Hakuna mtu ambaye ameishi kwenye sayari hii katika siku zote za uhai wake bila kukosea kwenye jambo lolote.Mafanikio yote tunayoyaona leo yametokana na makosa mengi ambayo watu waliyafanya siku za nyuma.Yaani kwa maana nyingine hatuwezi kujua tumepatia juu ya jambo fulani bila kujua kutokupatia kuna sura gani.Ili shilingi ijulikane ni shilingi lazima iwe na pande mbili.Hakuna shilingi ambayo siku zote ina upande mmoja ndivyo pia maisha yalivyo.
Ukisoma Historia za watu mbali mbali maarufu na mashuhuri utakuja kukuta hapo mwanzo walikosea sana juu ya kile walichokuwa wanakifanya baada ya kugundua kwamba wamekosea ndipo hujaribu kufanya marekebisho kwanza kuleta muonekano bora juu ya jambo waliloliamini kuwa ni sahihi.


1.Makosa Uliyoyafanya Wewe Binafsi(You are Own Past Mistakes)

Kukosea ni sehemu ya maisha lakini sio maisha yote,Unapogundua umekosea unanyanyuka na kuendelea mbele.Makosa yako binafsi ni moja ya walimu wazuri waliokufandisha ndio maana leo upo hivyo ulivyo,Hauwezi kuishi zaidi ya makosa ambayo uliyoyaona kwako binafsi.
Kama uliwahi kufukuzwa kazi kwa sababu umekosea kufanya jambo fulani kwa uangalifu,Siku unapopata kazi mpya unajitahidi sana kile kilichokufukuzisha kazi  usikirudie tena.Iwapo Kuna wakati huwa tunatumiaga hela zote bila kujali siku unapopatwa na dharura inayohitaji fedha ya muhimu sana na wewe fedha zote ulitumia vibaya inakufundisha kwamba siku ukipata fedha nyingi lazima kuna kutunza kiasi fulani cha fedha hata iwapo dharura itatokea tena usiaibike.Usiogope kukosea maana makosa yako ya leo ndio yanakusaidia kutengeneza maisha yako ya kesho.
Iwapo tusingejua maisha ya dhambi yakoje  na matokeo yake hapa Ulimwenguni tusingejua hata Mungu anafwananaje kwenye maisha yetu ya kila siku.
Mwanzuoni mmoja aliibuka na kusema Kwamba kama Haukuwahi Kukosea juu jambo lolote basi tambua haukuwahi kujaribu kitu kipya kwenye maisha yako.



2.Makosa ya Watu Wengine(Others Mistakes).

Wahenga walisema ukiona mwenzio ananyolewa Nywele basi wewe wewe weka maji Kichwa.Unapofanikiwa kumuona Mtu anakata mti na panga butu alafu akashindwa kumaliza kazi kwa wakati basi wewe kesho ukitaka kukata mti utajifunza kulinoa panga hilo.Hakuna mtu ambaye ana uwezo wa kuishi na kufanya kila kitu na kujifunza kwa makosa ya kwake binafsi tunawahitaji wengine ili kuweza kujifunza.Makosa ya mtu mwingine leo ndio Mafanikio yako ya kesho.
Ukiona mtu amefilisika na matumizi mabaya yake ya fedha na kushindwa kuendesha miradi alioianzisha siku zote utatumia makosa ya mtu yale kama sehemu ya rejeo ili kutoweza kufanya makosa aliyoyafanya yakapelekea matokeo mabaya.Mara nyingi watu waliojifunza kusikiliza na kuangalia makosa ya wengine juu ya jambo fulani kwa umakini wamekuwa na mafanikio zaidi kwenye jambo husika kuliko hata yule ambaye mwenyewe ambaye amewahi kukosea.
Tunawahitaji wengine ili kuweza kuendelea mbele.



Mwisho wa Siku tunaendelea kusema Epuka kuishi kwenye makosa yaliyopita lakini yatumie makosa kama mwalimu wako,Yaliopita si ndwele lakini tugange yajayo.Usiogope kukosea jaribu kufanya vitu vipya kukosea ni sehemu ya maisha.Maisha ni safari ambayo haina mjuzi bali wote tuwanafunzi kwenye kila jambo.Ishi ndoto zako jaribu kutafuta fursa mpya za maisha na jaribu kuzitumia bila woga kwa sababu Makosa yako ya Jana ndio Mafanikio yako ya Kesho.
Mwaka 1996 Sheria ya Ndoa za Jinsia Moja ilisainiwa na  aliyekuwa Raisi wa 42 wa Marakeni Bill Clinton ijulikanayo Kama Defense of Marriage Act a.k.a DOMMA.

Siku chache zilizopita Raisi huyu amaiomba Mahakama Kuu nchini Marekani kuifuta Sheria Hii kwa sababu ya Mapungufu Mbali Mbali yaliopo kwenye hii Sheria.

Raisi huyu Ameendela kueleza kwamba kwenye Sheria ya Ndoa ijulikanayo kama DOMA (Defense of Marriage Act )kusema wazi kwamba ndoa ni Muunganiko kati ya Mwanamke na Mwanaume tu na sio zaidi ya Hapo.Lakini zaidi ya hapo Mahakama Kuu ya Marekani imesema itatoa maamuzi yalio rasmi kisheria mwezi Juni mwaka huu kuhusu ndoa za jinsia moja.

Majaji wataamua kama Defense of Marriage Act kama inashabiliana na kanuni za Taifa linaloheshimu uhuru ,usawa na haki kwa ujumla na ambazo hazipingani na Katiba Mama ya Nchi Ya Marekani.

