Ukomavu kwenye matumizi ya mitandao ya jamii ni swala linalopaswa kwenye jamii ya Watanzania na matumizi ya vyombo mbali mbali vya habari.Je ivi unajisikiaje unavyoyasema mabaya ya mwenzio kwenye mkusanyiko mkubwa wa watu ili hali wewe una ya kwako?Matumizi ya mitandao ya kijamii na Media kwa ujumla inaonyesha namna gani mtu alivyokomaa kwenye uwezo wa kuchambua na kuendesha vitu kwenye maisha yake.Imani na jamii mbali mbali zina mifumo yake ya kutoa hukumu kwa wahusika wanapokosea na sio kuchafuana kwenye mitandao na kuwaacha wengine wakiwa mithiri hawajavaa nguo.Tafakari unasikikia siku Baba yako Mzazi naye amewekwa kwenye Media au kwenye mtandao wa Jamii na ameelezewa mabaya yake Je Utafurahia au utahuzunika?

1.Ki-Imani

Kila imani  ina mfumo wake wakutoa adhabu pale mtu anapokosea iwapo taaratibu za kushtaki kosa husika mahali husika.Inanishangaza sana kuona kosa la mtu mmoja wa Imani fulani linapochukuliwa na mtu wa Imani ile ile mwingine na kwenda kulishikilia bango na kulitangaza kwa watu wengine wasio wa Imani ile.Je unafikiri watu wa Imani nyingine wanawafukiriaje watu wa Imani ambayo mmoja wa waumini wake makosa yake yamewekwa hadharani.Je unajengaje nyumba yako mwenyewe  kwa kubomoa kila baaada ya kumaliza kozi moja ya ujenzi wa matofali?Ufalme ukishajifitini wenyewe hata siku moja hauwezi kuendelea Mbele.Kabla haujaamua kusema mabaya ya mwingine hadharani kwanza jiulize wewe hauna mabaya?Kumbuka kila mtu anachopanda ndicho utakachovuna.Ukimsema vibaya mwenzako wewe subiri tu kuna siku na wewe utasemwa vibaya zaidi na unapoelezea mazuri ya mwenzako tarajia kuna siku watu wataelezea uzuri wako.Baada ya Kufa ni hukumu kumbuka mahesabu yote tunayamaliza hapa hapa.

2.Ki-Jamii

 Kila kwenye jamii ya watu kuna taratibu na sheria husika za kudhibiti wahalifu wa makosa.Je unapomsema mtu hadharani bila kwenda kwenye mamlaka husika je unakuwa umsaidiaje muhusika na wanajamii wengine wasipatwe na tatizo ambalo lilishakukumba kwa kutendewa ubaya na mtu husika au jamii husika ya watu.Facebook na mitandao mingine ya kijamii ikiwa ni pamoja na media mbali mbali kazi yake sio kuelezea na kuonyesha ubaya wa wengine bali kuhakikisha jamii inapata habari kamili na mafunzo ambayo yana tija kwenye jamii.Iwapo unahisi kuna kosa na matatizo juu ya tuhuma kwa watu fulani fwata taratibu za kisheria na kijamii ili kuwasaidia wengine na sio kuishia kuchafuana.Kumbuka unapomchafua mtu akaamu kukufwatilia kisheria na kitaratibu unaweza kushtakiwa na kuadhibiwa kwa kuongea vitu ambavyo havina tija na uhakika kwenye jamii ya watu.

3.Uasili wa Dunia

Namna ulimwengu ulivyotengenezwa na ulivyoumbwa na Mungu ni namna ya ajabu sana.Kumbuka unapofanya kitu kizuri hata kama haukulipwa mazuri kwa muda huo kabla haujaondoka kwenye sayari hii ndivyo utakavyolipwa.Unapoendelea kuelezea makosa ya wengine na ipo siku kabla haujaondoka lazima na sisi tutasikia makosa yako na mabaya yako makubwa kuliko ulivyoelezea ya wengine.Epuka kuwa msemaji wa makosa ya wengine tumia muda wako kuendesha mambo mema na kuwasemea wengine maneno mazuri.Iwapo unaona hauwezi kuchukua hatua basi ni afadhali unyamaze kuliko kuelezea makosa ya wengine mahali pasipo sahihi.Hata siku moja usitegemee kupanda kokoto ukavune maharagwe.Kile unachopanda ndicho unachovuna.



Mwisho,Mitandao ya Kijamii sio sehemu ya kuhukumu dhambi za wengine.Iwapo unaona mtu wa imani yako au wa jamii yako amekosea tafuta msaada ya kisheria na kitaratibu kwenye mahala husika Facebook na kwenye media sio sehemu sahihi ya kuelezana mabaya bali ni sehemu ya kuisadia jamii kuapata maendeleo chanya na yenye tija kwa jamii yetu na taifa kwa ujumla .Safari ni ndefu kwa watanzania kwenye matumizi ya mitandao ya jamii na media kwa ujumla mpaka tukifikia ukomavu wa safari hii basi tumeshajeruhi na kuharibu maisha ya watu wengine wengi sana.


"Ukiona hauwezi kuficha Uchi wa Baba yako Basi Ipo Siku Utamcheka Mkweo kwa Utupu wake."
Kwa muda mrefu kidogo nchi ya Tanzania ambayo imekuwa ikiitwa Kisiwa Cha Amani ili hali si ukweli ila imekuwa Kisiwa Cha Utulivu na Uoga miongoni mwa wananchi wa Tanzania.Kwa Muda wa Miaka ya Karibuni kumekuwa na kujitokeza kwa aina mbali mbali za vurugu haswa zinazojihusisha na Muonekano wa Kidini lakini Pia na Katika Muonekano wa Kimaslahi kati ya Viongozi wa Serikali na Wananchi wa Nchi yenye Utulivu.Nimekuwa nikijiuliza mengi kila kukicha fujo zinatokea na hakuna ambaye anasimama kuzikemea kwamba haipaswi kuwa namna hii ilivyo sasa.Lakini matokeo yake mambo yalivyo watu wamekuwa wakikaa kimiya na viongozi wamekuwa wakivunga.Je ni nani anayefaidika na Hizi Vurugu zinazoendelea?

