Kumekuwa na Wimbi la Watu Maarafu kwenye Muziki,Watangazaji na Wanaharakati Mbali Mbali wenye Mitazamo tofauti wa Kuingia kwenye Harakati za Kisiasa na Kutangaza nia za Kugombea Nyazifa mbali mbali kwenye Taifa Hili la Tanzania.Kinachonishangaza ni kwamba watu hawa kabla hawatangaza nia za kuingia kwenye siasa na kushika nyazifa mbali mbali katika nchi hii,Huko walipokuwepo wamefanya nini kabla ya kuamua kuingia huku?Sisi Watanzania tunaweza kuwa sehemu ya majaribio kama kichwa cha mwendewazimu kwenye uongozi .Taifa lenye tija na nia ya maendeleo haliwezi kukurupuka kuwapa nyazifa muhimu watu ambao wamelala na kuamka asubuhi na kutamka nia yao ya Kigombea nyazifa Mbali Mbali Kwenye Taifa hili.

Hakuna Jambo Kubwa linaloanza na Ukubwa Wake,Kila jambo linaanza na udogo wake.Swali langu ni kwamba hawa ambao wanataka tuwape nyazifa za uongozi,je huko kwenye nyazifa ndogo ndogo wamefanya nini cha kukumbukwa?Je wameleta mapinduzi namna gani?Kila siku tunaweza kujikuta tunarudi pale pale kwa kuwapa watu uongozi ambao lengo lao ni kuanza kujifunza kwenye nyakati muhimu ambapo sisi tunahitaji kusonga mbele.Baada ya Miaka hamsini ya uhuru hatuhitaji kuwapa watu nyazifa za uongozi kwa nia ya kujifunza bali kwa nia ya kusonga mbele.Tuwapime kwanza si kwa wingi wa maneno ya vyombo vya habari bali kwa utendaji wao wa maisha yao ya kila na kwa kazi ndogo ndogo ambazo wanazo kwa sasa.Inakera na Inauma tunampa mtu uongozi ndio  kwanza yeye anaanza kujifunza kwenye migongo ya watanzania.Tusipoangalia ule msemo wa kichwa cha mwendewazimu hautakaa utoke ndani ya taifa hili la Tanzania.Tusikubali nchi yetu kuwa sehemu ya Mafunzo ya Uongozi.Tuchague watu wenye kujielewa na  kuweza kutufikisha mahali ambapo tunapataka kufika na sio ili mradi tumemaliza kuchagua kiongozi.Siku Moja Wajukuu Wetu watachapa Makaburi yetu Fimbo kwa Utoto ambao tumekuwa tukiufanya kwenye taifa letu kwa kushindwa kujisimamia.

Ni Ngumu sana kujua nia za hawa ambao wanaanza kutangaza nia za kutaka kugombea uongozi na nyazifa mbali mbali lakini kwanza tunaweza kupima nia zao kwenye maisha yao ya kila siku kabla hawajaanza nia ya kuamua kutangaza nia zao za kutaka uongozi.Je hapo Makazini walipo wamewatumikia vyema wafanyakazi wenzao?Je vyao walivyo navyo vimeleta tija kwa wafanyakazi wenzao au ndio Yale Yale ,Wanataka kujifunzia kwa Migongo yetu,Unafikiri kama mtu alikuwa mchoyo kwa Wafanyakazi wenzake unafikiri siku akipata cheo atakuwaje?Je unafikiri kama mtu alikuwa mbaguzi kwa wafanyakazi wenzake unafikiri siku aakipata cheo na nyazifa itakuwaje?Ukitaka kujua Nia ya Mtu na Miasha ya utendaji wake kwa Ujumla nagalia hata anavyoishi na Jirani zake pale mtaani,tutagundua mengi sana juu ya hawa wanaotaka kugombea uongozi na nyazifa mbali mbali.

Uongozi ni Tabia iliyojengeka Ndani kwa Muda Mrefu.Uongozi sio kitu ambacho kinazaliwa leo.Uongozi ni learning process.Iwapo mtu haukuwahi kuwa na tabia ya kujifunza tangu mwanzo wa maisha yake ya namna ya kuwa kiongozi ni ngumu kiongozi huyu kuweza kujifunza kuongoza watu kwa muda mchache.Kuongoza watu ni outcome na manifestation ya tabia fulani iliyojengeka ndani ya mtu kwa muda mrefu na sio kitu ambacho cha kukurupuka.Iwapo mtu anaweza kuuigiza kuwa kiongozi baada ya muda fulani tunaweza kuona uhalisia wake...Mfano Mtu anapotukana Bungeni sio kitu ambacho Kimetokea ghafla ni Kitu ambacho kimekuwepo ndani mtu muda mrefu anaweza asitamke mkiwa wote lakini akiwa pekee yake ndani mwake matusi ndio kitu kilichomo....Kitabu fulani cha Imani fulani Kinasema...Yaliomjaza mtu ndio Yanayomtoka.....Hauwei tukana then ukasema ni Bahati Mbaya,Hawezi Kuwa Mgomvi then Ukasema imetokeo tu. Uongozi ni Zaidi ya Chuki na Hasira za Mtu alizokuwa nazo Moyoni.Unaweza kumchukia mtu mmoja lakini kumbuka kuna wengine mamilioni wako nyuma yako,Wnasaikolojia fulani walisema unapokuwa na hasiri kichwani mwako Unakuwa kipofu kwenye maamuzi yako Mengi.Je Tunaendelea Kuongozwa na watu waliojaa hasira na viasai moyoni mwao?

Uongozi ni Uwakilishi wa Wananchi.Uongozi sio uwakilishi wa wewe na tumbo lako bali ni kujitoa kwa ajili ya wananchi.Iwapo mtu anapotaka kuwa kiongozi lazima ajue namna ya kuwasilisha hoja na matakwa ya wananchi anaowaongozo,Inanishangaza sana kuona inapokuwa kwenye vikao vya Bunge,Mbunge anakosoa bajeti na kueleza mambo kadha wakadha  ambayo mapungufu yake yanaonekana wazi kwenye bajeti mwisho wa siku utasikia Naunga Mkono Hoja,Je Unanga Mkono Makosa uliyo yasema au?Je wanauwezo wa kuishawishi serekali na wadau wake juu ya Maendeleo ya Taifa hili kwa Hoja zenye Mashiko na Msingi ambazo watazisimamia hata wakiwa wamelala kitandani mwao Usiku?

