanapoamua kudai haki zao kwa kutetea kile wanachotaka wao na wanachoona ni sahihi hugeuka kuwa adui wa maslahi ya watu hao wachache..Miradi Mingi imekuwa ikiendeshwa bila uwepo majadiliano na maamuzi ya wananchi wenyewe kuamua kitu gani wanataka juu ya Rasilimali zao lakini watu wachache wakiamua basi ndio yanatendeka.Hakuna elimu ya kutosha juu ya miradi na faida ambazo wananchi watapata baada ya Serikali kuingia Ubia na Mashirika ya Kimataifa.

Miradi Mingi imekuwa ikiendesha kiholela holela na pindi wananchi wanapodai haki zao kwa njia ya amani hawasikilizwi na matokeo yake huundiwa zengwe na kuonekana ni wabaya.Na wanapoamua mutumia nguvu huonekana ni wakorofi na wavunjifu wa amani?Je ni heri fujo na uvunjifu wa amani utokee sababu ya watu wachache?Muda utafika watu hawatakuwa tayari kuendelea na ujinga huu watu watasimama na ndipo muda huu wa neema utakapokuwa umekwisha na hapo ndipo nchi itashindwa kutawalika sababu ya misingi mibovu inayojengwa leo.

Mwisho,Niwazacho Mimi Kuna mtu au  watu watakuwa wanafaidika na Vurugu na Uvunjifu wa Utulivu tulio nao la sivyo basi hatua za Makusudi zingekuwa zimechukuliwa na katika kutatua matatizo haya ambayo kila siku yamekuwa yakikua na kuongezeka bila sauti za viongozi.

Je ni nani anayefaidika na Vurugu zinazoendelea Tanzania?

MUNGU IBARIKI AFRIKA,MUNGU IBARIKI TANZANIA
Kwa Mara Nyingine Napenda kuchukua nafasi hii kuwaasalimu wadau wote wa blogu katika mwaka 2013,Maana kwa Mara nyingine leo Ndipo tunakuta kwenye Programu yetu ya Kila Ijumaa iitwayo Punch of The Week.Leo katika Punch of The Week tumeamua kuangalia vitu kwa jicho la Pembeni kidogo lisemalo Urahisi wa Njia sio Uhakika wa Safari.

Maisha yetu ya kila siku muda mwingine yamekuwa hayana dira sababu ya kukosa mwelekeo sahihi wa kufanya vitu na kuviendeleza huku tukidhani kwamba hii ndio njia sahihi na huo ndio umekuwa mfumo ambao tumekuwa nao katika kila nyanja.Vitu vingi tumekuwa tikivifanya kwa zima moto huku tukidhani kwamba tunaweza kufikia kilele cha mafanikio ambayo yanaweza kudumu daima.

Maisha yetu yamejengwa kwenye kupenda njia za makato kuliko kufwata kanuni ambazo zipo na ndizo za uhakika kwenye maisha yetu kama wanadamu.Hakuna mtu ambaye amejenga mafanikio ya kudumu kwa kutumia njia za mkato.Uasili wa Dunia jinsi ulivyo ni kwamba ukipata kitu kwa dhuluma kitaondoka kwa dhuluma iwe leo au kesho.Mara nyingi tumeshindwa kuangalia mbele tumeangalia matokeo makubwa ya sasa lakini tunasahau kwamba maisha yanaendelea.Wahenga walisema Ukiua kwa Upanga Basi na Wewe utauwawa kwa Upanga wakimaanisha namna kitu kinavyopatikana ndivyo kitakavyoondoka.


Mafanikio yanayodumu ni yale yanayojengwa kwa mfumo wa Haki na kujituma siku zote.Hakuna mazingaombwe kwenye mafanikio wala uchawi.Iwapo unategemea uchawi,wizi na dhuluma kupata maendeleo habari nilio nayo ni kwamba tunasubiri anguko lako siku yeyote kuanzia sasa hata kama leo unaonekana unakula bata na kufurahia lakini kanuni za asili za kuendesha dunia huwa hazibadiliki siku zote.