1.Vurugu zenye Muonekano wa Kidini.
Vurugu hizi kila kukicha zimekuwa zikiongezeka bila sababu zinazoeleweka na zimekuwa zikifungiwa macho na viongozi wamekuwa wakiendelea kuvunga kanakwamba hakuna kinachotokea kwenye nchi yetu.Taasisi za Dini za Upande mmoja zinaposimama kusema ukweli juu ya Vurugu zinazoendela Utasikia Serikali inasemama na kuzikemea kwamba hazina haki ya Kuwa wasemaji ili hali waumini wa Taasisi wa Dini hizo wamekuwa Wahanga kila kukicha.Je Ni Serikali au Baadhi ya Watu wachache wanaofaidiaka na hizi Vurugu?
Siku za Karibuni kumekuwa na mvutano mkubwa kati ya Upande wa Dini ya Ki-Islamu na Wakristo na Upande mmoja umeonekana ukitetewa na kukaliwa kimiya kwa kila wanachofanya ili hali upande mwingine ukitishia kuchukua hatua huonekana na mbaya Je nani anayefaidika na Vurugu hizi?
Miaka yote tumekuwa tukiishi kwa utulivu huu pamoja na tofauti tuliozo nazo lakini hakuna mtu aliyethubutu kumshambulia mwenzake wala kumdharau Je kwanini wakati huu iwe hivyo?Basi kwa mtazamo wa haraka haraka kuna watu ambao watakuwa wanafaidika moja kwa moja au indirect kutokana na muendelezo wa Vurugu hizi.

2.Vurugu zenye Muonekano wa Kimaslahi(Kifedha na Kiuchumi)
Tumeshuhudia fujo kubwa kwa ndugu zetu wa kanda ya kusini juu ya sakata la gesi linaloendelea.Wananchi wenye mumkari wameshindwa kuvumilia juu ya maamuzi wanayofanyiwa wao bila ya wao kushirikishwa kwa muda mrefu nchi hii watu wachache wamekuwa wakiamua nini kifanyike na nani afanye na nani afaidike kwenye kila mradi unaohusisha fedha nyingi.

Wananchi wanapoamua kudai haki zao kwa kutetea kile wanachotaka wao na wanachoona ni sahihi hugeuka kuwa adui wa maslahi ya watu hao wachache..Miradi Mingi imekuwa ikiendeshwa bila uwepo majadiliano na maamuzi ya wananchi wenyewe kuamua kitu gani wanataka juu ya Rasilimali zao lakini watu wachache wakiamua basi ndio yanatendeka.Hakuna elimu ya kutosha juu ya miradi na faida ambazo wananchi watapata baada ya Serikali kuingia Ubia na Mashirika ya Kimataifa.

Miradi Mingi imekuwa ikiendesha kiholela holela na pindi wananchi wanapodai haki zao kwa njia ya amani hawasikilizwi na matokeo yake huundiwa zengwe na kuonekana ni wabaya.Na wanapoamua mutumia nguvu huonekana ni wakorofi na wavunjifu wa amani?Je ni heri fujo na uvunjifu wa amani utokee sababu ya watu wachache?Muda utafika watu hawatakuwa tayari kuendelea na ujinga huu watu watasimama na ndipo muda huu wa neema utakapokuwa umekwisha na hapo ndipo nchi itashindwa kutawalika sababu ya misingi mibovu inayojengwa leo.

Mwisho,Niwazacho Mimi Kuna mtu au  watu watakuwa wanafaidika na Vurugu na Uvunjifu wa Utulivu tulio nao la sivyo basi hatua za Makusudi zingekuwa zimechukuliwa na katika kutatua matatizo haya ambayo kila siku yamekuwa yakikua na kuongezeka bila sauti za viongozi.

Je ni nani anayefaidika na Vurugu zinazoendelea Tanzania?

MUNGU IBARIKI AFRIKA,MUNGU IBARIKI TANZANIA
Kwa Mara Nyingine Napenda kuchukua nafasi hii kuwaasalimu wadau wote wa blogu katika mwaka 2013,Maana kwa Mara nyingine leo Ndipo tunakuta kwenye Programu yetu ya Kila Ijumaa iitwayo Punch of The Week.Leo katika Punch of The Week tumeamua kuangalia vitu kwa jicho la Pembeni kidogo lisemalo Urahisi wa Njia sio Uhakika wa Safari.

Maisha yetu ya kila siku muda mwingine yamekuwa hayana dira sababu ya kukosa mwelekeo sahihi wa kufanya vitu na kuviendeleza huku tukidhani kwamba hii ndio njia sahihi na huo ndio umekuwa mfumo ambao tumekuwa nao katika kila nyanja.Vitu vingi tumekuwa tikivifanya kwa zima moto huku tukidhani kwamba tunaweza kufikia kilele cha mafanikio ambayo yanaweza kudumu daima.

Maisha yetu yamejengwa kwenye kupenda njia za makato kuliko kufwata kanuni ambazo zipo na ndizo za uhakika kwenye maisha yetu kama wanadamu.Hakuna mtu ambaye amejenga mafanikio ya kudumu kwa kutumia njia za mkato.Uasili wa Dunia jinsi ulivyo ni kwamba ukipata kitu kwa dhuluma kitaondoka kwa dhuluma iwe leo au kesho.Mara nyingi tumeshindwa kuangalia mbele tumeangalia matokeo makubwa ya sasa lakini tunasahau kwamba maisha yanaendelea.Wahenga walisema Ukiua kwa Upanga Basi na Wewe utauwawa kwa Upanga wakimaanisha namna kitu kinavyopatikana ndivyo kitakavyoondoka.