Taifa Letu sio Sehemu ya Mafunzo Ya Uongozi lazima Ifike sehemu tufanye maamuzi magumu kwa kuwakataa wale ambao wanaonekana hata kwenye nyazifa ndogo walizo nazo hawakonyesha mapnduzi ya kifikra wa ujenzi wa jamii huru katika maeneo yao ya kazi.Tusiwaamini Tuwapime kwa nyazifa zao za sasa badala ya Kutulisha maeneo matamu midhili ya Sukari Guru Mwisho wa Siku Watanzania ndio Tunahangaika na Kumbuka Mtu akishainga kwenye Mfumo wa Uongozi kulingana na Katiba yetu ni Ngumu Kumtoa ki-urahisi Labda Tusubiri Miaka Mitano na Muda Hautatungoja....

....Nazungumza Moyoni....Huko Walikotoka Wamefanya Nini....?
Kila Kukicha Nchini Mwetu Kumekuwa Kukizuka Vituko Kadha wa Kadha..Leo Katika Ndivyo Sivyo ..Tunajidili Kuhusu Mabloga Wetu.Kazi ya Blogging Kwenye Jamii za watu waliondelea ni moja ya kazi ambazo zimekuwa zikiheshimiwa kutokana na ufasaha wa kazi na ubunifu wa Kazi za Mablogger.Lakini Nchini Mwetu Imekuwa Ndivyo Sivyo.Mablogger wengi wamekuwa wakitamani kupata Umaarufu wa Haraka Haraka Kwa Kutoa Habari zinazoipotosha Jamii na Kuifanya Jamii kuona kama Jamii ya Bloggers kama ni Jamii isiyojua Kitu gani Inafanya.Lakini Ki-ukweli ukitaka Kuheshimika Fanya kazi yako kwa Heshima...Acha Habari za Uzushi ...Kuwa Blogger Sio Kukosa Kazi Bali ni Kuwa Mbunifu na kwa Kutafuta Habari zenye Kina na Maantiki zenye kuisogeza jamii yetu Mbele.Blogging sio Copying and Pasting....Blogging ni Ubunifu wa Kichwa chako kwenye Jamii Yetu.
Katuni Hii Kwa Hisani ya Marco
Kila Maji Yana Mkondo Wake,Wahenga Walisema.Ubora wa Kitu hautegemeani na Mlinganyo wa Kitu Kimoja Na Kingine.Muda mwingi tumeshindwa kufikia malengo yetu na kukata tamaa baada ya kujilinganisha na wengine huku tukijiona sisi ni Dhaifu.Katika kila ndani ya mtu mmoja kuna upekee ambao mtu mwingine hana ndio maana kwenye maisha kuna furaha ya kufurahia maisha.Fikiria iwapo wote tungekuwa tunawaza na kufanya vitu kwa matazamo mmoja maisha yangekuwa yanaboa na tungekuwa hatuna tofauti na maroboti maana ladha ya maisha isingekuwepo.Jamii yetu na kizazi chetu tumekuwa na watu feki zaidi kuliko watu halisia kama zilivyo bidhaa.Hatuwezi Kufwanana kwa kila jambo inagawa kuna vitu hatuwezi kupishana sana.Maisha yasiyo na uhalisia ni kama kujaribu kujaribu kuiga finger print ya mtu mwingine ili hali tunajua utapatia lakini hauwezi kufwana kwa kila kitu.Kwanini uwe nakala ya Mtu mwingine wakati wewe pekee ni nakala yako binafsi tosha.Kwanini Usitamani wengine wawe nakala yako baadala ya wewe kuwa nakala ya mtu mwingine?

Ujenzi wa maisha yenye kudhubutu na kufanya kile ambacho ni halisi huanza ndani mwa mtu hakuna kitu ambacho kinatokea hewani mithili ya mwanga wa jua kila asubuhi.Ujenzi wa tabia ya mtu ya ndani ndio mwanzo wa kila jambo kwenye  maisha.Hakuna mtu anayepaswa kukutengenezea ndoto maishani mwako bali wewe ndio unapaswa kujenga ndoto yako maishani mwako.Watu wengine wa nje wanapaswa kukusaidia kukuongoza na kukupa hekima ya namna ya kufika ndoto zako na si kukujengea ndoto zao ambazo zinatakuwa zinaisha ndani yako huku ndoto yako halisi ukiwa umeifukia chini.Ndoto yako maishani ndio furaha yako.Ukivaa kiatu cha kuazima ipo siku utakirudisha tu,Ni bora uvae cha kwako ambacho utakuwa nacho huru na utafurahia daima.

Watu wengine sio kipimo halisi cha Ndoto zako kwa sababu mwenye picha halisi ya ndoto zako ni wewe na sio mtu mwingine .Unapojaribu kujilinganisha na wengine ni kujaribu kuishi ndoto zao.Maisha halisi ya mtu ni mtu mwenyewe.Wakati unaanza kufukiria Kichwani mwako hakuna mtu amabaye alikuwa kichwani mwako.Ubora wa ndoto na Uhalisia wa ndoto unao wewe kichwani na sio mtu mwingine.Ukifwata watu wengine watasaidia kukatisha tamaa kwa sababu kuna sehemu fulani ya maisha yao walishindwa au wao ndio mwisho wa ndoto zao.Vipimo vya ndoto zao ndipo zilipoishia hapo.T.B.S huweka kiwango cha chini cha Bidhaa kuwa na ubora fulani lakini haimaishi kwamba hauwezi kutengeneza bidhaa ambayo ina ubora zaidi ya viwango walivyoweka.

