Mwanamuziki na Muimbaji nyimbo za injili hapa Tanzania Josiphine Minza Nkila anategemea kuachilia album yake ya pili itakayozinduliwa Tarehe 22 mwezi wa tisa 2013 kwenye ukumbi CCC Upanga kuanzia saa nane mchana na kuendelea.

Akiongea na Vyombo vya habari vya Kikristo na Bloggers wa Kikristo Josephine Minza Nkila aleza kwamba Albamu itakuwa na  

Jina la MAISHA YA IBADA( A LIFE OF WORSHIP) imeshirikisha waimbaji mbali mbali kwenye Utengenezaji wake Akiwemo Abednego Hango wa Band ya New Life kutoka Pale Arusha.

Pia alitaja Baadhi ya Waimbaji ambao watamsindikiza kwenye Uzinduzi wa Albamu Hii  ambao ni THE VOICE , DELICIA, EDSON MWASABWITE , DANIEL MBEPELA , VIJANA AIC MAGOMENI NA DAR KWAYA KUTOKA AIC MAGOMENI

Josiphine Minza Nkila akisikiza kwa Makini Maswali ya Waandishi wa Habari na Bloggers

Josephine Minza Nkila akiwa na Mwalimu Mgisa Mtebe Kama Project Manager wa Albamu hii ya Maisha Ya Ibada


Usitamani Kukosa Hakuna Kiingilio  ,Ni Bure Kabisa
Tarehe 1/9/2013,Majira ya Alasiri kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza Patawaka Moto kwa Pambano kali la Ndondi(Ngumi) Zisizokuwa na Ubingwa Kati ya watangazaji wawili Maarufu wa Kituo cha Radio za Injili hapa Tanzania.Akiendelea kuongea na Waandishi Wahabari na Bloggers wa Kikristo Neema Gasper alieleza kwamba Kundi Moja Maarufu la Dancing la Kikristo litakuwepo kwenye Ukumbi Siku Hiyo na Pia Bila Kusahamu Wanamitindo wa Kikristo watashiriki Kuonyesha Mavazi Mbali Mbali ya Kikristo Katika Ukumbi wa Huo

Siku chache zimepita tangu Neema Gasper alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari pamoja na Blog za Kikristo juu ya ujio wake mpya wa Albamu yake itwaayo "SHUJAA" akiendelea kuongea na Waandishi Wahabari na Bloggers ameeleza kua mapato yatakayopatikana katika uzinduzi huo asilimia fulani ya mapato itapelekwa kusaidia wajane na yatima  waishio katika mazingira magumu.Albamu ya "SHUJAA" itakuwa na Nyimbo Takribani 8.

Neema Gasper Akiongea na Bloggers na Waandishi wa Habari wa Kikristo
Akiendelea Kuongea na Waandishi wa Habari na Bloggers aliendelea kufafanua kwamba Mbunge Machachari na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta ndiye atakayekuwa Mgeni Rasmi kwenye Uzinduzi huo

Mh Sumuel Sitta,Waziri wa Ushikiano wa Afrika Mashariki
Waimbaji wengine wa nyimbo za injili watakaomsindikiza Neema Gasper katika uzinduzi wa album yake ni pamoja na Rose Mhando,Bahati Bukuku,Madam Ruth, Martha Mwaipaja, Everine Msoma, Ambwene Mwasongwe, Maxmillian Machumu, Edson Mwasabwite Enock Jonas na wengine wengi.


Vingilio katika uzinduzi huo vimepangwa kuwa Viti maalum Tshs 10,000/=, Kawaida Wakubwa Tshs 5000/= na watoto sh Tshs 2000/= wageni 50 wa kwanza watajipatia mafuta na Losheni kutoka kwa Gress Product

Ticket zinapatikana  Praise Power Radio,Wapo Radio, na pia ticket pia zitapatikana mlangoni siku hiyo hiyo ya uzinduzi katika ukumbi wa Ubungo Plaza.

Dont Dare To Miss!!!!