Kuna hasara njinyi sana kwenye kutegemea kupata vitu kwa njia ya mkato kuliko kufwata kanuni za msingi za kufanikiwa katika jambo lolote.Je wewe unafikiri ungekuwa umezaliwa siku ya kwanza then siku ya pili tunakuona unakimbia je unafikiri sisi tunaokuzunguka tungefikiria vipi?Au wewe mwenyewe ungewazaje?

1.Njia za Mkato mara zote hazitoi jibu la uhakika na linalodumu siku zote.Njia za mkato au zima moto husaidia kutatua tatizo kwa muda tu lakini mara nyingi hakuna uhakika wa kudumu wa suluhisho ambalo litadumu siku zote za maisha.Fikiria iwapo haujawahi kufanya biashara siku zote za maisha yako ghafla unakuwa na biashara kubwa kesho asubuhi unafikiri biashara hiyo itadumu?Jibu ni hapana sababu hauna mufundisho ya msingi juu ya uendeshaji wa biashara na namna ya kucheza na mzunguko wa fedha.Unapofwata hatua mbali mbali unajenda uwezo binafsi wa kujifunza na kuwa na uhakika wa kutokurudia makosa ambayo hautaweza kuyarudia tena.Kumbuka siku zote Vitu rahisi gharama yake ni kubwa zaidi.Mfano Mzuri ni pale ambapo tunapoumwa kichwa kwa ghafla huwa tunameza dawa za kutuliza maumivu tu lakini huwa bado hatujatatua ugonjwa wa msingi ambao umepelekea kuumwa kwa kichwa.Ili kutibu na kufahamu ugonjwa husika ni lazima umuone daktari upate vipimo na ndipo upewe dawa kamili za kutibu ugonjwa husika.

2.Mtu anayetegemea njia za mkato mara nyingi huwa hakomai kitabia na namna ya kuendesha vitu vyake maishani mwake siku zote.Unapoiona tabia fulani ya mtu ndivyo alivyo mwenyewe.Tabia hujengeka kutoka na mfumo wa maisha wa mtu wa kila siku alio nao.Iwapo unafikiri kwamba wizi ndio njia sahihi ya kuishi basi siku zote hautajua kwamba kuna namna nyingine ya kuishi sababu ndivyo ulivyojijengea.Maisha huenda na kubadilika kila siku kuna siku utashindwa kuiba je utaishi kwa namna gani?Ukiona mtu anakuwa na hasira na maamuzi mabaya siku zote usikimbiliea kumlaumu fwatilia ni wapi ameanzi na amekulia katika mazingira gani maana hayo ndiyo yaliyojenga mfumo maisha yake.Mara zote nimesema hakuna mtu anayeweza kusihi nje ya information mtu ambazo anazo kichwani.Na information hupatika katika njia tofouti tofauti  
(I)Mazingira 
(II)Marafiki 
(III) Malezi 
(IV)Vitu mtu anavyosoma kila siku n.k.
Ukomavu wa tabia nzuri huja kutokana na mafundisho magumu ya kufwata kanuni mbali mbali na mfumo wa asili wa dunia ulivyoweka bila kukubali kufwata njia za mkato na urahisi.

3.Mafanikio ni Mchakato na sio Mkato.Mafanikio yanayodumu yamejengwa kwenye njia ngumu ambazo mara nyingi tumeambiwa lakini tumekuwa tukipuuzia.Mafanikio yanayodumu yamejengwa kwenye uvumilivu ambao umejengwa katika muda mrefu ambao ndani yake kunakuwa na mchakato mgumu wa mafundisho ya asili na ambayo muda mwingine sio rahisi kuyaelewa na usipokuwa makini utaishia kulalamika na kukata tamaa.Waswahili Wanasema Njia Nyembamba na isiliyosonga ndio Inayoelekea uzimani n lakini njia nene ndio inayoelekea upotevuni.Hakuna mkato kwenye mafanikio yanayodumu.