Mafanikio yanayodumu ni yale yanayojengwa kwa mfumo wa Haki na kujituma siku zote.Hakuna mazingaombwe kwenye mafanikio wala uchawi.Iwapo unategemea uchawi,wizi na dhuluma kupata maendeleo habari nilio nayo ni kwamba tunasubiri anguko lako siku yeyote kuanzia sasa hata kama leo unaonekana unakula bata na kufurahia lakini kanuni za asili za kuendesha dunia huwa hazibadiliki siku zote.

Kuna hasara njinyi sana kwenye kutegemea kupata vitu kwa njia ya mkato kuliko kufwata kanuni za msingi za kufanikiwa katika jambo lolote.Je wewe unafikiri ungekuwa umezaliwa siku ya kwanza then siku ya pili tunakuona unakimbia je unafikiri sisi tunaokuzunguka tungefikiria vipi?Au wewe mwenyewe ungewazaje?

1.Njia za Mkato mara zote hazitoi jibu la uhakika na linalodumu siku zote.Njia za mkato au zima moto husaidia kutatua tatizo kwa muda tu lakini mara nyingi hakuna uhakika wa kudumu wa suluhisho ambalo litadumu siku zote za maisha.Fikiria iwapo haujawahi kufanya biashara siku zote za maisha yako ghafla unakuwa na biashara kubwa kesho asubuhi unafikiri biashara hiyo itadumu?Jibu ni hapana sababu hauna mufundisho ya msingi juu ya uendeshaji wa biashara na namna ya kucheza na mzunguko wa fedha.Unapofwata hatua mbali mbali unajenda uwezo binafsi wa kujifunza na kuwa na uhakika wa kutokurudia makosa ambayo hautaweza kuyarudia tena.Kumbuka siku zote Vitu rahisi gharama yake ni kubwa zaidi.Mfano Mzuri ni pale ambapo tunapoumwa kichwa kwa ghafla huwa tunameza dawa za kutuliza maumivu tu lakini huwa bado hatujatatua ugonjwa wa msingi ambao umepelekea kuumwa kwa kichwa.Ili kutibu na kufahamu ugonjwa husika ni lazima umuone daktari upate vipimo na ndipo upewe dawa kamili za kutibu ugonjwa husika.

2.Mtu anayetegemea njia za mkato mara nyingi huwa hakomai kitabia na namna ya kuendesha vitu vyake maishani mwake siku zote.Unapoiona tabia fulani ya mtu ndivyo alivyo mwenyewe.Tabia hujengeka kutoka na mfumo wa maisha wa mtu wa kila siku alio nao.Iwapo unafikiri kwamba wizi ndio njia sahihi ya kuishi basi siku zote hautajua kwamba kuna namna nyingine ya kuishi sababu ndivyo ulivyojijengea.Maisha huenda na kubadilika kila siku kuna siku utashindwa kuiba je utaishi kwa namna gani?Ukiona mtu anakuwa na hasira na maamuzi mabaya siku zote usikimbiliea kumlaumu fwatilia ni wapi ameanzi na amekulia katika mazingira gani maana hayo ndiyo yaliyojenga mfumo maisha yake.Mara zote nimesema hakuna mtu anayeweza kusihi nje ya information mtu ambazo anazo kichwani.Na information hupatika katika njia tofouti tofauti  
(I)Mazingira 
(II)Marafiki 
(III) Malezi 
(IV)Vitu mtu anavyosoma kila siku n.k.
Ukomavu wa tabia nzuri huja kutokana na mafundisho magumu ya kufwata kanuni mbali mbali na mfumo wa asili wa dunia ulivyoweka bila kukubali kufwata njia za mkato na urahisi.

3.Mafanikio ni Mchakato na sio Mkato.Mafanikio yanayodumu yamejengwa kwenye njia ngumu ambazo mara nyingi tumeambiwa lakini tumekuwa tukipuuzia.Mafanikio yanayodumu yamejengwa kwenye uvumilivu ambao umejengwa katika muda mrefu ambao ndani yake kunakuwa na mchakato mgumu wa mafundisho ya asili na ambayo muda mwingine sio rahisi kuyaelewa na usipokuwa makini utaishia kulalamika na kukata tamaa.Waswahili Wanasema Njia Nyembamba na isiliyosonga ndio Inayoelekea uzimani n lakini njia nene ndio inayoelekea upotevuni.Hakuna mkato kwenye mafanikio yanayodumu.

4.Njia ya Mkato haikujengei nidhamu ya kuheshimu na kuyatunza mafanikio ambayo umeyapata.Unapojifunza kujijenga kwa njia sahihi unajenga uwezo binafsi wa wewe kuheshimu na kuthamini mafanikio ambayo umeyapata kwa nguvu zako mwenye pia unasikia ufahari wa kujivunia kila ambacho umekipigani siku zote.Fikiria kama umetoa mtoto au mke wako sadaka kwa mizimu unafikiri wakati wa kujivuni mafanikio yako utajivunia Damu uliyoimwaga ya wapendwa wako au utakuwa mnafiki wa kujifanya unafurahi wakati ki ukweli moyoni unajua sivyo ilivyo?Mafanikio yaliyopatikana kwa juhudi binafsi hukujengea uwezo binafsi wa hata kuheshimu na kuthamnini wengine bila kuwadharau.

Kumalizia safari hii ya Urahisi wa Njia Sio Uhakika wa Safari jifunze kujenga mafanikio yako kwenye msingi utakaodumu vizazi na vizazi na hata ambapo hautakuwepo lakini mafanikio yako yatakuwepo na kuelezea sifa zako nzuri  kwa jamii nzima ya wanadamu.Fikiria umekufa halafu Kizazi ulichokiacha kinatukanwa na mafaniko ya wizi iwapo utakuwa na bahati ya kuona huko ulipo utajisikiaje.