Hii Ndio Tanzania Yetu,Unafikiri Kwa Namna Hii Tutaendelea?Je unafikiria wapi ni rahisi Kutoa mchango wa harusi na  kutoa mchango wa Ujenzi wa Shule?Jamii yenye kuhitaji maendeleo yenye kueleweka na yenye kumaanisha ni lazima iwekeze kwenye elimu na ujuzi kwa jamii ya watu wake.Serikali yenye kujali watu wake lazima ifanye kila liwezekanalo kuwekeza kwenye jamii katika ujuzi hali kadhalika jamii inawajibu wake wenyewe wa kuwekeze ipasavyo kwenye elimu na ujuzi kwa manufaa ya vizazi vyao na taifa kwa ujumla.
Kuishi kwingi ni Kuona Mengi.Mwanadamu ni munganiko wa vitu vingi sana ambavyo ukiviangalia juu juu unaweza usivielewe.Mkusanyiko wa mambo mengi unayoyaona leo ni mkusanyiko wa tabia nyingi zilizojengeka jana.Hakuna jambo ambalo linaibukaibuka kwa sababu limeibuka tu,kila jambo lina mwanzo wake ingawa inaweza kuwa ngumu kukubali au kulitafuta lilipoanzia.Ujenzi wa jamii bora yenye maendeleo ya kifikra na uhuru wa kuweza kutoa maoni na kusimama katika ukweli wa vitu kwenye Dunia ya tatu imekuwa ngumu kutokana na ujenzi wa jamii yetu tangu mwanzo tunapozaliwa.Unaweza kuona jamii ambao haipendi mabadiliko ukailaumu lakini kumbe ndivyo tangu mwanzo ilivyojengwa.Maisha yamewekwa kufurahiwa na sio kuhuzunika.

Unapomwona mtu leo alivyo na vitu vyake vingi anavyofanya ujue kuna maamuzi fulani aliyafanya jana inaweza isiwe moja kwa moja au inaweza kuwa moja kwa moja.Tabia fulani unayoiona mwa mtu ni matokeo ya kile ambacho mtu amekuwa nacho tangu mwanzo.Jaribu kuangalia jamii ambayo imejengwa kwenye uhuru wa kujielezea na kuthubutu utaona mtoto na Baba wanaweza kuwa marafiki na wakacheka na wakaambiana vitu mbali mbali.Lakini huku kwetu Afrika Baba akiingia Ndani ya Nyumba unaweza fikiri ni Jenerali ameingia nyumbani,Pia Mama akiingia nyumbani unaweza kufikiri ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwakaleli Mbeya.Je unafikiri mtoto anayelelewa kwenye mazingira haya siku akikua akawa na familia unafikiri Yeye naye atakuwaje?
Msingi wa kila jambo kwenye maisha ni kitu Muhimu.Iwapo unafwatilia vitu utakuja kugundua watu wengi ambao ni watu wazima leo wanapenda kusoma vitabu mbal mbali vya kujieleimisha utagundua walivyokuwa watoto walipenda sana kusoma vitabu vidogo vidogo vya Hadithi Mfano Manenge na Mandawa,Juma na Rosa n.k Usomaji wa Hadithi hizo kipindi hicho ndio ulijenga msingi mpaka leo watu hawa wwamekuwa watu wazima kupenda kusoma.Ni ngumu kuanza kitu ukubwani na ukakiendeleza Maana hautaweza kufikia ukamilifu wake na unaweza kukumbwa na vikwazo Mbali Mbali.

Siku za Karibuni tumekuwa na ujio wa Raisi Barack Obama Kutoka Marekani Hapa Nchini Mwetu Tanzania.Ukifwatilia kiumakini mji wa Dar es Salaam umekuwa msafi na wa kupendeza kwa namna ambayo haijawhi kutoke tangu naingi Dar es Salaa Takribani Miaka 23 Iliyopita.
Baada ya Raisi huyu Kumaliza Ziara yake Tumeanza kushuhidia uchafu umeanza kurudi na vurugu za foleni zilizokuwepo Barabarani zimeanza tena,ingawa kwa muda takribani siku mbili Mji ulikuwa tulivu.Je Unafikiri hii ni tabia ya kawaida?Tangu Siku za awali hatujajengewa mfumo wa kuwa wasafi kwenye maeneo yetu na mazingira ya mji je unafikiri hiki ni kitu ambacho kinaweza kuibuka tu?