4.Njia ya Mkato haikujengei nidhamu ya kuheshimu na kuyatunza mafanikio ambayo umeyapata.Unapojifunza kujijenga kwa njia sahihi unajenga uwezo binafsi wa wewe kuheshimu na kuthamini mafanikio ambayo umeyapata kwa nguvu zako mwenye pia unasikia ufahari wa kujivunia kila ambacho umekipigani siku zote.Fikiria kama umetoa mtoto au mke wako sadaka kwa mizimu unafikiri wakati wa kujivuni mafanikio yako utajivunia Damu uliyoimwaga ya wapendwa wako au utakuwa mnafiki wa kujifanya unafurahi wakati ki ukweli moyoni unajua sivyo ilivyo?Mafanikio yaliyopatikana kwa juhudi binafsi hukujengea uwezo binafsi wa hata kuheshimu na kuthamnini wengine bila kuwadharau.

Kumalizia safari hii ya Urahisi wa Njia Sio Uhakika wa Safari jifunze kujenga mafanikio yako kwenye msingi utakaodumu vizazi na vizazi na hata ambapo hautakuwepo lakini mafanikio yako yatakuwepo na kuelezea sifa zako nzuri  kwa jamii nzima ya wanadamu.Fikiria umekufa halafu Kizazi ulichokiacha kinatukanwa na mafaniko ya wizi iwapo utakuwa na bahati ya kuona huko ulipo utajisikiaje.

Tukatane tena Week Ijayo Kwenye Punch Of The Week
Mwanamuziki wa Injili anayeishi nchini Sweden Katika Mji wa Malmo anayejilikana Kwa Jina Rachel Sharp katika siku ya Jumamosi 26/1/2013 alizundua Albamu yake ya Pili hapa nchini Tanzani ijulikanayo kwa jina "NI MUNGU WA AJABU" yenye jumla ya nyimbo 10 zilizo katika mfumo wa CD na nyimbo 8 zilizo katika DVD.
Rachel Sharp alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari katika Eneo ya Nyumba yake katika Eneo La Tegeta Ambapo ndipo uzinduzi ulipofanyika alitoa Rai kwa Wanamuziki wa Tanzania Kuendelea Kuenzi Muziki wetu wa Asili kama Ilivyo Mdumange na Mdundiko pia aliongezea kwa kusema Lugha ya Kiswahili kwenye Muziki inalipa zaidi kuliko ilivyo Lugha za Kigeni tunazojaribu kutumia.Akitoa mkazo zaidi aliendelea kusema tuache kuiga miziki ya watu na sisi tukae chini tubuni aina yetu ya muziki ambayo inaweza kutumika kama utambulisho wetu kwenye soko la kimataifa la Muziki.


Mc wa Event Ritha Chuwalo akimtambulisha Rachel Sharp

Rachel Sharp akiwatambulisha Wazazi wake Kwa Waandishi
Rachel Sharp Akitoa Wito kwa Waandishi kufikisha Ujumbe alioukusudia

Mume wa Mtangazaji Maarufu Zawadi Machibya akiweka wakfu Albamu ya Rachel Sharp.

Hadi Kieleweke.....Mwanamuzi wa Injili Rachel Sharp akiwa kwenye Stage 

Mwanamuziki wa  Injili Rachel Sharp akienda sawa kwenye 

Nguli wa Muziki Nchini Tanzania Upendo Kilahiro akifanya kazi kwenye Stage
Rachel Sharp na Upendo Kilahiro wakiwa kwenye Jukwaa Moja
                                           