Tukatane tena Week Ijayo Kwenye Punch Of The Week
Mwanamuziki wa Injili anayeishi nchini Sweden Katika Mji wa Malmo anayejilikana Kwa Jina Rachel Sharp katika siku ya Jumamosi 26/1/2013 alizundua Albamu yake ya Pili hapa nchini Tanzani ijulikanayo kwa jina "NI MUNGU WA AJABU" yenye jumla ya nyimbo 10 zilizo katika mfumo wa CD na nyimbo 8 zilizo katika DVD.
Rachel Sharp alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari katika Eneo ya Nyumba yake katika Eneo La Tegeta Ambapo ndipo uzinduzi ulipofanyika alitoa Rai kwa Wanamuziki wa Tanzania Kuendelea Kuenzi Muziki wetu wa Asili kama Ilivyo Mdumange na Mdundiko pia aliongezea kwa kusema Lugha ya Kiswahili kwenye Muziki inalipa zaidi kuliko ilivyo Lugha za Kigeni tunazojaribu kutumia.Akitoa mkazo zaidi aliendelea kusema tuache kuiga miziki ya watu na sisi tukae chini tubuni aina yetu ya muziki ambayo inaweza kutumika kama utambulisho wetu kwenye soko la kimataifa la Muziki.


Mc wa Event Ritha Chuwalo akimtambulisha Rachel Sharp

Rachel Sharp akiwatambulisha Wazazi wake Kwa Waandishi
Rachel Sharp Akitoa Wito kwa Waandishi kufikisha Ujumbe alioukusudia

Mume wa Mtangazaji Maarufu Zawadi Machibya akiweka wakfu Albamu ya Rachel Sharp.

Hadi Kieleweke.....Mwanamuzi wa Injili Rachel Sharp akiwa kwenye Stage 

Mwanamuziki wa  Injili Rachel Sharp akienda sawa kwenye 

Nguli wa Muziki Nchini Tanzania Upendo Kilahiro akifanya kazi kwenye Stage
Rachel Sharp na Upendo Kilahiro wakiwa kwenye Jukwaa Moja
                                           
Mwisho wa yote Rachel Sharp alisisitiza Kuwa Mafanikio Yetu hayaji kirahisi kwenye Kila Kitu imetupasa kujituma katika kila jambo bila kujali wengine wanatonaje,akimaliza alisema Upendo na Umoja Miongoni mwa wanamuziki wa Injili kukaa chini na kuja na ubunifu mpya kutawaongezea mafanikio katika tasnia ya Muziki wa Injili ndani na Nje ya Mipaka ya Tanzania.
Miaka Michache iliyopita Tanzania kulikuwa na Blogs Chache sana na tulikuwa tunajiuliza ivi mtu anawezaje kumiliki blog,Lakini baada ya muda fulani kupita watu wengi tulijifunza angalau namna ya kuanzisha na kuendesha blog.Miaka ya 2005 teknolojia ya blog Tanzania ilikuwa ngeni kidogo lakini nashukuru kwamba kadri siku zinavyozidi kwenda blogs zinaongezeka na zimekuwa nyingi zaidi lakini pamoja na haya yote kutokana na ukuaji wa teknolojia hii nchi yetu imekuwa taratibu sana kutunga sheria au kufanya mabadiliko ya sheria mbali mbali yatakayoendana na ukuaji wa teknoloji mbali mbali.Sina mengi ya kujadili kwa upande huo.

Baada ya kufanikiwa kupitia blogs nyingi hapa Tanzania hata mwanzo naanzisha blog hii nilijua copying and Paste ndio namna ya uendeshaji wa blog lakini baadae baada ya kufwatilia kiundani kidogo nikajiuliza je mtu alianzisha teknolojia ya blog alikuwa na maana hii ya copy and paste au kulikuwa na maana nyingine zaidi?

Blog sio copying and Paste blog ni sehemu ya kuonyesha kile ulichonacho kwenye ubongo wako,Baada ya kufwatilia sana nimekuja kugundua tasnia ya uandishi hapa Tanzania ina Critical Thinker wachache na hata waliopo hawaandiki maswala yanayohusu jamii na maisha yetu ya kila siku katika kuikwamua jamii yetu.

Blog sio sehemu ya matangazo baada ya kufwatilia tena nimekuja kugundua yaani sisi huwa vitu vingi tunafanya kinyume nyume yaana baada ya kwenda mbele sisi tunarudi nyuma.Yaani siku hiz utakuta blog ina matangazo mpaka unaboreka,hata hamu ya kuendelea kuangalia blog hauna hamu.Na tatizo kwa walio wengi sio vibaya kuwa na matangazo lakini sababu na maana ya msingi ya kuwepo blog isifutwe au kupotezwa kwa tamaa ya fedha.

Blog ni kama diary ambayo unaweka kumbukumbu zako muhimu za maisha ambazo zinaweza kuwasaidia wengine na kuweza kutoa majibu ya maswali amabayo wengine wanayo juu ya maisha na maswala mbali mbali ya kijamii katika kila nyanja yaani kiuchumi , kijamii na hata kisiasa ili kuweza kuleta hamasa kwenye jamii yetu katika maisha yetu ya kila siku.

Je Blogger ni Mwandishi wa Habari ?Kuna tofauti gani kati ya Blogger na Mwandishi wa Habari?
Mwisho jifikirie kuna tofauti gani kati ya website na blog...Na kama blog ni website ndogo kwani kuna website kubwa....Nini maana ya neno www.ww.com na nini maana ya www.fm.blogspot.com
Then come up with answers,tuifanye tasnia ya blog kuwa kivutio na sio kero kwa watu.Fikiria na ufanye mabadiliko.Hivi ndivyo Niwazavyo Mimi

