Mara zote tumekuwa tukifanya vitu tukijua kwamba tupo sahahi lakini mara nyingi tumekuwa hatupo sahaihi kutokana na upeo wetu mdogo wa kufikiri vitu kwenye nyanja mbalimbali na athari mbali mbali zokanazo na vitu mbali mbali.Unapofanya kitu kwa fikra halisi na utimilifu wa mambo ndipo unaweza kugundua kwamba uko sahihi hapana mara nyingi matokeo mazuri ya kile ulichofanya ndio hutupa jibu kwamba input ambayo umeiweka/umeitumia ilikuwa sahihi au hapana.Maamuzi yetu huadhiriwa na vitu mbali mbali na hutufanya tuwe sahihi au hapana kutokana na vitu hivyo.Kwenda Kanisani Hakukufanyi kuwa Mkristo na Wala Kusimama Karibu na Karakana ya Magari hakukufanyi kuwa Gari.
1.Mazingira
Mazingira tuliyokulia yanamchango mkubwa sana kwenye maisha yetu na huwa na athari kubwa juu ya vile vitu ambavyo tunaishi na na namna tunavyofanya maamuzi yetu.Mfano Siku Moja tulipokuwa Kanisa fulani...Mzungu alisimama akitoa ushuhuda kwamba Yaani Maisha Mabaya sana kwake na Amechoka Kula Kuku kila siku,Wakati aliposimama Mama mmoja akaeeleza namna ambavyo hawana chakula kabisa.Ukifwatilia kinachowatofautisha hawa watu ni mazingira waliyo kulia.Lakini pamoja na yote Mazingira yanaweza kukufanya uwe sahihi au hapana kutokana pia na mtazamo wako binafsi.....Kwenda Kanisani hakukufanyi kuwa Mkristo wala Kusimama karibu na Karakana ya Magari hakukufanyi kuwa Gari
2.Information
Habari za kila siku ambazo tunazipata zinaathiri sana maisha yetu tunatoishi kila siku na katika nyanja tofauti tofauti embu fikiria kama tungekekuwa toka tumezaliwa kwenda shule isingekuwa ni lazima/kungekuwa na mfumo mwingine wa kusoma,Habari hizo ndizo zingekuwa chanzo cha namna tunavyofanya vitu vyetu na namna tunavyoralate na wengine na namna tunavyofanya maamuzi ya maisha yeyote kwenye maisha yetu.Fikiri kama tungeambiwa kula makande ni sumu toka tunazaliwa mpaka tulipo maamuzi yetu yangejengeka kwa namna hiyo bila kuzingatia maswala Mengine.Hembu fikiria kwamba tungekuwa tunambiwa Ukimwi hausababishi kifo na hauna madhara kwenye maisha yetu ya kila siku je ingekuwaje?
3.Watu
Marafiki,Ndugu na jamaa wanamchango mkubwa na maisha yetu katika kila tunachokifanya,Ndio maana wahenga walisema ukitembea na mwizi na wewe utakuwa mwizi basi si kama mwizi kwa asilimia zote bali lazima hata uamulie kuwa kibaka,Chuma hunoa chuma siku zote.Marafiki wanaokuzunguka wanamchango mkubwa sana kwenye maisha yako,Wataalamu wanasema ukitaka kujua pato la la mwezi kwene ajira yakeChukua marafiki wake watano wanaomzunguka kwa ukaribu sana,Tafuta wastani wao unaweza kujua pato lake la mwezi.Lakin pamoja na hayo yote ni vizuri kuaangalia marafiki ,ndugu na jamaa wanaotuzungumza wanamchango gani kwenye fikra zet na namna tunavyoishi kila siku.Haiwezekani ukatembea na Chizi wewe ukaonekana mwenye akili.
Pamoja na mambo yote unaweza ukawa umeathiriwa kwa namna mbaya kutokana na sababu hizo tatu za ambazo ndizo zimekuwa sehemu kubwa ya maisha yetu lakini kumbuka bado unaweza kufanya vizuri zaidi
Hata kama umefanya vibaya sana bado unaweza ukabadilika na kufanya vizuri zaidi...Kumbuka ...Kwenda Kanisani Hakukufanyi kuwa Mkristo wala Kusimama Karakana ya Magari Hakukufanyi Kuwa Gari..
...Kwenda Kanisani Hakukufanyi kuwa Mkristo wala Kusimama Karakana ya Magari Hakukufanyi Kuwa Gari..
|
Rising The Standard ndio ilikuwa kauli mbiu katika Campus Night iliyofanyika katika Mji wa Mbeya siku ya Ijumaa ya tarehe 16/11/2012 bila kusahau mji wa Dodoma nao uliendelea kutikiswa na Event hii ya Campus Night yenye kauli mbiu My Life,My Love , My All.Naam matukio haya pacha yaliwakutanisha wanafunzi wa elimu ya vyuo mbalimbali katika maeneo husika
Kama ilivyo ada Mc maarufu wa Mji Papaa Sebene ndio alikuwa mshereheshaji wa Event iliyofanyika Mbeya naam...
Katika Segment ya Comedy Mc Pilipili alitikisa mji wa Mbeya,Kama ilivyo ada ya King Chavalla hakukosekana akiwaacha wanafunzi hoi kwa comedy
Wasemaji wa Siku hiyo katika Mji wa Mbeya walikuwa ni Pastor Dr Huruma Nkone,Rose Mushi,Dr Kimambo,Mr Msigwa na Dr Maboko,Wote hawa walizungumzia namna ya ku-rise Spiritual Standard pia na maisha ya kawaida tu ya mwamini katika eneo la uanafunzi
Pastor Dr Huruma Nkone alisema ushalobaro wala utoz toz na u-sista du haumsaidia mtu kuwa na clear future only Jesus can Transform your life na ata-rise standard zako..Kwa mara nyingine tulishudia Radical Gospel ya Dr Huruma Nkone isiyokuwa na kificho.
Nabii Mke a.k.a Rose Mushi alishusha sindano za kurise starndard zako kwenye swala la mahusiano.Alisisitiza kuwa bila Yesu mahusiano yako ni bureee...Alikazia akasema ni Bora uachuke kwa kumtii Mungu kuliko kuumtii mwanadamu.Kama ilivyo ada akiwa hana mic unaweza kumwangalia na kumfikiria unavyopenda..Kosa linafanyika tu pale akiwa na Mic....Ukumbi mzima ulikuwa moved na Nguvu ya Mungu through Rose Mushi.
Dr Kimambo aliongelea swala la Academic and Execellence pindi uwapo shule pia..Akatoa kanuni na mfumo wa namnq ya kurise standard zako na namna ya ku-execel academically..It was more than Powerfully...Kama ulimisi hii na wewe ni mwanafunzi wa mji wa Mbeya pole.Katika yote aliyoongea alisema huwezi fanya chochote bila Yesu.
Dr Maboko aliendelea kuongelea swala Ujasiriamali kwa wanafunzi,alijaribu kushare expirience yake katika swala zima la ujasiriamali bila kusitasita alieleza namna ya kurise standard zako katika swala zima la fedha huku ukiwa bado ni mwanafunzi.Lakini mwisho wa Yote alisema ukitaka kurise standard zako ,Yesu ni jibu la lako.
|