Mafanikio yako kwenye maisha hayategemei kuna wengine wamefanikiwa kiasi gani.Picha halisi ya mafanikio unayoyataka unayo wewe ndani yako na sio kwa mtu mwingine.Unaweza kuona mtu mwingine amefanikiwa maishani lakini ukilinganisha na ndoto ulizokuwa nazo na kipimo cha kiwango chako inawezekana yupo chini ya kiwango cha kipimo cha mafanikio yako.Wewe binafsi ndio kipimo halisi ya kile unachopaswa kukifikia.Iwapo una uwezo wa kupata maksi 100 kwenye mtihani na ukapata 90 bado wewe umeshindwa kufikia mafanikio sababu uwezo wa kupata 100 uliokuwa nao na kipimo cha mafanikio yako wewe ndio unacho hata iwapo utapa maksi nyingi na kuwashinda watu wote Darasani lakini Bado utakuwa umeshindwa uwezo na kipimo chako sio unashindana na mtu gani bali unawezo kiasi gani.

Mara Nyingi inakuwa kichekesho kwenye maisha ya familia yenye malezi ya watoto.Mara nyingi jamii na familia zetu zimetumia jamii kama kipimo cha malezi na tabia za watoto wao.Ulezi wa mtoto hautegemei mtoto mwingine analelewa vipi.Mzazi ndie mwenye picha halisi ya mtoto wake anapaswa awe namna gani na sio mtu mwingine.Wakati wewe unaona mtoto wako ni Bora ukimpeleka kwenye familia nyingine aishi kuna makosa mabayo ataonekana nayo kwa sababu vipimo ni vya aina mbili tofauti lakini akija kwako utaona nyumbani utaona ni bora na mwenye kukupa furaha.Jamii hawezi kukuamulia uzuri wa mtoto na ubaya wake.Mzazi ndio mwenye kujua uzuri na ubaya wa mtoto.Mwenye kutoa guidelines za malezi na Baba na Mama na Sio Jamii.Jamii wao huona mtokeo ya kazi iliyofanywa na Wazazi.Iwapo mtoto wako Unaona ana Uwezo wa Kufanya vizuri zaidi kuliko wengine na akafnya chini ya kiwango,Hata kama atakuwa amewazidi watoto wengine bado atakuwa ameshindwa.......

Mwisho wa Siku Napenda Kusema kila Maji yana Mkondo Wake....Unapojaribu Kuwa mwingine mwisho wa siku Hautafikia Mafanikio Yako ya Kimaisha Bali utaishia Kufikia mafaniko ya wengine ambayo hayatakupa furaha ya kweli...Kumbuka Maji yajitahidi Kulowesha na Wala Moto Haujitahidi Kuunguza Na Mvua Haijihidi Kunyesha bali Ikinyesha ndipo uwezo wake...Ishi Wewe Mwenyewe Halisi ufurahie maisha yako..mwenyewe.
Wahenga Wa Nchi ya Upare Yaani Kwa Maana ya Wapare walisema...Mkodeka Sunga Henacho Evwene Kwa Maana nyingine Hakuna Mtu anayeinama Kuchungulia Uvunguni Kama Hakuna Alichokiona.Yaani Mtu anayechungulia Uvunguni Kuna Jambo ambalo ameliona Lina manafua kwake au Kwa Mwingine.Leo Kwenye Nazungumza Moyoni.. Tunaanza Hapa.Tanzania Yetu Imejulikana kama Kisiwa Cha Amani lakini Ki-Ukweli Ni Kisiwa Cha Utulivu ni Heri Ya Utulivu kuliko Kuukosa hata huo Utulivu ,Maana Wahenga Wanaendelea kusema Heri Nusu Shari Kuliko Shari Kamili.Pamoja na Kukosa Amani ya Kweli kwenye Nchi Yetu Hata Huu utulivu Unatutosha kwa Kiasi Fulani.Huu Utulivu unapotoweka ndipo Tunajiuliza nini kimetokea?
Miaka ya 1950's Kulikuwa na Wimbi Kubwa la Nchi za Kiafrika Kuanza Kupigania Uhuru wa Nchi za Kiafrika Ambao tuliuhitaji sana kuweza kujitawala na kujiendesha bila kuingiliwa kwenye kile tunachoamua kukifanya kwa manufaa ya nchi zetu.Mashujaa Mbali Mbali waliibuka na kuamua kujitolea kupigania Uhuru Wa Nchi Hizi.Mpaka Mwisho Mwa Miaka Ya 1980 Karibia Nchi zote za Kiafrika Zilikuwa Zimeshapata Uhuru wa Ki-Utawala zikiwa zimebaki Chache.Sahara ya Magharibi ilikuwa Bado haijapata Uhuru wake,Huku Afrika ya Kusini Kukiwa Kunaendelea Mapambano ya Vita dhidi ya Ubaguzi wa Rangi.Mwaka 1994 Ndipo Raisi wa Kwanza Mweusi Anafanikiwa Kunyakua Madaraka Baada ya Mapambano ya Muda Mrefu.

Baada ya Miaka Takribani 50 ya Uhuru wa Bara Hili baada lindi la Umaskini limekuwa kubwa na Bado Linaendelea kuongezeka kwa kiasi Kikubwa.Kumbuka Miaka 50 iliyopita kuna watu walijitoa kwa nguvu na kwa jasho pia na kwa Uhai wao ili kuweza kupata Uhuru wa Katika Siasa,Uchumi na Jamii.
Baada ya Kizazi Kile cha Ukombozi kupita,kimeibuka kizazi ambacho ni cha Ulafi na Kutokujali wengine huku watu wachache wakiendelea kujilimbikizia mali na kuwa fanya wengine kuendelea kubaki maskini.

Miaka ya Karibuni Kumekuwa na fujo katika Bara hili la Afrika Kutoka pande zote za Bara hili juu ya unyonyaji na utawala mbovu ambao umeendelea kujikita kwenye nchi Mbali mbali za Afrika Huku Viongozi wa Nchi hizo wakiendelea kuwa madikteta na Rasimu hata pale ambapo wanapoona wameshindwa kuongoza nchi zao.