Raisi huyo aliendelea kusema kwamba Wakati anapitisha Sheria hiyo Ulikuwa ni wakati tofauti na Sasa sababu hakuna hata jimbo moja lililokuwa linatambua ndoa za jinsia mmoja lakini majimbo mengine yilikuwa yinafikiria kufanya hivyo na wengi walikuwa wanataka mabadiliko ya haraka.Kwa Mfano Mpaka  kufikia sasa Majimbo zaidi ya Tisa ikiwemo Colombia District watu wenye mahusiano ya jinsia moja hawewezi kupatiwa huduma za kajamii kama ilivyo kwa watu wenye mahusiano ya jinsia tofauti…..USA Today ndio limeripoti .

Hii inaonyesha kwamba Viongozi wa Kisiasa wanapokuwa madarakani wanapenda kufanya maamuzi ambayo yatawapelekea wao kubaki kwenye madaraka au kulinda hadhi za vyama vyao vya kisiasa au kwa maslahi yao binafsi ama ya kundi fulani bila kuangalia athari zake za badae.
Mtandao wa Amazon ni miongoni mwa mitandao michache Ulimwenguni inayofamika kwa kufanya mauzo ya vitu mbali mbali kupitia njia ya Mtandao.Mtandao huu unauza Muziki na vitu kadha wa kadha kupitia njia ya Online lakini siku ya Leo Tumeamua Kuangalia Muziki wa Injili na Wanamuziki wake wanaofanya vizuri kwenye Mauzo kwa Muda mrefu zaidi kulingana na Mtandao huo.


1.Mountain High... Valley Low

Mountain High... Valley Low ni Albamu ya Muziki wa Injili iliyoachiliwa mwaka 1999 na Mwanamuziki Maarufu wa Injili nchini Marekani Yolanda Adams chini ya Lebo yake ya Elektra Records.Albamu hii mpaka sasa imeshachukua  tuzo mbali mbali kama Grammy Award pia kwa Mujibu wa Mitandao mingine ya Mauzo kwa ujumla mpaka sasa Yolanda Adams na Albamu Hii ameshafanya mauzo ya Nakala milioni 2,374,000.Albamu hii ina nyimbo takribani 11 na zote zimefanywa kwenye Studio ya Elektra Records.Hii ndio Albamu inayoshikilia namba moja kulingana na mtandao wa Amazon.


2.Tri-City4.Com

Mwaka 2001 Kundi la TRI-CITY SINGERS lilifanikiwa kupewa tuzo ya Grammy baada ya albamu yao ya TRI-CITY4.COM kufanya vizuri mwaka 2000.Albamu hii iliachili rasmi mwaka 200,februari 29.Albamu hii ina nyimbo takribani 16 zilizotengenezwa chini ya Lebo ya EMI Gospel.Kundi hili lilianza kufanya vizuri baada ya mwanamuziki Donald Lawrence kushika hatamu baada ya Director aliyekuwepo kung’atuka kwenye nafasi aliyokuwa anaishikili.Hili ni Kundi la Nchini Marekani ambalo lilichukulia kama kwaya bora kuwahi kufanya mauzo zidi kwenye Mtandao wa Amazon.Hiii ni Albamu namba Mbili kwa Mauzo kulingana na Mtandao wa Amazon.


3.2nd Chance

Siku ya July 30,2002 ndipo Albamu ya Pili Ya Mwanamuziki Karen  Clack Sheard ndipo ilipoingia Sokoni rasmi ikiwa na Jina la 2nd Chance.Kabla ya Kuachilia Albamu hii Mwanamuziki Karen Clack Sheard alisumbuliwa na Tatizo la Mishipa ya Damu ya kwenye paji la Uso Kupasuka.Madaktari walisema Uwekano wa kupona Ugonjwa huo ni Asilimi 2% na asilimia iliyobaki ilikuwa ni Kifo tu haya yote yalitokea mwaka 2001.Baada ya Kuanza kuachia Mauzo ya Albamu hii mwaka 2003 kupitia wimbo wa The Heavens Are Telling ndipo alipoweza kuchaguliwa kuingia kweny Kinyang’anyiro cha Tuzo za Grammy nchini Marekani.Mpaka sasa Albamu hii yenye nyimbo 13,Inaendelea kushikilia nafasi ya tatu kwa  kufanya mauzo makubwa ambayo hayajawahi kufikiwa mpaka sasa kwenye mtandao wa  Amazon.


4.I Believe

Mwaka 1996 mwezi Machi tarehe 12 Mwanamuziki Marvin Sapp ndipo alipoingia rasmi kwenye game za Muziki wa Injili nchini Marekani.Mpaka Sasa Marvin Sapp ameshaachilia albamu 9 za Muziki wa Injili.Kwa Mujibu wa Mtandao wa Amazon Albamu ya I Believe iliyoachiliwa June 11, 2002 ndio inayoshikilia nafasi ya Nne kwenye Mtandao huo kwa Mauzo makubwa kuwahi kutokea.Albamu hii ina jumla ya nyimbo takribani 13.Albamu hii ilitolewa chini ya Lebo ya Verity nchini Marekani.Hii ndio albamu ambayo rekodi yake pia ya mauzo haijawahi kuvunjwa na Inaendeelea kushikilia namba nne kwenye mtandao wa Amazon.


5.Grace & Mercy

Mwaka 1967 Mwanamuziki Marvin Sapp ndipo alipozaliwa kwenye mji Grand Rapids, Michigan nchini Marekani.Baada ya Mwaka 1996 kuamua kuimba Kama mwimbaji Binafsi mwaka Desemba 16,1997 ndipo  alipoachilia albamu ya Grace & Mercy.Mwaka 1998 albamu hii ichaguliwa kuingia kwenye Kinyang’anyiro cha Tuzo za Grammy.Albamu hii ina takribani Nyimbo 10 pekee yake.Huu ndie mwanamuziki pekee aliyefanikiwa sasa kuingiza Albamu 2 kwenye Tano bora kwa Mauzo ya Muda mrefu na yanayoshikilia Rekodi ambayo mpaka sasa haijavunjwa wala kuondolewa katika nafasi ya nne na ya tano kulingana na mtando huo wa Amazon.