Mwisho wa yote Rachel Sharp alisisitiza Kuwa Mafanikio Yetu hayaji kirahisi kwenye Kila Kitu imetupasa kujituma katika kila jambo bila kujali wengine wanatonaje,akimaliza alisema Upendo na Umoja Miongoni mwa wanamuziki wa Injili kukaa chini na kuja na ubunifu mpya kutawaongezea mafanikio katika tasnia ya Muziki wa Injili ndani na Nje ya Mipaka ya Tanzania.
Miaka Michache iliyopita Tanzania kulikuwa na Blogs Chache sana na tulikuwa tunajiuliza ivi mtu anawezaje kumiliki blog,Lakini baada ya muda fulani kupita watu wengi tulijifunza angalau namna ya kuanzisha na kuendesha blog.Miaka ya 2005 teknolojia ya blog Tanzania ilikuwa ngeni kidogo lakini nashukuru kwamba kadri siku zinavyozidi kwenda blogs zinaongezeka na zimekuwa nyingi zaidi lakini pamoja na haya yote kutokana na ukuaji wa teknolojia hii nchi yetu imekuwa taratibu sana kutunga sheria au kufanya mabadiliko ya sheria mbali mbali yatakayoendana na ukuaji wa teknoloji mbali mbali.Sina mengi ya kujadili kwa upande huo.

Baada ya kufanikiwa kupitia blogs nyingi hapa Tanzania hata mwanzo naanzisha blog hii nilijua copying and Paste ndio namna ya uendeshaji wa blog lakini baadae baada ya kufwatilia kiundani kidogo nikajiuliza je mtu alianzisha teknolojia ya blog alikuwa na maana hii ya copy and paste au kulikuwa na maana nyingine zaidi?

Blog sio copying and Paste blog ni sehemu ya kuonyesha kile ulichonacho kwenye ubongo wako,Baada ya kufwatilia sana nimekuja kugundua tasnia ya uandishi hapa Tanzania ina Critical Thinker wachache na hata waliopo hawaandiki maswala yanayohusu jamii na maisha yetu ya kila siku katika kuikwamua jamii yetu.

Blog sio sehemu ya matangazo baada ya kufwatilia tena nimekuja kugundua yaani sisi huwa vitu vingi tunafanya kinyume nyume yaana baada ya kwenda mbele sisi tunarudi nyuma.Yaani siku hiz utakuta blog ina matangazo mpaka unaboreka,hata hamu ya kuendelea kuangalia blog hauna hamu.Na tatizo kwa walio wengi sio vibaya kuwa na matangazo lakini sababu na maana ya msingi ya kuwepo blog isifutwe au kupotezwa kwa tamaa ya fedha.

Blog ni kama diary ambayo unaweka kumbukumbu zako muhimu za maisha ambazo zinaweza kuwasaidia wengine na kuweza kutoa majibu ya maswali amabayo wengine wanayo juu ya maisha na maswala mbali mbali ya kijamii katika kila nyanja yaani kiuchumi , kijamii na hata kisiasa ili kuweza kuleta hamasa kwenye jamii yetu katika maisha yetu ya kila siku.

Je Blogger ni Mwandishi wa Habari ?Kuna tofauti gani kati ya Blogger na Mwandishi wa Habari?
Mwisho jifikirie kuna tofauti gani kati ya website na blog...Na kama blog ni website ndogo kwani kuna website kubwa....Nini maana ya neno www.ww.com na nini maana ya www.fm.blogspot.com
Then come up with answers,tuifanye tasnia ya blog kuwa kivutio na sio kero kwa watu.Fikiria na ufanye mabadiliko.Hivi ndivyo Niwazavyo Mimi

Heri ya Mwaka  Mpya kwa Bloggers Wote Wa Tanzania 2013
Wakati nchi yetu ikiwa katika mchakato wa kukusanya maoni juu ya mbadiliko ya Katiba kwenye nhi yetu asilimia kubwa ya watanzania hawajui kinachoendela kabisa na umuhimu wake katika nhi yetu ya Tanzania kwa Miaka ijayo.
Tangu nchi hii kupata uhuru hatujawahi kuwa na Katiba yetu kama watanzania bali tumekuwa na Katiba ambayo ilaandaliwa na baadhi ya watu wachache kuendesha nchi yetu.Lakini 
kadri Siku zinavyozidi kwenda tumekuja kuona Katiba iliyopo sasa haikidhi mahitaji kwa kiasi kikubwa kulingana na wakati wa mabadiliko makubwa tulio nayo kwenye namna ya uendeshaji wa nchi na mifumo yake mbali mbali kuanzia kwa Watawala na Watawaliwa.
Kinachochangaza Watanzania tulio wengi ndio tulidai mabadiliko ya Katiba kwenye nchi yetu lakini katika mchakato huu wa Makusanyo ya Maoni ya mabadiliko ya Katiba kunashangaza,Tumekuwa waongeaji sana wa mitaani na vijiweni lakini kwenye utendaji kuwasilisha maoni yetu tumekuwa wavivu.Kumbuka unanaposhindwa kutoa maoni yako kuhusu namna Katiba ya nchi yako iweje siku maamuzi yanapotolewa usiwe wa kwanza kulalamika tena.Na itakupasa kulipa gharama kwa Muda wa Kipindi Kirefu kijacho.Maisha ya nchi hii wewe na vizazi vyako vyote vijavyo inategemea unafanya nini kwa sasa.

