Wahenga Wa Nchi ya Upare Yaani Kwa Maana ya Wapare walisema...Mkodeka Sunga Henacho Evwene Kwa Maana nyingine Hakuna Mtu anayeinama Kuchungulia Uvunguni Kama Hakuna Alichokiona.Yaani Mtu anayechungulia Uvunguni Kuna Jambo ambalo ameliona Lina manafua kwake au Kwa Mwingine.Leo Kwenye Nazungumza Moyoni.. Tunaanza Hapa.Tanzania Yetu Imejulikana kama Kisiwa Cha Amani lakini Ki-Ukweli Ni Kisiwa Cha Utulivu ni Heri Ya Utulivu kuliko Kuukosa hata huo Utulivu ,Maana Wahenga Wanaendelea kusema Heri Nusu Shari Kuliko Shari Kamili.Pamoja na Kukosa Amani ya Kweli kwenye Nchi Yetu Hata Huu utulivu Unatutosha kwa Kiasi Fulani.Huu Utulivu unapotoweka ndipo Tunajiuliza nini kimetokea?
Miaka ya 1950's Kulikuwa na Wimbi Kubwa la Nchi za Kiafrika Kuanza Kupigania Uhuru wa Nchi za Kiafrika Ambao tuliuhitaji sana kuweza kujitawala na kujiendesha bila kuingiliwa kwenye kile tunachoamua kukifanya kwa manufaa ya nchi zetu.Mashujaa Mbali Mbali waliibuka na kuamua kujitolea kupigania Uhuru Wa Nchi Hizi.Mpaka Mwisho Mwa Miaka Ya 1980 Karibia Nchi zote za Kiafrika Zilikuwa Zimeshapata Uhuru wa Ki-Utawala zikiwa zimebaki Chache.Sahara ya Magharibi ilikuwa Bado haijapata Uhuru wake,Huku Afrika ya Kusini Kukiwa Kunaendelea Mapambano ya Vita dhidi ya Ubaguzi wa Rangi.Mwaka 1994 Ndipo Raisi wa Kwanza Mweusi Anafanikiwa Kunyakua Madaraka Baada ya Mapambano ya Muda Mrefu.

Baada ya Miaka Takribani 50 ya Uhuru wa Bara Hili baada lindi la Umaskini limekuwa kubwa na Bado Linaendelea kuongezeka kwa kiasi Kikubwa.Kumbuka Miaka 50 iliyopita kuna watu walijitoa kwa nguvu na kwa jasho pia na kwa Uhai wao ili kuweza kupata Uhuru wa Katika Siasa,Uchumi na Jamii.
Baada ya Kizazi Kile cha Ukombozi kupita,kimeibuka kizazi ambacho ni cha Ulafi na Kutokujali wengine huku watu wachache wakiendelea kujilimbikizia mali na kuwa fanya wengine kuendelea kubaki maskini.

Miaka ya Karibuni Kumekuwa na fujo katika Bara hili la Afrika Kutoka pande zote za Bara hili juu ya unyonyaji na utawala mbovu ambao umeendelea kujikita kwenye nchi Mbali mbali za Afrika Huku Viongozi wa Nchi hizo wakiendelea kuwa madikteta na Rasimu hata pale ambapo wanapoona wameshindwa kuongoza nchi zao.

Tanzania yangu ni Moja ya Sehemu Ya Bara Hili,Baada ya Miaka 50 ya Uhuru.Hakuna Nafuu ya Kimaisha,Kiuchumi na Kijamii.Utawala Mbovu Ndio Imekuwa shida katika nchi hii Yetu ya Tanzania.Badaa ya Kujiuliza Maswali Kadha wa Kadha Bado Jibu limekuwa tata.Moja Ya Swali ambalo limekuwa halina majibu ni Hili Imekuwaje Raia ambao walikuwa watiifu wa Serikali yao,Wamegeuka kuwa waasi tena wa Serikali Yao?

CCM ndio Chama Tawala Katika Nchi Hii,Inakuwaje Wananchi Walio Wengi Wanageukia Chama Cha Upinzani Yaani Chadema..Jibu Ni Kwamba Kuna Majibu ya Maswali Mengi hajajibiwa ..Miaka Hamsini Baada ya Uhuru Bado tatizo la Ukoloni Limeendelea kwenye Jamii hii ya Watanzania Unaweza Usiwe Ukoloni wa Nguvu Bali Ukoloni wa Fikra wa watu wachache kuelekea UMMA wa Raia Walio Wengi.

Baada ya CCM kushindwa kutoa Majibu ya Maswali Mengi,Wananchi hawa wameendelea Kukiunga Chama Cha Upinzani Mkono Baada ya Matumaini Kuendelea kupotea.Miaka ya Karibuni Tumeshuhudia Fujo Nchini Kenya,Chanzo Cha Fujo Hizi ni Kiwango Kikubwa Cha Umaskini Kati ya Watawala na watawaliwa.Na Hakuna Jitihada zinazochukuliwa kuondoa Tatizo hili.

Ukona raia  Wanaasi Chama Tawala Tambua Kuna Jambo ambalo wameliona Upande wa Pili liwe zuri au Liwe baya....Mkodeka Sunga Henacho Evwene....Hakuna Mtu anayependa Kuonewa na Kunyanyaswa kwenye nchi yake..Juzi juzi Tumesikia Fujo Mtwara Leo Arusha Kesho tutasikia Mbeya,Wiki Nyingine Tutasikia Dar...Kinachonitia Shaka Watawala hawana habari juu yanayoendelea au wameyaona wanayafungia macho.Chuki inayojengeka miungoni mwa kizazi Cha Sasa itaigharimu Serikali kwenye Siku Ya kesho.Siasa za Maji taka na Ujinga Ndio Zinazolipeleka Taifa hili Kusiko eleweka.Ukosefu wa Ujuzi na Akili juu ya Kuendesha Nchi na Badala yake kuendelea kutumia Mabavu kunatengeneza Kizazi ambacho ni Sugu na Ambacho Hakitasikiliza Utawala Tena.Hata Uasi kwenye Nchi Nyingi za Afrika zinazopigana Vita Leo Ulinza Hivi.

Rai Yangu kwa Utawala Akili zakuendesha nchi na Kusoma Nyakati zinahitajika sana kuliko Kutumia Nguvu Nyingi.Nchi Ikifanikiwa Sifa Ni Kwa Utawala na Nchi ikianguka Lawama Kwa Utawala.
Ukiona Watoto wako Wanakimbilia Nyumba ya Jirani Kutafuta Hifadhi Tambua Nyumbani Kwako Kuna Shida Tatua Shida ya Nyumbani Kwako Kwanza ndipo uwafwate watoto wako kwa Jirani

............Mkodeka Sunga Henacho Evwene.......................
|
0 Responses