Kila Maji Yana Mkondo Wake,Wahenga Walisema.Ubora wa Kitu hautegemeani na Mlinganyo wa Kitu Kimoja Na Kingine.Muda mwingi tumeshindwa kufikia malengo yetu na kukata tamaa baada ya kujilinganisha na wengine huku tukijiona sisi ni Dhaifu.Katika kila ndani ya mtu mmoja kuna upekee ambao mtu mwingine hana ndio maana kwenye maisha kuna furaha ya kufurahia maisha.Fikiria iwapo wote tungekuwa tunawaza na kufanya vitu kwa matazamo mmoja maisha yangekuwa yanaboa na tungekuwa hatuna tofauti na maroboti maana ladha ya maisha isingekuwepo.Jamii yetu na kizazi chetu tumekuwa na watu feki zaidi kuliko watu halisia kama zilivyo bidhaa.Hatuwezi Kufwanana kwa kila jambo inagawa kuna vitu hatuwezi kupishana sana.Maisha yasiyo na uhalisia ni kama kujaribu kujaribu kuiga finger print ya mtu mwingine ili hali tunajua utapatia lakini hauwezi kufwana kwa kila kitu.Kwanini uwe nakala ya Mtu mwingine wakati wewe pekee ni nakala yako binafsi tosha.Kwanini Usitamani wengine wawe nakala yako baadala ya wewe kuwa nakala ya mtu mwingine?

Ujenzi wa maisha yenye kudhubutu na kufanya kile ambacho ni halisi huanza ndani mwa mtu hakuna kitu ambacho kinatokea hewani mithili ya mwanga wa jua kila asubuhi.Ujenzi wa tabia ya mtu ya ndani ndio mwanzo wa kila jambo kwenye  maisha.Hakuna mtu anayepaswa kukutengenezea ndoto maishani mwako bali wewe ndio unapaswa kujenga ndoto yako maishani mwako.Watu wengine wa nje wanapaswa kukusaidia kukuongoza na kukupa hekima ya namna ya kufika ndoto zako na si kukujengea ndoto zao ambazo zinatakuwa zinaisha ndani yako huku ndoto yako halisi ukiwa umeifukia chini.Ndoto yako maishani ndio furaha yako.Ukivaa kiatu cha kuazima ipo siku utakirudisha tu,Ni bora uvae cha kwako ambacho utakuwa nacho huru na utafurahia daima.

Watu wengine sio kipimo halisi cha Ndoto zako kwa sababu mwenye picha halisi ya ndoto zako ni wewe na sio mtu mwingine .Unapojaribu kujilinganisha na wengine ni kujaribu kuishi ndoto zao.Maisha halisi ya mtu ni mtu mwenyewe.Wakati unaanza kufukiria Kichwani mwako hakuna mtu amabaye alikuwa kichwani mwako.Ubora wa ndoto na Uhalisia wa ndoto unao wewe kichwani na sio mtu mwingine.Ukifwata watu wengine watasaidia kukatisha tamaa kwa sababu kuna sehemu fulani ya maisha yao walishindwa au wao ndio mwisho wa ndoto zao.Vipimo vya ndoto zao ndipo zilipoishia hapo.T.B.S huweka kiwango cha chini cha Bidhaa kuwa na ubora fulani lakini haimaishi kwamba hauwezi kutengeneza bidhaa ambayo ina ubora zaidi ya viwango walivyoweka.

Mafanikio yako kwenye maisha hayategemei kuna wengine wamefanikiwa kiasi gani.Picha halisi ya mafanikio unayoyataka unayo wewe ndani yako na sio kwa mtu mwingine.Unaweza kuona mtu mwingine amefanikiwa maishani lakini ukilinganisha na ndoto ulizokuwa nazo na kipimo cha kiwango chako inawezekana yupo chini ya kiwango cha kipimo cha mafanikio yako.Wewe binafsi ndio kipimo halisi ya kile unachopaswa kukifikia.Iwapo una uwezo wa kupata maksi 100 kwenye mtihani na ukapata 90 bado wewe umeshindwa kufikia mafanikio sababu uwezo wa kupata 100 uliokuwa nao na kipimo cha mafanikio yako wewe ndio unacho hata iwapo utapa maksi nyingi na kuwashinda watu wote Darasani lakini Bado utakuwa umeshindwa uwezo na kipimo chako sio unashindana na mtu gani bali unawezo kiasi gani.

Mara Nyingi inakuwa kichekesho kwenye maisha ya familia yenye malezi ya watoto.Mara nyingi jamii na familia zetu zimetumia jamii kama kipimo cha malezi na tabia za watoto wao.Ulezi wa mtoto hautegemei mtoto mwingine analelewa vipi.Mzazi ndie mwenye picha halisi ya mtoto wake anapaswa awe namna gani na sio mtu mwingine.Wakati wewe unaona mtoto wako ni Bora ukimpeleka kwenye familia nyingine aishi kuna makosa mabayo ataonekana nayo kwa sababu vipimo ni vya aina mbili tofauti lakini akija kwako utaona nyumbani utaona ni bora na mwenye kukupa furaha.Jamii hawezi kukuamulia uzuri wa mtoto na ubaya wake.Mzazi ndio mwenye kujua uzuri na ubaya wa mtoto.Mwenye kutoa guidelines za malezi na Baba na Mama na Sio Jamii.Jamii wao huona mtokeo ya kazi iliyofanywa na Wazazi.Iwapo mtoto wako Unaona ana Uwezo wa Kufanya vizuri zaidi kuliko wengine na akafnya chini ya kiwango,Hata kama atakuwa amewazidi watoto wengine bado atakuwa ameshindwa.......

Mwisho wa Siku Napenda Kusema kila Maji yana Mkondo Wake....Unapojaribu Kuwa mwingine mwisho wa siku Hautafikia Mafanikio Yako ya Kimaisha Bali utaishia Kufikia mafaniko ya wengine ambayo hayatakupa furaha ya kweli...Kumbuka Maji yajitahidi Kulowesha na Wala Moto Haujitahidi Kuunguza Na Mvua Haijihidi Kunyesha bali Ikinyesha ndipo uwezo wake...Ishi Wewe Mwenyewe Halisi ufurahie maisha yako..mwenyewe.
|
0 Responses