Wakati Nchi zetu za Ukanda wa Afrika Mashariki zikiwa na bado na maswali mengi juu ya viongozi wa Dini Wanawezaje kuwa Matajiri wa Kupindukia lakini Sivyo Ilivyo katika nchi za Afrika Magharibi haswaa nchini Nigeria.Siku Chache Zilizopita tumekuwa tukifwatilia mitandao mbali mbali ya chini Nigeria na tukakutana na hiki,Wachungaji wenye Asili Ya Nigeria na Wanaoishi Nigeria ambao ni matajiri zaidi kuliko wachungaji Wengine.

1.Bishop David Oyedepo

Huyu ndie mwanzilishi wa Kanisa na huduma ya  Living Faith World Outreach Ministry, a.k.a Winners Chapel Ulimwenguni mwote.Ndie Mchungaji na Askofu tajiri zaidi kuliko wote nchini Nigeria.Utajiri wake unakadiriwa kuwa kiasi cha Dola Milioni $ 150.Takwimu hizi zilikusanywa Mwaka 2011-2012.Huduma ya  Living Faith World Outreach Ministry, a.k.a Winners Chapel ilianzishwa mwaka 1981 pia ndio Kanisa kubwa zaidi kuwahi kutokea katika bara la Afrika.Kanisa lake linachukua zaidi ya Washirika 50,000 hawa wakiwa wamekaa kwenye viti bila bugudha yeyote.Mchungaji huyu anamiliki ndege 4 zake binafsi.Ni Mmiliki wa Chuo Kikuu kiitwacho Covenant University nchini Nigeria.Amefanikiwa kuwa na Kampuni Yake ya Uchapishaji Iitwayo Dominion Publishing House.Zaidi ya hapo anamiliki Shule yake Ya Sekondari Binafsi nchini humo ijulikanayo Kama Faith Academy.



2.Chris Oyakhilome

Huyu ndiye mwanzilishi wa Kanisa na Huduma ya Believers’ Loveworld Ministries, a.k.a Christ Embassy.Utajiri wake Unakadiriwa kufikia kati ya dola Milioni  $ 35 - $ 50 kwa mwaka 2011-2012.Kanisa la Believers’ Loveworld Ministries, a.k.a Christ Embassy lina Zaidi ya washirika 40,000 duniani kote na wengi wao wakiwa Viongozi wa Serikali na Wamiliki wa Makampuni Mbali mbali.Anamiliki Vitu mbali mbali ikiwepo Kituo cha Utangazaji cha Televisheni Chenye jina la LoveWorld TV Network. Pia amefikiria kuanza kuwekeza kwenye Hoteli na Nyumba za Upangaji sehemu Mbali mbali Ulimwenguni.


3.TB Joshua

Huyu ndio mwanzilishi wa Kanisa na Huduma ya Synagogue Church Of All Nations (SCOAN) nchini Nigeria.Utajiri wake unakadiriwa kufikia kiasi cha Dola Milioni $ 10 - $ 15 .Anamiliki Jengo la Kanisa lenye uwezo wa kuchukua Washirika 15000 wakiwa wamekaa bila Shika wa tatizo.Kanisa la Synagogue Church Of All Nations (SCOAN) lilianzishwa Mwaka 1987.Kwa sasa ana matawi katika nchi Mbali mbali nje na ndani ya Afrika.Miaka Minne aliyopita alitoa msaada wa Fedha Wenye thamani ya Dola Milioni $ 20 kwa kituo cha Matibabu cha Jeshi kilichokuwa kinaitwa Niger Delta Militants.Ni mmiliki wa Kituo Cha Utangazaji cha Televisheni chenye Jina La Emmanuel Tv.




4.Pastor Matthew Ashimolowo


Huyu ndiye mwanzilishi wa Huduma na Kanisa lijulikanalo kwa jina Kingsway International Christian Centre (KICC).Lenye Makazi yake nchini Uingereza.Utajiri wake Unakadiriwa kuwa Kiasi cha dola $6 – $10 .Mwaka 2009 Kanisa Kingsway International Christian Centre (KICC) lilitangazwa kwamba ndilo Kanisa Kubwa Zaidi la Kipentekoste nchini Uingereza.Pastor Matthew Ashimolowo ni mmiliki wa Baadhi ya Vituo vya Uandishi wa Vitabu  ambavyo Huandika Makala Mbali mbali za Vitabu pamoja na Utengenezaji wa Documentaries Mbali mbali.


5.Pastor Chris Okotie


Huyu ndiye Mwanzilishi wa Kanisa la Household of God Church nchini Nigeria.Utajiri wake unakadiriwa kufikia kiasi cha Dola Milioni $3  -$10.Miaka Michache iliyopita ni mmoja wa wachungaji waliojitokeza kugombea Uraisi wa Nchi ya Nigeria kwa vipindi vitatu tofauti na huku akiwa kiongozi wa Chama Chake Binafsi cha Siasa.Kiasi kikubwa cha Washirika wake ni Macelebrity wa Nigeria pamoja na watu wengine maarufu kwenye kila eneo.Pia kwenye Miaka ya 1980's ndie Mwanamuziki Mzuri wa Pop kwa kipindi hicho Nchini Nigeria.Anamiliki Vitu kadha wa Kadha ikiwemo magari yenye thamani kubwa zaidi Ulimwenguni kama Hummer na Porsche.

