Mara nyingi tumekuwa na hulka ya kurahisisha vitu kuliko ulivyo uhalisia wa vitu kwenye shughuli zetu za kila siku.Mara nyingi tumedharua vitu sababu hatujui gharama ya vitu hivyo kwenye maisha ya watu wengine na uhalisi wa shughuli hizo wanazozifanya.Sisi tunakuja kuona matokeo ya mchakato mkubwa sana ambao wamekuwa nao kwenye maisha yao na kazi zao za kila siku.Mfano "Ni Rahisi kumuona Konda anakusanya nauli kwenye Daladala ukamjibu/kumwangalia kwa kumdharau lakini hujui mpaka ameumua kufikia hapo amepitia nini pia hatujui gharama halisi ya kufanya kazi hiyo sisi tunaona matokeo tu ya kukusanya fedha muda huo,Kama ni rahisi basi jaribu kuifanya wewe utaelewa...."Laini Laini Maana yake Sio Rahisi"

Kondakta wa Mwenge Posta Via Shekilango Road
Ni rahisi kumuona mwingine amekosea kulio wewe kujiona umekosea.Watanzania tulio wengi tuna kipaji cha kukosoa kuliko kurekebisha kwenye kile mtu anachokosea.Mara nyingi huwa tunaona matokeo tu ya kile mtu anachokianya ndio maana tunapenda kukosoa Mfano"Ni Rahisi kumkosoa mchezaji wa mpira kuwa amekosea angepiga vile angefunga"Lakini tunasahau Gharama ya mazoezi anayoyafanya kufikia pale ni kubwa kama ingekuwa ni rahisi ungeamua kuwa mchezaji then tuone kama utakosoa au hapana.Kokosea sio tatizo lakini punishment tunayotoa haiendani na kosa lenyewe.Laini Laini Maana yake Sio Rahisi
Christiano Ronaldo
Sisi ni wavivu wa kufikiria mara nyingi,Hatupendi kufwatilia vitu ndio maana tunakuwa wepesi wa kuchukukia vitu vyote kuwa ni rahisi sana kumbe sivyo vilivyo kwenye uhalisia."Mfano...Makampuni ya simu yanapotoa matangazo yao wanakwambia hudumu fulani ni Bure,Je kweli ni Bure ?Je kwanini Baada ya kumaliza kutangaza utasikia "VIGEZO NA MASHARTI VITAZINGATIWA"Je hivi vigezo na masharti kuzingatiwa ni vipi?Basi kwa maana nyingine kuna gharama ya kulipa inaweza isiwe pesa lakini inaweza kuwa gharama ya kufwata vigezo na masharti inaweza kuwa kubwa zaidi.

Soma Chini kwenye picha kwenye Maandishi yamezungushiwa na alama Nyeusi

Wakati Steve Jobs anaanza kumpuni yake ya kwanza Apple akiwa Garage kwao na Mzee Paul Jobs ilikuwa ni rahisi sana kuwadharau kwa sababu huakuweza kufikiria mafanikio ambayo leo wangekuwa nayo.Watu wengi leo tunapenda kufurahia mafanikio ya wengine kitu ambacho si kibaya lakini hapo hapo tunayakosoa kwa kusema ningekuwa mimi ningefanya hivi na vile.ni bora ukae kimiya sababu hakuna mtu anayependa kukosea kwenye maisha kila mtu anapenda kufunya vizuri katika kila kona ya maisha pia kumbuka picha ya ndoto ya mtu anayo mtu mwenyewe na sio mwingine.Gharama ya mtu alolipa mtu mpaka tunafika kuona mafanikio sio ndogo.Leo tunatouch to Ipad na tunafurahia Simu za Iphones lakini haukumbuki kuna mtu alilipa gharama.Laini Laini ya kubofya Ipad na Simu za Iphones haimaanishi ni Rahisi.
Steve Jobs 
Ni vizuri kuwa na mtazamo halisi na gharama halisi na kile unachotaka kukifanya lakini pia ni muhimu kujua vya wengine na gharama za vile vitu wanavyofanya kuliko kukurupuka na kuanza kufikiria katika namna tofauti na jinsi uhalisia wa vitu ulivyo.Penda kufwatilia vitu vizuri kwanza ndipo ufikie kufikia kuhitimisha huku ukiwa na uhakika wa kile unachotaka kukifanya

