Pastor Gwajima

Sintofahamu katika Sakata ya issue ya Dr. Ulimboka imechukua sura mpya Baada ya Siku ya Ijumaa Jeshi la Polisi kujitokeza kwenye vyombo vya habari na kueleza Kuwa Mtuhumiwa wa Sekeseke la kumkamata na Kumtesa Dr. Ulimboka amekamatwa baada ya kwenda katika kanisa la Ufufuo na Uzima lililo chini ya Mch. Gwajima, Mchungaji huyo wa Kanisa hilo amefunguka siku ya jana na kueleza kuwa “Joshua The Kenyan” hakuwahi kwenda kwenye Kanisa hilo na wala Kanisa halina Utaratibu wa Kuungama kwa kusema dhambi.

Taarifa zilizotolewa juzi na kuibua maswali katikati ya Jamii ya Watanzania hususan Wakristo waliozipokea taarifa hizo kuwa Mtuhumiwa huyo aliyefikishwa kizimbani siku ya Ijumaa Asubuhi Mr. Joshua Mulindi Kwa maelezo ya Kova anafanya kazi chini ya kundi la Gun Star lililo chini ya Mkuu wa Kundi hilo Bw. Silence kutoka Nchini Kenya Walikuwa Wamekodiwa kuja Tanzania na Kigogo Mmoja kuja nchini kwa kazi moja ya Kutoa uhai wa Dr. Ulimboka na zoezi hilo kushindikana, ndipo kijana huyo wa Kikenya alikwenda kunako kanisa la Pastor Gwajima na Kukiri kuhusika na sakata zima la Dr. Ulimboka.












Kamanda Sulemani Kova akitoa maelezo ya Kukamatwa Joshua Mulindi

Siku Ya Jana Mch. Gwajima amefunguka na kuruka Kimanga kuhusu sakata hilo na kutaka Kanisa hilo lisihusishwe na Sakata la Dr. Ulimboka sababu huyo mtu mwenye jina la Joshua kutoka nchini Kenya hajawahi kutubu kwenye Kanisa hilo na kueleza kuwa Kanisa lake halina utaratibu wa Kuungama kwa Kusema dhambi za waumini kama ilivyo katika Makanisa mengine hususan RC (Kuungama).

Mch. Huyo ambaye anaamini ana mahasimu wengi katika Gospel ameenda mbali zaidi na kusema kama Mkenya huyo ameeleza hayo basi atakuwa ametumwa na baadhi ya Watu wasioitakia mema huduma hiyo maarufu kwa kurejesha Misukule hapa Tanzania.











Dr. Ulimboka baada ya Kutoka kuteswa na Joshua the Kenyan

Pamoja na taarifa hizi muhimu Blog inakamilisha taarifa muhimu ya kulitazama sakata hili kwa jicho la tofauti kwa kutafuta utata wa maeneo yafuatayo.
  1. Je ni kweli Kabisa kwa Intelligencia ya jeshi la Polisi, baada ya kupokea tu taarifa kwa mtuhumiwa walikwenda kwenye vyombo bila ku cross check ukweli na Kanisa la Mch. Gwajima??
  2. Ni kweli Jeshi la Polisi halikujua kuwa Mch. Gwajima atakataa au waliamini Mch. Gwajima atafunika Kombe Mwanaharamu apite??Kwanini Walifikiri kuna njiab ya Uchochoro kupitia Kanisa hilo.
  3. Ni kweli Kanisa hilo kuanzia sasa wataendelea kusali kwa Amani katika viwanja vya Kawe bila kuanza kusikika tuhuma mbalimbali dhidi ya Kanisa hilo baada ya Mch. Kutia mchanga Kitumbua Cha Dola ya Serikali??
  4. Baada ya Kujisafisha Kwa Mch. Gwajima katika Sakata hilo, Je huyu Joshua kutoka Kenya ni nani hasa???
  5. Baada ya Sakata la Jerry Muro na Mengine yanayofanana na hayo ni Kweli Jeshi la Inteligensia ya Polisi imefikia hapo ilipo???

Kuna mambo mengi ambayo kwa jicho la tatu yataanza kuonekana baada ya Sakata hili linaloendelea la Dr. Ulimboka, Mgomo wa Madaktari, Joshua ze Kenyan, Kanisa la Gwajima na Kuhusika kwa Serikali katika Sakata zima.

Kanisa kwa namna moja limeamua kuangalia pia kweli inasemaje na kujiweka sawa, kama Serikali ilivyoamua kuwa LIWALO na LIWE, basi Pastor Gwajima nae ameamua kuwa LIWALO na LIWE katika Sakata la Kukamatwa Joshua Mulindi. Lazima Jeshi la Serikali nayo ijifunze kusoma Alama Za Nyakati lakini pia kama kuna issue za ku-cook (kupika) basi inatakiwa Intelligencia ya hali ya juu hasa kama issue itahusu mambo ya Imani Za Watu.

Efathaaaa, maaana yake "Funguka". Blog inakamilisha Makala Muhimu iliyoahidi mwishoni mwa wiki jana ili iweze fanya "EFATHA" ya Ukweli.

Thanks to my Brother Papaa The Blogger

|
0 Responses