Huyu ndiye DNG

Baada ya Siku Chache zilizopita Kusadikika kwamba Mwanamuziki wa Secular Music Jaguar kutoka nchini Kenya ndiye aliyelipwa fedha nyingi zaidi na Kupitia chama Cha Mgombe U-Raisi Raila Odinga Katika Kipindi cha Kampeni lakini  Siku Ya Chache zilizopita Imekuja kugundulika kwamba Mwanamuziki wa Injili nchini Kenya DNG ndiye aliyelipwa fedha nyingi zaidi kwenye  Kipindi cha Kampeni na Mgombea wa kiti cha U-Raisi nchini Kenya Uhuru Kenyatta.
Inasadikika Mwanamuziki huyu amelipwa Mara 8 zaidi ya Mwanamuziki Jaguar kuendesha Burudani kwenye Kampeni Nchini Kenya kupitia Chama Cha Uhuru Kenyatta.
Wahenga walisema Tabia ya Mtu ni Mtu Mwenyewe.Hakuna mtu anayeweza kuishi nje ya tabia yake ambayo imo ndani mwake.Jinsi unavyomwona mtu mara zote na vitu anavyovifanya ndivyo alivyo.Tabia ya mtu ni udhihirisho wa vitu vingi sana vilivyo ndani mwake.Unapoona mtu anafanya kitu fulani si kitu ambacho kinaibuka mara moja na kutokeza tu bali ni hali ya ndani iliyojengwa muda mrefu kutokana na mambo kadha wa kadha anayokutana nayo kwenye maisha.

Mwanazuoni Mmoja alisema kwa asili Binadamu ni Wabaya lakini wanajaribu kujibadilisha kutoka kwenye ubaya kuelekea kwenye Uzuri wao.Akaendelea kusema kubadilisha tabia si kazi rahisi kama ilivyo kubadilisha nguo ya mwili.Inakuchukua muda mrefu na kufanya vitu mbali mbali kutoka kwenye ubaya wa tabia kwenda kwenye tabia nzuri.


Mwanazuoni mwingine aliibuka na kusema mtu hawezi kuishi nje ya tabia yake ya asili aliyoijenga maishani mwake na akaendelea kusema zaidi kwenye maisha ya binadamu hakuna siri.Tabia za mtu unazoziona kwenye maisha yake ni udhihirisho wa siri nyingi zilizo ndani mwake,Ingawa kwa sisi binadamu hatupendagi kufwatilia tabia ya mtu hatua moja kwenda nyingine.Lakini Unapofanikiwa kufwatilia tabia na namna wanavyoishi ndipo kuna uwezekano wa kugundu mambo kadha wa kadha ndani ya mtu huyo.

Kujenga tabia mpya na njema kwenye maisha ya mtu ni maamuzi na sio aina fulani ya nguvu ambayo inahitajika kutoka nje.Mungu alipomuumba mwanadamu alimuumba kwa ukamilifu wote ikiwa na uwezo wa kukibadilisha kila anachokutana nacho kwenye maisha.Mfano Dunia iliiumbwa katika Utupu bali kulikuwa na Malighafi tu ambazo zilikuwa hazitumiwa kwa namna yeyote.Baada ya Binadamu Kuumbwa ndipo mabadiliko yalipoanza kutokea kutokana na utumizi wa rasilimali hizo.Kila badiliko unalolitaka kwenye maisha yako lipo ndani yako.Hakuna mtu mzee zaidi ambaye ataamua kubadilisha tabia yake akashindwa.


Maisha ya Binadamu ni mfano wa Chupa ya Maji iliyojaa maji machafu Lakini Chupa hii inapokwenda kuikingwa maji kwenye Bomba la Maji ndipo Maji safi yapozidi kuingia na Maji machafu yanapozidi kutoka,Unapofanya kitu hiki kwa muda mrefu utakuja jua maji machafu yameshatoka na masafi ndiyo yaliobakia.Unapotaka kubadilisha tabia mbaya kwenda nje jaribu kutafuta tabia mpya nzuri ianze kuishi bila kuangalia tabia mbaya ulio nayo,Unapoendelea kuishi inafika siku unakuta una tabia mpya ambayo ni njema lakini mbaya imeshaondoka.

Information mbali mbali tunazoingiza kwenye maisha yetu kwa njia ya kusoma,mazingira,watu zinaathari kubwa kwenye maisha yetu na tabia kwa ujumla.Mfano mtu anapokuwa muagaliaji wa picha za Ngono kwenye Luninga,Je unafikiri anajenga tabia ya namna gani?Tabia haiingi mara moja tu kwenye maisha ya mtu bali ni mchakato wa muda mrefu ambao unajuisha mambo kadha wa kadha.Hakikisha inaformation unazoingiza kichwani mwako na maishani mwako moja kwa moja zina reflect kuelekea kwenye aina ya tabia ambayo unaipenda.No Body can Act against Information alizonazo kichwani iwe ni nzuri au mbaya.Hakikisha unafanya mabadiliko kuleta tabia mpya na njema kwenye maisha yako ya kila siku.Hakuna fisadi ambaye alianza kuwa fisadi bali alianza kidogo kidogo toka akiwa mtoto na alianza kwa udokozi wa vitu vidogo vidogo.