Tanzania yangu ni Moja ya Sehemu Ya Bara Hili,Baada ya Miaka 50 ya Uhuru.Hakuna Nafuu ya Kimaisha,Kiuchumi na Kijamii.Utawala Mbovu Ndio Imekuwa shida katika nchi hii Yetu ya Tanzania.Badaa ya Kujiuliza Maswali Kadha wa Kadha Bado Jibu limekuwa tata.Moja Ya Swali ambalo limekuwa halina majibu ni Hili Imekuwaje Raia ambao walikuwa watiifu wa Serikali yao,Wamegeuka kuwa waasi tena wa Serikali Yao?

CCM ndio Chama Tawala Katika Nchi Hii,Inakuwaje Wananchi Walio Wengi Wanageukia Chama Cha Upinzani Yaani Chadema..Jibu Ni Kwamba Kuna Majibu ya Maswali Mengi hajajibiwa ..Miaka Hamsini Baada ya Uhuru Bado tatizo la Ukoloni Limeendelea kwenye Jamii hii ya Watanzania Unaweza Usiwe Ukoloni wa Nguvu Bali Ukoloni wa Fikra wa watu wachache kuelekea UMMA wa Raia Walio Wengi.

Baada ya CCM kushindwa kutoa Majibu ya Maswali Mengi,Wananchi hawa wameendelea Kukiunga Chama Cha Upinzani Mkono Baada ya Matumaini Kuendelea kupotea.Miaka ya Karibuni Tumeshuhudia Fujo Nchini Kenya,Chanzo Cha Fujo Hizi ni Kiwango Kikubwa Cha Umaskini Kati ya Watawala na watawaliwa.Na Hakuna Jitihada zinazochukuliwa kuondoa Tatizo hili.

Ukona raia  Wanaasi Chama Tawala Tambua Kuna Jambo ambalo wameliona Upande wa Pili liwe zuri au Liwe baya....Mkodeka Sunga Henacho Evwene....Hakuna Mtu anayependa Kuonewa na Kunyanyaswa kwenye nchi yake..Juzi juzi Tumesikia Fujo Mtwara Leo Arusha Kesho tutasikia Mbeya,Wiki Nyingine Tutasikia Dar...Kinachonitia Shaka Watawala hawana habari juu yanayoendelea au wameyaona wanayafungia macho.Chuki inayojengeka miungoni mwa kizazi Cha Sasa itaigharimu Serikali kwenye Siku Ya kesho.Siasa za Maji taka na Ujinga Ndio Zinazolipeleka Taifa hili Kusiko eleweka.Ukosefu wa Ujuzi na Akili juu ya Kuendesha Nchi na Badala yake kuendelea kutumia Mabavu kunatengeneza Kizazi ambacho ni Sugu na Ambacho Hakitasikiliza Utawala Tena.Hata Uasi kwenye Nchi Nyingi za Afrika zinazopigana Vita Leo Ulinza Hivi.

Rai Yangu kwa Utawala Akili zakuendesha nchi na Kusoma Nyakati zinahitajika sana kuliko Kutumia Nguvu Nyingi.Nchi Ikifanikiwa Sifa Ni Kwa Utawala na Nchi ikianguka Lawama Kwa Utawala.
Ukiona Watoto wako Wanakimbilia Nyumba ya Jirani Kutafuta Hifadhi Tambua Nyumbani Kwako Kuna Shida Tatua Shida ya Nyumbani Kwako Kwanza ndipo uwafwate watoto wako kwa Jirani

............Mkodeka Sunga Henacho Evwene.......................


Huku Kuabudu wageni sijui Kutaisha lini,Tunawafukuza na kuharibu maisha ya raia wetu Kwa Kipindi cha Ugeni wa Muda Mfupi.Tunasahau Wageni hao wakiondoka ,Raia tuliowafukuza maeneo yao ya kujipatia kipato ndio tunaobaki nao.Tunatengeneza chuki ya daima kwenye mioyo ya watu kwa ugeni wa mtu wa siku Mbili.Fikiria Je wewe watoto wako wageni wakija Nyumbani,Unawalaza njaa na kwenye sakafu kisa mgeni kaja? Au wewe unafanyaje....Ndivyo Sivyo ni Ndivyo Si Vyo......Karibu ya Muuza Mgahawa haimanishi Chakula Utakula Bure....Ndivyo Sivyo

Katuni...Kwa Hisani ya Masoud
Ni rahisi mtu tajiri akifilisika kurudi kuwa tajiri,kuliko mtu Maskini Kuwa Tajiri.Matumizi ya Rasilimali ambazo tumepewa hapa Duniani ni Kitu Muhimu sana.Kuna Aina Nyingi za Rasilimali kwenye Kufiki Hatma ya Maendeleo ambayo tunayataka.Mungu alipotuwuweka hapa duniani alitupa uwezo na akili tuweze kushikiana pamoja naye katika uumbaji wa Nchi hii Ndio maana alipotuumba alituweka rasimali ghafi(Raw Materials) Badala ya Kututengenezea kila Kitu.Mungu hakushindwa kutengeneza maghorofa au Vitu vingine tunavyovihaji kisha akauweka tufurahie maisha yetu lakini Badala yake aliona tutaboreka hapa kwenye sayari hii.Fikiria Tangu unazaliwa Mpaka una kufa yaania mwaka Mmoja Hadi Sabini Kazi Yako iwe Kula Kulala hakuna Kingine cha Kufanya ungejisikiaje?

Hakuna Mtu ambaye aliumbwa na Mungu Hapa Duniani Kwa Bahati Mbaya,Tulichotofautiana ni Mazingira Tuu Ya Utungwaji Mimba na Eneo La Kuzaliwa Lakini Mwisho wa Siku Wote Tuko Hapa kwenye Sayari hii.Mfano Samaki aliyevuliwa Kwa Baruti,Nyavu na Mtego Wote Wamevuliwa na Wote Tunawakuta sokoni,Yaani Mwisho Wa Siku tunawakuta kwenye tenga la mvuvi.Mungu Hakoseagi kuumba wala Kupanga.Kila Alichokiumba ni Bora na tena kina Uwezo Kamili na Kinaweza Kuishi Kulingana na Mipango na Mazingira aliyokitengenezea.Kusema Umeumbwa kwa Bahati Mbaya ni Kumtukana aliyekuumba.