Ukiona Mtu anaamua kufanya maamuzi magumu kwenye maisha yake ujue kuna mahali ametokea na amaechoshwa na jambo fulani.Ni ngumu kufanya maamuzi magumu kwenye maisha bila kujua umetokea wapi na kipi unachokihitaji maishani mwako.
Jamii yenye kudhubutu na Kuamua ni jamii ambayo tangu mwanzo kuna msingi uljengwa maisha mwako.Ni Raisi kwenda kwenye ATM machine na Unakuta Mlinzi kawekwa na Huku Kwenye Eneo hilo Kuna Kamera za Ulinzi ndani ..Cha kujiuliza Je Teknolojia tunaitumiaje?Ni Raisi Kupanda Kwenye Dala Dala huku Konda anatukana na Nauli Utampa tu..Pamoja na maneno Mabovu anayoongea..Je unafikiri ni sawa?Maamuzi unayoyaona leo ya mtu yameathiriwa na hali fulani ya jana kwenye maisha yake.

Mbwa akishizeeka sana Meno Hung'oka Usitarajie utampa mfupa mgumu atafune kwani kwake itakuwa mateso.Uzee Wa umri pia ni Uzee wa Tabia fulani kwenye maisha yako..Unafikiri Upomuona leo Jambazi alianza na Ujambazi?Hapa alianza kuwa kibaka...Na Tabia ikishajengeka kwenye maisha ya mwanadamu kuiondoa ni shughuli kubwa ni kama kujaribu kuondoa ngozi ya mwili.Inahitaji muda na uvumilivu... 
Ni vizuri Kujenga tabia njema ya ujenzi wa jamii huru kwenye kila jambo tangu mwanzo wa utoto wetu.
Leo Hii tunapata shida kupata Kikosi cha Timu ya Taifa sababu Wachezaji wengi ni Wazee na Wameshachoka.Unafikiri ni Ngumu kumchukua Mchezaji wa miaka 25 au 26 kufundisha namna mpya uchezaji maana tangu mwanzo ndivyo alivyolelewa......Ukiendelea kumlazimisha kwa hapa Tanzania kwetu utaambiwa mnoko na Unaweza kuambulia Matusi tu.

Mbwa Mzee Hafundishwi Mbinu Mpya,Ukimlazimisha Sana Atakung'ata.
Kumekuwa na Wimbi la Watu Maarafu kwenye Muziki,Watangazaji na Wanaharakati Mbali Mbali wenye Mitazamo tofauti wa Kuingia kwenye Harakati za Kisiasa na Kutangaza nia za Kugombea Nyazifa mbali mbali kwenye Taifa Hili la Tanzania.Kinachonishangaza ni kwamba watu hawa kabla hawatangaza nia za kuingia kwenye siasa na kushika nyazifa mbali mbali katika nchi hii,Huko walipokuwepo wamefanya nini kabla ya kuamua kuingia huku?Sisi Watanzania tunaweza kuwa sehemu ya majaribio kama kichwa cha mwendewazimu kwenye uongozi .Taifa lenye tija na nia ya maendeleo haliwezi kukurupuka kuwapa nyazifa muhimu watu ambao wamelala na kuamka asubuhi na kutamka nia yao ya Kigombea nyazifa Mbali Mbali Kwenye Taifa hili.