Mwisho wa Safari yetu siku ya leo kwenye Punch Of The Week Naendea kusema Impossible is The Word Found In Fools Dictionary. Anza hapo ulipo na kitu ulicho nacho kuelekea kwenye tabia njema.Wataalamu wanasema tabia njema si kwa ajili tu ya kukufanya kuishi kwenye jamii kwa amani na furaha bali tabia nje husaidia hata kujenga maisha yako ya kiafya na kiakili,Kuna uwezekano wa tabia zako mbaya zinapeleka kukuharibu kiakili na Kiafya pia.Hakuna mtu aliyezaliwa akiwa anajua kila kitu na kuwa na tabia njema katika kila Idara lakini wote tumezaliwa tukiwa na lengo la kujifunza.Tabia yako kwenye maisha ya kila Siku ni Zaidi ya Upepo wa Kisuli Suli ,Uangamivu wa Maisha yako Inategemea kiasi gani umejenga tabia mbaya.Na kufanikiwa zaidi kwenye maisha inategemea kiasi gani umejenga tabia njema

Kila asubuhi jamii kubwa ya wanadamu wanaamka na kwenda sehemu mbali mbali kwa ajili ya kwenda kujishughulisha ili kupata mahitaji muhimu ya kila siku kwenye maisha yao na jamii kwa ujumla.Tumekuwa tukizungukwa na changamoto mbali mbali kutokana na sababu mbali mbali lakini mwisho wa siku lazima lengo halisi litimie kufikia maswala muhimu ya kimaisha na kijamii.Maisha huchosha na hukatisha tamaa iwapo tunapoona njia ya kufikia yale tunayoyataka kuwa ngumu kupita kawaida lakini Unapofikiria Kuchoka Kabla ya Muda wa Kuchoka Haujafika unakuwa sawa sawa na mkulima anayepanda mbegu zake kwenye Jiwe akitegemea ziote.

1.Mazingira
Mazingira tunayoishi kila siku tangu tunaingia kwenye sayari hii itwayo Dunia yamekuwa na nguvu kubwa ya kututengeneza namna tunavyoweza kupambana na changamoto mbali mbali za kimaisha tunazokutana nazo,Ukitaka kufahamu ili kama ni ukweli au uongo mchukue Mang'ati aliyekaa porini tangu siku anazaliwa kisha baada ya miaka 20 mlete Mjini ndipo utaelewa nachosema.Ndio maana kuna mwingine Changamoto inapotokea hukimbilia kusema huu ndio mwisho wa maisha yangu lakini kwa mwingine husema huu ndio wakati muafaka wa kusonga mbele.Ukifwatilia kwa ukaribu kati ya hawa watu wawili Mazingira na vitu walivyokutana navyo vinawapa uwezo wa kujua iwapo wanaweza kuvuka juu ya changamoto fulani au hapana.

2.Watu
Kariba za watu wa aina mbali mbali tunaokutana nao zinauwezo mkubwa pia wa kutufanya tufikiri namna tunavyoweza kushinda vikwazo na taabu mbali mbali tunazokutana nazo kila siku.Wakati mtu mmoja akikutana na Pope Benedict XVI swali la kwanza watakalomuuliza ni kwanini Umejiuzulu kuwa Pope Mtu Mashuhuri zaidi Ulimwenguni?Lakini kuna watu wengine hawafikiria kumuuliza kwanini Amejiuzulu "Watamuuliza  Je umefanikiwaje kufika kwenye Hiki cheo cha Kuwa Kiongozi wa Kanisa lenye wafuasi wengi zaidi Duniani?Ukifwatilia kuna mwingine amekutana na watu wenye mtazamo wa kimaskini lakini mwingine amekutana na watu wenye mtazamo wa kujua mbinu za kufikia mafanikio.Jiulize wewe je ukikutana na Mengi leo Utakimbilia Kumwomba Pesa au Utamwomba Ushauri ambao utakaokuzalishia Pesa zaidi ya alizokupa Siku hiyo?

3.Ufahamu
Mtu jasiri anayejua anapokwenda kufikiria kuchoka kabla ya Safari yake haijafika ni mwisho.Mtu mwenye kutafuata maarifa na ufahamu juu ya namna ya kuendesha na maisha na kushinda changamoto siku zote hawezi kuwa mkata tamaa.Unapofikiria Kuchoka Kabla ya Muda wa Kuchoka Haujafika ni sawa na kujaribu Kujaribu kuendesha gari lenye pancha ukitegemea litakufikisha Mbeya wakti ndio kwanza unatoka Sinza KIjiweni.Ufahamu hukupa mbinu mbadala za namna ya kutatua changamto husika bila ya kuweza kuishia njia.Tambua vita yeyote duniani unayoiona kwanza huanza kwenye Kichwa cha mtu.Hakuna vita inayoanza nje ya kichwa cha mtu.Jaribu kutafuta ufahamu kila siku.Safari bado ni ndefu usifikiri kuishia njiani wakati unaanza safari ulijua utafika.Jipe Moyo na Usonge Mbele VIkwazo na Changamoto ni sehemu ya maisha ndio maana viliwekwa kuonyesha namna ulivyo hodari na shujaa.

Hakuna Hodari wa Vita anayeweza kujisifia ni Mshindi wakati haukuwahi kupigana vita vya namna yeyote.Changamoto na vikwazo ni Sehemu ya Ushindi ndio maana vipo.Changamoto na vikwazo havikuwekwa kwa ajili ya wanyonge bali kwa ajili ya washindi.Changamoto na Vikwazo havikuwekwa kwajili ya Wanyama ,Viliwekwa kwa ajili ya Binadamu.Siku zote Mshindi hupata Ushindi kabla ya Kufika Eneo la Mapambano La Vita lakini Watu dhaifu hushindwa kabla hawajafika hata eneo la Mapambano.Acha Kufikiria kuchoka kabla y.a Muda wa Kuchoka Kufika.Changomoto na Vikwazo kwenye maisha nivifwananisha na Gereza ambalo hawakutengezewa Kuku bali Watu na ndivyo Changamoto zilivyo ni Kwa ajili ya Watu ambao wamejizatiti kufikia hatma yao ya Maisha na Sio Aina Nyingine ya Viumbe Visivyokuwa na Utashi.
Ukomavu kwenye matumizi ya mitandao ya jamii ni swala linalopaswa kwenye jamii ya Watanzania na matumizi ya vyombo mbali mbali vya habari.Je ivi unajisikiaje unavyoyasema mabaya ya mwenzio kwenye mkusanyiko mkubwa wa watu ili hali wewe una ya kwako?Matumizi ya mitandao ya kijamii na Media kwa ujumla inaonyesha namna gani mtu alivyokomaa kwenye uwezo wa kuchambua na kuendesha vitu kwenye maisha yake.Imani na jamii mbali mbali zina mifumo yake ya kutoa hukumu kwa wahusika wanapokosea na sio kuchafuana kwenye mitandao na kuwaacha wengine wakiwa mithiri hawajavaa nguo.Tafakari unasikikia siku Baba yako Mzazi naye amewekwa kwenye Media au kwenye mtandao wa Jamii na ameelezewa mabaya yake Je Utafurahia au utahuzunika?