Mungu alipomuumba Mwanadamu Aliweka Rasilimali ambazo zitamtosheleza Mpaka Mwisho wa Uhai wake.Mpaka Sasa Duniani ina Takribani watu karibia Bilioni 8 lakini Hakuna Siku Umesikia Dunia imejaa mpaka watu wakakosa pa kukaa.Kama Haiwezi Kujaa Basi hata Rasimali za Kutufanya tuishi zipo na zinatutosha bila hata mmoja kupunjika,Akili yako Ionavyo ndivyo Utakavyokuwa.Mungu ameweka Namna ya Ajabu ambayo Inatutofautisha sisi na viumbe wengine.Viumbe Wengine Hufikiri Kula,Kalala Kuzaliana na Kufa lakini binadamu Tumekuwa na uwezo wa kufikiria zaidi ya Hapo.Je tunafanyanye kwenda zaidi ya hapo.Ukiona wewe unafikiria Kula,Kulala,Kuzaliana na Kufaa hauna tofauti na Mnyama Mwingine yeyote bali unapofikiria zaidi ya hapo ndipo tofauti yako na wanyama wengine inaoonekana.

Wakati tukiwa tumepewa uwezo wa kuzitumia rasilimali zlizopo kwenye sayari yetu na hatuzitumii na kama kujaribu kufanya Pengo Lionekane Kama Mwanya.Unapojilazimisha kuishi maisha yasiyo yako ni sawa na kujaribu Kulifanya Pengo la Mdomoni Linonekane kuwa Mwanya ili Hali Pengo ni jino Limeng'olewa na Mwanya ni Nafasi ambayo ipo yenyewe imetokanama na uasili wa maumbile ya Mdomo.Mungu alijua Kabisa utahitaji Kitu fulani wakati unaishi Hapa kwenye sayari ndio Maana akakuwekea na Mazingira ya Kukipata.Akili ulio nayo ndio Muujiza wako ndio Utajiri wako.Tutumie Fursa ambazo zipo kuweza kujiletea maendeleo tuache kuleta vingizio visivyo na Maana.

Wakati Unaumbwa hakuna mtu ambaye alipewa wajibu wa kukufanya wewe uendelee mbele bali wewe ndio unapaswa kujiendeleza.Hakuna sehemu yeyote kwenye kitabu chochote cha Dini ambacho Kimeandikwa Ukishazaliwa Utaikuta Serikali Na Serikali Itakufanya Ufikie Malengo yako ya Kimaisha kwa Kuitegemea.je iwapo Kusingekuwa na Serikali Ungemlaumu Nani?Tufanye kwanza kwa Sehemu Yetu ndipo tuwatupie lawama wengine.Tusianze kulaumu ili hali hata hatua moja haujapiga.

Ukiamua Kufikia Malengo fulani ya Kimaisha utafikia tu ku-amua kufikia Malengo haya inategemea kiasi gani umejipanga kufikia malengo yako.Fursa Zipo na Zitaendelea kuwepo hazitaisha siku zote za Maisha Yetu.Tulizikuta na Tutaziacha kinachopaswa ni wewe binafsi kusimama na kutetea hatma yako binafsi na kwa kufanya maamuzi sahihi.Maamuzi ndio yanayotofautisha watu wote.
Ubongo wa Mwanadamu ni Mithili Ya Hardaware ya Computer na Taarifa zinazoingia kwenye Ubongo Ni Mithili ya Operating System inayokuwa-installed kwenye Ubongo.Unapoona Computer Haifanyi kazi Vizuri nenda kaangalie Hiyo Operating System iliyokuwa Installed ni Sahihi..Unawez Ukakuta Computer yako inahitaji Windows 94 wewe unailazimisha Window 8 na Ubuntu Kitu ambacho hakipo.Ukitaka Matokea mazuri ya Computer Ifanye kazi Tafuta Recommended Operating System ndio U-Install  kwenye Computer yako Hai kadhali Kwenye Ubongo ndivyo kulivyo tafuta Proper Information Ndio Uweke kwenye Ubongo wako ili kuweza kupata Matokeo Thabiti na sahihi ya Kile unachokihitaji.

Kwenye Uhalisia Wa Fikra Hakuna Mtu ambaye hana Ajira ila Wapo watu ambao hawataki Kuajiriwa.Tumezoeshwa Formal Way ya Kuajiriwa yaani kwenda ofisini na Kurudi,Lakini Kuna namna nyingi za ajira mbona kuna Watu Wanamewekeza kwenye Hisa za Makampuni na bado wanapata kipato chao halali cha fedha na Maisha yanaenda na Huku wakiendelea kufanya vitu vingine.Tusijaribu Kutafuta visingizio visivyi na maana kwa kuwabebesha wengine mizigo yetu wenyewe.Kutokuendelea kwako ni Uamuzi wako Mwenyewe...