Heri ya Mwaka  Mpya kwa Bloggers Wote Wa Tanzania 2013
Wakati nchi yetu ikiwa katika mchakato wa kukusanya maoni juu ya mbadiliko ya Katiba kwenye nhi yetu asilimia kubwa ya watanzania hawajui kinachoendela kabisa na umuhimu wake katika nhi yetu ya Tanzania kwa Miaka ijayo.
Tangu nchi hii kupata uhuru hatujawahi kuwa na Katiba yetu kama watanzania bali tumekuwa na Katiba ambayo ilaandaliwa na baadhi ya watu wachache kuendesha nchi yetu.Lakini 
kadri Siku zinavyozidi kwenda tumekuja kuona Katiba iliyopo sasa haikidhi mahitaji kwa kiasi kikubwa kulingana na wakati wa mabadiliko makubwa tulio nayo kwenye namna ya uendeshaji wa nchi na mifumo yake mbali mbali kuanzia kwa Watawala na Watawaliwa.
Kinachochangaza Watanzania tulio wengi ndio tulidai mabadiliko ya Katiba kwenye nchi yetu lakini katika mchakato huu wa Makusanyo ya Maoni ya mabadiliko ya Katiba kunashangaza,Tumekuwa waongeaji sana wa mitaani na vijiweni lakini kwenye utendaji kuwasilisha maoni yetu tumekuwa wavivu.Kumbuka unanaposhindwa kutoa maoni yako kuhusu namna Katiba ya nchi yako iweje siku maamuzi yanapotolewa usiwe wa kwanza kulalamika tena.Na itakupasa kulipa gharama kwa Muda wa Kipindi Kirefu kijacho.Maisha ya nchi hii wewe na vizazi vyako vyote vijavyo inategemea unafanya nini kwa sasa.

Takwimu kutoka kwenye Tovuti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba

Katika awamu ya tatu iliyomalizika tarehe 6 Novemba, 2012, Tume ilifanya mikutano 522 katika mikoa yote tisa ingawa ilipanga kufanya mikutano 496. Hali hii ilitokana na mahitaji mapya katika maeneo mbalimbali ya mikoa hiyo na kuifanya Tume kuitisha mikutano ya ziada ili kuwapa fursa wananchi wengi zaidi. Katika awamu ya pili, Tume ilifanya mikutano 449 ambapo Awamu ya kwanza Tume ilifanya mikutano 388.
 Katika awamu hii ya tatu, jumla ya wananchi 392,385 walihudhuria mikutano. Jumla ya wananchi 21,512 walitoa maoni yao kwa kuzungumza katika mikutano hiyo na wananchi 84,939 walitoa maoni yao kwa maandishi. Aidha, katika awamu hii ya tatu, jumla ya wananchi 1,639 walitoa maoni yao kwa kuzungumza na pia kwa maandishi katika mikutano hiyo.
Mwitikio wa wananchi kuendelea kutumia simu za mkononi, ukurasa wa facebook, tovuti na posta kutoa maoni nao umeongezeka kwa kiasi kikubwa. Kwa mfano, jumla ya wananchi 27,992 walikuwa wametembelea ukurasa wa facebook wa Tume katika kipindi cha awamu ya tatu tofauti na watu 21,789 waliotembelea katika kipindi cha awamu ya pili. Aidha, ujumbe mfupi wa simu (sms) 6,909 umepokewa na Tume katika awamu hii ukilinganishwa na sms 75 katika kipindi kilichopita;
Idadi ya wananchi wanaohudhuria na kutoa maoni katika mikutano nayo imeongezeka. Kwa mfano, idadi ya wananchi waliohudhuria mikutano ya awamu ya kwanza walikuwa 189,526.  Awamu ya pili ni 325,915 wakati wananchi waliohudhuria mikutano ya awamu ya tatu ni 392,385. Aidha, wananchi waliotoa maoni kwa kuzungumza katika mikutano ya awamu ya   kwanza walikuwa 17,127. Awamu ya pili walikuwa 12,334 wakati wananchi 21,512 walizungumza katika awamu ya tatu;

Ukifwatilia hizi takwimu hapa juu utagungua Maamuzi ya Nchi hii yanye watu takribani Milioni 40 na kuendela kwa sasa watu ambao hawafiki hata milioni tatu ndio wanaamua nini kifanyike juu ya nchi hii kwa Miaka mingine Mingi ijayo.
Inatia Hasira kuona watu wachache namna hii ndio wanato maamuzi ya nch hii sisi wengine Vijiweni,kuchati facebook,Twitter,kwenye simu zetu za mkononi,Kusubiri Ze Comedi ni lini au Tamasha La Fiesta ni lini au Rose Muhando anazindua lini?
Ni muhimu kujua habari mbali mbali katika nchi lakini Kumbuka kuna baadhi ya vitu maishani mwako vinaamua hatma yako kwenye kila jambo.

Njia Ambazo Unaweza kutuma Maoni yako.

1. Njia ya simu 
+255 22 2133425
2. Barua pepe 
katibu @katiba.go.tz
3. Tovuti ya Tume ya Mbadiliko ya Katiba 
http://www.katiba.go.tz/index.php/toa-maoni-yako
4.Facebook
https://www.facebook.com/pages/Tume-ya-Mabadiliko-ya-Katiba-Tanzania/323414977745643?fref=ts
5.Tume ya Mabadiliko ya Katiba
Makao Makuu
Sanduku La Posta 1681,
Dar es Salaam, Tanzania.

MUNGU IBARIKI AFRICA , MUNGU IBARIKI 
TANZANIA
Katika namna ambavyo mfumo wa kuishi umewekwa na uhalisia wa mambo ulivyo katika sayari yetu iitwayo Dunia Kukua ni mchakato na sio Muujiza.Kitu chochote ili kikue kufikia utimilifu lazima kinapitia mchakato fulani kabla ya kufikia ukamilifu wowote.Hakuna kitu ambacho kinaweza kukua ghafla bila kupitia mchako wa aina Yoyote iwe ni Kiroho au Kimwili.Binadamu ili kufikia hatua ya kukua na kufikia na ukamilifu wake lazima kuna hatua na mchakato fulani amepitia.lazima Mtoto azaliwe,Akue afikie Ujana ,Uzee ndio Unakuwa tamati na kifo huchukua mkondo wake.
Katika maisha yetu ya kila siku tumekuwa tukikumbana na changamoto na vitu mbali mbali ambavyo tunashindwa kuelewa kanuni za msingi za kuendesha vitu.Katika kila unachofanya lazima kwanza kinaanza na kuzaliwa,Hatua ya Katikati ndipo utimilifu wa juu wa kitu hufikia.Unapomuona mtu mzima leo(Mzee) lazima alipitia hatua zote tatu Muhimu.