1.Ki-Imani

Kila imani  ina mfumo wake wakutoa adhabu pale mtu anapokosea iwapo taaratibu za kushtaki kosa husika mahali husika.Inanishangaza sana kuona kosa la mtu mmoja wa Imani fulani linapochukuliwa na mtu wa Imani ile ile mwingine na kwenda kulishikilia bango na kulitangaza kwa watu wengine wasio wa Imani ile.Je unafikiri watu wa Imani nyingine wanawafukiriaje watu wa Imani ambayo mmoja wa waumini wake makosa yake yamewekwa hadharani.Je unajengaje nyumba yako mwenyewe  kwa kubomoa kila baaada ya kumaliza kozi moja ya ujenzi wa matofali?Ufalme ukishajifitini wenyewe hata siku moja hauwezi kuendelea Mbele.Kabla haujaamua kusema mabaya ya mwingine hadharani kwanza jiulize wewe hauna mabaya?Kumbuka kila mtu anachopanda ndicho utakachovuna.Ukimsema vibaya mwenzako wewe subiri tu kuna siku na wewe utasemwa vibaya zaidi na unapoelezea mazuri ya mwenzako tarajia kuna siku watu wataelezea uzuri wako.Baada ya Kufa ni hukumu kumbuka mahesabu yote tunayamaliza hapa hapa.

2.Ki-Jamii

 Kila kwenye jamii ya watu kuna taratibu na sheria husika za kudhibiti wahalifu wa makosa.Je unapomsema mtu hadharani bila kwenda kwenye mamlaka husika je unakuwa umsaidiaje muhusika na wanajamii wengine wasipatwe na tatizo ambalo lilishakukumba kwa kutendewa ubaya na mtu husika au jamii husika ya watu.Facebook na mitandao mingine ya kijamii ikiwa ni pamoja na media mbali mbali kazi yake sio kuelezea na kuonyesha ubaya wa wengine bali kuhakikisha jamii inapata habari kamili na mafunzo ambayo yana tija kwenye jamii.Iwapo unahisi kuna kosa na matatizo juu ya tuhuma kwa watu fulani fwata taratibu za kisheria na kijamii ili kuwasaidia wengine na sio kuishia kuchafuana.Kumbuka unapomchafua mtu akaamu kukufwatilia kisheria na kitaratibu unaweza kushtakiwa na kuadhibiwa kwa kuongea vitu ambavyo havina tija na uhakika kwenye jamii ya watu.

3.Uasili wa Dunia

Namna ulimwengu ulivyotengenezwa na ulivyoumbwa na Mungu ni namna ya ajabu sana.Kumbuka unapofanya kitu kizuri hata kama haukulipwa mazuri kwa muda huo kabla haujaondoka kwenye sayari hii ndivyo utakavyolipwa.Unapoendelea kuelezea makosa ya wengine na ipo siku kabla haujaondoka lazima na sisi tutasikia makosa yako na mabaya yako makubwa kuliko ulivyoelezea ya wengine.Epuka kuwa msemaji wa makosa ya wengine tumia muda wako kuendesha mambo mema na kuwasemea wengine maneno mazuri.Iwapo unaona hauwezi kuchukua hatua basi ni afadhali unyamaze kuliko kuelezea makosa ya wengine mahali pasipo sahihi.Hata siku moja usitegemee kupanda kokoto ukavune maharagwe.Kile unachopanda ndicho unachovuna.



Mwisho,Mitandao ya Kijamii sio sehemu ya kuhukumu dhambi za wengine.Iwapo unaona mtu wa imani yako au wa jamii yako amekosea tafuta msaada ya kisheria na kitaratibu kwenye mahala husika Facebook na kwenye media sio sehemu sahihi ya kuelezana mabaya bali ni sehemu ya kuisadia jamii kuapata maendeleo chanya na yenye tija kwa jamii yetu na taifa kwa ujumla .Safari ni ndefu kwa watanzania kwenye matumizi ya mitandao ya jamii na media kwa ujumla mpaka tukifikia ukomavu wa safari hii basi tumeshajeruhi na kuharibu maisha ya watu wengine wengi sana.


"Ukiona hauwezi kuficha Uchi wa Baba yako Basi Ipo Siku Utamcheka Mkweo kwa Utupu wake."
Kwa muda mrefu kidogo nchi ya Tanzania ambayo imekuwa ikiitwa Kisiwa Cha Amani ili hali si ukweli ila imekuwa Kisiwa Cha Utulivu na Uoga miongoni mwa wananchi wa Tanzania.Kwa Muda wa Miaka ya Karibuni kumekuwa na kujitokeza kwa aina mbali mbali za vurugu haswa zinazojihusisha na Muonekano wa Kidini lakini Pia na Katika Muonekano wa Kimaslahi kati ya Viongozi wa Serikali na Wananchi wa Nchi yenye Utulivu.Nimekuwa nikijiuliza mengi kila kukicha fujo zinatokea na hakuna ambaye anasimama kuzikemea kwamba haipaswi kuwa namna hii ilivyo sasa.Lakini matokeo yake mambo yalivyo watu wamekuwa wakikaa kimiya na viongozi wamekuwa wakivunga.Je ni nani anayefaidika na Hizi Vurugu zinazoendelea?