Takwimu kutoka kwenye Tovuti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba

Katika awamu ya tatu iliyomalizika tarehe 6 Novemba, 2012, Tume ilifanya mikutano 522 katika mikoa yote tisa ingawa ilipanga kufanya mikutano 496. Hali hii ilitokana na mahitaji mapya katika maeneo mbalimbali ya mikoa hiyo na kuifanya Tume kuitisha mikutano ya ziada ili kuwapa fursa wananchi wengi zaidi. Katika awamu ya pili, Tume ilifanya mikutano 449 ambapo Awamu ya kwanza Tume ilifanya mikutano 388.
 Katika awamu hii ya tatu, jumla ya wananchi 392,385 walihudhuria mikutano. Jumla ya wananchi 21,512 walitoa maoni yao kwa kuzungumza katika mikutano hiyo na wananchi 84,939 walitoa maoni yao kwa maandishi. Aidha, katika awamu hii ya tatu, jumla ya wananchi 1,639 walitoa maoni yao kwa kuzungumza na pia kwa maandishi katika mikutano hiyo.
Mwitikio wa wananchi kuendelea kutumia simu za mkononi, ukurasa wa facebook, tovuti na posta kutoa maoni nao umeongezeka kwa kiasi kikubwa. Kwa mfano, jumla ya wananchi 27,992 walikuwa wametembelea ukurasa wa facebook wa Tume katika kipindi cha awamu ya tatu tofauti na watu 21,789 waliotembelea katika kipindi cha awamu ya pili. Aidha, ujumbe mfupi wa simu (sms) 6,909 umepokewa na Tume katika awamu hii ukilinganishwa na sms 75 katika kipindi kilichopita;
Idadi ya wananchi wanaohudhuria na kutoa maoni katika mikutano nayo imeongezeka. Kwa mfano, idadi ya wananchi waliohudhuria mikutano ya awamu ya kwanza walikuwa 189,526.  Awamu ya pili ni 325,915 wakati wananchi waliohudhuria mikutano ya awamu ya tatu ni 392,385. Aidha, wananchi waliotoa maoni kwa kuzungumza katika mikutano ya awamu ya   kwanza walikuwa 17,127. Awamu ya pili walikuwa 12,334 wakati wananchi 21,512 walizungumza katika awamu ya tatu;

Ukifwatilia hizi takwimu hapa juu utagungua Maamuzi ya Nchi hii yanye watu takribani Milioni 40 na kuendela kwa sasa watu ambao hawafiki hata milioni tatu ndio wanaamua nini kifanyike juu ya nchi hii kwa Miaka mingine Mingi ijayo.
Inatia Hasira kuona watu wachache namna hii ndio wanato maamuzi ya nch hii sisi wengine Vijiweni,kuchati facebook,Twitter,kwenye simu zetu za mkononi,Kusubiri Ze Comedi ni lini au Tamasha La Fiesta ni lini au Rose Muhando anazindua lini?
Ni muhimu kujua habari mbali mbali katika nchi lakini Kumbuka kuna baadhi ya vitu maishani mwako vinaamua hatma yako kwenye kila jambo.

Njia Ambazo Unaweza kutuma Maoni yako.