1.Kuzaliwa(Formation)
Kuzaliwa ni moja ya hatua muhimu ya maisha na uhai wa kitu chochote,katika hatua hii unaweza ukawa umependa kitu kizaliwe au kisizaliwe lakini mwisho wa siku wote tunajikuta kwenye uwanja wa Mapambano.Je unaendelea kulaumu kwa nini kitu fulani kilizaliwa?Hapana,yaani hata kama ukilauma ndio tayari kimeshaonekana kwenye Ulimwengu wako.
Mfano Kuna watoto walizaliwa kwa Uzazi wa Mpango na Wengine Ghafla Bini Vuu wakajitokeza kwenye Hii sayari,Aliyezaliwa kwa uzazi wa mpango na wa Ghafla Bini Vuu Mwisho wa siku wote wako kwenye Sayari hii itwayo Dunia.Kulaumu kwako hakukufanyi urudi tumboni kwa Mama bali ndio Umeshafika sasa.
Yaani Samaki aliyevuliwa kwa Baruti na Wengine kwa Njia Sahihi lakini mwisho wa Yote wamevuliwa na wameshatolewa baharini.

Hapa ndivyo ilivyo kwenye maisha yetu ya kawaida unaweza ukapanga kufanya kitu fulani kwenye maisha au Usipange lakini mwisho wa siku ndio umeshajikuta humo.Je Unafanyaje?Kulaumu hakutasaidia kutatua hilo tatizo au hicho kitu ambacho umekutana nacho.

Kitu kinapozaliwa kinaweza kisiwe na mwelekeo sahihi lakini wewe mlezi wa kitu ndio una uwezo wa kufanya kitu kiwe sahihi,ndio Maana Wahenga husema Mtoto uleavyo Ndivyo akuavyo.usitegemee Utamlea mtoto katika hali ya uvivu na Uzembe alafu akikua awe Mchapa Kazi...
Unapotaka kuanza Biashara lazima Izaliwe kwanza,Unapotaka Kuanza kazi lazima iwe na mwanzo wake...Hakuna kitu kina kua tu...Kumbuka Hata Mbuyu ulianza kama Mchicha Ila Sijui...Kiroboto alianza kama nini....mwisho wa Siku Kukua ni Mchakato na Sio Muujiza........


2.Kukua(Growth)
Siku hizi kwenye jamii kumekuwana matatizo mengi sana ambayo watu wengi tumeshindwa kupata majibu kwa sababu hatujui mchakato wa vitu hivyo vimeaanzi wapi,Mfano Wakati unakuwa nyumbani kwenu unakuta Style ya Maisha ni Matusi na Ngumi kuanzia kwa Baba na Mama Mpaka Kaka/Dada zako.Je Unahisi hapa itakuwaje?Je unapomwona Mtu ni Mlevi unahisi alinza ghafla tu..Hapana Kukua kwenye jambo lolote ni Mchakato na sio Muujiza hata Ukisoma kwenye Vitabu vya Dini Dhambi ili iwe dhambi Kuna mchakato imepitia mpaka kufikia Tamati
Kufikia hatua ya kukua kwenye kila jambo inategemea msingi uliojengwa tangu mwanzo wakati jambo linaanza..Unaapomwona mfanyabiashara mkubwa leo amefanikiwa hakuanza kama uyoga bali kuna mchakato alioupiti kugia Hapo.Mara nyingi tunasahau kwamba hakuna kitu ambacho kinaibuka tu kwenye maisha Yetu ya kila Siku..tangu Mwanzo ukijenga tabia ya kusoma vitabu na kutafuta maarifa na kubuni vitu na ukaendelezwa ndivyo utakavyokua.
Usimshangae mtu alivyo Leo Maana Hukuona Jana Yake,Tabia na Maisha ya Mtu ilivyo leo Inatagemea kwenye hatua za mwanzo alianzaje?
Mara nyingi nimekuwa nikipishana na watu sana kwenye kuwahukumu watu kwenye maisha yao kwa sababu sisi tunaona matokeo lakini hatujui huyu mtu alianzaje...Imekupasa kulaaumu msingi wake ulivyojengwa na sio hii hatua ya Katikati ya Kukua.


3.Maturity(Ukomavu)
Hatua iliyopita ni moja kati ya hatua muhimu ambazo zinaweza zikatoa Majibu ya maswali mengi kufikia kuelekea hatua hii ya Ukomavu(Maturity).
Kutokana na mfumo wa Malezi yetu Watanzani kama si waafrika tulio wengi tunakuja kugundua vitu vingi si sahihi kwenye hatua ya Kukua wakati msingi ulishajengwa vibaya.Mfano wa Ghorofa Ikishajengwa vibaya toka chini kwenye Msingi ndivyo itakavyoendelea Mbele kwenye Ujenzi.Iwapo Fundi hakushtuka basi ujenzi huo utaendelea mpaka mwisho wa safari na Mwisho wa Siku tunashuhudia Ghorofa zinaanguka na kuua watu.
Pamoja na maisha yetu ya kila siku kujengwa Hivyo mpaka tikufikia ujana ndio tunagundua kwamba hiki hakikuwa sahihi Je unafanyaje?Je unaendele kuishi kwenye Ubaya?Je Unavunja Msingi huo Uanze tena?
Kuna maswali mengi ya kujiuliza sasa.
Unapokua kipindi cha Ujana unaweza kufanya Mabadiliko Mengi sana ambayo yanaweza kuleta matoke chanya kwenye kipindi cha Ukomavu wa Jambo lolote.Hakikisha unafanya maamuzi yalio Sahihi kwenye Jambo lolote..hakuna Muujiza...hapa...Hata Uwapo unataka kukuza kiwango chako cha Kufikiria vitu anza mwanzo na utsonga mbele taratibu hakuna Muujiza hapa ....
Jambo Lolote linapofikia mwisho ndipo tunaona Matokea kutokana na hatu mbili zilizopita na Hapa ndio watu wengi tunatoaga hukumu ya Maswali Mengi sana na vitu vingi sana maishani mwetu....Katika yote ukumbuke hili....Growing is a Process Not A Miracle..................