Pengo Si Mwana na Mwanya Si Pengo....
V.Jina Kamili: 
Äteritsiputeritsipuolilautatsijänkä (Herufi 35 )
Nchi:Finland
Lugha ya Eneo Husika:
Lahaja za Kaskazini Mwa Finland
Taarifa Fupi:
Jina Refu Zaidi la Sehemu nchini Finland
  
IV.Jina Kamili:
Tweebuffelsmeteenskootmorsdoodgeskietfontein (Herufi 44)
Nchi: Afrika Kusini
Lugha ya Eneo Husika: 
Lugha za Asili
Taarifa Fupi:
Jina Refu Zaidi la Sehemu Nchini Afrika Kusini
  
III.Jina Kamili
Llanfairpwllgwyngyllgogerychwyrndrobwllllantysiliogogogoch
 (Herufi 51 )
Kifupi Cha Jina
Llanfairpg (Herufi 10 )
Nchi:Wiles
Taarifa Fupi:
Jina Refu Zaidi la Sehemu Barani Ulaya na Nchi Ya Wiles

II.Jina Kamili
Taumatawhakatangjjihangakoauauotamateaturipukakapikimaungahoronukupokaiwhenuakitanatahu. (Herufi 85)
Kifupi Cha Jina:
Taumatawhakatangihangakoauauotamateapokaiwhenuakitanatahu.(Herufi 57 )
Nchi:New Zealand
Taarifa Fupi:
Jina Refu Zaidi la Sehemu nchini New Zealand



I.Jina Kamili
Krung­thep­maha­nakorn­amorn­ratana­kosin­mahintar­ayutthay­amaha­dilok­phop­noppa­ratrajathani­burirom­udom­rajaniwes­mahasat­harn­amorn­phimarn­avatarn­sathit­sakkattiya­visanukamprasit.(Herufi 163)
Kifupi cha Jina:
Krungthep(Herufi 9) 
Nchi:Thailand
Lugha ya Eneo:Ki-Thailand
Taarifa Fupi:
Jina Refu la Sehemu Nchini Thailand na Duniani kwa Sasa
Maisha ya mwanadamu yamejengwa katinga msingi wa uwajibikaji wa mtu binafsi kwenye maswala mbali mbali ambayo tunakutana nayo kila siku kwenye maisha yetu.Bila uwajibikaji a kuchukua hatua kwenye kila jambo na kuwa watendaji kwenye kile tunachokiamini ni sawa na kupigia mbuzi gitaa ukitegemea acheze,Wahenga walisema Kuwa Ukitwanga PiliPili kwenye Kinu Mshahara wake ni Kukohoa,Kwa Maana nyingine kile anachopanda mtu ndicho anachovuna mtu.Ukipanda maisha ya kulaumu kwa makosa na changamoto mbali mbali kwenye maisha unayokutana nayo hakukufikishi kokote,mwisho wa siku utaishia kuvuna lawama na malalamiko.

Maisha yetu ya jamii na utendaji wetu wa kila siku tumeyajenga kwenye kulaumu chanzo cha tatizo zaidi badala ya kutumia muda mrefu kujadili sulihisho la tatizo.Utamaduni wa kulaumu kwenye maisha ya mtanzania ni kama uji na mgonjwa.Mara zote tunashindwa kuweza kutafuta suluhisho wa tatizo na changamoto tunazokumbana nazo.

Siku za Karibuni tumepatwa na Kifo Cha Mwanamuzi wa Bongo Fleva Anyejulikana kwa Jina la Albert Magwair.Baada ya Kifo chake kutokea Watu wametumia Muda Mrefu kukilaumu kwamba Kituo Fulani cha Radio ndio Kimesababisha Kifo chake,Baada ya Kusoma Report ya Madaktari ambayo imekuwa ikisambazwa kwenye mitandao Mbali Mbali Imekujulikana Kwamba Ndugu yetu alikufa kutokana na Uchovu na Matumivi ya Vilevi na Dawa Za Kulevya Baada ya Mwili wake kufanyiwa Uchunguzi(Habari Zisizo Rasmi).Nikajiuliza Je  Kituo hiki Ndio Kilimtuma atumie Vilevi na Madawa ya Kulevya.Je Kama Kituo Hiki kilimnyonya na Kusabishia Msongo Wa Mawazo Kwanini Yeye Binafsi asingetafuta njia Mbadala ya Kujinasua Kwenye Jambo hili la Kunyonywa?Kuna Mengi Sana.Lakini Baada ya tukio la Kifo kutokea Je hawa wengine waliobaki ambao wengine ni waathirika wa Matumizi ya Madawa ya Kulevya na Vilevi tunawasaidiaje?Malaumu hayasaidii.Tunapaswa kutafuta suluhisho la kudumu juu ya matatizo yetu Binafsi yanayotukabili badala ya Kutupia wengine lawama.

Mtu binafsi ndiye Suluhisho la Matatizo na Changamoto zake Binafsi,Hakuna mtu anayeweza kusimamia kukusaidia kuleta utatuzi wa changamoto zako binafsi.Unapolaumu wengine na wao wankulaumu pia kwa uzembe ulioufanya.

Wewe binafsi ndio unaweza kusimama na kuweza kutafuta suluhisho la kudumu kwenye kila kunachokukabili kwenye kila hali maishani mwako.Muda Mwingi wa lawama na malaumu hausaidii.Mara nyingi tumekutana na mfano wa Kesi za Mama wa Kambo na Watoto wa Kambo.Watoto hawa wa tumewajengea uwezo mkubwa wa kuwalaumu wamama ambao wanawalea na kuwafanya waonekane wabaya.Pamoja na Changamoto wanazokutana nazo tulipaswa kwajengea uwezo wa kupambana na changamoto wanazokutana nazo badala ya kuwajengea uwezo wa kulaumu.Kumbuka hata wakiwa watoto ipo siku Moja watakuwa watu wazima je hapo wataendelea kuwalaumu Mama zao wa Kambo .hapana.Hapa ndipo watapaswa kujisimamia wenyewe kwa majukumu yao ya kimaisha.Suluhisho la Mtu na Changamoto ni Mtu Mwenyewe na Sio Lawama.

Shangazi yangu siku Moja alinieleza kwamba mara nyingi watu ambao wengi ni wepesi wa kulaumu basi hata utendaji wao na maisha yao ni ya kubahatisha.Ni Rahisi kuilaumu Serikali Yetu haitupi fursa za maendeleo lakini cha kushangaza kuna watu wanaendelea je hawa wanaendeleaje?Je wao wana Mabawa au Wao ni Super Human?