Hakuna Jambo Kubwa linaloanza na Ukubwa Wake,Kila jambo linaanza na udogo wake.Swali langu ni kwamba hawa ambao wanataka tuwape nyazifa za uongozi,je huko kwenye nyazifa ndogo ndogo wamefanya nini cha kukumbukwa?Je wameleta mapinduzi namna gani?Kila siku tunaweza kujikuta tunarudi pale pale kwa kuwapa watu uongozi ambao lengo lao ni kuanza kujifunza kwenye nyakati muhimu ambapo sisi tunahitaji kusonga mbele.Baada ya Miaka hamsini ya uhuru hatuhitaji kuwapa watu nyazifa za uongozi kwa nia ya kujifunza bali kwa nia ya kusonga mbele.Tuwapime kwanza si kwa wingi wa maneno ya vyombo vya habari bali kwa utendaji wao wa maisha yao ya kila na kwa kazi ndogo ndogo ambazo wanazo kwa sasa.Inakera na Inauma tunampa mtu uongozi ndio  kwanza yeye anaanza kujifunza kwenye migongo ya watanzania.Tusipoangalia ule msemo wa kichwa cha mwendewazimu hautakaa utoke ndani ya taifa hili la Tanzania.Tusikubali nchi yetu kuwa sehemu ya Mafunzo ya Uongozi.Tuchague watu wenye kujielewa na  kuweza kutufikisha mahali ambapo tunapataka kufika na sio ili mradi tumemaliza kuchagua kiongozi.Siku Moja Wajukuu Wetu watachapa Makaburi yetu Fimbo kwa Utoto ambao tumekuwa tukiufanya kwenye taifa letu kwa kushindwa kujisimamia.

Ni Ngumu sana kujua nia za hawa ambao wanaanza kutangaza nia za kutaka kugombea uongozi na nyazifa mbali mbali lakini kwanza tunaweza kupima nia zao kwenye maisha yao ya kila siku kabla hawajaanza nia ya kuamua kutangaza nia zao za kutaka uongozi.Je hapo Makazini walipo wamewatumikia vyema wafanyakazi wenzao?Je vyao walivyo navyo vimeleta tija kwa wafanyakazi wenzao au ndio Yale Yale ,Wanataka kujifunzia kwa Migongo yetu,Unafikiri kama mtu alikuwa mchoyo kwa Wafanyakazi wenzake unafikiri siku akipata cheo atakuwaje?Je unafikiri kama mtu alikuwa mbaguzi kwa wafanyakazi wenzake unafikiri siku aakipata cheo na nyazifa itakuwaje?Ukitaka kujua Nia ya Mtu na Miasha ya utendaji wake kwa Ujumla nagalia hata anavyoishi na Jirani zake pale mtaani,tutagundua mengi sana juu ya hawa wanaotaka kugombea uongozi na nyazifa mbali mbali.

Uongozi ni Tabia iliyojengeka Ndani kwa Muda Mrefu.Uongozi sio kitu ambacho kinazaliwa leo.Uongozi ni learning process.Iwapo mtu haukuwahi kuwa na tabia ya kujifunza tangu mwanzo wa maisha yake ya namna ya kuwa kiongozi ni ngumu kiongozi huyu kuweza kujifunza kuongoza watu kwa muda mchache.Kuongoza watu ni outcome na manifestation ya tabia fulani iliyojengeka ndani ya mtu kwa muda mrefu na sio kitu ambacho cha kukurupuka.Iwapo mtu anaweza kuuigiza kuwa kiongozi baada ya muda fulani tunaweza kuona uhalisia wake...Mfano Mtu anapotukana Bungeni sio kitu ambacho Kimetokea ghafla ni Kitu ambacho kimekuwepo ndani mtu muda mrefu anaweza asitamke mkiwa wote lakini akiwa pekee yake ndani mwake matusi ndio kitu kilichomo....Kitabu fulani cha Imani fulani Kinasema...Yaliomjaza mtu ndio Yanayomtoka.....Hauwei tukana then ukasema ni Bahati Mbaya,Hawezi Kuwa Mgomvi then Ukasema imetokeo tu. Uongozi ni Zaidi ya Chuki na Hasira za Mtu alizokuwa nazo Moyoni.Unaweza kumchukia mtu mmoja lakini kumbuka kuna wengine mamilioni wako nyuma yako,Wnasaikolojia fulani walisema unapokuwa na hasiri kichwani mwako Unakuwa kipofu kwenye maamuzi yako Mengi.Je Tunaendelea Kuongozwa na watu waliojaa hasira na viasai moyoni mwao?