1.Vurugu zenye Muonekano wa Kidini.
Vurugu hizi kila kukicha zimekuwa zikiongezeka bila sababu zinazoeleweka na zimekuwa zikifungiwa macho na viongozi wamekuwa wakiendelea kuvunga kanakwamba hakuna kinachotokea kwenye nchi yetu.Taasisi za Dini za Upande mmoja zinaposimama kusema ukweli juu ya Vurugu zinazoendela Utasikia Serikali inasemama na kuzikemea kwamba hazina haki ya Kuwa wasemaji ili hali waumini wa Taasisi wa Dini hizo wamekuwa Wahanga kila kukicha.Je Ni Serikali au Baadhi ya Watu wachache wanaofaidiaka na hizi Vurugu?
Siku za Karibuni kumekuwa na mvutano mkubwa kati ya Upande wa Dini ya Ki-Islamu na Wakristo na Upande mmoja umeonekana ukitetewa na kukaliwa kimiya kwa kila wanachofanya ili hali upande mwingine ukitishia kuchukua hatua huonekana na mbaya Je nani anayefaidika na Vurugu hizi?
Miaka yote tumekuwa tukiishi kwa utulivu huu pamoja na tofauti tuliozo nazo lakini hakuna mtu aliyethubutu kumshambulia mwenzake wala kumdharau Je kwanini wakati huu iwe hivyo?Basi kwa mtazamo wa haraka haraka kuna watu ambao watakuwa wanafaidika moja kwa moja au indirect kutokana na muendelezo wa Vurugu hizi.

2.Vurugu zenye Muonekano wa Kimaslahi(Kifedha na Kiuchumi)
Tumeshuhudia fujo kubwa kwa ndugu zetu wa kanda ya kusini juu ya sakata la gesi linaloendelea.Wananchi wenye mumkari wameshindwa kuvumilia juu ya maamuzi wanayofanyiwa wao bila ya wao kushirikishwa kwa muda mrefu nchi hii watu wachache wamekuwa wakiamua nini kifanyike na nani afanye na nani afaidike kwenye kila mradi unaohusisha fedha nyingi.

Wananchi wanapoamua kudai haki zao kwa kutetea kile wanachotaka wao na wanachoona ni sahihi hugeuka kuwa adui wa maslahi ya watu hao wachache..Miradi Mingi imekuwa ikiendeshwa bila uwepo majadiliano na maamuzi ya wananchi wenyewe kuamua kitu gani wanataka juu ya Rasilimali zao lakini watu wachache wakiamua basi ndio yanatendeka.Hakuna elimu ya kutosha juu ya miradi na faida ambazo wananchi watapata baada ya Serikali kuingia Ubia na Mashirika ya Kimataifa.

Miradi Mingi imekuwa ikiendesha kiholela holela na pindi wananchi wanapodai haki zao kwa njia ya amani hawasikilizwi na matokeo yake huundiwa zengwe na kuonekana ni wabaya.Na wanapoamua mutumia nguvu huonekana ni wakorofi na wavunjifu wa amani?Je ni heri fujo na uvunjifu wa amani utokee sababu ya watu wachache?Muda utafika watu hawatakuwa tayari kuendelea na ujinga huu watu watasimama na ndipo muda huu wa neema utakapokuwa umekwisha na hapo ndipo nchi itashindwa kutawalika sababu ya misingi mibovu inayojengwa leo.

Mwisho,Niwazacho Mimi Kuna mtu au  watu watakuwa wanafaidika na Vurugu na Uvunjifu wa Utulivu tulio nao la sivyo basi hatua za Makusudi zingekuwa zimechukuliwa na katika kutatua matatizo haya ambayo kila siku yamekuwa yakikua na kuongezeka bila sauti za viongozi.

Je ni nani anayefaidika na Vurugu zinazoendelea Tanzania?

MUNGU IBARIKI AFRIKA,MUNGU IBARIKI TANZANIA
Kwa Mara Nyingine Napenda kuchukua nafasi hii kuwaasalimu wadau wote wa blogu katika mwaka 2013,Maana kwa Mara nyingine leo Ndipo tunakuta kwenye Programu yetu ya Kila Ijumaa iitwayo Punch of The Week.Leo katika Punch of The Week tumeamua kuangalia vitu kwa jicho la Pembeni kidogo lisemalo Urahisi wa Njia sio Uhakika wa Safari.

Maisha yetu ya kila siku muda mwingine yamekuwa hayana dira sababu ya kukosa mwelekeo sahihi wa kufanya vitu na kuviendeleza huku tukidhani kwamba hii ndio njia sahihi na huo ndio umekuwa mfumo ambao tumekuwa nao katika kila nyanja.Vitu vingi tumekuwa tikivifanya kwa zima moto huku tukidhani kwamba tunaweza kufikia kilele cha mafanikio ambayo yanaweza kudumu daima.

Maisha yetu yamejengwa kwenye kupenda njia za makato kuliko kufwata kanuni ambazo zipo na ndizo za uhakika kwenye maisha yetu kama wanadamu.Hakuna mtu ambaye amejenga mafanikio ya kudumu kwa kutumia njia za mkato.Uasili wa Dunia jinsi ulivyo ni kwamba ukipata kitu kwa dhuluma kitaondoka kwa dhuluma iwe leo au kesho.Mara nyingi tumeshindwa kuangalia mbele tumeangalia matokeo makubwa ya sasa lakini tunasahau kwamba maisha yanaendelea.Wahenga walisema Ukiua kwa Upanga Basi na Wewe utauwawa kwa Upanga wakimaanisha namna kitu kinavyopatikana ndivyo kitakavyoondoka.