1. Njia ya simu 
+255 22 2133425
2. Barua pepe 
katibu @katiba.go.tz
3. Tovuti ya Tume ya Mbadiliko ya Katiba 
http://www.katiba.go.tz/index.php/toa-maoni-yako
4.Facebook
https://www.facebook.com/pages/Tume-ya-Mabadiliko-ya-Katiba-Tanzania/323414977745643?fref=ts
5.Tume ya Mabadiliko ya Katiba
Makao Makuu
Sanduku La Posta 1681,
Dar es Salaam, Tanzania.

MUNGU IBARIKI AFRICA , MUNGU IBARIKI 
TANZANIA
Katika namna ambavyo mfumo wa kuishi umewekwa na uhalisia wa mambo ulivyo katika sayari yetu iitwayo Dunia Kukua ni mchakato na sio Muujiza.Kitu chochote ili kikue kufikia utimilifu lazima kinapitia mchakato fulani kabla ya kufikia ukamilifu wowote.Hakuna kitu ambacho kinaweza kukua ghafla bila kupitia mchako wa aina Yoyote iwe ni Kiroho au Kimwili.Binadamu ili kufikia hatua ya kukua na kufikia na ukamilifu wake lazima kuna hatua na mchakato fulani amepitia.lazima Mtoto azaliwe,Akue afikie Ujana ,Uzee ndio Unakuwa tamati na kifo huchukua mkondo wake.
Katika maisha yetu ya kila siku tumekuwa tukikumbana na changamoto na vitu mbali mbali ambavyo tunashindwa kuelewa kanuni za msingi za kuendesha vitu.Katika kila unachofanya lazima kwanza kinaanza na kuzaliwa,Hatua ya Katikati ndipo utimilifu wa juu wa kitu hufikia.Unapomuona mtu mzima leo(Mzee) lazima alipitia hatua zote tatu Muhimu.


1.Kuzaliwa(Formation)
Kuzaliwa ni moja ya hatua muhimu ya maisha na uhai wa kitu chochote,katika hatua hii unaweza ukawa umependa kitu kizaliwe au kisizaliwe lakini mwisho wa siku wote tunajikuta kwenye uwanja wa Mapambano.Je unaendelea kulaumu kwa nini kitu fulani kilizaliwa?Hapana,yaani hata kama ukilauma ndio tayari kimeshaonekana kwenye Ulimwengu wako.
Mfano Kuna watoto walizaliwa kwa Uzazi wa Mpango na Wengine Ghafla Bini Vuu wakajitokeza kwenye Hii sayari,Aliyezaliwa kwa uzazi wa mpango na wa Ghafla Bini Vuu Mwisho wa siku wote wako kwenye Sayari hii itwayo Dunia.Kulaumu kwako hakukufanyi urudi tumboni kwa Mama bali ndio Umeshafika sasa.
Yaani Samaki aliyevuliwa kwa Baruti na Wengine kwa Njia Sahihi lakini mwisho wa Yote wamevuliwa na wameshatolewa baharini.

Hapa ndivyo ilivyo kwenye maisha yetu ya kawaida unaweza ukapanga kufanya kitu fulani kwenye maisha au Usipange lakini mwisho wa siku ndio umeshajikuta humo.Je Unafanyaje?Kulaumu hakutasaidia kutatua hilo tatizo au hicho kitu ambacho umekutana nacho.

Kitu kinapozaliwa kinaweza kisiwe na mwelekeo sahihi lakini wewe mlezi wa kitu ndio una uwezo wa kufanya kitu kiwe sahihi,ndio Maana Wahenga husema Mtoto uleavyo Ndivyo akuavyo.usitegemee Utamlea mtoto katika hali ya uvivu na Uzembe alafu akikua awe Mchapa Kazi...
Unapotaka kuanza Biashara lazima Izaliwe kwanza,Unapotaka Kuanza kazi lazima iwe na mwanzo wake...Hakuna kitu kina kua tu...Kumbuka Hata Mbuyu ulianza kama Mchicha Ila Sijui...Kiroboto alianza kama nini....mwisho wa Siku Kukua ni Mchakato na Sio Muujiza........