Uongozi ni Uwakilishi wa Wananchi.Uongozi sio uwakilishi wa wewe na tumbo lako bali ni kujitoa kwa ajili ya wananchi.Iwapo mtu anapotaka kuwa kiongozi lazima ajue namna ya kuwasilisha hoja na matakwa ya wananchi anaowaongozo,Inanishangaza sana kuona inapokuwa kwenye vikao vya Bunge,Mbunge anakosoa bajeti na kueleza mambo kadha wakadha  ambayo mapungufu yake yanaonekana wazi kwenye bajeti mwisho wa siku utasikia Naunga Mkono Hoja,Je Unanga Mkono Makosa uliyo yasema au?Je wanauwezo wa kuishawishi serekali na wadau wake juu ya Maendeleo ya Taifa hili kwa Hoja zenye Mashiko na Msingi ambazo watazisimamia hata wakiwa wamelala kitandani mwao Usiku?

Taifa Letu sio Sehemu ya Mafunzo Ya Uongozi lazima Ifike sehemu tufanye maamuzi magumu kwa kuwakataa wale ambao wanaonekana hata kwenye nyazifa ndogo walizo nazo hawakonyesha mapnduzi ya kifikra wa ujenzi wa jamii huru katika maeneo yao ya kazi.Tusiwaamini Tuwapime kwa nyazifa zao za sasa badala ya Kutulisha maeneo matamu midhili ya Sukari Guru Mwisho wa Siku Watanzania ndio Tunahangaika na Kumbuka Mtu akishainga kwenye Mfumo wa Uongozi kulingana na Katiba yetu ni Ngumu Kumtoa ki-urahisi Labda Tusubiri Miaka Mitano na Muda Hautatungoja....

....Nazungumza Moyoni....Huko Walikotoka Wamefanya Nini....?
Kila Kukicha Nchini Mwetu Kumekuwa Kukizuka Vituko Kadha wa Kadha..Leo Katika Ndivyo Sivyo ..Tunajidili Kuhusu Mabloga Wetu.Kazi ya Blogging Kwenye Jamii za watu waliondelea ni moja ya kazi ambazo zimekuwa zikiheshimiwa kutokana na ufasaha wa kazi na ubunifu wa Kazi za Mablogger.Lakini Nchini Mwetu Imekuwa Ndivyo Sivyo.Mablogger wengi wamekuwa wakitamani kupata Umaarufu wa Haraka Haraka Kwa Kutoa Habari zinazoipotosha Jamii na Kuifanya Jamii kuona kama Jamii ya Bloggers kama ni Jamii isiyojua Kitu gani Inafanya.Lakini Ki-ukweli ukitaka Kuheshimika Fanya kazi yako kwa Heshima...Acha Habari za Uzushi ...Kuwa Blogger Sio Kukosa Kazi Bali ni Kuwa Mbunifu na kwa Kutafuta Habari zenye Kina na Maantiki zenye kuisogeza jamii yetu Mbele.Blogging sio Copying and Pasting....Blogging ni Ubunifu wa Kichwa chako kwenye Jamii Yetu.
Katuni Hii Kwa Hisani ya Marco
Kila Maji Yana Mkondo Wake,Wahenga Walisema.Ubora wa Kitu hautegemeani na Mlinganyo wa Kitu Kimoja Na Kingine.Muda mwingi tumeshindwa kufikia malengo yetu na kukata tamaa baada ya kujilinganisha na wengine huku tukijiona sisi ni Dhaifu.Katika kila ndani ya mtu mmoja kuna upekee ambao mtu mwingine hana ndio maana kwenye maisha kuna furaha ya kufurahia maisha.Fikiria iwapo wote tungekuwa tunawaza na kufanya vitu kwa matazamo mmoja maisha yangekuwa yanaboa na tungekuwa hatuna tofauti na maroboti maana ladha ya maisha isingekuwepo.Jamii yetu na kizazi chetu tumekuwa na watu feki zaidi kuliko watu halisia kama zilivyo bidhaa.Hatuwezi Kufwanana kwa kila jambo inagawa kuna vitu hatuwezi kupishana sana.Maisha yasiyo na uhalisia ni kama kujaribu kujaribu kuiga finger print ya mtu mwingine ili hali tunajua utapatia lakini hauwezi kufwana kwa kila kitu.Kwanini uwe nakala ya Mtu mwingine wakati wewe pekee ni nakala yako binafsi tosha.Kwanini Usitamani wengine wawe nakala yako baadala ya wewe kuwa nakala ya mtu mwingine?