Maisha ya Maendeleo ya Jamii Ni Watu wenyewe,Serikali yoyote duniani unayoiona ni Taswira ya Wananchi wake.Kuishutumu Serikali Kwenye Miasha yetu mabovu ya kila siku ni Kama kujaribu Kupigana na Kivuli Chako Mwenyewe.Unapoona Ubabaishaji kwenye Serikali,Tafuta Muda uangalie utendaji wa maisha ya Wananchi wake wa kila siku,ndipo utagundua serikali na wananchi wake hawatofautiani kwenye maswala mbali mbali.Kumbuka Serikali ni Watu na Iliwekwa na Watu.Kuendelea kulaumu hakusaidi.Dawa ni Kutafuta Suluhisho kile kinachotukabili kwenye maisha yetu ya kila Siku.Tutumie Muda mwingi kufikria kitu gani tunapaswa kuwa nacho maishani mwetu badala ya kulaumu kusiko na sababu za msingi.Sisi  tuwajibike kwanza ndipo tutafute mengine.

Wakati unatumia muda mwingi kulaumu kwenye tatizo ulilo nalo Wengine wanatumia fursa za lawama zako kuendelea.

Wakati wewe unaona lawama ndio suluhisho la maisha yako ndipo wenye akili wanapokaa chini na kusaidia kutafuta sulusho ya lawama zako na mwisho wa siku suluhisho la mtu mwingine kwako huwa la Muda tu sababu hajui ni haswa unahitaji maishani mwako,Suluhisho la kudumu lipo Ndani yako,Na watu wanapoendelea kutafuta suluhisho zaidi juu ya tatizo lako kwenye maisha yako ya lawama siku zote utaendelea kuwa mtumwa kwao,maana utatumia nguvu nyingi na gharama kubwa kuweza kupata suluhisho la Muda la mtu mwingine kwenye maisha yako.Kuchukua kutumia suluhisho la Mtu Mwingine kwenye maisha yako ni kama kujaribu Kuiba Kivuli cha Jirani yako Kisha Ukitegemea kifwanane na wewe na kikutoshe.

Mwisho wa Siku wakati Lawama zako zinaendelea kwa watu wengine Maisha Bado yanaendelea kila siku na Watu wanafanikiwa kwenye ndoto zao kwa Kukufanya mtumwa wa kutumumikia ndoto zao.Kufa kwa Imamu Sio Mwisho wa Ibada,Maisha yanaendelea na kazi zinaedelea na Ujenzi wa Fikra Huru na za Haki Unaendelea.Unapoendelea kulaumu hata siku zako za kuishi zinakuwa chache maana utayatumikia matatizo badala ya kutumikia Kufurahia maisha ambayo wewe binafsi ndio jibu la Maisha yako.
Nikiwa nimeamka Siku ya Tarehe 1/1/1994,Mama aliniambia Hata sisi tuliwahi kuwa kama wewe ulivyo.Wakati maneno hayo yanasemwa sikuelewa yana maana gani,Maana sikuwahi kufafanuliwa ila niliona siku zikienda na zikisogea mbele,Mara nikajikuta namaliza Level Moja Ya Elimu huku nikienda Nyingine na Mara Elimu Ya Juu.Naam Muda unaenda na Muda haurudi.Kufanya malengo yoyote bila kuwa na mipaka ya muda bado hauwezi kufikia lengo.Hakuna Lengo Lisilokwenda na Muda.

Jamii yetu ya Kitanzania imelelewa kuishi kwamba kesho ipo tu,Lakini cha kushangaza hatufikirii kama hiyo kesho sio yetu maana hakuna kilicho na uhakika wa kuiona Kesho hiyo.

Baada ya Kusoma Kidogo..Zamani tukiwa tunakuwa Shule za Msingi Tulikuwa tunafundishwa kumeza Nyakati Mbali Mbali za Sentensi kwa Kingereza Yaani Tenses,Kwa Mara ya Kwanza Nilisikia Kitu Kinaitwa Future Tense Mwaka 1996,Niliimeza Baada Ya Miaka Michache Kupita Kuna Siku Nikajiuliza Ivi Kuna Future Tense au ni Future Time na Hiyo Future Time or Future Tense Zinatoka wapi....Ingawa sikuwa na Uelewa Mpana,Baada ya kufwatilia nilikuja kupata Ufumbuzi kwamba Hakuna Future Tme wala Future Tense...Wewe Binafsi Ndio Future Tense na Future Tense....Fikiria kama wewe ukiwa Haupo Je kuna kuwa na future Tense au Future Time??

Dunia ya Kwanza yaani Naamanisha Nchi zilizoendelea Muda kwao ni Muhimu wanafanya Kila liwezekanalo kuweza kuokoa Muda ili kuweza kufikia malengo wanayojiwekea,Kuanzia kwenye usafiri na Utendaji wao wa shughuli za kila siku.Kuna wakati unajiuliza Kama unakaa kwenye Foleni ya Gari Masaa Matatu na Unapokwenda Ukitumia Mguu hayazidi hata Masaa Mawili kwanini usichague kutembea???Kizazi chetu kina Excuse nyingi....Utasikia Jua kali,Je wazazi wetu hawakuliona Jua?Au Sisi Ndio Ngozi Zetu zina ukakasi kuliko wao?Swali la kujiuliza??Maisha yetu hapa duniani yamefungwa kwenye Muda,yaani Unapochezea Muda ndio Unachezea maisha yako Pia.


Unapochezea Muda Unachezea Maisha yako pia,Ni ngumu kumshauri mtu aliyezoea kuishi kwenye maisha yasiyozingatia Muda,Ukimwambia Utasikia "No Hurry In Africa".Mtu huyu akikwama juu ya jambo fulani ukimwambia jambo hili ulipaswa ufanye miaka mitano iliyopita ananza kutoa macho,Sasa unabaki unajiuliza huyu vipi,Tangu tunakuwa kuna watu hawaendi mbele wala hawarudi Nyuma yaani wapo wapo,Ukimwambia na Ukimshauri Utasikia Sisi Tumeliona Jua Kabla yako.Kumbuka Kila unachofanya Hapa duniani kina mwisho wake kama kilikuwa kina mwanzo basi mwisho Upo.