2.Kukua(Growth)
Siku hizi kwenye jamii kumekuwana matatizo mengi sana ambayo watu wengi tumeshindwa kupata majibu kwa sababu hatujui mchakato wa vitu hivyo vimeaanzi wapi,Mfano Wakati unakuwa nyumbani kwenu unakuta Style ya Maisha ni Matusi na Ngumi kuanzia kwa Baba na Mama Mpaka Kaka/Dada zako.Je Unahisi hapa itakuwaje?Je unapomwona Mtu ni Mlevi unahisi alinza ghafla tu..Hapana Kukua kwenye jambo lolote ni Mchakato na sio Muujiza hata Ukisoma kwenye Vitabu vya Dini Dhambi ili iwe dhambi Kuna mchakato imepitia mpaka kufikia Tamati
Kufikia hatua ya kukua kwenye kila jambo inategemea msingi uliojengwa tangu mwanzo wakati jambo linaanza..Unaapomwona mfanyabiashara mkubwa leo amefanikiwa hakuanza kama uyoga bali kuna mchakato alioupiti kugia Hapo.Mara nyingi tunasahau kwamba hakuna kitu ambacho kinaibuka tu kwenye maisha Yetu ya kila Siku..tangu Mwanzo ukijenga tabia ya kusoma vitabu na kutafuta maarifa na kubuni vitu na ukaendelezwa ndivyo utakavyokua.
Usimshangae mtu alivyo Leo Maana Hukuona Jana Yake,Tabia na Maisha ya Mtu ilivyo leo Inatagemea kwenye hatua za mwanzo alianzaje?
Mara nyingi nimekuwa nikipishana na watu sana kwenye kuwahukumu watu kwenye maisha yao kwa sababu sisi tunaona matokeo lakini hatujui huyu mtu alianzaje...Imekupasa kulaaumu msingi wake ulivyojengwa na sio hii hatua ya Katikati ya Kukua.


3.Maturity(Ukomavu)
Hatua iliyopita ni moja kati ya hatua muhimu ambazo zinaweza zikatoa Majibu ya maswali mengi kufikia kuelekea hatua hii ya Ukomavu(Maturity).
Kutokana na mfumo wa Malezi yetu Watanzani kama si waafrika tulio wengi tunakuja kugundua vitu vingi si sahihi kwenye hatua ya Kukua wakati msingi ulishajengwa vibaya.Mfano wa Ghorofa Ikishajengwa vibaya toka chini kwenye Msingi ndivyo itakavyoendelea Mbele kwenye Ujenzi.Iwapo Fundi hakushtuka basi ujenzi huo utaendelea mpaka mwisho wa safari na Mwisho wa Siku tunashuhudia Ghorofa zinaanguka na kuua watu.
Pamoja na maisha yetu ya kila siku kujengwa Hivyo mpaka tikufikia ujana ndio tunagundua kwamba hiki hakikuwa sahihi Je unafanyaje?Je unaendele kuishi kwenye Ubaya?Je Unavunja Msingi huo Uanze tena?
Kuna maswali mengi ya kujiuliza sasa.
Unapokua kipindi cha Ujana unaweza kufanya Mabadiliko Mengi sana ambayo yanaweza kuleta matoke chanya kwenye kipindi cha Ukomavu wa Jambo lolote.Hakikisha unafanya maamuzi yalio Sahihi kwenye Jambo lolote..hakuna Muujiza...hapa...Hata Uwapo unataka kukuza kiwango chako cha Kufikiria vitu anza mwanzo na utsonga mbele taratibu hakuna Muujiza hapa ....
Jambo Lolote linapofikia mwisho ndipo tunaona Matokea kutokana na hatu mbili zilizopita na Hapa ndio watu wengi tunatoaga hukumu ya Maswali Mengi sana na vitu vingi sana maishani mwetu....Katika yote ukumbuke hili....Growing is a Process Not A Miracle..................

                      
             ...................Kukua Ni Mchakato   Na .............Sio ...............Muujiza..........................