Ujenzi wa maisha yenye kudhubutu na kufanya kile ambacho ni halisi huanza ndani mwa mtu hakuna kitu ambacho kinatokea hewani mithili ya mwanga wa jua kila asubuhi.Ujenzi wa tabia ya mtu ya ndani ndio mwanzo wa kila jambo kwenye  maisha.Hakuna mtu anayepaswa kukutengenezea ndoto maishani mwako bali wewe ndio unapaswa kujenga ndoto yako maishani mwako.Watu wengine wa nje wanapaswa kukusaidia kukuongoza na kukupa hekima ya namna ya kufika ndoto zako na si kukujengea ndoto zao ambazo zinatakuwa zinaisha ndani yako huku ndoto yako halisi ukiwa umeifukia chini.Ndoto yako maishani ndio furaha yako.Ukivaa kiatu cha kuazima ipo siku utakirudisha tu,Ni bora uvae cha kwako ambacho utakuwa nacho huru na utafurahia daima.

Watu wengine sio kipimo halisi cha Ndoto zako kwa sababu mwenye picha halisi ya ndoto zako ni wewe na sio mtu mwingine .Unapojaribu kujilinganisha na wengine ni kujaribu kuishi ndoto zao.Maisha halisi ya mtu ni mtu mwenyewe.Wakati unaanza kufukiria Kichwani mwako hakuna mtu amabaye alikuwa kichwani mwako.Ubora wa ndoto na Uhalisia wa ndoto unao wewe kichwani na sio mtu mwingine.Ukifwata watu wengine watasaidia kukatisha tamaa kwa sababu kuna sehemu fulani ya maisha yao walishindwa au wao ndio mwisho wa ndoto zao.Vipimo vya ndoto zao ndipo zilipoishia hapo.T.B.S huweka kiwango cha chini cha Bidhaa kuwa na ubora fulani lakini haimaishi kwamba hauwezi kutengeneza bidhaa ambayo ina ubora zaidi ya viwango walivyoweka.

Mafanikio yako kwenye maisha hayategemei kuna wengine wamefanikiwa kiasi gani.Picha halisi ya mafanikio unayoyataka unayo wewe ndani yako na sio kwa mtu mwingine.Unaweza kuona mtu mwingine amefanikiwa maishani lakini ukilinganisha na ndoto ulizokuwa nazo na kipimo cha kiwango chako inawezekana yupo chini ya kiwango cha kipimo cha mafanikio yako.Wewe binafsi ndio kipimo halisi ya kile unachopaswa kukifikia.Iwapo una uwezo wa kupata maksi 100 kwenye mtihani na ukapata 90 bado wewe umeshindwa kufikia mafanikio sababu uwezo wa kupata 100 uliokuwa nao na kipimo cha mafanikio yako wewe ndio unacho hata iwapo utapa maksi nyingi na kuwashinda watu wote Darasani lakini Bado utakuwa umeshindwa uwezo na kipimo chako sio unashindana na mtu gani bali unawezo kiasi gani.

Mara Nyingi inakuwa kichekesho kwenye maisha ya familia yenye malezi ya watoto.Mara nyingi jamii na familia zetu zimetumia jamii kama kipimo cha malezi na tabia za watoto wao.Ulezi wa mtoto hautegemei mtoto mwingine analelewa vipi.Mzazi ndie mwenye picha halisi ya mtoto wake anapaswa awe namna gani na sio mtu mwingine.Wakati wewe unaona mtoto wako ni Bora ukimpeleka kwenye familia nyingine aishi kuna makosa mabayo ataonekana nayo kwa sababu vipimo ni vya aina mbili tofauti lakini akija kwako utaona nyumbani utaona ni bora na mwenye kukupa furaha.Jamii hawezi kukuamulia uzuri wa mtoto na ubaya wake.Mzazi ndio mwenye kujua uzuri na ubaya wa mtoto.Mwenye kutoa guidelines za malezi na Baba na Mama na Sio Jamii.Jamii wao huona mtokeo ya kazi iliyofanywa na Wazazi.Iwapo mtoto wako Unaona ana Uwezo wa Kufanya vizuri zaidi kuliko wengine na akafnya chini ya kiwango,Hata kama atakuwa amewazidi watoto wengine bado atakuwa ameshindwa.......