...........................................Laini Laini maana yake sio Rahisi......................................
Watanzania na jamii yetu kwa ujumla tumejengwa na kukuzwa zaidi katika hali ya kupenda kufikiria kushindwa kuliko kushinda katika maisha yetu na kila siku kutokana  na malezi na namna mfumo wa vitu vingi wa maisha unavyoendeshwa.Mfumo wa maisha yetu tangu tunaanza tungu nyumabani tukiwa wadogo na hata tunapoanza shule mazingira yetu hayaamini katika kushinda kuliko kushindwa.Kujiamini katika kila tunachofanya ni kama umekuwa mzimu ulio hai unaosumbua maisha yetu tangu tungali wadogo mpaka watu wazima.Muda mwingine tumejitungua misemo ambayo ukifwatila haina mashiko zaidi ya kutaka kutuondoa uoga tu na sio zaidi...."Tukiwezeshwa Tunaweza".Swali la msingi je hao waliweza waliwezeshwa na na nani na wana vichwa vingapi na wamewezaje kufika hapo.
Tukiendelea kwa namna hii safari ya ukombozi katika nyanja mbali mbali yaani Kifikra,Kiuchumi,Kijamii,Kisiasa na hata kidini itakuwa ni kama kumtafuta kuku anayenyoshesha tukitaka atupatie maziwa....


 Mambo machache ambayo yanaweza kutufanya tupende kufikiria  katika kushindwa zaidi kuliko katika kushinda................


1.System(Mfumo)
Mfumo wetu wa malezi kuanzia watoto na hata mfumo wa uongozi katika nchi yetu katika nyanja mbali mbali hauutupi mwanya wa kuweza kufikiria na kuamini katika kushinda katika kila tunalolifanya zaidi ya kufikiria na kupenda kushindwa zaidi bila ya sisi wenyewe kujua nini tatizo limeanzia wapi.
             
Pamoja na mfumo mbovu katika kila nyanja ya maisha yetu ambao tumekutana nao sio kigezo cha kutufanya iwe kisingizio kwamba tusiamini katika kushinda zaidi ya kufikiria katika kushinda.."System haipo kwa ajili ya walio nje ya system bali system ipo kuwapa favour  wale waliopo kwenye system tu"Ni jukumu lako kuamua kubadilisha mfumo wako mwenyewe kwenye fikra zaidi kuiko kuendelea mfumo sababu utaishia kulaumu tu na hautafika kokote.

2.Historical  Background(Maisha yetu na Historia za Nyuma)

Familia zetu nyingi za kiafrika haziamini katika kushinda zaidi kuliko kushindwa.Ni familia bora na chache sana ambazo zinaweza kuamini katika kushinda kuliko kushindwa tangu tukiwa wadogo..Familia nyingi zimekuwa na mtazamo hafifu tangu watoto wanapoanza shule kuanzia maneno wanayotakiwa mpaka matendo wanayofanyi katika nyanja mbali mbali hii haikupi njanya ya kufikiria na uwanda mpana wa kuamini ushindi unawezeka..utasikia wanasema ..."Yaani Baba yako aliishia hapo ,Babu hapo hapo,Mimi mwenyewe mama yako pamoja na wote sisi kuwa na akili kwenye ukoo wetu bado nimeishi hapo ...je wewe utaweza au ndio unajifanya una akili sana?"Wanashindwa kujua wao ni wao na sisi ni sisi kwani kuna vitu vingi vimebadilika sana.
          
Ndio utasikia hata mtu akishindwa kwenye jambo dogo tu...Yaani sisi sijui tunamikosi gani....Yaani hii ni tatizo kubwa katika jamii...wewe ndio mkosi wa kwanza wa kushindwa kufanya maamuzi sahihi.


3.Relationship Break ups.

Katika kizazi chetu kutokana na sarakasi nyingi za kimahusiano ambazo tumekuwa zikitupata kwa kuvunjika na kushindwa kuwa na mahusiano bora ya kimapenzi imetupelekea kushindwa na kujiamini katika kila tunachokifanya.Huu msuko suko wa kupiga vibuti na kupigwa vibuti(Kuacha na Kuachwa) limekuwa ni tatizo kubwa la kufanya watu wengi kutosonga mbele na kupiga hatua mpya katika maisha yetu ya kila siku.
                         
Mara tu anapoonza kugika hatua mpya ndani yake bado anasutwa unasikia maneno haya "lakini wewe umeachwa na sijui kama utapendwa tena".Matokeo yanayopelekea watu kujitungia maneno ya ambayo hayana hata mashiko na uelewa timamu.Utasikia watu wanasema."Wanaume wote si sawa..yaani wote baba na mama mmoja au Wanawake wote si wale wale".Ukisikia mtu anasema hivyo fwatilia yaani kuna sehemu katendwa.

4.Past Failures.