Unapochezea Muda Pia na Hata Resources nazo Zinapotea.Fikiria Mfano wewe ndio Mchezaji Mpira,Mwili wako ndio Resources moja wapo ya kutumia ili kukuwezesha kufikia malengo fulani kwenye maisha yako.Kumbuka kadri unavyokuwa mtu mzima Resources hiyo inazeeka na mwishowe kuchakaa na kutokuweza kutumika tena na kama itatumika sio katika kiwango husika kwenye maisha yako.Fikiria wewe ni mwimbaji Sauti yako ndio resources yako ,Je unafikiri Unavyoweza kuimba leo na Ndani ya Miaka 30 ijayo utaweza kuimba hivyo hivyooo???Anayekupotezea Muda,Anakipotezea Malengo.

Mwisho wa Siku Nashaangaa yaani mtu kazunguka huko katafuta cha kufanya kakosa anakuja kwako anakuambia twende mahali fulani,Ukifika Kule mahali utasikia twende mahali kwingine,Mwisho siku unamaliza siku nzima umechoka una umetumia muda wako kuzurura barabarani bila kufanya kitu cha maana unapoona kuna vitu vunaweza poteza muda wako kataa kuvilea,Badilisha mfumo wa maisha.Kumbuka hakuna wakati ujao,Wakati Ujao ni sasa na Wakati Ujao ni Wewe.Usifikirie ya Kesho wakati ya Leo Haujayamaliza.

Maisha Yetu Yamefungwa katika Muda,Baada ya Muda fulani unapaswa uwe umefanya jambo fulani,Ndio maana kwa sisi mabachela mtu akifika hadi Miaka 40 hajaoa watu wanajiuliza kwanini hajaoa,Tatizo sio Kuoa tatizo ni muda wa kuoa.Zingatia Muda wako kwenye Kila jambo Maana Muda ni Wewe na Wewe ni Muda.

...Punch Of The Week..............Anayepoteza Muda,Anapoteza Malengo

Mara nyingine katika Punch Of The Week Tunaendelea kuangalia Mada Mtambuko na Zinazotuzunguka kwenye maisha yetu ya Kila Siku....Naam...Leo Tunaangalia Mada inayosema Watu Hawasemi Lakini Wanaambiana.

Mara Nyingi kwenye maisha yetu ya kila siku tumeona watu wanakuwa wanatunyamazia kwa nama moja au nyingine kuhusu swala/jambo fulani linalokuhusu wewe binafsi ili hali wewe ukifikiri wako kimiya,ukweli ni kwamba watu hawasemi tu lakini wanaambiana kuhusu wewe na kila jambo unalolifanya kwenye maisha yako ya kila siku.Mara nyingi kuna mambo mengi yanaweza kuwa yanajadiliwa kuhusu wewe lakini hauwezi jua maana hakuna anayekumbia.Tambua kila unachofanya kwenye maisha yako ya kila siku watu wanaambiana hata kama kiwe kizuri au kibaya unachofanya,kiwe cha kupendeza au cha kuchukiza lakini wataambiana tu.

Mara chache sana watu wanakaa kuzungumza habari za mafanikio ya mtu namna mtu anavyopiga hatua kwenye maisha yake kwenye nyanja mbali mbali na kuweza kufanikiwa kuanzia kwenye Imani,Kiuchumi,Kisiasa na hata kijamii pia.Watu wengi wanapokaa pamoja mara nyingi huongea mambo ambayo sa nyingine yanaweza yasikufurahishe ukiyasikia lakini ndivyo watu walivyo.Ni ngumu kuyasikia maana hawakwambia.Tambua kila jambo unalolifanya kwenye maisha yako ya kila siku unaweza ona watu wamekufungia mdomo na kama hawako na wewe lakini jua ni moto wa kuotea mbali.Hakikisha kila hatua na jambo unalolifanya hakikisha unalifanya kwa usahihi na umakini mkubwa hata iwapo watu hawakuoni.Wanaweza kujifanya hawakoni lakini kiukweli wanakutazama tu wanagojea wakutane na watu wengine ambao wako kama wao na waanze kuzungumza bila ya wewe kujua.

Mara nyingi Habari Mbaya za Mtu husambaa mapema zaidi kuliko nzuri.Mwana saikolojia mmoja alisema Binadamu kwa Asili ni Wachoyo na Walafi yaani hawapendi kuona mwingine anafanikiwa kwenye jambo fulani kwenye maisha yake.Yuko tayari kuharibu kwa kusema mabaya yako hata kama hayana ukweli ili mradi akuharibie maisha yako.Ki-Ukweli wewe unawez ukawa unatembea njia na kuona hamna shida na unacheka na wengine lakini Watu hawasemi Tu ila wanazungumza kwa muda wao wanaoujua zaidi.Je umeshawahi kujiuliza,je kama ungepewa nafasi ya kusikiza maongeze ya watu kwenye simu pale TCRA ya 
kil siku unahisi ukijisikiaje??Watu hawasemi Lakini Wanaambiana.Makosa ya mtu huonekana zaidi kuliko uzuri wa mtu,Waswahili wanasema Baya moja Hufuta Wema 1000 ulioutenda.Ni rahisi kusemwa ubaya wako kuliko uzuri wako Maana kwa asili binadamu ni Wabaya kama Alivyosema mwanasaikolojia.

Mwisho Napenda Kusema imekupasa kuwa makini namna unavyojiwakilisha mbele ya watu,awe mtu wako wakaribu unayemwamini au usiyemwamini ni muhimu kuchukua tahadhari mapema.Fanya maswala yako kwa uminifu ili hali kama ungetamani wengine wakufanyie hata iwapo watu hawakuoni.Make Sure haufanyi vitu kwa ujinga,fanya kwa umakini huenda wanajifanya hawakuoni lakini wanakuona.Fanya kwa kiwango cha Juu lakini pale ambapo unaona umefika mwisho acha,Jitahidi kuweka juhudi kwenye kila jambo unalolifanya na kwa umakini mkubwa sana.Watu hawasemi lakini Wanaambiaana...


..................Watu Hawasemi Lakini Wanaambiana.............................