Mwisho wa Siku Napenda Kusema kila Maji yana Mkondo Wake....Unapojaribu Kuwa mwingine mwisho wa siku Hautafikia Mafanikio Yako ya Kimaisha Bali utaishia Kufikia mafaniko ya wengine ambayo hayatakupa furaha ya kweli...Kumbuka Maji yajitahidi Kulowesha na Wala Moto Haujitahidi Kuunguza Na Mvua Haijihidi Kunyesha bali Ikinyesha ndipo uwezo wake...Ishi Wewe Mwenyewe Halisi ufurahie maisha yako..mwenyewe.
Wahenga Wa Nchi ya Upare Yaani Kwa Maana ya Wapare walisema...Mkodeka Sunga Henacho Evwene Kwa Maana nyingine Hakuna Mtu anayeinama Kuchungulia Uvunguni Kama Hakuna Alichokiona.Yaani Mtu anayechungulia Uvunguni Kuna Jambo ambalo ameliona Lina manafua kwake au Kwa Mwingine.Leo Kwenye Nazungumza Moyoni.. Tunaanza Hapa.Tanzania Yetu Imejulikana kama Kisiwa Cha Amani lakini Ki-Ukweli Ni Kisiwa Cha Utulivu ni Heri Ya Utulivu kuliko Kuukosa hata huo Utulivu ,Maana Wahenga Wanaendelea kusema Heri Nusu Shari Kuliko Shari Kamili.Pamoja na Kukosa Amani ya Kweli kwenye Nchi Yetu Hata Huu utulivu Unatutosha kwa Kiasi Fulani.Huu Utulivu unapotoweka ndipo Tunajiuliza nini kimetokea?
Miaka ya 1950's Kulikuwa na Wimbi Kubwa la Nchi za Kiafrika Kuanza Kupigania Uhuru wa Nchi za Kiafrika Ambao tuliuhitaji sana kuweza kujitawala na kujiendesha bila kuingiliwa kwenye kile tunachoamua kukifanya kwa manufaa ya nchi zetu.Mashujaa Mbali Mbali waliibuka na kuamua kujitolea kupigania Uhuru Wa Nchi Hizi.Mpaka Mwisho Mwa Miaka Ya 1980 Karibia Nchi zote za Kiafrika Zilikuwa Zimeshapata Uhuru wa Ki-Utawala zikiwa zimebaki Chache.Sahara ya Magharibi ilikuwa Bado haijapata Uhuru wake,Huku Afrika ya Kusini Kukiwa Kunaendelea Mapambano ya Vita dhidi ya Ubaguzi wa Rangi.Mwaka 1994 Ndipo Raisi wa Kwanza Mweusi Anafanikiwa Kunyakua Madaraka Baada ya Mapambano ya Muda Mrefu.

Baada ya Miaka Takribani 50 ya Uhuru wa Bara Hili baada lindi la Umaskini limekuwa kubwa na Bado Linaendelea kuongezeka kwa kiasi Kikubwa.Kumbuka Miaka 50 iliyopita kuna watu walijitoa kwa nguvu na kwa jasho pia na kwa Uhai wao ili kuweza kupata Uhuru wa Katika Siasa,Uchumi na Jamii.
Baada ya Kizazi Kile cha Ukombozi kupita,kimeibuka kizazi ambacho ni cha Ulafi na Kutokujali wengine huku watu wachache wakiendelea kujilimbikizia mali na kuwa fanya wengine kuendelea kubaki maskini.

Miaka ya Karibuni Kumekuwa na fujo katika Bara hili la Afrika Kutoka pande zote za Bara hili juu ya unyonyaji na utawala mbovu ambao umeendelea kujikita kwenye nchi Mbali mbali za Afrika Huku Viongozi wa Nchi hizo wakiendelea kuwa madikteta na Rasimu hata pale ambapo wanapoona wameshindwa kuongoza nchi zao.