                      
             ...................Kukua Ni Mchakato   Na .............Sio ...............Muujiza..........................
Baada ya wiki Moja iliyopita kwenye Miji ya Dodoma Na Mbeya kutikiswa na tukio la Campus Night,Jana usiku(23/11/2012) ilikuwa ni zamu ya mji wa Singida kutikiswa na tukio hili Adhimu nchini Tanzania,Rise and Shine ndio ilikuwa theme mjini Singida,Baada ya blog hii kupata habari kutoka kwenye chombo cha kuaminika kwamba zaidi ya watu 700 waliamua kumpa Yesu maisha yao huku takribani watu yapata zaidi ya 5000 wakihudhuria kwenye tukio hili ambalo linatokea mara moja tu kwa mwaka

Pata Matukio katika Picha 



Hapa tupo Katika ya Safari kuelekea  Singida 
Victor & Chavala

Ndani Ya Singida

Costa Mbili Watu Full...

Watu Wakifanya Furaha za Shangwe kwa Bwana


Samuel Yonah... the best guitarist, composer, arranger of all times


Watu pipoz...


The audience Praising and dancing


Prosper ,Steve Wambura,and Chavala


Mungu wa Mapendo...


Students Joint Mass Choir


Papaa Ze Blogger(T-shirt Nyeupe) Mc wa Shughuli akienda sawa


Pastor Dr Huruma Nkone na Daniel a.k.a Kenge wakimsifu Mungu


The Mass Choir perfoming


Hata Baada ya Kumaliza Honey Moon siku chache zilizopita lakini  Steve Wambura hakuacha kumsifu Bwan


The Empire wakifanya Vitu vyao


700 peoples received Jesus


Steven Wambura a.k.a Le grand Mopao akiendesha jahazi
Kama kawa Swahiba Mc Pilipili Hakubaki Nyuma..Pasua Mbavu Singida


Rivers of Joy International wakienda Sawa kwenye Praise and Worship


Katika Yote Ujumbe Mkuu ulikuwa Hauwezi songa Mbele Bila Yesu...Yesu Ni Jibu La Mambo yote
Mara zote tumekuwa tukifanya vitu tukijua kwamba tupo sahahi lakini mara nyingi tumekuwa hatupo sahaihi kutokana na upeo wetu mdogo wa kufikiri vitu kwenye nyanja mbalimbali na athari mbali mbali zokanazo na vitu mbali mbali.Unapofanya kitu kwa fikra halisi na utimilifu wa mambo ndipo unaweza kugundua kwamba uko sahihi hapana mara nyingi matokeo mazuri ya kile ulichofanya ndio hutupa jibu kwamba input ambayo umeiweka/umeitumia ilikuwa sahihi au hapana.Maamuzi yetu  huadhiriwa na vitu mbali mbali na hutufanya tuwe sahihi au hapana kutokana na vitu hivyo.Kwenda Kanisani Hakukufanyi kuwa Mkristo na Wala Kusimama Karibu na Karakana ya Magari hakukufanyi kuwa Gari.

1.Mazingira

Mazingira tuliyokulia yanamchango mkubwa sana kwenye maisha yetu na huwa na athari kubwa juu ya vile vitu ambavyo tunaishi na na namna tunavyofanya maamuzi yetu.Mfano Siku Moja tulipokuwa Kanisa fulani...Mzungu alisimama akitoa ushuhuda kwamba Yaani Maisha Mabaya sana kwake na Amechoka Kula Kuku kila siku,Wakati aliposimama Mama mmoja akaeeleza namna ambavyo hawana chakula kabisa.Ukifwatilia kinachowatofautisha hawa watu ni mazingira waliyo kulia.Lakini pamoja na yote Mazingira yanaweza kukufanya uwe sahihi au hapana kutokana pia na mtazamo wako binafsi.....Kwenda Kanisani hakukufanyi kuwa Mkristo wala Kusimama karibu na Karakana ya Magari hakukufanyi kuwa Gari

2.Information 

Habari za kila siku ambazo tunazipata zinaathiri sana maisha yetu tunatoishi kila siku na katika nyanja tofauti tofauti embu fikiria kama tungekekuwa toka tumezaliwa kwenda shule isingekuwa ni lazima/kungekuwa na mfumo mwingine wa kusoma,Habari hizo ndizo zingekuwa chanzo cha namna tunavyofanya vitu vyetu na namna tunavyoralate na wengine na namna tunavyofanya maamuzi ya maisha yeyote kwenye maisha yetu.Fikiri kama tungeambiwa kula makande ni sumu toka tunazaliwa mpaka tulipo maamuzi yetu yangejengeka kwa namna hiyo bila kuzingatia maswala Mengine.Hembu fikiria kwamba tungekuwa tunambiwa Ukimwi hausababishi kifo na hauna madhara kwenye maisha yetu ya kila siku je ingekuwaje?

3.Watu

Marafiki,Ndugu na jamaa wanamchango mkubwa na maisha yetu katika kila tunachokifanya,Ndio maana wahenga walisema ukitembea na mwizi na wewe utakuwa mwizi basi si kama mwizi kwa asilimia zote bali lazima hata uamulie kuwa kibaka,Chuma hunoa chuma siku zote.Marafiki wanaokuzunguka wanamchango mkubwa sana kwenye maisha yako,Wataalamu wanasema ukitaka kujua pato la la mwezi kwene ajira yakeChukua marafiki wake watano wanaomzunguka kwa ukaribu sana,Tafuta wastani wao unaweza kujua pato lake la mwezi.Lakin pamoja na hayo yote ni vizuri kuaangalia marafiki ,ndugu na jamaa wanaotuzungumza wanamchango gani kwenye fikra zet na namna tunavyoishi kila siku.Haiwezekani ukatembea na Chizi wewe ukaonekana mwenye akili.