Mafanikio yanayodumu ni yale yanayojengwa kwa mfumo wa Haki na kujituma siku zote.Hakuna mazingaombwe kwenye mafanikio wala uchawi.Iwapo unategemea uchawi,wizi na dhuluma kupata maendeleo habari nilio nayo ni kwamba tunasubiri anguko lako siku yeyote kuanzia sasa hata kama leo unaonekana unakula bata na kufurahia lakini kanuni za asili za kuendesha dunia huwa hazibadiliki siku zote.

Kuna hasara njinyi sana kwenye kutegemea kupata vitu kwa njia ya mkato kuliko kufwata kanuni za msingi za kufanikiwa katika jambo lolote.Je wewe unafikiri ungekuwa umezaliwa siku ya kwanza then siku ya pili tunakuona unakimbia je unafikiri sisi tunaokuzunguka tungefikiria vipi?Au wewe mwenyewe ungewazaje?

1.Njia za Mkato mara zote hazitoi jibu la uhakika na linalodumu siku zote.Njia za mkato au zima moto husaidia kutatua tatizo kwa muda tu lakini mara nyingi hakuna uhakika wa kudumu wa suluhisho ambalo litadumu siku zote za maisha.Fikiria iwapo haujawahi kufanya biashara siku zote za maisha yako ghafla unakuwa na biashara kubwa kesho asubuhi unafikiri biashara hiyo itadumu?Jibu ni hapana sababu hauna mufundisho ya msingi juu ya uendeshaji wa biashara na namna ya kucheza na mzunguko wa fedha.Unapofwata hatua mbali mbali unajenda uwezo binafsi wa kujifunza na kuwa na uhakika wa kutokurudia makosa ambayo hautaweza kuyarudia tena.Kumbuka siku zote Vitu rahisi gharama yake ni kubwa zaidi.Mfano Mzuri ni pale ambapo tunapoumwa kichwa kwa ghafla huwa tunameza dawa za kutuliza maumivu tu lakini huwa bado hatujatatua ugonjwa wa msingi ambao umepelekea kuumwa kwa kichwa.Ili kutibu na kufahamu ugonjwa husika ni lazima umuone daktari upate vipimo na ndipo upewe dawa kamili za kutibu ugonjwa husika.

2.Mtu anayetegemea njia za mkato mara nyingi huwa hakomai kitabia na namna ya kuendesha vitu vyake maishani mwake siku zote.Unapoiona tabia fulani ya mtu ndivyo alivyo mwenyewe.Tabia hujengeka kutoka na mfumo wa maisha wa mtu wa kila siku alio nao.Iwapo unafikiri kwamba wizi ndio njia sahihi ya kuishi basi siku zote hautajua kwamba kuna namna nyingine ya kuishi sababu ndivyo ulivyojijengea.Maisha huenda na kubadilika kila siku kuna siku utashindwa kuiba je utaishi kwa namna gani?Ukiona mtu anakuwa na hasira na maamuzi mabaya siku zote usikimbiliea kumlaumu fwatilia ni wapi ameanzi na amekulia katika mazingira gani maana hayo ndiyo yaliyojenga mfumo maisha yake.Mara zote nimesema hakuna mtu anayeweza kusihi nje ya information mtu ambazo anazo kichwani.Na information hupatika katika njia tofouti tofauti  
(I)Mazingira 
(II)Marafiki 
(III) Malezi 
(IV)Vitu mtu anavyosoma kila siku n.k.
Ukomavu wa tabia nzuri huja kutokana na mafundisho magumu ya kufwata kanuni mbali mbali na mfumo wa asili wa dunia ulivyoweka bila kukubali kufwata njia za mkato na urahisi.

3.Mafanikio ni Mchakato na sio Mkato.Mafanikio yanayodumu yamejengwa kwenye njia ngumu ambazo mara nyingi tumeambiwa lakini tumekuwa tukipuuzia.Mafanikio yanayodumu yamejengwa kwenye uvumilivu ambao umejengwa katika muda mrefu ambao ndani yake kunakuwa na mchakato mgumu wa mafundisho ya asili na ambayo muda mwingine sio rahisi kuyaelewa na usipokuwa makini utaishia kulalamika na kukata tamaa.Waswahili Wanasema Njia Nyembamba na isiliyosonga ndio Inayoelekea uzimani n lakini njia nene ndio inayoelekea upotevuni.Hakuna mkato kwenye mafanikio yanayodumu.

4.Njia ya Mkato haikujengei nidhamu ya kuheshimu na kuyatunza mafanikio ambayo umeyapata.Unapojifunza kujijenga kwa njia sahihi unajenga uwezo binafsi wa wewe kuheshimu na kuthamini mafanikio ambayo umeyapata kwa nguvu zako mwenye pia unasikia ufahari wa kujivunia kila ambacho umekipigani siku zote.Fikiria kama umetoa mtoto au mke wako sadaka kwa mizimu unafikiri wakati wa kujivuni mafanikio yako utajivunia Damu uliyoimwaga ya wapendwa wako au utakuwa mnafiki wa kujifanya unafurahi wakati ki ukweli moyoni unajua sivyo ilivyo?Mafanikio yaliyopatikana kwa juhudi binafsi hukujengea uwezo binafsi wa hata kuheshimu na kuthamnini wengine bila kuwadharau.

Kumalizia safari hii ya Urahisi wa Njia Sio Uhakika wa Safari jifunze kujenga mafanikio yako kwenye msingi utakaodumu vizazi na vizazi na hata ambapo hautakuwepo lakini mafanikio yako yatakuwepo na kuelezea sifa zako nzuri  kwa jamii nzima ya wanadamu.Fikiria umekufa halafu Kizazi ulichokiacha kinatukanwa na mafaniko ya wizi iwapo utakuwa na bahati ya kuona huko ulipo utajisikiaje.

Tukatane tena Week Ijayo Kwenye Punch Of The Week