Tanzania yangu ni Moja ya Sehemu Ya Bara Hili,Baada ya Miaka 50 ya Uhuru.Hakuna Nafuu ya Kimaisha,Kiuchumi na Kijamii.Utawala Mbovu Ndio Imekuwa shida katika nchi hii Yetu ya Tanzania.Badaa ya Kujiuliza Maswali Kadha wa Kadha Bado Jibu limekuwa tata.Moja Ya Swali ambalo limekuwa halina majibu ni Hili Imekuwaje Raia ambao walikuwa watiifu wa Serikali yao,Wamegeuka kuwa waasi tena wa Serikali Yao?

CCM ndio Chama Tawala Katika Nchi Hii,Inakuwaje Wananchi Walio Wengi Wanageukia Chama Cha Upinzani Yaani Chadema..Jibu Ni Kwamba Kuna Majibu ya Maswali Mengi hajajibiwa ..Miaka Hamsini Baada ya Uhuru Bado tatizo la Ukoloni Limeendelea kwenye Jamii hii ya Watanzania Unaweza Usiwe Ukoloni wa Nguvu Bali Ukoloni wa Fikra wa watu wachache kuelekea UMMA wa Raia Walio Wengi.

Baada ya CCM kushindwa kutoa Majibu ya Maswali Mengi,Wananchi hawa wameendelea Kukiunga Chama Cha Upinzani Mkono Baada ya Matumaini Kuendelea kupotea.Miaka ya Karibuni Tumeshuhudia Fujo Nchini Kenya,Chanzo Cha Fujo Hizi ni Kiwango Kikubwa Cha Umaskini Kati ya Watawala na watawaliwa.Na Hakuna Jitihada zinazochukuliwa kuondoa Tatizo hili.

Ukona raia  Wanaasi Chama Tawala Tambua Kuna Jambo ambalo wameliona Upande wa Pili liwe zuri au Liwe baya....Mkodeka Sunga Henacho Evwene....Hakuna Mtu anayependa Kuonewa na Kunyanyaswa kwenye nchi yake..Juzi juzi Tumesikia Fujo Mtwara Leo Arusha Kesho tutasikia Mbeya,Wiki Nyingine Tutasikia Dar...Kinachonitia Shaka Watawala hawana habari juu yanayoendelea au wameyaona wanayafungia macho.Chuki inayojengeka miungoni mwa kizazi Cha Sasa itaigharimu Serikali kwenye Siku Ya kesho.Siasa za Maji taka na Ujinga Ndio Zinazolipeleka Taifa hili Kusiko eleweka.Ukosefu wa Ujuzi na Akili juu ya Kuendesha Nchi na Badala yake kuendelea kutumia Mabavu kunatengeneza Kizazi ambacho ni Sugu na Ambacho Hakitasikiliza Utawala Tena.Hata Uasi kwenye Nchi Nyingi za Afrika zinazopigana Vita Leo Ulinza Hivi.

Rai Yangu kwa Utawala Akili zakuendesha nchi na Kusoma Nyakati zinahitajika sana kuliko Kutumia Nguvu Nyingi.Nchi Ikifanikiwa Sifa Ni Kwa Utawala na Nchi ikianguka Lawama Kwa Utawala.
Ukiona Watoto wako Wanakimbilia Nyumba ya Jirani Kutafuta Hifadhi Tambua Nyumbani Kwako Kuna Shida Tatua Shida ya Nyumbani Kwako Kwanza ndipo uwafwate watoto wako kwa Jirani

............Mkodeka Sunga Henacho Evwene.......................


Huku Kuabudu wageni sijui Kutaisha lini,Tunawafukuza na kuharibu maisha ya raia wetu Kwa Kipindi cha Ugeni wa Muda Mfupi.Tunasahau Wageni hao wakiondoka ,Raia tuliowafukuza maeneo yao ya kujipatia kipato ndio tunaobaki nao.Tunatengeneza chuki ya daima kwenye mioyo ya watu kwa ugeni wa mtu wa siku Mbili.Fikiria Je wewe watoto wako wageni wakija Nyumbani,Unawalaza njaa na kwenye sakafu kisa mgeni kaja? Au wewe unafanyaje....Ndivyo Sivyo ni Ndivyo Si Vyo......Karibu ya Muuza Mgahawa haimanishi Chakula Utakula Bure....Ndivyo Sivyo

Katuni...Kwa Hisani ya Masoud