Baada ya watu kuweza kushindwa katika maisha yetu katika kipindi fulani cha nyuma imepelekea mioyo yetu kushindwa kujiamini katika kila hatua mpya ambayo tunataka kuichukua ili kuweza kuendelea mbele.Kushindwa katika jambo fulani katika kipindi cha nyuma haina maana ya kwamba hauwezi kushinda katika jambo lingene katika maisha....Mfano "Watoto wengi wakifeli Kidato cha Nne huamini kuwa maisha yameishia hapo kumbe maisha bado yanaendelea ."
                     
Kumbe ni wakati wakujaribu fursa mpya za kimaisha na mambo Mengine.Imekupasa kujaribu tena katika kila unachokifanya hata kama ulishindwa nyuma hiko sio kigezo kwamba utashindwa tena na wala sio sababu ya msingi ambayo unaweza ukaeleza watu.Fanya tena na tena...

"Mbunge wangu wa Ubungo Mh.John Mnyika alipojaribu mwaka 2005 kugombania Ubunge kwenye jimbo la Ubungo alishindwa lakini hiyo haikuwa tiketi ya kukata tamaa matokeo yake mwaka 2010 alijaribu tena..ndipo ushindi ulipopatikana..Leo hii tunachekelea na kufurahia kumbe ni hatua ya mtu aliyoamua kuchukua maamuzi mwenyewe.

........Jenga tabia ya  kufikiria kushinda zaidi kuliko kushindwa zaidi...
Wanafunzi wengi wa Jamii ya Kitanzania tumejengewa mfumo ambao haupendi/hatupendi kujifunza na kutafuta mafundisho nje ya masomo yetu haswaa kipindi tukiwa kwenye vyuo na shule lakini sisi wenyewe tumeshindwa kutafuta upenyo wa kujifunza nje ya maisha ya shule kwa sababu moja au nyingine.....Lakini safari hii Kanisa la Victoria Christian Center Tabernacle a.k.a VCCT limeamua kukuletea Seminar yenye Jina SHAPING YOUR DESTINY chini ya Kitengo cha kanisa hilo kinachoitwa CAMPUS MINISTRY.
Usafiri utatolewa Bure kutoka kwenye vyuo vyote hapa Dar es Salaam mpaka eneo la Tukio katika Hema la Kisasa la Kanisa hilo Mbezi Beach.......
Topic zitakazokuwa presented.......!!!

1.How to Live a Balanced 
2.Discovering Talents and Opportunities while in a College
3.Maintaining and Building Meaningful Relationship
4.How to Excel In and Out Of The Class 

Presenter are :-


Pastor Dr Huruma Nkone
Chris Mauki
Samuel Sasali a.k.a Papaa Ze Blogger
John Lisu





















                                       




DONT DARE TO MISS !!!!!!!!!
| |
| |

PART III


Ikiwa tunamalizia sehemu ya mwisho ya nini cha kufanya baada ya kuongelea SIFA ZA MTU MWENYE MAJERAHA AU UCHUNGU NDANI YA MOYO
Tambua uchungu/majeraha ya ndani mwasisi wake ni shetani kwa maana nyingine ni mbegu ya shetani kwenye maisha na jamii za watu. Ili uweze kupona majeraha ya ndani au uchungu ni muhimu kuzingatia yafwatayo.

1.Kubali kwanza umejeruhiwa na una uchungu moyoni.Unapokiri wewe mwenyewe kuwa una uchungu au majeraha ya ndani kwenye moyo ni mwanzo wa ukombozi wa maisha yako.Uchungu na majeraha ya ndani husababishwa na vitu mbali mbali kwenye maisha yako.Unapokiria kuwa una majeraha ya ndani ni dalili ya kuwa umeshatambua kosa lako wewe binafsi.Na ni mwanzo wa hatua mpya katika maisha yako binafsi

2.Jifunze kusamehe na kuachilia kabisa.Majeraha ya ndani na uchungu husababishwa  na vitu mbali mbali ikiwemo watu,vitu na hata wewe binafsi.Watu wengi wameshindwa kujisamehe kutokana na makosa waliofanyiwa au kujifanyia wao wenyewe kwenye maisha yao.Kuishi na majeraha ndani ya moy/uchungu hakusaidii kuponya moyo au kuleta amani ya kudumu bali huendelea kujenga chuki kwa muda mrefu ambapo hata kipindi utakapotaka kuchukua hatua ya kusamehe pia itakuchukua muda mrefu.