Pamoja na mambo yote unaweza ukawa umeathiriwa kwa namna mbaya kutokana na sababu hizo tatu za ambazo ndizo zimekuwa sehemu kubwa ya maisha yetu lakini kumbuka bado unaweza kufanya vizuri zaidi
Hata kama umefanya vibaya sana bado unaweza ukabadilika na kufanya vizuri zaidi...Kumbuka ...Kwenda Kanisani Hakukufanyi kuwa Mkristo wala Kusimama Karakana ya Magari Hakukufanyi Kuwa Gari..

...Kwenda Kanisani Hakukufanyi kuwa Mkristo wala Kusimama Karakana ya Magari Hakukufanyi Kuwa Gari..
Rising The Standard ndio ilikuwa kauli mbiu katika Campus Night iliyofanyika katika Mji wa Mbeya siku ya Ijumaa ya tarehe 16/11/2012 bila kusahau mji wa Dodoma nao uliendelea kutikiswa na Event hii ya Campus  Night yenye kauli mbiu My Life,My Love , My All.Naam matukio haya pacha yaliwakutanisha wanafunzi wa elimu ya vyuo mbalimbali katika maeneo husika

Kama ilivyo ada Mc maarufu wa Mji Papaa Sebene ndio alikuwa mshereheshaji wa Event iliyofanyika Mbeya naam...


Katika Segment ya Comedy Mc Pilipili alitikisa mji wa Mbeya,Kama ilivyo ada ya King Chavalla hakukosekana akiwaacha wanafunzi hoi kwa comedy

Wasemaji wa Siku hiyo katika Mji wa Mbeya walikuwa ni Pastor Dr Huruma Nkone,Rose Mushi,Dr Kimambo,Mr Msigwa na Dr Maboko,Wote hawa walizungumzia namna ya ku-rise Spiritual Standard pia na maisha ya kawaida tu ya mwamini katika eneo la uanafunzi



Pastor Dr Huruma Nkone alisema ushalobaro wala utoz toz na u-sista du haumsaidia mtu kuwa na clear future only Jesus can Transform your life na ata-rise standard zako..Kwa mara nyingine tulishudia Radical Gospel ya Dr Huruma Nkone isiyokuwa na kificho.

Nabii Mke a.k.a Rose Mushi alishusha sindano za kurise starndard zako kwenye swala la mahusiano.Alisisitiza kuwa bila Yesu mahusiano yako ni bureee...Alikazia akasema ni Bora uachuke kwa kumtii Mungu kuliko kuumtii mwanadamu.Kama ilivyo ada akiwa hana mic unaweza kumwangalia na kumfikiria unavyopenda..Kosa linafanyika tu pale akiwa na Mic....Ukumbi mzima ulikuwa moved na Nguvu ya Mungu through Rose Mushi.

Dr Kimambo aliongelea swala la Academic and Execellence pindi uwapo shule pia..Akatoa kanuni na mfumo wa namnq ya kurise standard zako na namna ya ku-execel academically..It was more than Powerfully...Kama ulimisi hii na wewe ni mwanafunzi wa mji wa Mbeya pole.Katika yote aliyoongea alisema huwezi fanya chochote bila Yesu.

Dr Maboko aliendelea kuongelea swala Ujasiriamali kwa wanafunzi,alijaribu kushare expirience yake katika swala zima la ujasiriamali bila kusitasita alieleza namna ya kurise standard zako katika swala zima la fedha huku ukiwa bado ni mwanafunzi.Lakini mwisho wa Yote alisema ukitaka kurise standard zako ,Yesu ni jibu la lako.

Mr Msigwa .a.k.a Branch Manager wa CRDB Mbozi mjini,aliendele kusema zaidi kuhusu Mahusiano na Changamoto ambazo kama vijana tunazipitia alieeza namna bora ya kupata mke au mume ambaye anaweza akakufaa na ukaendela kuonekana kuwa bado wewe ni bora na unafanya vizuri kati maswala mengine ya maisha pia
Rose Mushi a.k.a Nabii Mke akiendelea kufwatilia nini kinachoendelea kwenye Campus Night

Pastor Dr Huruma Nkone akeendela kukata Gospel ya ulweli

Music Director Pastor Mathew Sasali pamoja na Mama Pastor Rebecca Sasali wakiongoza jukwaa la Praise and Worship 

Sauti ya Dubu ukipenda Mr Dr Nyanda akiwa kazini kama Mc wa siku hiyo

Praise and Worship chini ya Mama Pastor ikifanya kaziii.....

Watu Pipoz

Sebene ya Yesu ikiwafanya watu wadance

Twende Sawa

Watu Pipoz

Moja ya Matunda ya Campus Night zilizopita akitoa ushuhuda

Mc Shupavu a.k.a Papaa Ze Blogger akiendelea na Kaziii

Twende Sawaaa

Makofi kwa ajili ya Yesuu!!!

Twende Sawa

Pastor  Dr Huruma Nkone akiendelea kukata Gospel kama Katapila

Wanafunzi wakimpa Yesu Maisha yao

Wanafunzi wakimpa Yesu Maisha yao

Dr Kimambo akikata shule 

Watu Pipoz

Nabii Mkee akitabiria Watu

Haikuwa Ya kitoto hata Vice President wa Mzumbe Campus ya Mbeya alikuwepo(Mwenye Top ya Kijani)

Mc Pilipili akiwa Kazini

Dr Maboko akiendelea kuongelea Ujasiriamali

Mr Msigwa akiendela kukata shule ya Mahusiano

King Chavalla akipasu mbavu za watu
Hembu angalia huu umati hapa karibia na Saa kumi na moja asubuhi..lakini watu wapo tuu

Hitimisho katika Jumbe zote zilizoongelewa katika Campus Night hizi ni kwanmba Yesu ndio jibu la kila kitu kwenye kila idara ya maisha na kila kona .Yeye ndio mwanzo tena ni mwisho wa kila jambo.