3.Chukua hatua mpya ya maisha yako.Usiendelee kukaa pale pale kwenye maisha ya uchungu na majeraha ya ndani.Amua kufanya kitu ambacho kitakuletea amani na furaha kwenye maisha yako.Amua kuongeza ujuzi mpya.Amani na Furaha ni kitu cha muhimu kuliko kitu chochote kwenye maisha ya mwanadamu.



"Linda Moyo wako kuliko vyote ulindavyo maana shina la uchungu lisije chipuka ndani yako."


...................................THE END............................................
| |
Baada ya mwezi mmoja uliopita Program ya Wanafunzi wa rika zote pamoja na wadau mbali mbali hapa mjini  inayojulikana kama SOUL BREAKFAST kufanya vizuri  chini ya aliyekuwa Presenter mwenye Vipaji lukuki Papaa Ze Blogger a.k.a Samuel Sasali ni Title yenye jina THINK DIFFERENTLY ,MAKE A DIFFERENCE.

Siku ya tarehe 29/09/2012 ,Muda wa Saa wa 0830 Asubuhi  tutakuwa tunaingia Season II Episode IX pale katika Eneo la VIctoria Christian Centre at Victoria Petrol Station..Muda huu tukiwa na Presenter mwingine machachari ambaye ni Director wa Women Ministry katika Kanisa  la VCCT,MRS FLORENCE MBAGO  atakuwa ki-present topic inayoitwa ENJOYING YOUTHHOOD IN CHRIST.


                 DON'T DARE TO MISS!!!!
| |

Jicho letu katika siku ya leo limefaniliwa kuangazia katika maswala ya kiulinzi katika nchi mbali mbali.Dunia ikiwa katika aina mbali mbali ya mapigano ya vita juu ya umiliki wa rasilimali na utajiri unaopatika katika nchi husika lakini pia nchi kujiahakikishia ulinzi binafsi katika nchi zake.



Ili nchi ifikie viwango vya kuwa na ubora katika majeshi yake kuna sifa mbali mbali zinazotakiwa na pia ubora wa huduma ambazo zinatolewa katika majeshi husika ikiwa ni pamoja na maisha binafsi ya wanajeshi kwa pamoja.
Blog yetu leo imefanikiwa kuangalia nchi kumi duniani zenye majeshi makubwa na ambayo yamekidhi viwango vya kimataifa vya ubora vya majeshi.

Nchi kumi duniani zenye majeshi Bora .

NAFASINCHI
ENEO LA NCHI 

(sq kms)
BAJETI YA MWAKA KWA JESHIIDADI YA WANAJESHINDEGE ZA KIVITAMELI ZA KIJESHISILAHA ZA NYUKLIA
IUSA9,826,630$692 billion1,500,00024,5002,5008,500
IIRussia17,075,200$56 billion1,200,0003,30040011,000
IIIChina9,596,960$100 billion2,300,0005,400700240
IVIndia3,287,590$36 billion1,350,0003,300200100
VUK244,820$74 billion225,0002,250125225
VITurkey780,580$25 billion615,0002,800300NA
VIISouth Korea99,720$27 billion650,0002,300195NA
VIIIFrance643,427$45 billion360,0002,550325300
IXJapan377,835$70 billion240,0002,500170NA
XIsrael20,770$16 billion185,0002,65070200

NOTE:Baadhi ya nchi zilizopo kwenye idadi hazikuruhusiwa kumiliki Silaha za Nyuklia kutokana na Sababu mbali Mbali za Ki-usalama na kihistora ambazo zilisababisha nchi hizo kuwekewa masharti na kusaini mikataba mbali mbali iliyozizui kumiliki silaha za Nyuklia Ulimwenguni
| |
PART II.

Huu ni mwendelezo wa somo amabalo linazungumzia sifa za mtu mwenye majeraha au uchungu ndani ya moyo.Somo hili lilianza wiki iliyopita



6. Ni watu ambao hukaa vinyongo moyoni kwa muda mrefu na hawapendi kusamehe.Mara nyingi watu wa aina hii kusamehe watu wengine ni ngumu sana.Inapofika kwao swala la kusamehe ni afadhali kutafuta mbadala kuliko wao kusamehe mtu makosa waliowafanyia.

7. Ni watu wasumbufu  mara kwa mara na hupenda kulalamika mara kwa mara hata pale ambapo haikupaswa kulalamika bila sababu za msingi.Ulalamishi kwao huwa ni jambo la kawaida ila wao huwa hawapendi kulalamikiwa hata wanapokosea.

8.Hawapendi kushirikiana na watu wengine juu ya mambo mbali mbali ya kijamii mpaka pale watakapojisikia wao wenyewe tu.Pia hawapendi kusaidiwa hata pale ambapo wanapaswa kupata msaada kwa sababu wanajua watajenga ukaribu na watu kitu ambacho wao hawakipendi na wala hawakitaki.

9. Ni watu wanaoongozwa na misisimuko na hisia zaidi kuliko uhalisia.Mara utakuta wana furaha mara baada ya muda mfupi wana huzuni,mara wamekasirika.Hisia zao haziko constant kuwa anafurahi muda wote..au mechukia muda wote.Yaani tabia na hisia zao huwa hazieleweki.Hisia zao huwa kutokana na anavyojisikia siku hiyo au muda huo.


………………Kaa  tayari kwa ajili ya Part III ..ambayo ni ya mwisho..................

Stay tunned…….


| |
PART I
Tatizo la kujawa na uchungu moyoni yaani kutokusamehe limekuwa ni moja kati ya tatizo kubwa katika kizazi hiki.Nimekutana na watu wengi na hata mimi mwenyewe nimeshawahi kujeruhiwa na kuwa na uchungu kwa namna moja ua nyingine.Lakini muda mwingine nilishindwa kusamehe bila kujua mimi mwenyewe kuwa ni muhanga wa majeraha ya ndani ya moyo ambayo ni uchungu.

Wanawake wengi ndio wamekuwa wahanga wa hili tatizo pia wameshindwa kulificha kuliko wanaume.Kumgundua mwanaume kuwa amejeruhiwa au anauchungu moyoni mwake ni ngumu mpaka ukae naye kwa ukaribu sana.Baada ya kufwatilia kwangu binafsi na kwa wengine hiki ndicho nilichogundua kuwa zifwatazo ni dalili na sifa za kumjua mtu mwenye uchungu au alijeruhiwa ndani ya nafsi yake.Muda Mwingine kumgundua mtu mwenye uchungu au aliyejeruhiwa ndani ya moyo inahitaji umakini zaidi lakini mara nyingi utamgundua kwa njia ya matendo zaidi(Actions)
  1. Mara nyingi mtu aliye na uchungu moyoni huwa hajali kuhusu wengine hufanya vitu tu bila kufikiria kuwa atawaumiza wengine(They show a lack of concern for others. A bitter person cares very little about anybody else).Pale anapoona mwingine ameumia kama yeye ndani yake hujisikia burudani na furaha kwa sababu kiu yake imetimizwa.Lakini furaha yao huwa ya muda tu.
  1. Mara nyingi mtu mwenye uchungu au aliyeumizwa hupenda kujishtukia stukia hata pale ambapo hapa muhusu(They're sensitive and touchy.) For instance, if a bitter person walks into a room where two other people are talking, and those people get quieter as he walks in, the bitter person thinks, “they’re talking about me.".Huu ni moja kati ya mifano ambayo ni kweli na halisi.
  1. Hupenda kuchagua marafiki pia huwa na urafiki na watu wachache sana ,Pia mara chache watu hawa kuwa na marafiki wa karibu(They become very possessive with just a few friends, and rarely ever have any really close friends) They tend to avoid meeting new people.
  1. Mara zote huwa si watu wa shukrani au kukubali kazi ya mtu mwingine pale anapoifanya kwa usahihi.Yaani hawapendi kutoa Pongezi kwa wengine hata kama aliyefanya kile kitu amepatia au ni sahihi(They show little or no gratitude at all)
  1. Hupenda kuongea maneno ya chuki pia hupenda kukosoa mara zote hata pasipohitajika kukosoa au ambapo hapana ulazima wa kukosoa kitu.(They will usually speak words of empty flattery or harsh criticism.)

Next week siku kama ya leo nitaendelea na hili somo kumalizia sifa zilizobaki na tiba yake ya kudumu....Stay tuned.....Siku Kama ya Leo.....

| |
This very strange birth story took place in a Church along old Sapele-Benin Expressway in Edo state today, Tuesday Sept 11th, 2012. 
During a special program at the church, a woman gave birth to a horse.
We learnt the woman in question started screaming during the live prayer session and all of a sudden, blood started gushing out of her vagina like that of a woman giving birth.

According to an eyewitness of this bizarre birth, several worshippers took to their heels as they behold the strange creature that just came out of the woman.

Before the arrival of news crew, the horse has passed out.
One Evangelist Silva told reporters that a revelation came forth during the prayer meeting that a woman with an issue has something blocking her womb.
He further stated as prayers intensified, the woman screamed like a woman in labour and the object came out.



NOTE:Habari hii imetolewa katika mtandao wa http://naijagists.com/woman-gives-birth-to-a-horse-in-edo-church/
| |